Alinishauri mwenyewe ila sasa ananitangaza vibaya kwa watu

K Mwita

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
356
314
Nilimaliza chuo kikuu mwaka 2019 kule UDOM na sasa nipo kitaa bila kazi maalum.

Kuna jamaa mmoja yeye ni mjumbe wa nyumba kumi ni kabila moja na mimi akaja akaniambia nianze kuendesha bodaboda ili nipate pesa ya kujikimu.

Nilianza kuendesha bodaboda mwaka jana 2020 nikawa napata pesa za vocha ila jambo la kushangaza jamaa anaanza kuwaambia watu kuwa "mnamuona mwita amesoma sana mpaka chuo kikuu lakini ameishia kuwa dereva wa bodaboda kama vijana walioishia darasa la saba tu".

Sasa sijui nimfanyeje mtu huyu?
 
Nilimaliza chuo kikuu mwaka 2019 na sasa nipo kitaa bila kazi maalum. Kuna jamaa mmoja yeye ni mjumbe wa nyumba kumi ni kabila moja na mimi akaja akaniambia nianze kuendesha bodaboda ili nipate pesa ya kujikimu. Nilianza kuendesha bodaboda mwaka jana 2020 nikawa napata pesa za vocha ila jambo la kushangaza jamaa anaanza kuwaambia watu kuwa "mnamuona mwita amesoma sana mpaka chuo kikuu lakini ameishia kuwa dereva wa bodaboda kama vijana walioishia darasa la saba tu". Sasa sijui nimfuate nikamtukane?
mtukane tu 😂😂 ubaya ubaya mwana
 
Hiyo elimu yako haiwezi kukusaidia kamwe kwa akili hiyo

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Jamaa yako anajisikia vizuri Sana kwa 'kukupatia mchongo'. Pia anatamani kupewa credits kuwa yeye anahusika kwa wewe kuwepo ulipo. Na pengine hajasoma kiivo, sasa ni faraja Sana kwake kwamba unapiga mishe sawa na ambae hajapiga shule kivile; kwa kifupi alikupa ushauri ambao hakudhani ungeutendea kazi.

Endelea na kazi, Endelea kufanya applications; siku moja ashtuke tu wewe haupo tena level iliyo nayo. Lakini wala 'huvimbi'.
 
Muwekee mchele kidogo kwenye bia yake then ile burger iweke yai hatakusimanga tena
 
Back
Top Bottom