Alinishauri mwenyewe ila sasa ananitangaza vibaya kwa watu

Nilimaliza chuo kikuu mwaka 2019 kule UDOM na sasa nipo kitaa bila kazi maalum. Kuna jamaa mmoja yeye ni mjumbe wa nyumba kumi ni kabila moja na mimi akaja akaniambia nianze kuendesha bodaboda ili nipate pesa ya kujikimu. Nilianza kuendesha bodaboda mwaka jana 2020 nikawa napata pesa za vocha ila jambo la kushangaza jamaa anaanza kuwaambia watu kuwa "mnamuona mwita amesoma sana mpaka chuo kikuu lakini ameishia kuwa dereva wa bodaboda kama vijana walioishia darasa la saba tu". Sasa sijui nimfuate nikamtukane?
Ukienda kumtukana itaonekana kweli we ni darasa la saba


Unacho takiwa kujali ni kuwa huibi cha mtu wala huombi kwake


We pambana bodaboda ni kazi kama kazi nyingne
 
Najua mjumbe Aliekushauri ni darasa la Saba B..
Unajitutumua umemaliza UDOM.

Alafu unaomba ushauri ukamtukane!

Nakuahidi darasa la saba B atakupeleka jela na hiyo elimu yako itazidi kuwa hovyo....
 
Hiyo KLMY hapo mbele ya Mwita imenifanya nimkumbuke mchizi wangu mmoja hivi mpambanaji kitaa...
 
Wewe msubiri siku anakuja kukukodi umpeleke sehemu, akipanda unaangalia mti mkubwa unambamiza hapo akaugue miezi sita wewe unajifanya umeruka halafu unaanza kumsema jamaa angeruka tusingepata ajali, usikubali jino kwa jino na ukimuacha tu atakuzoea
 
Back
Top Bottom