Nililogwa ili nife kwa kisukari na pressure

Kinengunengu

JF-Expert Member
May 3, 2021
1,719
4,310
Hii ni kitu kilochonitokea Mimi Binafsi wakati nikiwa naishi Wilaya ya Mlele (Inyonga) Mkoa wa Katavi. Sitataja majina halisi ya watu waliohusika na nitajitahidi kuficha baadhi ya vitu ili kuficha uhalisia wangu.

Kwa majina naitwa Kinengunengu, nikiwa nimegraduate SUA pale na kupata kazi Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi. Nilinunua kiwanja na kujenga nyumba yangu. Nilipomaliza kujenga, nikawa na mpango wa kujenga fence kuzunguka nyumba niliyojenga.

Nilianza ujenzi wa fence ya tofali ya kuchoma. Wakati wa ujenzi wa fence, walikuja vijana fulani na wakaniambia wao wanafyetua tofali za kuchoma na wanazo wanauza.

Nikanunua tofali zao kisha nikawapa tender ya kunichomea tofali 20,000 za kuchoma. Wakaanza kazi ya kunichomea.

Kutokana na kutingwa na kazi na kipindi hiko sikuwa nimeoa, nilimpa kijana mmoja kati ya wale waliokuwa wananifyetulia tofali chumba pale kwangu kwani sikuwa nimehamia nilitaka mpaka ukuta uishe.

Nilimpa chumba ili alinde nyumba pia awe anawasimamia wenzake waliokiwa wanafyetua tofali.

Jamaa walifyetua tofali na nilimaliza kujenga ukuta ila sikuhamia mapema na sikuwa na hamu ya kuhamia pale. Kijana aliyekuwa anakaa pale akaleta mke wake.

Nikawa namhudumia mimi yeye na mkewe. Niliwanunulia godoro, vyombo vidogo vidogo vya ndani pia nilikuwa nawanunulia chakula pia kuwahudumia pindi mwanamke au jamaa akiumwa. Nilimfanyia wema yule kijana pamoja na mke wake.

Hamu ya mimi kuhamia kwangu ikaisha na nikaanza kupachukia pale kwangu bila sababu yoyote.

Hali ya kupachukia na kutokuwa na hamu na kwangu iliendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja na jamaa walikuwa wananishangaa kwanini sihamii kwangu.

Baadaye mwanamke niliyekuwa na mahusia o naye akaniambia ana ujauzito na kihsa alikuja jifungua. Baada ya kujifungua, nikamueleza Baba yangu na alikuja then nikaenda kujitambulisha ukweni ikiwemo kutoa mali na kumuoa mke wangu rasmi.

Baada ya kuoa na nikiwa na mke na mtoto, mke akasema tuhamie kwetu rasmi. Nikahamia kwangu huku yule kijana akiwemo mule ila walishindwana na mkewe mke akaondoka. Nikawa namlisha, namvalisha na kumtunza. Nikakaa naye miezi sita huku huduma zote za msingi nafanya mimi kama Baba mwenye nyumba. Jamaa akanogewa kwani alikuwa hafanyi shughuli zake za vibarua vya mtaani kwani alikuwa na uhakika wa kula, kuvaa na kuoga. Alipokuwa anahitaji vocha nilikuwa nampa.

Siku moja nimetoka kazini, namsikia mke wangu ananiambia, fulani kasema "anataka akupeleke kwa mganga ukaoshwe nyota ili upendwe na kupandishwa cheo kazini". Nikamwambia toka nizaliwe sijawahi kwenda kwa Mganga mimi ni mkristo na ninamuamini Mungu aliyenilinda toka nikiwa mdogo, akanisimamia masomo hadi chuo kikuu na kunipatia kazi kwenye hii kampuni.

Sina chale wala sijawahi kwenda kwa Mganga kwa hiyo akirudi mwambie sitaki huo ujinga wake.

Hilo likapita, siku moja usiku kama saa 7 hivi nikiwa nimelala nikasikia harufu ya udi/uvumba ule wa kupandishia mashetani. Nikaamka na kumuuliza, unafanya nini usiku huu nyumbani kwangu? Kwanini kuna harufu ya udi/uvumba usiku huu? Akaniambia, anazindika mizimu!!!!!!

Itaendelea.
 
Kwa majina naitwa Kinengunengu, nikiwa nimegraduate SUA pale na kupata kazi Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Itaendelea.
Uchawi haupo na hauta kuwepo
 
Hadithi za washirikina ndio daima haziishi kwa siku moja, lazima muandike itaendelea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom