alimvalisha pete ya uchumba chini ya shinikizo, sasa anataka kumwacha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

alimvalisha pete ya uchumba chini ya shinikizo, sasa anataka kumwacha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbunge wa CCM, Dec 30, 2009.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeona thread moja inayohusu pete ya uchumba na imenikumbusha kisa nilichowahi kusuluhisha cha wanandoa kulani waliotaka kuachana, nimeona niwamegee kidogo. kisa chenyewe ni hiki:

  yalikuwepo mapenzi kati yao na muda si mrefu binti akapata mimba. alipanga kuitoa ile mimba kwan hakutaka aibu ya kuzalia nyumbani. kutokana na hamu ya mtoto bwana akaamua kumuoa ili asitoe mimba. wakati wa mandalizi ya harusi, kama kawaida ikapangwa siku ya kuvishana pete. nami nilialikwa katika hafla ile fupi iliyofanyika pale milenium towers.

  cha kushangaza kila mtu, binti alifika kwenye hafla ile akiwa na haraka na alitaka hata kukataa kukaa kwenye kiti. alikuwa akisema amepita pale kuvalishwa pete yake anataka kwenda kupumzika. jitihada zilifanyika. mchumba wake alimuita kando kumsihi asvuruge hafla ile, lakini wakati akiendelea kumsihi, tulishtukia maneno makali yakitolewa na yule dada.

  alisema kama hataki, yeye hamlazimishi lakini wasilaumiane mbele ya safari na maneno mengine mengi tu. ilibidi nasi wageni tujaribu kutuliza hali, binti alikubali kukaa lakini akitoa sharti la kukaa dakika tano tu, tukizidisha mbwembwe anaondoka! ilibidi mambo yaende haraka, akavalishwa pete yake, mara akanyanyuka,

  wakati anaondoka, bwana alitaka kumbusu akakataa kuwa ameishachelewa. shughuli ikaisha!

  ndoa ilifungwa, lakini baada ya muda wa kama mwaka mmoja, migogoro ilizuka, wakaanza mchakato wa talaka..............

  baadaye mume alinidokeza kuwa ugomvi wao uliopelekea kutaka kummpa talaka ulianzia hotelini siku ya honey moon yao, toka hapo hawaelewani kabisa,

  mna ushauri gani kwa hawa wandoa?
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280

  mkuu labda unaweza kujua tatizo lenyewe lililopelekea talaka kuzungumziwa?
   
 3. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hao watu wana mambo mengi sana, unaweza kufikiri wamelazimishwa kuoana, hasa mwanamke. kule honey moon mwanaume alitaka ngono, mwanamke akakataa bila sababu yoyote, hivyo utaona kuwa hawakufurahia honey moon. mwanamke anasema siku hiyo ya oney moon mumewe alimbaka kwani alimlazimisha na yeye hakuwa tayari kwa ngono siku hiyo.

  mwanamme alimsamehe akidhani kuwa huenda tabia ile ilisababishwa na ujauzito. lahaula, alipojifungua ndio tabia ilizidi kumchanganya, kwani alikataa kufanyane mapenzi moja kwa moja hadi walipopata ushauri nasaha kutoka kwa daktari!!!!!!!!!!!!

  nilipomuuliza kama mumewe hamridhishi, yeye alisema yuko bize na mtoto. mume asubiri hadi atakapopata nafasi !!!!!!!!!!!

  ilikuwa kaaazi kwelikweli
   
 4. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa ufupi huyu dada hafai,UNAWEZAJE KUA NA HARAKA katika occassion muhimu kama kuvalishwa pete?
  Hii si ilipangwa kabla na taarifa akapewa sasa hiyo kuwa na haraka ni dalili ya kama dharau fulani vile,halafu kingine KITENDO CHA KUKATAA TENDO ktk honeymoon ni dharau au mapenzi yaliyopotea,mie ningemshauri jamaa apunguze makali ya kumpenda huyu dada,asiende nae spidi,
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Huyu dada inabidi apate msaada wa kiakili, nadhani kuna something wrong hapo
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ama kweli kwenye miti hakuna wajenzi !!!!

  hapakupaswa kuwa na ndoa hapo, huyo jamaaa aliona vituko kama hivyo na bado akamuoa???

  hilo pozitu siku ya engegement ni dalili tosha kuwa mambo yasingekuwa mazuri, lakini jamaaa akaendelea na ndoa.

  wajaribu kupata usuluhisho wazeee ikibidi talaka!!
   
 7. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Mi dada kama hii dawa yake ni kuiletea mwenzake on the same bed,kama haijakimbia ndoa lazima awe chizi,wenzake kila siku wanapiga goti waolewe yeye analeta mbwembwe?Huyu jamaa asilete uoga wa kiapo cha biblia au msaafu,akina Lowasa walisha apa navyo sana hivyo vitabu na vilevile wamevikana viapo vyao,ndio iwe yeye?
   
 8. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu na ukimwi wote huu? Hapo utakuwa umeua!!!!!!!
   
Loading...