Tena 7 mara 70biblia inatufundisha sisi wakristo kusameheana mkuu.
Aisee babaangu eee.. ukurudi ujue kifutacho ni majanga coz lazima alipize kisasi. Kama mtu alikuwa na ujasiri wa kukuambia the door is open huyo mtu sio wa mchezomchezo, ila kama namwona vile na saa hiyo wewe unarembua kama ngómbe.Za asubuhi wadau wanajukwaa.
Kwa takribani miezi kadhaa toka mwaka huu uanze nilikua na mahusianao ya kimapenzi na mrembo mmoja hapa mjini, ambapo wakati penzi linaanza lilikua tamu kiasi kwamba nikajiona natawala dunia yaani Trump ni kama secretary wangu lol.
Sasa as usual baada ya muda kupita penzi likashamiri akaanza kujiona ameniweka mfukoni na kuanza visa sijui kama alikua serious au alikua anatania, tukikwazana kitu kidogo anaishia "the door is open" sentensi ambayo ilikua inaninyima raha sana nikawa nakausha tu labda utani.
Ikawa ndio hivyo penzi likaanza visa na revenge za hapa na pale mpaka moyo wangu ukapasuka akatoweka kabisa.
Wiki kadhaa zilizopita tulizinguana kidogo akarudia maneno yake hapo ndipo alielewa maana ya choupa moting maana nilimpa makombora ya Korea Kaskazini mpaka akashangaa ndio yule ambaye nilikua namshika mpaka sharubu au ni mwingine.
Sasa ngoma imehamia kwake, baada ya kumpiga chini akadhani natania mwisho wa siku anaona siku zinakata sina time nae nafanya yangu simpigii simu wala SMS wala salamu yake sina haja nayo mi nafanya yangu.
Amebaki akipiga simu na SMS za kila namna kila wakati mi sina time nazo nafanya yangu na maisha yanaenda kama kawaida. Amefikia point anaiuliza "wewe mwanaume gani hujui kusamehe unaona raha mi nikipata taabu"
Anaomba sana msamaha amefikia mpaka kupitia kwa washikaji zangu ili wanishawishi mi sina time nawaambia kama wanamtaka waendee nae mi sirudiagi matapishi. Kwa kweli anatia huruma, naskia huko kazini kwao hata kazi haziendi analialia tu kila time.
Angalizo: Wadada msifanye msiyoyaweza mwisho mnatia huruma tu.
Choupa moting.
Mkuu asubuhi yote hii umeamua kuandika kuhusu huyo binti? Acha kutuzuga bana.....najua kamoyo bado kanadunda kiaina kwake. Mapenzi hayafutiki kwa wiki kadhaa mkuu! Rudiana naye tu but muonye kuwa next time akirudia kauli zake ndo mazima. This time "Tump" atakuwa kama mpiga deki tu kwenye utawala wako .... 😀
Hii tabia akina dada wengi wanayo, binafsi huwa sipendagi kuanzisha mahusiano mapya mara kwa mara so nikipataga binti huwa natulia kweli kweli, nilimpata binti na yeye alikua ana tabia hyo hyo yani mkigombana kidogo tu anaishia bwana kama vipi tuachane, mara ya kwanza nilikua najifanha mjinga nikajua ni utoto tu unasumbua, ila ikawa too much, yani haipiti week au mwezi bila hii kauli kusikika,
Mwanzo wa mwezi huu tukagombana kidogo tu basi akarudia hyo kauli yake na mm ndo nlkua naisubiria.. Na mim nmempotezea mazima.. Sipokei simu yake wala sijbu message yake..
Mrudie huyo dada mkuu men don't loveAsee ningekua nampenda ningesharud ila i have nothing to loose. Ukinizingua nakua mbogo mm
Basi hukumpenda ile kikweliiAsee ningekua nampenda ningesharud ila i have nothing to loose. Ukinizingua nakua mbogo mm
Wew Dada mbn una akil kubwa na tofaut na wenzio?Sana tu akili ndogo kweli,hii jamii iliyonizunguka naona mengi sana