Alikiba Chekecha Cheketua (Here is the song)

msafwa93

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Messages
4,493
Points
2,000

msafwa93

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2011
4,493 2,000
Niaje wana JF,

Mwana wenu karudi tena. Kama ilivokua kwa wimbo wa Mwana, JF ndo ilikua ya kwanza kuupata kupitia mimi basi nimeona nisiwe mchoyo niwape tena huu wa Chekecha Cheketua..

Nimeusikiliza huu wimbo kama Wiki mbili hivi nimegundua ni sheedah nyingine hapa mjini..

Kwa taarifa tu ni kwamba, Alikiba atazidi kukimbiza kwa sababu ni msanii pekee mkubwa wa TZ ambaye bado anaimba mziki wa asili ya Bongofleva na sio ule WesternAfricaFleva (Naija na Ghana)..

Wakati wasanii wengi kwa sasa wakiiga vibwagizo vya Nigeria kama vile 'chai', 'sii', yeye akaona awe mbunifu na kubuni kibwagizo chake mwenyewe ambacho kwa sauti yake tamu hakuna msanii mwngne anaweza kukiiga 'yooo'..

Baada ya wimbo wa 'Mwana', kuna nyimbo mbili (HELA na WIFE WA DUNIA) za Alikiba zilichuja na kuwachanganya watu wakadhani ni official release wakati sio hivyo..

Nisiongee sana..

HERE IS ALI's NEW FLAGSHIP SONG.

Huu hapa 
Last edited by a moderator:

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Messages
4,316
Points
2,000

el nino

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2013
4,316 2,000
Chai n siii origin yake sio west africa hivyo vibwagizo michael jackson ameanza kuvitumia kitambo tu.....

Halaf kingine kuimba eti muziki kwa asili ya kitanzania havikufanyi uwe msanii mkubwa maana hata best naso anaimba original bongo fleva..

Tusisahau kuangalia top 10 ya trace music Africa...kuna kitu fulani amazing
 

McDonaldJr

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Messages
6,413
Points
2,000

McDonaldJr

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2013
6,413 2,000
Unafiki kando Alli K anafanya muziki wake katika levo tofauti na kitu kingine kajitengenezea ladha yake ambayo inampa utambulisho fulani ukisikiliza midundo ya nyimbo zake hakuna u-Magharibi,u-Naija wala Mikwaito ambayo wengi wameing'ang'ania.
Ila yeye na timu yake wajitazane upya kwenye video wanazotengeneza wanahitaji kuwekeza sana ili kuingia kwenye ushindani wa soko maana wanamuziki wenzie wengi wamewekeza huko tena wengi wana nyimbo mbaya ila video zinawafanya kua juu.
 

Forum statistics

Threads 1,380,709
Members 525,856
Posts 33,777,500
Top