Alichosema John Locke kuhusu sheria na haki

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,134
2,010
Habari my comrades

Kuna maneno mengi sana yanasemwa na mwanadamu kuhusu namna mbalimbali ndani ya jamii zetu, Lakini kuna sentensi zilizosemwa ambazo zitabaki na sisi wanadamu muda wote ambao tutakuwa wakazi kwenye hii sayari yetu ya tatu kutoka nyota jua. Mwanadamu kiumbe ambacho kazi yake hapa ulimwenguni ni kufikiri tuu na katika kufikiri ndipo binadamu anaweza pata tunu ya kuishi milele, si kimwili bali katika fikra, kuna sentensi ziliwahi kutolewa na john ambazo nitaziwasilisha kwa baathi ya maneno yaliyotolewa.

JOHN LOCKE

Mojawapo ya philosopher wa kuheshimiwa sana kutokana yale ayopata kufikiri na kufumbua wengine. Huyu john alisema mambo mengi kuhusiana na serikali, watu, jamii na mengine kedekede kwa mimi alinigusa sana maneno aliyosema juu ya sheria ambako anasema hivi.

Kazi ya sheria ni kuhakikisha inatunza na kukuza haki za wananchi.

Katika hii sentence inabidi ishikwe na wadau wote wanaohusika na sheria za nchi. Kwanza yapaswa kujua katika miaka hiyo locke alishabainisha haki ambazo hazikwepeki kwa binadamu haki ya kuishi, haki ya kumiliki mali, haki ya kufanya maamuzi binafsi pasipo kuingiliwa hizi ndizo haki ambazo zapaswa kutunzwa na sheria kuhakikisha serikali ambayo ipo madarakani haisababishi hizi haki kupokonyoka. Bunge kama chombo cha serikali chenye jukumu tukufu la kutunga sheria za nchi sehemu ya pili ya sentensi hiyo ya bwana locke inawahusu katika kukuza haki za wananchi katika sheria inazotunga isije ikatokea bunge linatunga sheria ambazo zinakuwa zinapunguza haki za wananchi bali inabidi kwa kutumia hekima inatunga sheria mpya ambazo zinakuza haki ambazo raia watawaliwo watanufaika.

JOHN STUART MILL

John huyu pia ni mwingereza alipata kusema juu nadharia mbalimbali za uchumi na uendeshaji wa serikali. Katika maneno ambayo alipata kutamka ya kuonya ni yafuatayo

tujihadhari na ukandamizaji kwa wale wachache katika jamii.

Hii taathari alitoo kipindi hicho cha nyuma Lakini imekuwa ipo na watu wengine wamekuwa wakinyanyasa raia wenzao kwa kutumia kigezo cha wingi wao. Yapaswa kujua ya kuwa kuwa wengi kukubaliana haimaanishi jambo hilo ni sawa, tumeona serikali ya marekani katika mfumo wao wa kupiga kura wakijaribu kuzuia hii hitilafu ya wengi kunyanyasa wachache kupitia electrol vote. Sasa kutokana na mambo yanavyoenda inaelekea bunge letu kuwa na wingi wa watu wa CCM wengi hivyo kupata chance ya kunyanyasa wabunge wengine kwa kutumia wingi wao wa kura.

Haya mambo yalishaweka bayana miaka ya 1700 na 1800, na history imeonyesha kwamba yapo mataifa yanayotilia maanani maneno haya ya watu wa kalamu na yakapiga hatua kubwa za uelewa Lakini yapo pia mataifa yameendelea kufanyiziwa na history viongozi wake waendelee kutenda makosa mpaka pale watakapojifunza alafu ukipita mda kidogo vizazi vyao visahau sentensi hizo viongozi wao kutenda makosa upya tena na tena.

Na hao ni john wawili ambao walisama yao na kuheshimiwa.
 
Back
Top Bottom