Elections 2010 Alichosema Dr. Slaa kuhusu nyumba za Tembe na Mabango ya Mgombea

Kweli jamaa anaongea anachokijua. Kwa maisha kama haya halafu unabandika bango hilo sizani kama utachukia ukiambiwa kuwa una akiri za nyani
 
Huo ni mfano tu, kwanza hiyo si ipo upright! zipo zilizoinama yaani zinakaribia kuanguka lakini bado tu wamebandika bago la gharama kubwa
Mungu atusaidie
 
Kweli jamaa anaongea anachokijua. Kwa maisha kama haya halafu unabandika bango hilo sizani kama utachukia ukiambiwa kuwa una akiri za nyani

Policy za UN za kutaka watu wasome ni pigo kubwa sana kwa CCM. They really hate it although hawana jinsi inabidi watekeleze kwa shingo upande.
 
Nashawishika kuamini kuwa pengine ni makada wa CCM wanakuja kuyabandika na kwa hao masikini kwao ni kama mapambo. They are absolutely naive.
 
Policy za UN za kutaka watu wasome ni pigo kubwa sana kwa CCM. They really hate it although hawana jinsi inabidi watekeleze kwa shingo upande.

Na kwa hilo linawapa taabu kweli kweli, japo kwa wao lazima kuchakachua maana wanajenga shule bila samani halafu wanafunzi walete. Na haohao watoto michango kibao, wao mipesa wanatia ndani.
Kwa hiyo si kwa shingo upande tu, Wanaiba mshiko wa maana sana katiaka hilo.

Majizi yapumzike mwaka huu jamani!
 
Mwabeja! Usukumani...Jamani ndugu zangu wasukuma wakati wa mabadiliko ni sasa vinginevyo mtajiju. Kuna mtu alileta mada ya kwa nini CCM inapendwa mikoa maskini (umaskini kama relative term maana wote tuko hoi) nikafikiri siyo kweli sasa huu ushahidi ni red handed! Tena siyo bango moja ni mengi yaani kila ukuta maana hata mbele (kama kweli ni mbele maana naona mraba fulani) lipo. Kazi kweli kweli!
 
Jamani, nadhani huyo mwenye nyumba ametumia hilo bango kuziba tundu lililokuwepo kwenye ukuta wa tembe lake. Kule vijijini wengi wanavaa t-shirts za CCM si kwa sababu wanataka kukitangaza chama hicho, bali hiyo ni nguo mpya ambayo wameipata katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na ndio maana zinavaliwa sana
 
Ujinga wa Watanzania ndiyo mtaji wa CCM. Hata hizi shule za kata ingawa bado ni duni lakini ndiyo kichocheo cha mabadiliko katika fikra za watu katika uchaguzi wa mwaka huu. Uliwahi kuona wapi sera za Chama cha siasa zinakubalika kwa wananchi vijijini (kisomo cha chini) na hazikubaliki kwa wasomi? Ina maana kuwa waliosoma uelewa wao ni mdogo kuliko ambao wamesoma kidogo? Kuna maana gani kwenda shule kama uelewa wa mtu hauongezwi na kisomo? najua kuwa kuna wasomi wasiojali maslahi ya nchi, lakini hao ni wachache na wengi wao wapo kwenye nafasi za uongozi wa CCM.
 
Ngarama za kampeni zinatokana na uwezo wa chama. Sikumsikia Slaa akisema Mbowe asitumie Helicopter 2005 kuwafikia wapiga kura na badala yake ajenge shule. Licha ya uwezo mdogo wa kifedha

Basi na Chadema pesa wanazotumia kufanya kampeni, wazitumie kujenga shule...

Don't be fooled by politicians...
 
Nilishasema kuwa huyu rais mtarajiwa yuko juu na haropoki kama ni data basi kwake ni makao makuu!
 


Huko kijijini... (Picha toka FB)

Nyumba kama hii ukisimama kwa nje unakuwa unaizidi urefu. Kwa hiyo huwa zina basement floor. Yaani unaingia kwa kupinda mgongo, then ukishakudumbukia ndiyo inakuwa inakuzidi urefu. Zipo nyingi sana maeneo ya Dodoma, Makao Makuu ya Tanzania (kwa mujibu wa Ramani ya Africa).

Watanzania Amkeni jamani!! Kwa nini munakubali kuwa masikini wa fikra???
 
Kweli bwana hata huko kijijini kwetu mitaa ya Singida, mabango yaliyobandikwa yanathamani kuliko nyumba zetu "full suit" a. k.a cake.

Sijui tutaamka lini jamani tujue kwamba CCM ni adui namba mmoja wa nchi hii!
 
attachment.php


attachment.php
 
Nafikiri CCM na washirika wao akina Mbatia hawaingii tena humu jamvini. Na kama wanaingia basi hii ndio dhambi hao ya asili. Hawatakaa wauone ufalme wa Mungu kamwe. Mateso yao yataanzia hapa hapa duniani na sii mbali sana toka 31/10/2010.
 
Kuna nyumba nyingine unakuta zina bendera kubwa ya CCM. nyumba hizi ikitokea upepo kidogo tu zinaweza kuangushwa na bendera. Na hawa ndio mashabiki wakubwa wa CCM. JK Akiwaambia kuwa akiingia Ikulu ni siagi tu wanashangilia na kuchekelea.
 
Back
Top Bottom