Wiki mbili tatu zilizopita nilianzisha uhusiano na binti ambaye nilimtamani kama sio kumpenda.
Moyo wangu ulivutiwa na umbo lake na baada ya kuongea naye kidogo nikajisemea rohoni huyu ndio atakula matunda ya kazi yangu.
Nilikuwa najiuliza huyu binti mzuri hivi waharibifu hawajamuona? labda nilipangiwa mimi kuwa naye nk.
Siku moja akaniambia yeye ana mtoto mdogo ambaye amemkabidhi aliyezaa naye, nikaanza kuwa na maswali iweje amkabidhi mtoto kwa baba angali mdogo wa miezi minne tu?
Kadri siku zinavyoenda nimekuwa nam finance vizuri tu kiasi kwamba hata kwao wamemshtukia,wanamuuliza mbona unapendeza hivo siku hizi na yeye anawajibu ni kawaida tu! Kwa kweli nam feel moyoni.
Sasa jana kaninyima usingizi, kaniambia hana uhakika kama nampenda kweli, anasema sisi wanaume ni waongo sana.
Eti kuna mwanaume alimsaliti na hivyo ameachana kabisa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote.
Mpaka sasa ana miezi saba hajafanya mapenzi, akijisikia hamu huimaliza kwa kuangalia picha za xxx.
Ninachojiuliza kwanini hakuniambia siku zote hizo mpaka ananiambia hivi leo wakati mimi nimejitoa kwa hali na mali kumjali?
Sasa wenye mauzoefu niambieni nifanyeje ili niufungue moyo wake uliojeruhiwa.