trudie
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 3,335
- 7,662
Habari wana JF,
Mimi ni mama wa mtoto mmoja binti wa miaka 4. Mtoto akiwa na miezi 3 tulishindwana na baba wa mtoto hivyo nikaondoka kwake, tulikuwa tunaishi pamoja (alinitolea mahari, hatukufunga ndoa).
Yeye anaishi Mwanza mimi nipo Dar, katika kipindi chote alikuwa anatoa matunzo ya mtoto bila shida na tulikuwa na mawasiliano mazuri kabisa. Mwaka jana alikuja Dar kumsalimia mtoto na akakaa naye wiki moja kwa ndugu zake, akamrudisha, sikuwa na shida maana bado ni baba yake.
Mwezi uliyopita akapata likizo amekuja Dar, kama kawaida akaomba kumwona mtoto na nikamruhusu. Akamchukua, akaa naye siku 3, nikamwomba mtoto nitoke nae mtoko, jioni akamchukua tena.
Sikutaka kuwa namsumbua sana, nikamwachia nafasi akae na binti yake likizo anavyoenda Mwanza amrudishe. Wiki iliyoisha nikampigia simu naomba nitoke mtoko na mtoto wikiendi kama bado upo likizo utaendelea kukaa naye, akawa ananipiga chenga.
Ikabidi nimshirikishe mdogo wake ambapo ndiyo alifikia hapa Dar Madale, ndiyo jana napata taarifa baba mtoto kaondoka na mtoto kaenda naye Mwanza bila kuniambia. Mtoto ana miaka 4 kiukweli nilipaniki na sikupenda.
Je, alichofanya ni sahihi kuondoka na mtoto bila kuniambia? Kisheria imekaa vipi? Naombeni maoni yenu.
NOTE: Bado hajaoa na anaishi peke yake. Yeye anaona kama kafanya kitu sahihi. Yupo humu JF, najua atasoma pia hapa.
UPDATE: Mtoto nimeshamchukua na amesharudi Dar baada ya muda mrefu. Namshukuru Mungu wote tupo salama na pande zote tupo sawa.