maishapopote
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 3,277
- 5,514
Nikiwa Darasa la Saba Mwaka 1995, kama kijana yoyote wa Moshi Mjini Nilikua na Hamasa Kubwa Kisiasa, Na Moshi Mjini Ilikua Imewaka Moto Kisiasa.
Bwana Mrema Alikua Amejiunga na NCCR Mageuzi, Nayo NCCR ikaunganisha Nguvu Na CHADEMA Wakaweka mgombea Ubunge Bwana MTUI...na Urais Akawa Bwana Lyatonga Mrema..Kampeni Zikapamba Moto.
Timu ya Mrema ikapita kuomba Kura Uwanja wa Mashujaa Moshi ukajaa na kutapika..mimi nimo mbele kabisa Huku Mrema,Pale Makongoro Nyerere.
Wakatuelekeza kwa unyenyekevu kabisa Kwamba Wiki Ijayo Baba wa Taifa Na Mgombea wake Bwana Mkapa watakuja kwahiyo Fanyeni Hivi Na Hivi..Hao wakaondoka zao wakaenda Arusha.
Baada Ya wiki Kweli Mzee wetu Baba wa Taifa akaingia Moshi,Niliwahi Uwanjani Tokea saa Tano, Kumbe Hakuja Na Mzee Mkapa Bwana, Akaanza Hotuba na vile vichekesho vyake
Mwisho Akainua Picha ya Mkapa Nakumbuka ile picha ni ya kuchora akasema Nawaomba Mumpe kura huyu kwa Maendeleo ya nchi Yetu...
Uwanja Wote wa Mashujaa Ukanyamaza kimya Kabisa,kimya halafu wakainua vidole viwili ile Alama inayotumiwa na CHADEMA uwanja wote ukawa unapunga huku watu wamenyamaza kimya kabisa..
Mwalimu Akiwa amefura kwa hasira,akatamka nikiwa namuona na kumsikia. MTAKE, MSITAKE HUYU ATAKUA RAIS halafu akatupa ile picha chini...akaitupa kabisa halafu akashuka jukwaani Akaenda zake mkutano ukafia hapo.
Ilasikuwahi kumuona Tena Live Mwalimu Hadi Alipokufa nikiwa Form Four mwaka 1999...ila nilikua namfatilia sana hotuba zake
Tutamsema Vibaya Lakini Hakuna wa Kuvaa Viatu Vyake na Hatatokea Alikua Baba, kiongozi, mkombozi, mwalimu, mwanafalsafa, mpenda kusali, na mengine mengi. Namkumbuka na Atakumbukwa na Taifa Hili kwa Miaka Yote Hadi Ukamilifu wa Dahari...Siku Mwenye Mali Yake Atakapopenda na kusema Mwisho ndio Huu..
MP...JF LEGEND
.