Alichokifanya Mwalimu Nyerere Mwaka 1995 mbele ya Macho yangu

HV makongoro kwann alimsaliti baba yake
Kiukweli elimu ya uraia, inahitajika sana, Baba kuwa CCM, Mama au mtoto kuwa chama kingine chochote ni hakuna usaliti wowote, na kwa msiojua, Uchaguzi huo wa 1995, Mwalimu Nyerere alimpigia debe mgombea wa NCCR Mageuzi ubunge wa Musoma vijijini Butiama ilipo na akashinda. Utasema Mwalimu aliisaliti CCM?.
P
 
Ndy aliisaliti ccm huko butiama kama hakuisaliti kwann asimpigie debe mgombea wa ccm
Pia kumbuka si kila anaye jadili siasa za tz ni mtanzania!
Hvy elim ya uraia kwangu haina nafasi
 
Sasa huyo mkuu anawasiwas wa hii story, weee utudanganye upate faida gan kwa mfano ? Ikizingatiwa hatukujui!!!
Hapa JF ni Kisima cha maarifa Mkuu..
Atatokea mtu tu...anaijua hii story na atasema ni kweli au uwongo..na kama ni uwongo ni kwa kiasi gani au ukweli kiasi gani
 
Huo no uongo mkubwa, Nyerere siku zote alikuwa muumini wa nguvu ya hoja na sio hoja ya nguvu. Kipindi Cha kampeni za urais mwaka 95 Mrema alisumbuliwa Sana na vyombo vya dola huku watu wakitaka kumbeba aliyekuja kusimamisha usumbufu huo alikuwa me. Nyerere aliyewakanya na kuwaambia hata maiti inabebwa na tamko hili alilitoa Iringa.
Labda umechanganya na kauli ya mgombea mwenza wa ccm aliyesema mpige kura msipiga ccm itashinda.
 
I'm very sorry, I seriously doubt the authenticity of this story.
P
Ni kweli kabisa. Alinyanyua picha hiyo wananchi walipoiona wengine walianza kuzomea kama kumkataa huyo aleyekuwepo kwenye picha yan Mkapa. Aliinyoshea kifimbo chake ile picha akasema “Mnamuona huyu...Taka msitake, huyu ndo rais wenu”, akaidondosha chini na akashuka jukwaani kwenda kupanda gari na kuondoka hapo hapo.
 
Pascal...Nakuhakikishia Comrade nilikua uwanjani that day..na hata mkutano wa makongoro nilienda...
 
Kuna watu wanadhani MTAKATIFU Nyerere hawezi kukosea.

Pia kuna wajinga wanadhani uhuru uliletwa na Nyerere kumbe kuna watu walipambana ila ubinafsi wa Nyerere akawa anajipa kiki peke yake.
 
Nikiwa Darasa la Saba Mwaka 1995, Kama Kijana Yoyote wa Moshi Mjini Nilikua na Hamasa Kubwa Kisiasa, Na Moshi Mjini Ilikua Imewaka Moto Kisiasa...

Bwana Mrema Alikua Amejiunga na NCCR Mageuzi,Nayo NCCR ikaunganisha Nguvu Na CHADEMA Wakaweka mgombea Ubunge Bwana MTUI...na Urais Akawa Bwana Lyatonga Mrema..Kampeni Zikapamba Moto...

Timu ya Mrema ikapita kuomba Kura Uwanja wa Mashujaa Moshi ukajaa na kutapika..mimi nimo mbele kabisa Huku Mrema,Pale Makongoro Nyerere..

Wakatuelekeza kwa unyenyekevu kabisa Kwamba Wiki Ijayo Baba wa Taifa Na Mgombea wake Bwana Mkapa watakuja kwahiyo Fanyeni Hivi Na Hivi..Hao wakaondoka zao wakaenda Arusha.

Baada Ya wiki Kweli Mzee wetu Baba wa Taifa akaingia Moshi,Niliwahi Uwanjani Tokea saa Tano, Kumbe Hakuja Na Mzee Mkapa Bwana, Akaanza Hotuba na vile vichekesho vyake

Mwisho Akainua Picha ya Mkapa Nakumbuka ile picha ni ya kuchora akasema Nawaomba Mumpe kura huyu kwa Maendeleo ya nchi Yetu...

Uwanja Wote wa Mashujaa Ukanyamaza kimya Kabisa,kimya halafu wakainua vidole viwili ile Alama inayotumiwa na CHADEMA uwanja wote ukawa unapunga huku watu wamenyamaza kimya kabisa..

Mwalimu Akiwa amefura kwa hasira,akatamka nikiwa namuona na kumsikia ..MTAKE,MSITAKE HUYU ATAKUA RAIS halafu akatupa ile picha chini...akaitupa kabisa halafu akashuka jukwaani Akaenda zake mkutano ukafia hapo..

Ilasikuwahi kumuona Tena Live Mwalimu Hadi Alipokufa nikiwa Form Four mwaka 1999...ila nilikua namfatilia sana hotuba zake

Tutamsema Vibaya Lakini Hakuna wa Kuvaa Viatu Vyake na Hatatokea Alikua Baba,kiongozi,mkombozi,mwalimu,mwanafalsafa,mpenda kusali,na mengine mengi.....Namkumbuka na Atakumbukwa na Taifa Hili kwa Miaka Yote Hadi Ukamilifu wa Dahari...Siku Mwenye Mali Yake Atakapopenda na kusema Mwisho ndio Huu..

MP...JF LEGEND
.
Umeelezea vizuri sana. Na mimi nilikuwepo. Bado nakumbuka watu walivyomzomea aliposema wampe Mkapa kura. Na ni kweli alikasirika na kutamka hivyo. Na huyo ukawa ndiyo mwisho wa mkutano. Mji mzima wa Moshi ukajaa watu wakinyoosha vidole viwili juu. Bendera za CCM zikatupwa kwenye mitaro na mashabiki wake wakazomea japo walikuwa wachache sana.
 
Unamjua Mwalimu vizuri?
Hii habari haiendani na aiba ya Mwalimu

Akafura, na Akatupa Picha Chini...,
Moja akatupa picha chini ili iweje ?,

Mbili haikuwa ajabu watu kutoka uwanjani wala kukataa na kumpinga Mwalimu kuhusu Mkapa; watu hawakumjua Mkapa, watu walimkubali Mrema na kila kiwanja alichoenda Mwalimu watu walikuwa wanapinga..., Sasa kwa kufura ghafla na kushangaa ingekuwa ni mtu aliyeshangazwa na kilichotokea wakati nina uhakika alikitegemea kilichotokea...., ila hakukata tamaa aliendelea kutembea nchi nzima na kupata upinzani mkubwa... (Mkapa alikuwa habebeki)
 
I'm very sorry, I seriously doubt the authenticity of this story.
P
Pascal ni kweli kabisa. Hata mimi nilikuwepo. Mwalimu alizomewa sana na watu wakaanyoosha vidole viwili juu. Mwisho akasema ''msitake msitake. huyu ndiyo atakuwa rais''. Watu wakazidi kuzomea. Jamaa kaelezea kwa ufasaha mno mno. Hakuongeza wala kupunguza chochote. Jaribu kuwauliza watu waliokuwepo kwenye msafara wa mwalim watakuambia ni kweli.
 
Kwa nini alifuta mfumo wa vyama vingi kama alikuwa muumini wa nguvu ya hoja?
Huo no uongo mkubwa, Nyerere siku zote alikuwa muumini wa nguvu ya hoja na sio hoja ya nguvu. Kipindi Cha kampeni za urais mwaka 95 Mrema alisumbuliwa Sana na vyombo vya dola huku watu wakitaka kumbeba aliyekuja kusimamisha usumbufu huo alikuwa me. Nyerere aliyewakanya na kuwaambia hata maiti inabebwa na tamko hili alilitoa Iringa.
Labda umechanganya na kauli ya mgombea mwenza wa ccm aliyesema mpige kura msipiga ccm itashinda.
 
Hata mimi aise...NCCR mageuzi na alama ya CHADEMA wapi na wapi?
By then CHADEMA ya akina Kasanga Tumbo na ofisi yao pale Magomeni, haikuwa hata mashuhuri...
Unadhani alama ya vidole viwili ni ya Chadema? Hii imeanza kutumika tangu enzi za NCCR Mageuzi.
 
QUOTE="Pascal Mayalla, post: 40497056, member: 17813"]
I'm very sorry, I seriously doubt the authenticity of this story.
P
[/QUOTE]
I also doubt his/her story...Nadhani Kuna kutia chumvi hapo..Hilo la kutupa picha chini na kabla ya hapo uwanja kuwa kimya ni uongo
 
Uchaguzi huo!ndio ulienda na maisha ya IMRAN KOMBE!!!!MAANA NCHI ILIKUA INAENDA UPINZANI NA KOMBE ALIUNGA MKONO VUGU VUGU LILE!!!!RIP KOMBE!!CCM HAIJAANZA LEO!!!
Kuua watu. Eti walimfananisha na jambazi sugu la magari. CCM imekunywa damu nyingi sana.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom