upendodaima
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 4,086
- 4,527
Ile uliyowahi kuiona kabla hii haikua official video ile walitengeneza tu na kuunga vipande vya matukio ya nyimbo za watu wengine...angalia vizuri yale matukio ni ya nyimbo za wasanii wengine tofauti tofauti
tusubirie Na Video Ya Ay Ft Seankingstone Itakuaje
Wabongo tunashida sana.. assume wimbo huohuo ingetumika kizulu naamini wabongo wangeipenda hii video.
Tatizo mnajitengezea video zenu kichwani lakini yeye hajelenga soko la ndani tu yupo internationally..
Safi sana...Hiyo ndo inaitwa kazi ya sanaa...Hapa watu walikuwa na mavideo yao kichwani ya maigizo....Jamaa amewacha waswahili wanashangaa....wanataka kuona maigizo eti binti katoka kijijini....
Big up Kiba....Video bombaaaa sans
Ha ha ha haaaa. Sasa unadhan mashabiki wangapi wanayajua haya? Unaongea nn ww? He should deliver what we want na sio kutuletea huu ulimbukeni wa kujifanya unajua aina video... Kazingua. Video ya kawaida... Soon itapotea na kusaulika.
Yaani kwa akili zao walitegemea kisa cha Mwana kingetosha kwenye video ya dakika nne? Kuna kilaza mmoja hapa eti alishauri ingekuwa anakutana na mateja njiani wakati anatembea, hajui kwamba tukio hilo lingeleta maana nyingine kabisa katika video.
Kwani wimbo wa Kipi Sijasikia umemalizwaje na video? Ni kwa kulazimisha maigizo kwenye video na ndio maana wakarudi studio kuongeza baadhi ya vitu kwenye audio, lakini hata hivyo bado haikuendana.
Ova
Ila tambua mimi nilichokifanya ni benchmarking, sasa sijui ulitaka nimlinganishe na msanii gani hapa bongo?
Hussein machozi labda, Baba Levo...kidoogo Ommy Dimpoz
Diamond sio level yake...yani ni ile hakunagaaaa.....
Lakini upande wa videos lazima tukubali kuwa ame-improve. Hii ndo video yake bora kabisa na imezifunika baadhi ya video za Diamond. Kwa mtazamo wangu, video pekee ya Diamond ambayo naweza sema ina ubora na creativity nzuri ni number one remix.
Kuna Dogo alifanya video ya "Kabla hajatoka Dayamondi" anaitwa Dogo S Kide kamfunika Kiba, unaimba Mwana DSM unashindwa kuonesha mitaa ya DSM, unashindwa kumwonyesha mtu yuko kwenye mishe mishe za Kimwana DSM, unashindwa kumwonesha alivyokuja kutaabika.
Inabidi Salam Jabir arudishe kipindi chake cha kuchambua video za wasanii wetu kama enzi zile za Planet Bongo!
SijAwahi ona video mbovu kama hii.
Picha haiendani na stori nadhani anayeongelewa angeigiza hapo: i.e wazazi wakimlilia, kaanza kulewa, mademu, madawa. ....yule jamaa wa kibajaji angenogesha sana hii video
Safi sana...Hiyo ndo inaitwa kazi ya sanaa...Hapa watu walikuwa na mavideo yao kichwani ya maigizo....Jamaa amewacha waswahili wanashangaa....wanataka kuona maigizo eti binti katoka kijijini....
Big up Kiba....Video bombaaaa sans
Kwa ambaye hajui kiswahili akiiangalia hii video, hatoweza ku-guess Kiba anaimba nini.