Ali Kiba Fans' Special Thread...


Nianze kwa kumuomba Mungu haya maelezo nitakayokupa yasisababishe tukakwazana katika wakati huu wa saumu, coz saumu ni muhimu kuliko yote haya.
Kwa kuwa maelezo yako ni kama yameonesha kuwa unahitaji msaada wa uelewa toka kwetu, basi itakuwa ni aibu kubwa kwa Family kukuacha uondoke bila kukusaidia.
Umeonesha una tatizo la uelewa wa Sanaa ya video za muziki na ina kazi gani kwa jamii. Na pengine maoni yako yamefuata mkumbo au kusukumwa na chuki binafsi.
Na bado umeonesha kutokuwa na ufahamu kuhusu fashion.

Twende Sasa.
Kisa cha video ya Chekecha Cheketua kinaeleza kuwa Kiba ni mgeni kabisa katika mji ule, ndio maana ulioneshwa akiwasili huku akiwa amevunja amri ya ukimya kwa kusikiliza muziki wa Mwana.
Kwanini alivaa suit? Katika kisa cha video hii Kiba ni mgeni mwenye hadhi (daraja) ya juu na ndio maana ulioneshwa alikuwa ameketi kwenye kiti cha nyuma huku akiendeshwa, hivyo muongozaji akamuamuru kuvaa suit ili kuikamilisha hadhi yake.
Unaweza kuona kwa Rais wako hukaa kiti kipi anapokuwa kwenye gari na huvalia vazi gani hata anapokwenda kwenye nchi ya King Mswati ambako wana sheria kale kwamba mabinti bikira wa nchi nzima ni wachumba wa mfalme.
Hivyo Kiba alikuwa huru kwa mavazi bila kuathiri fasihi na kuendelea kuuvaa uhusika wake.

Kuhusu Fashion
Kwa kifupi suit sio vazi la kisasa, coz limeanza kuvaliwa tangu mwishoni mwa karne ya kumi na nane, hivyo mwanzoni tu mwa karne ya kumi na tisa vazi hilo likaanza kusambaa katika nchi tofauti.
Historia inasema vazi hili lilianzia UK, lakini kuna utata kidogo kutokana na jina lake kutoholewa katika lugha ya Kifaransa (suite - following).
Hata blue jeans sio vazi la kisasa kabisa, kwani lilianza tangu kwenye miaka ya 1800 huko na ndio maana Levi's ina miaka 162 tangu kuanzishwa kwake, Lee ina miaka 126 tangu kuanzishwa kwake.
Na kuhusu hizo kofia za mzunguko ndio kitu cha kale zaidi kwani kilianza kuvaliwa kabla ya kuzaliwa Kristo, ila zikaboreshwa zaidi kwenye karne ya 18 na 19.

Hasidi hana sababu!
Ajabu, watu walewale waliokuwa wanaponda video ya Mwana, leo wanasema ni nzuri. Walewale walioponda audio ya Chekecha, leo wanasema audio ila video mbaya.
Jaribuni kuwa na kumbukumbu basi, na hata unapokosoa kitu uje na hoja za kiufundi ili usijichanganye na maoni yako uliyotoa siku za nyuma, vinginevyo utakuwa na chuki binafsi tu.
Sasa kwa sisi mashabiki wa muziki mzuri tutabaki kujiuliza huyu naye kakosewa nini na Kiba? Maana Nassib tunajua anamchukia Kiba kwa sababu alimgongea dada ake (Queen Darleen) then akamtosa. Sasa ninyi wengine kuna kisa gani?
Ova
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaaa!! Mdakuzi bwana hapo tu ndipo ninapokupendea, ila sasa hivi vichwa vya nazi ni taabu kweli kudeal navyo, yaani wao ni mihemko tuuuuuu, Kiba endelea kunichekechea hawa mburula mpaka waelewe.
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaaa!! Mdakuzi bwana hapo tu ndipo ninapokupendea, ila sasa hivi vichwa vya nazi ni taabu kweli kudeal navyo, yaani wao ni mihemko tuuuuuu, Kiba endelea kunichekechea hawa mburula mpaka waelewe.

umesema vichwa nazi hahahahaha umetisha
 
Last edited by a moderator:

Napigia mstari para yako ya mwisho.
 

mi nimegundua kitu kia washabiki wa daimond ni watu wenye roho mbaya,wanafki na waswahili mnooo

hizo video wanazosifia za daimond zina uzuri gani vile mtu anakimbia kimbia km kaachwa na treni

team mondi wako hivi wanapenda wasifie wao tu hata km vibovu
na lengo wanaiponda ili isiangaliwe na ipate viewers wachache u tube

siku zote wapo kifitna zaidi ndo maana siwafagilii siku hizi nshawajua ni wanafki na wakaanga sumu
 
umesema vichwa nazi hahahahaha umetisha

Havielewi mpaka uviponde na chuma, Mdakuzi aliviponda wakasema notes(brn taabu kweli), Matola akaongezea nyundo walaaaa wanatoa majicho tu, haya shemdarling kapigilia tena zaidi ila sijui hizi ni nazi za wapi!!! Subiri uone watakavyokuja kujihemesha hapa!
 
Last edited by a moderator:

yaani mi nashindwa hata kuwaelewa hawa watu
 

asanteeeee.....!!!nashukuru sana sana sana....!!
 

Hahahaaaaaa my ribs, eti km mtu kaachwa na treni, na ule mtambaara mfukoni km teja sijui ndio nn, hawayaoni hayo kazi kuhorojoka tu na king wetu, ovyooooooo!!
 

hao jamaa wawili uliowataja wameshusha point sana. ila kuna watu wanajifanya vichwa nazi sana
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaaa my ribs, eti km mtu kaachwa na treni, na ule mtambaara mfukoni km teja sijui ndio nn, hawayaoni hayo kazi kuhorojoka tu na king wetu, ovyooooooo!!

unafkri yaani mbona video iko poa sana
hizo wanazosifu mi naonaga uchafu kiukweli sizielewagi hata kidogo ila lengo lao ni kudiscourage hadhira ili isipendwe
si watu wazuri timi daimond hata kidogoo
 
unafkri yaani mbona video iko poa sana
hizo wanazosifu mi naonaga uchafu kiukweli sizielewagi hata kidogo ila lengo lao ni kudiscourage hadhira ili isipendwe
si watu wazuri timi daimond hata kidogoo

Na hakuna kitu kinawauma kama kuona King kumbe ana fans wenye mapenzi ya dhati naye basi ndio wanatamani wajitundike, mie kuna mmoja aliwahi kunipm akiniuliza je nina undugu wowote na Kiba? Hata sikumjibu shwain yule, na hawatoweza kuondoa atention yetu kwa king maana we r here to stay.
 
Hahahaaaaaa my ribs, eti km mtu kaachwa na treni, na ule mtambaara mfukoni km teja sijui ndio nn, hawayaoni hayo kazi kuhorojoka tu na king wetu, ovyooooooo!!

Na ile style ya kurusha vibega kama kuku mwenye mdondo!
Style zake za kucheza very familiar...video zake very presictable.
Jamaniii mniwacheeee acheni niwe wa tofautiii
 
Na ile style ya kurusha vibega kama kuku mwenye mdondo!
Style zake za kucheza very familiar...video zake very presictable.
Jamaniii mniwacheeee acheni niwe wa tofautiii

Washazoea km ilivyo kwa show zake inavyojulikana ataingia hivi na atamaliza hivi basi hata na video zake ni hivyo hivyo, unajua tu atarusha tu vibega km mtu mwenye pepo, atarusha miguu, atakimbia kimbia, baasi, sasa King ni unpredictable anakuja na vitu vilivyokwenda shule yaani mpaka uwe unaijua fasihi ndio uielewe, sanaa ni "ufundi" sasa km unachezea tu sanaa na kufanya vitu vyepeeeesi wewe tukuiteje labda,

Kiba ni brand ati, kipaji kisichotakiwa kuchezewa hata kwa bahati mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…