Mkuu, hakuna wimbo uliotoka vizuri kabisa halafu ukaombwa ukafanyie remix kesho yake tu baada ya kuachiwa. DJ Maphorisa anataka akarekebishe audio kwa sababu mixing imefanywa vibaya, sauti ya Nassib haisikiki vizuri kama ilivyo sauti ya Flavour.
Sio kila kitu kiwe kwa ajili ya kufanyia ubishi, sio kila maoni yanayotolewa kwake huwa yenye lengo baya. Mikasi ya kwanza ya Ngwair (RIP) ilifanywa mixing vibaya la Ludigo, kisha Majani akairudia kesho yake na kuitoa Mikasi Remix ambayo ikabamba.
Kasikilize sauti ya Nassib kwenye Number One, kisha kasikilize kwenye Nana, Bum Bum na ule wimbo alioimba na Waje ndio utaelewa vizuri ninachojaribu kueleza hapa.
Tatizo wengi wanaamini kukosoa ni chuki dhidi ya anayekosolewa, huku ni kumjenga jamani, ndio kama tunavyomwambia akamuuguze baba yake.
Kwa sababu sitaki kurudia rudia jambo moja, naomba ukanisome vizuri kwenye uzi unaozungumzia hili suala la kuombwa kufanyia remix huo wimbo uliotoka jana tu.
Ova