Ali Kiba Fans' Special Thread...

Usijizuie kuchukua upande,fuata kitu roho inapenda,as for us,tumejizuiaaaa weeee ila tumeshindwaaa!!
mi napenda muziki na nikisema muziki namaanisha muziki kwahiyo yeyote anayefanya vizuri nitampenda na kumuunga mkono. nikisema muziki hapo manake ni kwamba napenda aina yoyote ile ya muziki, nazani utashangaa nikikuambia hata classical naupenda ile mbaya. sister angu huwa ananitania kwamba inawezekana nilitaka kuzaliwa ulaya lakini kwa bahati mbaya mungu akakosea akanipa ngozi nyeusi kwahiyo ikambidi anidondoshe tu huku huku afrika. sababu ya kusema hivyo ni kwamba eti mwafrika na classical music wapi na wapi. mzima lakini @Ms. Lincoln
 
Hivi mashabiki wa diamond si wana thread yao mbona anakuja hadi huku? hawa ndo walifanya id yangu ifungiwe milele

Ni ID gani hiyo?Hebu iseme bwana isijekua ni member tukiyekuzoea humu sasa nakuona mgeni....
Hao mashabiki ni pasua kichwa wenzio tumeshawazoea
 

Mdomo mkubwa shogaa...haufungi vizuri!
Oh dear God utanisamehe!
 

Rudia kunisoma ili uone hoja yangu. Hakuna dissing kwenye tukio la P Square na Nassib. Ila kuna ushauri wa kuzingatia utambulisho wa muziki wako. Haukuwa ushauri unaomfaa Nassib peke yake, unamfaa kila mwanamuziki wa Tanzania anayefanya Naija's music style.
Kulikuwa na maana kwamba, unaweza kuimba muziki wa kwenu na hata sisi Nigeria tukapenda kama ulivyofanya katika hizi mbili. Ni ujumbe wamepeleka, na imekuwa hivi kwa sababu P Square sio wageni Tanzania wanajua wanamuziki hapa na wanaujua vizuri muziki wa hapa.
Katika hoja yangu hapa sikusema Nassib ni mwanamuziki mbaya, is a good singer but he isn't as good as Ali Kiba na wote hapa wanajua kwamba kauli yangu kwa sasa iko hivyo. Ni vizuri kuwa unasoma hoja na kuelewa ili usihame au kubadili maana ya hoja wakati wa kuchangia.
Ova
 
Usijizuie kuchukua upande,fuata kitu roho inapenda,as for us,tumejizuiaaaa weeee ila tumeshindwaaa!!

Haha haaaa,shida ya nini?eti nawapenda wote!Diamond na Kiba ni kama simba na yanga....huwezi kuwapenda wote at the same time.
Ila ameshasema kua anampa credit Kiba kuliko Diamond.....
Hujamuelewa tu?
 
Ni ID gani hiyo?Hebu iseme bwana isijekua ni member tukiyekuzoea humu sasa nakuona mgeni....
Hao mashabiki ni pasua kichwa wenzio tumeshawazoea
hunitakii mema kwa mod, au? tena inabidi ni-delete hiyo post wasije wakagundua nimekuja kivingine. kuhusu kunizoea, sio kivile manake huku nilikuwa nakujaga kuchunguliaga tu. mi ni mfuasi wa jukwaa la jokes, science & gadgets, chit chat na kwa kiasi fulani siasa.
 
then kashawahi kufanya ngoma nyingine yenye dizain za kinaigeria?
Unamaanisha nini? Ukishafanya umefanya mkuu, hata kama ulifanya nusu. Wakristo wanasema ukitamani tu kuzini ni tayari umeshazini, sasa unataka idadi toka kwangu mkuu? Kwa hiyo hata wao wanajua ameshafanya na ndio maana kupitia hilo wamekumbusha kubaki kwenye Bongo Flava.
Na hilo ni kwa kila mwanamuziki wa Bongo anayefanya Naija's music style au hata Kwaito music style, kwa sababu wao zina maana zao, na ndio maana hata hapa kwetu huwa nawaona wasanii wa Bongo wanadance kwa style za msibani za Kwaito, lakini hawajui kwa sababu wameiga tu.
Ova
 
ni bahati mbaya sana nimetoa hoja hiyo kwenye post yako lakini ndivyo watu walivyoelewa. kuhusu ushauri wa P-Square, namuunga mkono kwa 100% manake binafsi niliposikia nyimbo ya nemo na dimpoz walikera kwa 1000% manake ile nyimbo kuanzia beat, melody hata uchezaji ni naija style. walinikera kiasi kwamba hata nikiona ile nyimbo kama ni kwenye tv, nabadilisha channel.binafsi pamoja na kwamba napenda bongo flavor napenda zaidi ukiwa na vionjo vya asili kama ile nyimbo ya vanessa na ile ya Lina. i love those songs hadi basi
 

Ooh,ok then...nilidhani ni mwenzetu hapa Kiba fans
 

Have a good day mr.
 
mwenzenu kwenye muziki mzuri. tena umenikumbusha, ngoja niende youtube kuangalia video ya mwana manake nimeicheki zaman sana. naenda kukumbushia

Hahahahaaaa,haya nenda ukaicheki mimi ni kama dose ya kutwa mara 3!
 
Uwiiiiii,kwa hiyo zile kwaito tunazodance hata maharusini ni za misibani?
Kuna Kwaito dance ya harusini na msibani. Ile namna ya kupiga miguu na kuteleza. Wenyewe hudance kwa message ya wimbo, kama wa furaha au huzuni. Lakini mara nyingi wasanii wa Bongo huzicheza zote mbili katika wimbo wa furaha au kucheza ya huzuni kwenye wimbo wa furaha.
Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…