Alfred Ngotezi hatunaye tena

Mwenyezi Mungu Mwenye Rehma Nyingi Amuweke pahari panapomstahili.. Marehemu Atabeba Mzigo wake Mwenyewe.
 
poleni sana familia ya ya Ngotezi
just imagine unajua baba kasafiri kikazi atarudi ghafla unaambiwa katangulia bila hata kuaga.
 
OMG... one of free minds pale Daily News.. nimemsoma hivi majuzi tu (just few days ago) RIP Ngotezi. After Lusekelo, nilikuwa napenda kumsoma huyu bwana..
Mkuuu............imenigusa sana katika namna hiyo hiyo mkuu!!!

Duh!!.........mbaya sana.
 
Jamani kama kuna mtu anapaelewa kwake marehemu hapa dar anijulishe nikatoe rambirambi zangu maana nasikia mwili wake unaletwa hapa leo kuagwa rasmi,kabla haujapelekwa Sengerema kwa mazishi.
 
Inasadikiwa kuwa mwandishi mkongwe nchini, Alfred Ngotezi ambaye alifariki usiku wa Jumamosi iliyopita katika hoteli moja maeneo ya Mianzini Arusha, alipewa sumu.

Hivi sasa maofisa wa NSSF ambako Ngotezi alikuwa akifanya kazi kama meneja uhusiano wanahangaka kufanya postmoterm au autopsy kubaini chanzo cha mauti yake ya ghafla.

"Alikuwa mzima kama chuma cha pua, alisafiri mwenyewe kutoka dar hadi arusha kwa ajili ya mkutano wa kimataifa wa hifadhi za jamii (ISSA) na kabla hajaanguka na kupoteza uhai alikuwa anapata chakula cha jioni na wafanyakazi wenzake kisha akainuka kwenda kucheza muziki na alipokuwa narudi kuketi akapiga chini!" alisema mmoja wa wafanyakazi wa NSSF.

Wengi wanasema ni sumu lakini kama mhusika ni moja ya wale waliokuwepo si ajabu ukweli ukafichwa ili kusevu jina la NSSF
Huyu marehemu alishafanya kazi kwenye maeneo ya AICC, alikuwa na political mentality alikwenda kugombea ubunge kwao kama Biharamulo au Ngara nimesahau. R.I.P. Alfred Ngotezi.

 
Huyu marehemu alishafanya kazi kwenye maeneo ya AICC, alikuwa na political mentality alikwenda kugombea ubunge kwao kama Biharamulo au Ngara nimesahau. R.I.P. Alfred Ngotezi.

Aligombea jimbo la BUCHOSA,alikuwa ni mtu rahisi kuzoeleka.Tulikutana mara ya kwanza AICC hospital mwaka 2005 kwenye foleni ya kumwona dr tulizoeana palepale.RIP bro
 
Nimepata taarifa za kifo chake kwa mshtuko mkubwa kwani alikuwa mtu muhimu kwa siasa za sengerema na mwanza kwa ujumla alipenda kuwa mwakilishi wetu lakini kura hazikutosha pumzika kwa AMANI A,D NGOTEZI
 
Acha kupandikiza mawazo ya chuki na uongo. Postmoterm imeonyesha alifariki kwa hypertension. Mimi ni rafiki yake wa karibu nilikuwa nae siku anafariki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom