Alfred Ngotezi hatunaye tena

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
833
ngo1.jpg

Kama kuna mtu alikuwa anamsoma kwenye gazeti la Daily News atakuwa anamjua.

Nilikuwa nafahamiana naye kama uncle wangu na to be honest I'm still in shock

The same week tuliyompoteza David Wakati na Mwenyezi Mungu kaamua kumchukua mja wake Uncle Ngotezi ambaye ametutangulia mbele ya haki.

Inna lillahi wa inna ilaahi Rajuun
 
R.I.P Ngotezi, nitakumiss Daily news, Makongoro, Makwaia, Lymo..... hold it down!
Damn!!
 
Inasadikiwa kuwa mwandishi mkongwe nchini, Alfred Ngotezi ambaye alifariki usiku wa Jumamosi iliyopita katika hoteli moja maeneo ya Mianzini Arusha, alipewa sumu.

Hivi sasa maofisa wa NSSF ambako Ngotezi alikuwa akifanya kazi kama meneja uhusiano wanahangaka kufanya postmoterm au autopsy kubaini chanzo cha mauti yake ya ghafla.

"Alikuwa mzima kama chuma cha pua, alisafiri mwenyewe kutoka dar hadi arusha kwa ajili ya mkutano wa kimataifa wa hifadhi za jamii (ISSA) na kabla hajaanguka na kupoteza uhai alikuwa anapata chakula cha jioni na wafanyakazi wenzake kisha akainuka kwenda kucheza muziki na alipokuwa narudi kuketi akapiga chini!" alisema mmoja wa wafanyakazi wa NSSF.

Wengi wanasema ni sumu lakini kama mhusika ni moja ya wale waliokuwepo si ajabu ukweli ukafichwa ili kusevu jina la NSSF
 
Nimepokea taarifa za kifo cha Alfred Ngotezi au BABA MUGISA kwa masikitiko makubwa, lakini sisi tulimpenda lakini mwenyezi mungu amempenda zaidi na amemchukua kwa pumziko la milele- amina
 
10_09_hpvxa1.jpg
Breaking news:

Afisa uhusiano mwanadamizi wa shirika la taifa la hifadhi ya jamii amefariki ghafla huko Arusha alikokuwa kikazi kwa maandalizi ya mkutano wa mashirika ya Afrika ya hifadhi ya jamii utakaoanza kesho. Aliwahi kuwa mwandishi mwandamizi wa gazeti la serikali la Daily News.

Taarifa zinasema alikuwa meza ya chakula, alinyanyuka kwenda kujisaidia, mara akaanguka ghafla na na mauti kumchukua na kuanza safari rasmi ya kwenda kumwona baba wa milele.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom