Albamu bora ya Kanisa Katoliki

Albamu bora ya Kanisa Katoliki

Wadau polen na Majukumu ya hapa na Pale..Naomba mtu Mwenye Church instrumentals kama za kina Poul Mwarabu.Severin Lwila n.k ani wekee apa au Aniambie nimpe Jins ya kunitumia nna Shida nazo sana Pleae
 
St.Peters Oysterbay inapatikana kwa Mamu, Kariakoo

Heshima yako Mkuu LIKUD,tumsifu Yesu Kristo,mimi nina shida sana ya Nyimbo moja inaitwa ''Mimi sio Mkamilifu'' moja ya tunzi bora na za mwisho kabisa za Mwl. Victor Murishiwa. Na pengine kama nitapata Collection za Victor Murishiwa,Mzee John Mgandu na Paschal Mwarabu nitafurahi sana.
 
Hongereni sana wadau mimi ni mwanakwaya nimeimba na kwaya nyingi. Za hivi karibuni. Kuna wimbo mmoja umeimbwa na kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Singida unaitwa URITHI. Nautafuta sana mwenye nao anirushie au kama anaweza nisaidia kupata album nzima ya video. Nyimbo nyingine ni pamoja na NAOGOPA KUTEMBEA KWENYE MAJI. Nipo tayari kununua album ikipatikana.
 
Mkuu samahani kidogo, hiyo album inaitwa KARIBU TANZANIA BABA MTAKATIFU YOHANE PAULO II imeimbwa mwaka 1992 na kwaya ya SHIKWAKWA Dar es salaam nyimbo zingine ni pamoja na
WEWE NDIWE PETRO
KRISTU MSHINDA
BWANA MFALME
WATEULE WA BWANA
ROHO YANGU
N.K
Mkuu ni mwaka 1990 sio 1992
 
Hakika ben mukasa amejaaliwa kipaji kikubwa. Sana binafsi nikione cd inauzwa iwe ya kwaya yeyote yenye wimbo wa mukasa nanunua. Na hata kwenye simu yangu nmedownload nyimbo zake baadhi
Wewe ni MUNGU kila wakati hata mimi wanigusa mno
 
Aisee nyimbo katoliki za zamani zilikuwa bomba mbaya mkuu,kuna wimbo unaitwa nalikuwa nimelala,aagghh ni balaaa,unaamsha ari ya kumpenda kristo,ingekuwa kule kwa wapenda sifa na kujikweza tungesema una upako
Hahahahahaha
 
Yan Mukasa ana kipaji cha ajabu.. kuna huu wimbo mpya sijui kama wameshaurekodi unaitwa WEWE NI MUNGU KILA WAKATI. Yan nautafuta kweli yan..
Tayari upo! It's good! Japo mimi ni mpenzi wa audio, hasa sauti nzuri ya kinanda.
Je kuna channel maalumu, hasa inayomikiwa na kwaya, kwa ajili ya nyimbo za RC?
 
Mimi sio Mroma lakini napenda sana nyimbo za RC hasa za zamani, Nikiziangalia mbingu, Bwana unihifandhi, nikupe nini,haleluya haleluya na nyingine nyingi Hasa sa Mt. cesilia wale wanajua sana
 
Mtunzi sio Kalluh mkuu, ni Fr. Malema Mwanampepo.
Mwenye mikono safi na moyo mweupe hata hupanda mlima wa bwana,kirumba Mwanza. Mtunzi marehem Karu,ukiimbwa kanisa zima linaimba.
 
Mt Cecilia (Kwaya kuu toka jimbo kuu katoliki Arusha parokia ya St Theresa) ni kwaya yangu bora ya muda wote. Hawajawahi kuniangusha na ninshukuru hadi leo hawajaingia mkumbo wa kuimba mapambio ya kama kwaya zingine, wamesimama katika style yao ya muda mrefu na wanaiboresha tu.
 
Mt Cecilia (Kwaya kuu toka jimbo kuu katoliki Arusha parokia ya St Theresa) ni kwaya yangu bora ya muda wote. Hawajawahi kuniangusha na ninshukuru hadi leo hawajaingia mkumbo wa kuimba mapambio ya kama kwaya zingine, wamesimama katika style yao ya muda mrefu na wanaiboresha tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom