Simulizi: Mauaji ya Kasisi

bioto

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
1,261
2,095
RIWAYA: MAUAJI YA KASISI
MTUNZI: richard MWAMBE
WHATSAPP: +255 766 974865
UTANGULIZI
MAUAJI YA KASISI
© Richard Richard Mwambe
Ni kizaazaa katika jiji la Nairobi, Kasisi wa kanisa
katoliki anauawa katika lango kuu la kuingilia
kanisani hapo mapema alfajiri. Sajini Maria na
wasaidizi wake wanaingia kazini kuwasaka wauaji.
Nyuma ya pazia la mauaji hayo, jasusi linalotafutwa
na idara mbalimbali za usalama duniani ikiwemo ile
ya Tanzania (TSA), Bill Van Getgand, anahusishwa
na mauaji hayo kwa kuwakodi majambazi ambao
anawalipa pesa nyingi kumuua kasisi huyo na kisha
kuiba monstrance iliyotoka makao makuu ya kanisa
hilo, Vatican, kwa ajili ya adhimisho la jubilee ya
miaka 100 ya Ukristo nchini Kenya.
Idara mbalimbali za usalama duniani ikiwemo ile ya
Tanzania zinatambua uwepo wa jasusi huyo, hivyo
msako unaanza ndani ya jiji la Nairobi na viunga
vyake.
Kamanda Amata anajikuta tena katika sakata hili
gumu ambalo linaihatarisha kazi yake na maisha
yake kwa ujumla. Anarudishwa Tanzania akiwa hoi,
hajitambui. Anapopata fahamu anaamua kumrudia
jasusi huyo ili kumfunza adabu wakati huo akiwa
hatambuliki na idara yake ya usalama.
Bill anatoroka baada ya kuipata ile monstrance na
kuwaua walio jirani nae ili wasije kutoa siri endapo
watajikuta mikononi mwa polisi. Baada ya kazi nzuri
ya Kamanda Amata mpaka kugundua ni wapi jasusi
huyo yupo, idara yake inamrudisha kazini na
kumtuma ama kumkamata au kumuua kabisa jasusi
huyo anayesumbua dunia.
Ndani ya mji wa Aachen, Ujerumani Kamanda Amata
anafanya kazi ngumu akipata vikwazo kutoka shirika
la upelelezi la USA…. Nini kilijiri huko Ujerumani?
Soma riwaya hii tamu MAUAJI YA KASISI na
mwenyewe utasema hakika hii ni riwaya kali kuliko
zote…
*****************************************************
SEHEMU YA KWANZA
1
HOLY FAMILY BASILICA
NAIROBI – saa 01:00 asubuhi
HAKUNA mtu aliyeamini anachokiona mbele yake,
kila aliyepita njia alitikisa kichwa na wengine
kuangusha machozi. Polisi kutoka kituo cha kati cha
Nairobi walikuwa hapo mbele ya kanisa hilo kubwa
wakifanya uchunguzi wa hili na lile. Mwili usio na
uhai ulikuwa umelala chini na majeraha makubwa
kifuani yakiwa yameganda damu nzito. Hakuna
asiyejua mwili ule ni wa nani, kila aliyepita
alisikitika, wengine hata walighairisha safari zao za
kazini, vilio vilitawala eneo lile. Kila mtu alionekana
kuguswa kwa namna moja au nyingine na mauaji ya
Kasisi huyu wa kanisa la Roman Catholic, Rev Fr
Frederick Gichuru, hakuna aliyejua kwa nini na ni
nani aliyetekeleza mauaji haya ya kinyama. Baada
ya kumsachi hakuna cha ziada walichokikuta katika
kanzu ya kasisi huyo zaidi ya rozari iliyokuwa
mkononi mwake.
“Bila shaka alikuwa katika sala zake za asubuhi”
sauti ya kukwaruza kutoka kwa koplo
Otholong’ong’o ilipenya sikioni mwa sajenti Maria
Kariuki ambaye kwa muda huo alikuwa bado
amepigwa na butwaa. Sajenti Maria alisikitika na
kujutia nafsi yake, alijiona kama mwenye makosa
mbele ya Mungu kwa kifo hicho.
“Ndiyo, afande, daima asubuhi kabla ya misa
makasisi wa kikatoliki huwa na wajibu wa kusali
kwanza wao weyewe” Sajenti Maria alimjibu koplo
Otholong’ong’o huku ukungu mzito ukimtoka
kinywani mwake kuashiria baridi kali ya mwezi wa
sita hapo Nairobi. Bado sajenti Maria alikuwa
kajiinamia jirani kabisa na mwili ule akiuangalia kwa
makini jinsi ulivyoharibiwa kwa risasi, maganda
saba ya Colt 45 yalikuwa mkononi mwake, huku
akiyarusharusha alijinyanyua taratibu na kuamuru
mwili ule uondolewe na kupelekwa chumba cha
maiti cha hospitali ya rufaa.
§§§§§
Inspekta Simon Saitoti alimkazia macho sajenti
Maria aliyekuwa ameketi mbele yake akiwa na
jalada moja la khaki lililoandikwa juu ‘MAUAJI YA
KASISI’, alionekana kama mtu ambaye haelewi
anachoelezwa, alilivuta jalada lile na kuliperuzi
kurasa zake chache kwa dakika kadhaa, kisha
akainua macho yake kutazama ukutani ambako
kulipambwa kwa picha ya muasisi wa taifa hilo,
hayati Jomo Kenyatta.
“Umesema paroko wa kanisa hilo hamjamkuta,
sivyo?” Inspekta Saitoti alimtwanga swali sajenti
Maria.
“Ndiyo afande, na tulipowauliza masista walisema
kuwa kawaida wanakuwa na zamu ya kufanya misa
za asubuhi vigangoni, hivyo paroko alikuwa
amekwenda kigangoni” Maria alijibu kwa ukakamavu
wa kipolisi.
“Ok, mauaji kama haya hayajawahi kutokea hapa
kwetu hii ni mara ya kwanza, na naomba sana iwe
mara ya mwisho, endelea kufanya uchunguzi wa
tukio hili kwa kina ukishirikiana na koplo
Otholong’ong’o na mnipe taarifa za kina, ili tuwatie
mbaroni wauaji.”
“Sawa afande” sajenti Maria alisimama na kurudi
nyuma hatua mbili na kupiga saluti ikiwa ni kitendo
cha kuonesha heshima kwa mkubwa wake kadiri ya
nidhamu za kipolisi.
§§§§§
Kijua cha haja kililing’aza jiji kubwa la Nairobi, jiji
lenye pilikapilika za kila aina katika ukanda wa
Afrika ya Mashariki. Watu walionekana wakitembea
na kuvuka barabara kwa haraka haraka kuashiria
kuwa ukichelewa tu matatu itakugonga. Bado hali ya
ubaridi ilikuwa ikiendelea na kila mtu alionekana
kujidhatiti kwa hali hiyo.
Kwenye kituo kimoja cha basi, mwanaume mmoja
mrefu alikua amesimama akisubiri matatu, mara tu
matatu moja ikafika na muziki mkubwa ndani yake,
akaikaribia na kupanda ndani yake, mkononi alikuwa
na mfuko wa plastiki ulioandikwa UCHUMI, bila
shaka alikuwa akitoka supermarket, safari yake kwa
matatu hiyo iliishia katika kitongoji cha Uthiru Kenoo
barabara kuu ya kwenda Uganda. Kwa mwendo wa
wastani alivuka kwa kupitia daraja kubwa na kufika
upande wa pili wa barabara hiyo ambapo kuna
biashara nyingi, aliliendea gari aina ya Hammer
lililokuwa limepaki hapo, ndani yake hakukuonesha
dalili yoyote ya kuwapo mtu, alifungua mlango kwa
kidubwasha maalum na kuuweka ule mfuko katika
kiti cha mbele kisha akatokomea kusikojulikana.
Takribani nusu saa hakuna aliyeisogelea gari ile,
mara akaja mtu mwingine mnene wa haja pamoja
na mwanamke mmoja mrefu na mwenye mwii
ulioumbika vizuri, wakaingia ndani ya gari ile na
kujifungia milango.
“Shit, washakosea tena” alisikika Yule mtu mnene
akimwambia Yule mwanamke
“Nini tena?”
“Hawako makini na kazi yao, tunawalipa pesa nyingi
lakini hawajui nini cha kufanya, nguruwe wakubwa
hawa”
“Kwani nini?” Yule mwanamke alizidi kudadisi
“Ah, we yaache tu, hutakiwi kujua”
“Aaa jamani, yani umelala na mimi umenambia
vingapi mpaka hili usinambie?”
“Mambo ya kazi haya, achana nayo”.
Ile gari ilitiwa moto na kurudi mjini, hakuna ambaye
angekaa bila kulitupia macho gari hilo kwa jinsi
lilivyo na uzuri wa aina yake na gharama yake ndiyo
iliyotia kiwewe.
Moja kwa moja gari ile ilisimama karibu kabisa na
mtaa wa Koinange, mtaa unaosifika kwa
machangudoa hapo Nairobi.
“Nitakucheki usiku twende club” mtu mnene
mwenye asili ya kihindi alimwambia Yule
mwananmke na kumpa noti za shilingi elfu moja
moja tano za Kikenya.
§§§§§
Askofu mkuu wa jimbo kuu la Nairobi, Mhashamu
Gregory Julius Maina, akiwa ofisini kwake alishikwa
na huzuni kubwa kwa habari ya mauaji ya Fr
Gichuru, alimlilia na kumuombea lakini hakujua ni
nini hasa chanzo cha kifo hicho. Alitafakari na
kuumiza kichwa, kisha akainua macho yake na
kutazama jopo lile la makasisi lililokuwa mbele
yake, kila mmoja alikuwa ama akiangusha au
akijifuta machozi, ukumbi wa parokia ya Maria
Consolatha katika eneo la Westland ulikuwa
umetulia kimya kabisa kana kwamba hakukuwa na
watu ndani yake.
“Nawasalimu katika jina la Bwana” Askofu
aliwasalimu makasisi wale wapatao kama mia mbili
weupe kwa weusi.
“Amen” waliitikia.
“Nina masikitiko moyoni, kuwatangazia rasmi kifo
cha kasisi mwenzetu padre Frederick Gichuru,
paroko msaidizi wa parokia ya Familia Takatifu,
kilichotokea leo alfajiri kwa kupigwa risasi tatu
kifuani na kupoteza uhai papo hapo” alifuta machozi
na kukaa kimya kidogo, kisha akaendelea
“Tunalaani vikali kabisa mauaji haya yasiyo na
sababu inayoeleweka, hatuna cha kusema zaidi ila
sisi kama kanisa tunaiomba serikali na vyombo
vyake vya dola vifanye kazi ya kuwatia nguvuni wote
wanaohusika, na tunawaomba raia wema wanaojua
tetesi yoyote ya kifo hiki kutoa taarifa polisi au hata
kwetu ili kusaidia katika kupambana na kadhia hii.
Zaidi ya yote Bwana awasamehe kwa maana
hawajui watendalo. Ibada ya mazishi itafanyika
keshokutwa katika Basilica la Familia Takatifu”
alimaliza Askofu kutoa tamko kwa niaba ya kanisa,
kisha kuwapatia Baraka na wote wakatawanyika.
“Baba, pole kwa msiba” Kasisi mmoja alimsalimu
paroko wa Basilica la Familia Takatifu ambaye
msaidizi wake ndiye aliyeuawa asubuhi hiyo.
“Tumeshapoa, Mungu mwenyewe anajua”
Mara gari ya polisi aina ya Land Cruiser iliingia
katika viwanja vya kanisa hilo la Consolata, sajenti
Maria alikuwa wa kwanza kuteremka, akiwa ndani ya
suruali yake ya buluu na shati la buluu bahari
alipendeza kwelikweli. Alifanya juu chini kumpata
Padre Joe Smith, raia wa Marekani ambaye ni
paroko wa Basilica lililotokea mauaji, alipompata
alimuomba kuongea naye machache na wote
wakaelekea katika ofisi ya parokia hapo Consolatha.
“Pole sana baba kwa msiba, naitwa sajenti Maria
kutoka kituo cha polisi cha kati Nairobi”
“Asante, tumeshapoa” alijibu Fr Joe Smith kwa
Kiswahili chake kinachopendwa na wengi hasa
anapotoa mahubiri.
“Wakati tukio linatokea, wewe ulikuwa wapi asubuhi
hiyo?”
“Mimi nilikuwa nimekwenda kufanya misa ya
asubuhi kigangoni”
“Siku hiyo ni wewe ulitakiwa uende kigangoni?”
“Hapana, kadiri ya ratiba siku hiyo haikuwa zamu
yangu”
“Enhe sasa ilikuwaje ukaenda?”
“Fr Gichuru, usiku wa jana alinambia kuwa yeye
hajisikii vizuri, hivyo angependa kubaki parokiani”
alimjibu sajenti Maria ambaye alionekana kuandika
vitu Fulani kwenye kitabu chake.
“Je unafahamu lolote kama marehemu alikuwa na
ugomvi na mtu, au hali yoyote tofauti iliyokuwa
katika maeneo yenu kama wachungaji?”
“Kwa kweli katika siku hizi, kumekuwa na mambo
ya ajabu kabisa, kuna watu walikuwa wanakuja sana
pale parokiani na kuuliza mambo mengi kwa watoto
watumishi, wakati Fulani tulimkuta mtu anapekua
Sacristia, walipomuuliza akawachapa makofi.”
“Mlichukua hatua gani?”
“Niwaulize ninyi polisi, mimi nilipiga simu polisi na
mkaahidi kuja kufanyia uchunguzi lakini bho!
Sikuwaona”
“Sawa, msaidizi wako alikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mtu yeyote awe sista au mwingine
yeyote?”
Fr Joe alishtuka kidogo kwa swali hilo. Sajenti
Maria akatoa tabasamu lake lisilo nahisia hata
kidogo mbele ya watu.
“Mbona umeshtuka baba?”
“Eh nikikuuliza wewe kama una mahusiano na
kasisi hautashtuka?” wote wakacheka kisha Joe
akaendelea “Hakuna kitu kama hicho, kama kipo
basi mimi sijui”
“Haya, asante sana baba, kama nikikuhitaji
nitakutafuta” wakapeana mikono na kuagana.
Sista Rose alikuwa akibubujikwa na machozi mbele
ya sajenti Maria.
“Usilie Sista, ni maswali machache tu nataka
kukuuliza”
“Sawa afande”
“Wakati mauaji yanatokea wewe ulikuwa wapi?”
“Muda huo mimi nilikuwa natoka nyumbani kwetu
naenda kuandaa misa kanisani…
Ilivyokuwa
…Ilikuwa yapata saa kumi na moja na nusu alfajiri,
sista Rose alikuwa na zamu ya kwenda kuandaa
misa, aliamka na kujiandaa, kisha akiwa ndani ya
mavazi ya kitawa alitoka nje ya nyumba ‘coventi’
yao na kwa mwendo wa taribu na rozari yake
mkononi alikatisha kauwanja kanakotenganisha
nyumba yao na kanisa, mara alisimama ghafla
moyo wake ulifanya paaah! Hakujua kwa nini, kwa
mbali alimuona Fr Gichuru akiingia kwenye uwanja
wa kanisa hilo akiwa kwenye vazi lake jeusi na kofia
nyeusi yenye nyoya katikati, alivaa kikasisi hasa na
si mara nyingi kuonekana katika mavazi haya.
Alikuwa akitembea taratibu na mara walikutana na
sista Rose katikati ya uwanja, wakasalimiana kwa
ishara lakini Fr Gichuru alibaki kasimama
akimwangalia sista Rose, akamuonesha ishara ya
kuwa ainamishe kichwa chake, sista Rose akafanya
hivyo na Fr Gichuru akamuwekea mikono kichwani
kumbariki, mara mwanga wa taa za gari
ukawamulika kutoka getini, hakuna liyejua ni gari ya
nani, Fr Gichuru akamuacha Sr Rose aendelee na
shughuli yake yeye akaliendea geti…
Sista Rose alikuwa kajibanza kwenye ua kubwa lililo
karibu kabisa na mlango wa kuingilia sakristia,
akiangalia kinachoendelea, baada ya mabishano
mafupi kati ya Fr Gichuru na wale jamaa waliokuja
na ile gari mara alishuhudia kasisi yule akianguka
chini kwa kishindo na sauti ya kike iliamuru wengine
kupanda garini na kuondoka kwa kasi. Sista Rose
alibaki akitetemeka huku machozi yakimwagika na
si kumbubujika, alishindwa afanye nini, awaamshe
wenzake au aende kumsaidia Fr Gichuru, alikuwa
njia panda hakujua afanye nini. Gari ile ilipoondoka
alirudi nyumbani kwao akilia na kuwapa taarifa
wenzake ambao wote waliamka na kwenda kuona
tukio hilo kisha kupiga simu polisi na kwa paroko
ambaye alikuwa ameenda kigangoni kwa misa ya
alfajiri…
“Poleni kwa msiba huo mzito” sajenti Maria alitoa
pole akiwa na macho makavu kabisa, “Labda sista
niambie, unaweza kukumbuka aina ya gari
walilokuja nalo?”
“Kwa kweli ni shida kulikumbuka kwa kuwa
kulikuwa na giza na mi nilikuwa mbali kidogo” sista
alijibu.
“Kipi cha pekee unachokumbuka katika tukio hilo?”
“Sauti ya mwanamke iliyokuwa ikimhimiza
mwenzake kumaliza kazi, nilisikia wakitamka jina
‘Black Cheetah’” alimaliza na kutungua kilio.
“Ok waweza kwenda tutakapokuhitaji tutakupa
taarifa.
§§§§§
Black Cheetah, jambazi sugu linalotafutwa na polisi
ukanda wote wa Africa Mashariki, linajikuta katika
sakata jipya, sakata la mauaji ya kasisi. Kila mtu
aliamini kuwa jambazi hilo si bure tu bali linatumia
hata nguvu za giza kwa jinsi linavyoweza
kuwatoroka polisi katika mazingira ya kutatanisha
hata wenyewe kushindwa kujielewa inakuwakuwaje.
Hakuna aliyekuwa halijui jina hili, si mtoto wala mtu
mzima, jina la Black Cheetah halikuisha midomoni
mwao.
Sajenti Maria alishtushwa kusikia jina hilo likitajwa
na sista Rose kuwa aliisikia sauti ya kike ikilitamka
katika tukio hilo. Alitafakari akaona kibarua hicho si
cha kitoto ni kucheza na mtu au watu waliokomaa
kwenye taaluma.
Black Cheetah, kama anavyojiita ni kijana mtukutu,
mkakamavu, muasi aliyetoroka katika kundi lao la
M23 huko mashariki mwa Congo, aliyetokea kuwa
jambazi sugu na tishio katika ukanda wote wa
Afrika ya mashariki, alikuwa akikodiwa na matajiri
wakubwa kutekeleza mauaji au wizi wa kutumia
silaha. Mara kadhaa ameshahusishwa na wizi wa
benki uliotokea Dar es salaam Tanzania miaka
michache iliyopita, mlipuko wa bomu uliotokea
Kampala wakati watu wakiangalia mpira na matukio
mengi yaliyotukia huko Kenya ambayo hata
hatuwezi kuyaainisha hapa, kwa ujumla alikuwa
gaidi.
Mwezi mmoja uliopita
Ngong Hills Hotel-Nairobi
GARI AINA ya Hammer nyeusi ilisogea taratibu
katika maegesho ya hoteli ya Ngong Hills, watu
watatu, wanaume, wakashuka wakiwa ndani ya suti
nyeusi zilizotanguliwa na shati nyeupe, mmoja kati
yao mwenye mwili mnene alikuwa akitembea kwa
msaada wa fimbo maalum, taratibu waliingia
hotelini hapo na moja kwa moja wakaelekea
sehemu ya chakula na kuchukua meza yenye viti
vine na kuketi, kiti kimoja kilibaki wazi wakaagiza
vyakula na vinywaji na kuanza maongezi yao.
Maongezi yaliendelea na baada ya muda kidogo
kijana mmoja aliingia mahali pale akiwa kavalia koti
kubwa la bluu nyeusi akiwa na kofia kubwa aina ya
pama, kwa hatua za maringo aliijongea meza hiyo,
kila mtu alimuangalia kwa mwendo wake hususan
camera za usalama. Alifika katika meza ile na
kuvuta kiti kimoja kilichobaki kikimsubiri yeye,
akaketi na kuiweka bilauri yake vizuri kabla ya
kuimiminia kinywaji kilichokuwa hapo.
“Yes, Cheetah…” yule bwana anaetembea kwa
msaada wa fimbo alimkaribisha
“Nimeitika wito wako, bwana Bill” Cheetah alijibu.
“Vizuri, hawa ni wadau wenzangu ambao sote
tumekuita ili tukupe kazi maalum” aliendelea
“Nawasikiliza”
“Kuna kazi ndogo tunataka utufanyie” alizungumza
bwana Wambugu, akajikohoza na kuendelea
“Tunataka kitu kinachoitwa Monstrance,
kimehifadhiwa katika kanisa kuu la Familia Takatifu
hapa Nairobi, of course ni kazi ndogo tu”
“Hakuna kazi ndogo kama itahitaji kumwaga damu,
hasa damu ya watu wasio na hatia” Cheetah
alimjibu Wambugu
“No! hatumwagi damu, ni kujua ilipo na kuichukua
basi”
“Unafikiri tutaipata kwa urahisi kama unavyofikiria?
Maana ingekuwa hivyo basi hata wewe ungeenda
pale na kuichukua, lakini kama umeniita mimi
maana yake ni kwamba hiyo si kazi ndogo kwa
vyovyote lazima vyuma vitaongea” Cheetah alimaliza
kauli yake na kuinua bilauri iliyojaa kilevi na
kujimiminia kinywani mwake baada ya
kulishuighulikia pande la nyama lililokuwa ndani ya
sahani hiyo.
“Hilo nalo neno bwana Cheetah. By the way wewe
utajua la kufanya, sisi tunachotaka ni Monstrance
basi” alimaliza bwana Wambugu.
“Ok, tusipoteze muda, mimi nitaunda kikosi kazi
kitakachoweza kufanikisha kazi hiyo, lakini mjue
kule ni kanisani, wale makasisi wana mazindiko
yao, hivyo lazima mnipatie fedha iliyotakata”
“Ha ha ha ha ha hilo usitie shaka bwanaaa bwana
Cheetah” cheko la kivivu lilimtoka yule bwana
anyetembea kwa fimbo, kisha akainua simu yake na
kubofya namba kadhaa, punde tu vijana wawili
waliingia pamwe na briefcase ndogo mkononi,
ikawekwa mezani, kwa ishara ya mkono ya mkono
yule bwana alimuomba Wambugu kuifungua, baada
ya kuzungusha vijinamba Fulani mara yenyewe
ilifyatuka kuashiria kuwa kilichopo kiljaa ndani yake
kwa kukandamizwa hasa. Naam manoti yenye sura
za Moi na Kenyatta yalipangwa na kubanwa katika
mabandali kibao, Black Cheetah macho yalimtoka
pima.
“Ukifanikisha kazi basi hata briefcase hii ni mali
yako” yule bwana alizungumza kivivu.
Black Cheetah alitikisa kichwa juu chini juu chini
kuashiria amekubaliana nao. Kwa kuanzia alipewa
mabandali kadhaa katika mfuko wa plastiki.
Waliagana wane hao na Cheetah akaondoka zake
akiwaacha wao wakiendelea kutumbua mavyakula
yaliyojaa mezani hapo.
Katika maegesho ya magari, Cheetah aliisogelea
gari yake na kusimama kidogo kisha akaangalia uku
na huku, hakuona yeyote wala chochote cha
kushuku, akaingia na kukaa nyuma ya usukani,
milango ikafungwa na vyoo vyote vikabaki juu.
Aliufungu ule mfuko wa karatasi na kuhesabu
burungutu zile, si haba takribani laki mbili za Kenya,
alikenua kwa furaha na kulazimisha tabasamu
ambalo halikuendani na uso wake khasilan. Alitia
gia na kuyaacha maegesho, baada ya kulivuka geti
moja kwa moja aliningia barabara ya Ngong na
kurudi katikati ya jiji la Nairobi.
“Hivi unafikiri tutafanikiwa kuipata?”Wambugu
alimwuliza yule bwana anyetembelea fimbo
“Ha ha ha ha Wambugu unanichekesha sana, kazi
iko kwa Cheetah lazima atararua mpaka tuipate, na
tukishaitia mkononi yule Don kule Ujerumani
atatukatisha kwa pesa nyingi, si ya kitoto” aliongea
kwa sauti yake ya kivivu huku mdomoni akitafuna
vyakula aina aina.
“Don!” Wambugu alishangaa
“Yeah, Don, anaitwa Don Fredrick Schurmann, ni
tajiri sana katika mji wa Achen, yeye ndiye
anayetaka hiyo Monstrance, amesema tukiifikisha
mikononi mwake tutapata pesa nyingi sana, ha ha
ha ha !” alimaliza kwa kucheka na kunyanyua bilauri
yake iliyojaa mnvinyo wa Sant Raphael.
§§§§§
Katika bar kubwa ya Dagoreti Corner super pub,
watu walijaa sana wakiburudika kwa vinywaji, nyama
choma huku muziki laini wa The Mushroom
ukisikika kutoka katika spika kubwa zilizozunguka
eneo hilo. Hakuna aliyefikiria kesho kila mmoja
alijiachia kwa starehe zake alizoziona kuwa
zinamfaa, ilimradi siku ilipita katika mtindo huo.
Katika kona moja ya pub hiyo watu watatu waliketi
katika mtindo wa mzunguko mmoja wao alikuwa
mwanamke walionekana kana kwamba wana
mazungumzo mazito sana, hivyo hakuna mtu
ambaye alisogelea eneo lile zaidi ya mhudumu wa
pub hiyo, naye alikuja tu kuleta alichoagizwa na
kuondoka zake.
“Ndiyo vijana, kuna kazi ya kuifanya haraka
iwezekanavyo” Cheetah alianzisha mazungumzo.
“Tunakusikia mkuu” sauti pekee ya kike iliiitikia
kauli hiyo.
“Tunatakiwa kuchukua mzigo pale Holy Family
Basilica”
“Mapesa mangapi tukachukue?” aliuliza kijana
mwingine aliyeketi hapo.
“Siyo pesa Bwana Gichui, kuna kitu kinaitwa
Monstrance, mnakijua?” Cheetah aliwauliza na wote
wakatazamana.
“Monstrance!?” Mellina Wanjiku alishtuka na
kujishika kifua kwa mshangao.
“Unashtuka nini, unaijua?” Cheetah aliuliza, na yeye
alionekana kushtuka kidogo na kuanza kujiuliza
kama kapokea mbuzi kwenye gunia safari hii.
“Naijua Monstrance, ni chombo kitakatifu sana,
kukishika kwa hila inaweza kuwa matatizo kwetu”
Mellina alijibu kwa upole sana, akatulia kidogo
kisha akaendelea “Pamoja na ujambazi ninaoufanya
sikuwa kufikiri kuligeukia kanisa, kuna nini kwenye
Monstrance hiyo?” aliuliza Mellina
“Ah vile vitu vya wakatoliki huwa vinatengenezwa
kwa dhahabu tu, itakuwa ndiyo wanayoitaka” alijibu
Gichui.
Black Cheetah alijikuta kwenye mtihani mgumu,
kama kuna vitu aliviogopa ni miujiza ya Kimungu
ambayo mara nyingi aliisoma kati vitabu vitakatifu,
mtihani mkubwa! Alijiona amefanya ujinga
kutokuuliza nini kilichomo katika monstrance hiyo,
je kama wakizikuta nyingi ni ipi ya kuichukua, utata!
“Cheetah!” aliita Mellina.
Black Cheetah alishtushwa na wito huo kutoka
katika lindi la mawazo, akawatazama wanakikundi
wenzake ambao yeye aliona wangefaa kwa kazi hiyo
lakini sasa walimfanya hata yeye kushikwa na
wasiwasi.
“Ok, tunafanya kazi au hatufanyi tuchague moja”
aliwapa mtego. Baada ya kutafakari mara mbili
mara tatu wote waliamua kuingia kazini kuisaka hiyo
monstrance.
ITAENDELEA HAPAHAPA MPAKA MWISHO... ILA
UKIITAKA YOTE NIFUATE WHATSAPP UKIWA NA
Tsh 3000 MKONONI
ATT
KITABU CHA 'HARUFU YA KIFO' KITAKUWA SOKONI
MEI. KAMA WAKITAKA MAPEMA WEKA ODA KWA
KUNIANDIKIA SMS 0766974865
 
RIWAYA: MAUAJI Y KASISI
MTUNZI: richard MWAMBE
WHATSAPP: +255 766 974865
Black Cheetah alishtushwa na wito huo kutoka
katika lindi la mawazo, akawatazama wanakikundi
wenzake ambao yeye aliona wangefaa kwa kazi hiyo
lakini sasa walimfanya hata yeye kushikwa na
wasiwasi.
“Ok, tunafanya kazi au hatufanyi tuchague moja”
aliwapa mtego. Baada ya kutafakari mara mbili
mara tatu wote waliamua kuingia kazini kuisaka hiyo
monstrance.
SEHEMU YA 2
Miaka kumi nyuma… Al-hamis kuu 1996
KANISA la Holy Family lilisheheni watu mpaka nje
wakifuatilia misa takatifu ya alhamis kuu ambapo
yalifanyika maadhimisho ya karamu ya mwisho.
Hakukuwa hata na njia ya kupita kuelekea popote
kila mtu alipo basi ni hapohapo.
Katika madhabahu makasisi wapatao sita pamoja
na baba Askofu walikuwa wakiendesha misa hiyo
kubwa ambayo mwisho wake huwa inakuwa na
maandamano ya kuhamisha mwili wa Bwana
kuupeleka mahali pengine ili waumini wapate
kuabudu. Watu waliketi kimya kumsikiliza baba
Askofu Njue mara baada ya misa hiyo kuhitimika
“Tuna furaha kuwatangazia kuwa mwaka huu
tumepokea Monstarnce maalum kwa maadhimisho
ya misa maalum. Monstrance hii ambayo ina
historia kubwa katika kanisa ilitengenezwa miaka ya
1878 huko Tanzania katika abasia kubwa ya
Wabenedictin iliyopo Peramiho. Na ilitolewa zawadi
kwa Baba Mtakatifu Leo XIII na kuhifadhiwa pale
Roma. Leo hii imeletwa hapa kwetu kwa ajili ya
maadhimisho ya jubilee ya miaka mia moja ya
Ukristu hapa Kenya. Na itahifadhiwa hapa mpaka
tukio hilo litakapokwisha ndipo tutairudisha Roma”
alimaliza maelezo yake na kujongea madhabahuni,
akainyanyua juu ile Monstrance kubwa iliyokuwa
iking’aa kwa rangi ya dhahabu hasa ilipomulikwa na
taa zilizowekwa kwa umaridadi ndani ya kanisa hilo,
kengele zililia na kisha maandamano kutoka nje ya
kanisa yalifanyika mpaka kwenye kikanisa kingine
kidogo, ikahifadhiwa hapo na kuacha watu
wakipeana zamu za kufanya ibada usiku huo.
1878
Mahali Fulani huko Tanzania
VIBARUA wa wakolono walikuwa wakichimba
mashimo makubwa kuingia chini ya milima
iliyozunguka eneo hilo, huku wakiwa
wamesimamiwa na askari hatari wa kijerumani. Kazi
ilikuwa ngumu lakini walifanya hivyo hivyo, walitoa
mchanga na kuuchekecha kwenye chekeche maalum
na wale wazungu waliondoka na udongo walioutaka
na kuingia nao katika chumba maalumu na
kuuhifadhi.
Katika milima ile baadaye kulijengwa majengo
makubwa na yale mashimo yakawa ndani yake, kila
kukicha wazungu wengi walikuwa wakiingia hapo,
hawa wakisafiri na hawa wakifika ilimradi shughuli
zilikuwa nyingi katika eneo hilo.
Peter Schurmann alikuwa busy kugongagonga
chuma kimoja kilichokuwa katika mtindo wa
samaki, jasho lilimtoka mwili mzima lakini yeye
hakujali aliendelea na kazi yake, na aliporidhika na
kile alichokitengeneza alichukua kitu kama uji mzito
wa moto na kumwagia ndani yake kisha akauacha
upoe kwa muda. Alipokuja kutoa baadae alipata
kituchenye umbo la samaki, akaketi na kuanza
kukifanyia nakshinaksh. Hakika kazi ya mhunzi yule
ilikuwa safi sana chombo kile kilikuwa kiking’aa
sana hasa wakati ambapo kinapigwa na mwanga,
kishapo akatengeneza mkitako safi kikubwa na
kukiunganisha kwa chini ya chombo kile ili kiweze
kusimama chenyewe na kweli ilikuwa hivyo, kisha
wakakihifadhi katika kanati maalumu. Yake
mashimo yaliyopo kule ndani yote yakafukiwa lakini
kilibakishwa chumba kimoja ambacho hicho
haruhusiwi kuingia mtu yeyote mpaka leo hii. Katika
milima iliyozunguka walisimika vitu kama misalaba
mikubwa na kuijengea kwa sementi kali sana
ambayo si rahisi kuivunja kwa zana za kawaida
tulizozizoea. Kile chombo baada ya kukamilika
kilihamishwa na kupelekwa kwao.
Chombo kile kilipelekwa huko Italia na kuhifadhiwa
kati chumba maalum ndani kabisa ya kanisa la
Mtakatifu Petro, Vatican. Chombo hicho
kilichojulikana kwa jina la Monstrance kilitolewa
mara moja tu kwa mwaka na daima kiliwekwa
sehemu maalumu ambayo kila mmoja angeweza
kwenda kuadudu huko.
Wiki chache nyuma
Jomo Kenyatta International Airport
Rev. Fr Frederick Gichuru aliketi katika viti vya
kupumzikia akisubiri muda wake ufike aingie
ndegeni kuelekea Roma kwa kazi maalumu. Watu
walikuwa ni wengi uwanjani hapo na kila mmoja
wao alikuwa na safari yake, hakuna aliyefuatilia
mwenzake anafanya nini au anataka nini.
Tangazo lilisikika kwenye chombo cha kupaaza
sauti kuwataka abiria wanaosafiri kwa ndege ya
shirika la ndege la uswiss kuingia ndegeni tayari
kwa safari. Pembeni ya Fr Gichuru alikaa mtu
mmoja mnene aliyeshiba vizuri, inaonekana ndege
hiyo yeye aliipanda kutokea Dar es salaam au
Kilimanjaro, alimsalimia Fr Gichuru kwa kumpa
mkono wake wa kuume.
§§§§§
Na baada ya ndege hiyo kuwa angani mazungumzo
baina yao yalichukua nafasi. Mtu huyu mnene
alikuwa akielekea Ujerumani kwa shughuli za kikazi
na Fr Gichuru nae alikuwa akielekea Roma kwa
shughuli za kikazi vilevile. Ndege ilipotua katika
uwanja wa kimataifa wa Geneva, ndipo Fr Gichuru
alipogundua kuwa yule mtu mnene mwenye sauti ya
kivivu alikuwa akitembea kwa msaada wa fimbo.
Waliagana na kila mmoja kuchukua njia yake.
Akiwa kwenye gari iliyokuja kumchukua Fr Gichuru
alididimia kwenye kisima kirefu cha mawazo,
alijaribu kuyarudisha maongezi yale aliyokuwa
akiongea na yule mtu mnene kwenye ndege,
ilionekana alikuwa akifahamu vitu vingi labda katika
kuzunguka sna nchi mbalimbali za dunia hii, lakini
alishtushwa kwa jinsi alivyoizungumzia kwa tuo
monstrance ile ambayo Fr Gichuru alikuwa akienda
kuifuata ili kuileta Nairobi, Kenya.
Baada ya itifaki zote za kikanisa kukamilika Fr
Gichuru alikabidhiwa ile monstrance, aliitazama kwa
udadisi na kuigeuzageuza ‘Kile ni chombo cha
thamani sana, hata pale kilipo hakuna aneujua
uthamani wake’, maneno ya yule bwana
yalimrudiarudia kichwani mwake. Aliiweka juu ya
kijimeza kidogo na kufanya ishara ya msalaba kisha
akaitumbukiza kwenye kisanduku maalumu kwa kazi
hiyo tayari kwa safari. Baada ya chakula cha jioni Fr
Gichuru alikuwa katika mazungumzo na makasisi
mbalimbali katika ukumbi maalum, wakibadilishana
mawazo na pia akiwaalika katika adhimisho la
jubilee hiyo.
Fr Gustav Macker, alikuwa akizungukazunguka
katika bustani ndogo iliyo karibu na lango kuu
akiongea na simu bila kuchoka kwa lugha yao ya
kijerumani, alionekana mara kama anatoa melekezo
Fulani, wakati mwingine kama anajibishana na mtu
kwa ukali. Alipomaliza alimuona Fr Gichuru akiwa
tayari ameketi ndani ya gari akimngoja kwa safari ya
uwanja wa ndege.
“Oh Father, nilikuwa naongea na nyumbani kidogo,
tunaweza kwenda?”
“Ndiyo nipo tayari.”
Fr Gustav aliondoa gari na kuelekea uwanja wa
ndege, njia nzima hakuna aliyeongea na mwenzake,
mara kwa mara Fr Gichuru alikuwa akistuka kila
alipokumbuka mzigo alioubeba aliingiwa na giza la
hofu.
“Haya Father , mi nakutakia safari njema na Bwana
akutangulie” Fr Gustav alimuaga Fr Gichuru,
akamkumbati na kumpa mkono kisha yeye
akageuza gari na kurudi alikotoka.
Akiwa ndani ya ndege alikuwa akisoma kitabu chake
cha riwaya ya ‘Msitu wa Solondo’ kilitungwa huko
Tanzania, kilimvutia sana hasa alipojua kuwa kwa
nini wazungu hupenda sana kudadisi mambo,
alikuwa mara ancheka mwenyewe, mara anakunja
uso, mara anajishika moyoni kuonesha mshtuko
basi ilimradi riwaya hiyo ilimkamata vilivyo.
Baada ya takribani masaa nane angani, ndege ya
shirika la ndege la Uswiss ilikanyaga ardhi ya
Nairobi na kujiegesha vyema katika maegesho yake.
Watu walishuka mmoja baada ya mwingine na
mwisho kabisa Fr Gichuru alishuka akiwa na
kijisanduku kile mkononi mwake. Alilakiwa na
paroko wake Fr Joe Smith na kumuongoza kuelekea
kwenye gari aina ya Land Rover 110 Defender mali
ya jimbo kuu la Nairobi. Wakati wanatoka pale
uwanja wa ndege na kushika barabara kubwa ya
kurudi mjini waliipita gari aina ya Hammer iliyokuwa
imeegeshwa na mara tu ile gari iliingia barabarani.
Ikiwa nyuma kama gari ya tatu hivi ilikuwa
aikiifuatilia ile Land Rover 110.
“Karibu sana Fr Gichuru, safari yako imekuwaje?”
“Safari imekuwa nzuri sana, lakini kuna kitu Fr
kinanitia mashaka sana”
“Ooh kitu gani tena Fr?”
Fr Gichuru alimsimulia mazungumzo yote
aliyozungumza na yule mtu mnene kule kwenye
ndege, juu anavyoijua ile monstrance na jinsio
alivyomueleza mara ngapi amewahi kuiona na ni
nchi tofauti tofauti na ameahidi kuja Nairobi katika
adhimisho hilo la jubilee.
“Ananitia mashaka sana, kwa nini kila inapokwenda
na yeye anaenda, ni kipi kinamvutia?” Fr Gichuru
alimuuliza Fr Joe
“Inategemea kabisa, lakini labda anapenda kuiona
inavyopendeza au ni Mkristo kwelikweli anayedumu
sana katika imani”
Walipokaribia katika geti la kanisa ile Hammer
iliwapita kwa kasi na kusimama mbele sana. Fr Joe
aliichukua monstrance ile na kuihifadhi katika
chumba maalumu kilichopo ndani ya nyumba yao.
2
1961
Munichen – Ujerumani
“ULE NI URITHI wa ukoo wetu, babu wa baba yangu
alisema lazima tufanye juu chini tukauchukue
popote utakapokuwepo” mzee wa zaidi ya miaka
themanini alikuwa akiongea na mjukuu wake wakiwa
shambani juu ya trekta aina ya Massey Furgasson.
“Ha, kumbe eee!” Mjukuu wa miaka saba alikuwa
akimsikiliza babu yake kwa makini sana.
“Sasa, wewe mjukuu ndiyo unatakiwa ufanye kazi
hiyo, wewe unaonekana mjanja sana”
“Mimi, ah! Naogopa.”
“Usiogope, muda ukifika utajua la kufanya. Ila
mjukuu wangu wewe unapenda kufanya nini ukiwa
mkubwa?”
“Mimi ningependa kuwa mwanajeshi, nipigane vita.”
“Ha ha ha ha Mjukuu wangu Gustav, vita si jambo
jema. Unajua ni kitu gani nilikuwa nafikiria juu
yako?”
“Hapana niambie babu”
“Wewe uwe Padre, uongoze kanisa, uchunge kondoo
wa Bwana”
“Ha! Nitakuwa nakunywa divai yote” mjukuu alimjibu
babu yake na babu mtu alitungua kicheko kadiri ya
mawazo ya mjukuu wake.
Miaka michache baadae
Munichen – Ujerumani
GUSTAV Macker alimaliza masomo yake na
kujiunga na seminari kuu ya Mt Augustino iliyopo
kati jimbo la Munichen, alikuwa mtii kwa viongozi
wake na hata kupendwa na waalimu na walezi wake
katika seminari yao. Alimaliza miaka mitano ya
falsafa na baada ya kupata stashahada yake
alichaguliwa kwenda mji wa Achen hukohuko
Ujerumani kuendelea kusoma teolojia kwa miaka
mingine mitano, alikuwa ni kijana mpole,
mnyenyekevu na mtii kwa kila jambo, daima kila
alipoonekana al;ikuwa katika hali ya unyenyekevu wa
hali ya juu.
Siku moja alitembelewa na mtu asiyemjua, baada ya
mazungumzo marefu sana walifahamiana kuwa
kumbe wao ni ndugu, na sasa huyu ambaye
angetakiwa kumwita kaka alikuwa ni mtu mkubwa
kwatika mji huo wa Achen.
“Ndiyo, mimi ni Andreas Schurmman, baba yangu
mimi mzee Ernst Schurmman alizaliwa tumbo moja
na mama yako Angela Schurmman, wakati wa vita
ya pili ya dunia ndipo walipopoteza maisha katika
mazingira tofauti na wewe ulichukuliwa ukiwa
mdogo na babu yako aliyemzaa mama yako, mimi
nililelewa na msamalia mwema tu mpaka nimekuwa
hivi nilivo.”
Gustav alitikisa kichwa juu chini kuonesha kuwa
aliielewa hiyo safari ya maisha jinsi ilivyokuwa.
“Umejuaje kama nipo hapa?”
“Nina rafiki yangu ambaye ni mfanya kazi hapa
ndiye aliyeniambia lakini hata yeye hajui kuwa mimi
na wewe tuna undugu, ila mimi nilijua kwa kuwa
ninalikumbuka jina hili Gustav Macker, karibu sana
nyumbani uje unitembelee”.
Baada ya mazungumzo yao waliagana na kila mtu
kubaki na na hamsini zake, ‘Sasa ishu yangu
itakamilika’, Don Andreas Schurmann alijiwazia
wakati akiingia kwenye gari yake aina ya Mercedes
Benz na kuuacha uwanja wa seminari hiyo.
§§§§§
“Hutakiwi kushangaa wala kushtuka” Don Andreas
alimweleza Gustav Macker.
“Sishangai kwa unachoniambia, bali nashangaa kwa
nini babu aliweka utajiri huo huko?! Inatia uchungu”
“Hapana babu yangu alikuwa na akili sana, alikuwa
anatafuta mahali salama pa kuihifadhi siri ile ya
utajiri kwa kizazi chake cha sasa” Don Andreas
akajimiminia glass yake ya pombe kali na kusafisha
koo kwa kujikohoza kidogo, kisha akaendelea,
“Vatican, ni sehemu yenye usalama sana duniani, na
si uongo. Mzee Peter Schurmann aliiweka pale siri
ile ya utajiri mkubwa kwa ukoo wake. Sikia Gustav,
utakapokuwa Padre nitafanya kila njia uhamishiwe
Vatican ili ufanye uchunguzi ujue jinsi gani tunaweza
kuipata Monstance ile irudi mikononi mwetu.”
Gustav aliinama kwa sekunde chache akiangalia
sakafu ile ya marumaru safi ambayo ilimruhusu
kuiona taswira yake mwenyewe kwa jinsi ilivyokuwa
safi.
“Gustav!” Don aliita, “Usihofu, haya ni mambo
madogo sana, na nina hakika tutafanikiwa na kuishi
kifalme”. Maneno matamu ya Don Andreas
yalianzisha mapigano ya nafsi na roho ndani ya
kijana huyu ambaye kanisa liliridhia kumpa ukasisi
miezi michache ijayo, ama kweli kwenye mkono wa
Mungu hapakosi mguu wa shetani. Mazungumzo ya
wawili hao yalikuwa marefu sana na mwishowe
makubaliano yalifanyika na mpango mahsusi
ukapangwa na tajiri huyo, Don Andreas, kama
alivyojulikana.
Baada ya miezi sita Gustav Macker alipewa daraja
la upadre na kuwa kasisi rasmi katika kanisa
Katoliki, hakuamini masikio yake alipopata taarifa
kuwa kituo chake cha utume kitakuwa Vatican,
katika makao makuu ya kanisa hilo.
Dagoreti Corner Super Pub
BLACK Cheetah alinyanyuka na kusimama wima na
wengine wakafanya hivyo hivyo.
“Vijana tuingie kazini, tutengeneze pesa” Cheetah
aliwaeleza wenzake na wote wakahafiki.
Walipomaliza vinywaji hivyo waliliendea gari ya
Black Cheetah aina ya Subaru na kupotelea mjini.
Ilikuwa tayari majira ya saa nne usiku Subaru ile
ilipoegeshwa katika maegesho ya viwanja vya Uhuru,
wote wakateremka na kupotelea katika club kubwa
inayojulikana kama Nairobi by night, humo starehe
za aina zote zilikuwa zikipatikana, walijichanganya
na wadau wengine wakisubiri mida yao ya kazi ifike
ili wafanye wanalolihitaji.
* * *
Ilitimu saa sita ya usiku, Cheetah na wenzake
walipoegesha gari yao karibu kabisa na jingo la
kanisa hilo na kushuka.
“Hivi nyie mnaosali, hiyo monstrance sijui nini huwa
inahifadhiwa wapi?” Cheetah aliwauliza wenzake
“Kawaida kwenye chumba cha kuvalia makasisi,
ambacho huwa ni kanisani” alijibu Mellina wakati
Gicui akiliangalia jingo lile kubwa lililojengwa kwa
kuta nene ajabu likiwa katikati ya mji wa Nairobi.
“Ok, nafikiri mmoja wetu aingie huko kwenye hicho
chumba halafu wengine waangali usalama wa ndani
na nje” Cheetah alitoa oda.
“Sawa Cheetah!” Gichui aliitikia kama
aliyekurupushwa usingizini.
Dakika chache baadae Gichui alikuwa ndani ya wigo
wa kanisa hilo akitalii hapa na pale, akiangalia hiki
na kile, usiku mnene usio na mbala mwezi, aliifanya
kazi hiyo kwa ustadi hata walinzi hawakugundua
chochote, Mellina na Cheetah walibaki nje lakini kila
mmoja upande wake, Mellina katika ulinzi wa nje na
Cheetah akiwa makini na tayari kumuokoa Gichui
kama itatokea la kutokea. Akiwa ndani ya wigo ule
Gichui alitembea kwa uangalifu sana akichungulia
kwenye vitundu vidogo vilivyojengewa kwenye ukuta
huo wa kanisa, ndani aliona tu kataa kekundu
kakiwakawaka mithili ya mshumaa, alikaangalia na
kukumbuka kuwa pale huwa makasisi
wanawekaweka vikombe Fulani, labda ni penyewe.
Aliendelea na kutokea upande wa nyuma wa kanisa
hilo, milango kadhaa ilikuwako hapo na yote
imefungwa imara kabisa kwa vitasa vya kiitaliano,
kila aliyoutikisa ulikuwa imara kabisa, akatoa funguo
zake zinazofungua kotekote akatumbukiza moja na
kujaribu ikagoma, akachukua nyingine akatumbukiza
mlango ukakutii amri na kufunguka, akiwa na sox
yake kichwani akaingia ndani ya chumba hicho
ambako alikutana na makabati mengi ambayo
yalimchanganya, kabati kubwa la mbele
liliunganishwa na meza kubwa sana iliyofunikwa
kwa Formica safi, akatulia na kuatafakari, kabati lipi
hasa analolihitaji, kwake aliiona kazi hiyo ikiwa
rahisi kabisa ni kiasi cha kufungua makabati tu na
kubeba anachotaka kisha kuondoka. Alilijongea
kabati hilo kubwa na kujaribu milango yake, ilikuwa
wazi, ndani kulikuwa na nguo tu za ibada
zinazotumiwa na makasisi.
§§§§§
Fr Frederick Gichuru, alishtuka usingizini, ndoto
mbaya ilimsongasonga hata kuufanya moyo wake
kwenda mbio, alikaa kitandani na kuitafakari ndoto
hiyo hakupata maana, machozi yalimtoka, alipiga
magoti mbele ya msalaba na kutulia kimya, baada
ya dakika kadhaa alishtuka na kusikia kelele za
mlango kama mtu anaufungua kwa kutumia nguvu,
alisikiliza kwa makini na kukuguundua kuwa ulikuwa
mlango wa Sakristia (sakristia ni chumba
kinachojengwa pamoja na kanisa ambacho
uhifadhiwa mavazi na vitu mbalimbali vya ibada),
mlango ambao Gichui alikuwa akiufungua taratibu
sana lakini Fr Gichuru aliusikia kwa kelele. Aliinuka
na kuchuku kanzu lake zito jeusi ili kujistiri na baridi
kali ya Nairobi, alienda mpaka chumba cha Fr Joe,
akamkua mzee huyo anakoroma kwa usingizi mzito
akaamua kumuacha, akatoka nje kuelekea kanisani
kushuhudia nini kinafanyika, alishtuka na kusimama
ghafla alipoona mlango wa sakristia uko wazi,
alikibanza kwenye ua kubwa la yugiyugi lililomficha
vizuri, ‘wanataka nini?’ alijiuliza asipate jibu,
aliangalia lakini hakuona mtu kutoka, alivuta hatua
ndogindogo na kuufikia mlango huo, akazipanda
ngazi na kuingia ndani, aligeuka huku na huku
hakuona mtu isipokuwa milango wazi ya makabati.
“Tulia apo hapo, usijitikise” sauti ilitoka upande wa
makabati ya nyuma.
Fr Frederick alitulia na kunyoosha mikono yake juu
kujisalimisha.
“Wanaume wanapokuwa kazini wewe hutakiwi
kuamka amka” Gichui alimwambia Fr Gichuru, Fr
Gichuru aling’ata meno kwa hasira, hakujali kama
mtu huyo ana silaha gain alishusha mikono na
kugeuka na kutazamana na domo la bastola aina ya
Smith and Wesson.
“Wewe ni nani?” Fr Gichuru aliuliza
“Usitake kujua” alijibiwa
Fr Gichuru alimkazia macho Gichui, Gichui alijikuta
akiishiwa nguvu na kushusha bastola yake.
“Kwa nini mnataka kulidhulumu kanisa?” akauliza Fr
Gichuru, “Nani aliyekutuma? Na mnataka nini?”
kimya kilitawala kati yao, “Sema nitakusaidia, kazi
ya kanisa ni kusaidia wahitaji na wenye shida,
sema.” Gichui aliinua bastola yake tena na kuondoa
kiguu cha usalama kuruhusu risasi ipande juu tayari
kabisa kufyatuliwa.
“Siogopi risasi, maana risasi itaua mwili lakini
kamwe haiwezi kuuwa roho” Fr Gichuru alimueleza
jambazi yule. Gichui alishusha pumzi bado
akimnyoshea bastola kasisi huyo.
“Sikiliza kijana, weak bastola yako mahali pake
uende kwa amani, maadam sijakuona sura yako na
hii itabaki kuwa siri yetu mimi na wewe tu,” Fr
Gichuru alimaliza na kuanza kufunga makabati yake.
Alipogeuka baadae hakumuona yule jambazi mahali
pale, akafanya ishara ya msalaba na kurudi
nyumbani kwake. Usingizi haukuwako tena mpaka
kulipokucha.
ITAENDELEA....
UKIITAKA YOTE NJOO WHATSAPP NA 3000
MKONONI 0766974865
 
RIWAYA: MAUAJI YA KASISI
MTUNZI: richard MWAMBE
WHATSAPP: 0766 974865
“Sikiliza kijana, weak bastola yako mahali pake
uende kwa amani, maadam sijakuona sura yako na
hii itabaki kuwa siri yetu mimi na wewe tu,” Fr
Gichuru alimaliza na kuanza kufunga makabati yake.
Alipogeuka baadae hakumuona yule jambazi mahali
pale, akafanya ishara ya msalaba na kurudi
nyumbani kwake. Usingizi haukuwako tena mpaka
kulipokucha.
SEHEMU YA 3
§§§§§
“Uuuuh!” Gichui alipumua kwa nguvu baada ya
kuingia kwenye gari yao akiwa na wenzake tayari
kuondoka.
“Tupe ripoti” Cheetah alitoa ombi kwa Gichui
“Haaaa, siamini”
“Huamini nini, umeona nini huko?” Cheetah alidadisi
“Makabati makubwa na nguo za kasisi, sijaona
monstrance”
“Lakini Gichui unaonekana kuna kitu hutaki kusema”
mellina alidakia kutokapale nyuma ya usukani
alikpokaa.
“Kanisani, si pa kuiba” alijibu, “Nimekutana na
Kasisi Gichuru ana kwa ana pale kanisani” akaweka
tuo kidogo na kuendelea “Nilijikuta naishiwa nguvu,
sikuweza kufanya lolote, akaniruhusu kuondoka”.
“We bwege kweli, ungembana huyohuyo akueleze”
Meliina aling’aka.
“Mellina mi nashindwa kukueleza, wale jamaa sijui
wana dawa!” aliongea kwa mshangao Gichui.
“Basi, tutarudi kwa nguvu mpya” Cheetah aliwapoza
wenzake na kuondoka zao.
“Una uhakika kuwa hiyo monstrance ipo huku?”
Cheetah alimuuliza mtu mnene kwa njia ya simu.
“Mi siyo mtoto Cheetah, najua na nina uhakika na
hilo, hakikisha tunaipata” alijibiwa.
“Maana jana tumefanya upekuzi mle kanisani
hatukuiona” aliendelea kuongea Cheetah
“hata kama haipo kanisani, lakini ipo maeneo hayo,
fanya kila unaloweza uipate” alimaliza mtu mnene
na kukata simu.
“Sasa wajukuu, hapa kilichobaki ni kufanya mbinu
zote kumteka Fr Gichuru tumbane mpaka atueleze
maana yeye ndiye aliyeuleta ule mzigo” Cheetah
aliwaelezawenzake na wote wakaafikiana na
kupanga mikakati.
§§§§§
“Baba Joe, leo usiku nimeota ndoto mbaya sana
hata nikaamka usiku kusali” Fr Frederick alimueleza
Fr Joe walipokuwa mezani wakipata chai.
“Ni nini tena umeota Fr?” Joe aliuliza
“Ah, ndoto mbaya sana” alisema huku akitua slesi
za mkate katika sahani na kuiinamia meza
akitegemeshwa na mikono yake miwili. Fr Joe
aliona matone kama matone ya maji yakidondoka
juu ya meza hiyo.
“Fr, ni nini, nieleze nikusaidie” Fr Joe aliinuka kitini
na kulmuendea Fr Gichuru huku akimueleza maneno
hayo, alitoa kitambaa chake na kumfuta machozi. Fr
Gichuru aliinuka kitini pamoja na Fr Joe wakatoka
nje kwenye kabustani kadogo na kutembeatembea
wakiwa na rozali zao mikononi.
“Fr Joe! Nililala kama kawaida mara baada ya
masifu ya jioni, katikati ya usiku huo niliota nipo
Roma makao makuu ya kanisa, nipo juu kabisa ya
mnara wa jengo hilo, niliangalia chini palikuwa
parefu sana, isingekuwa rahisi hata kuruka, sikuwa
na msaada, nililia na machozi yangu yalikuwa ni
machozi ya damu, yalitirirka na kulowesha kanzu
yangu nyeupe lakini hayakufika chini bali yote
yalituama kifuani upande wa moyo wangu.
Nilimuona Malaika kasimama mbele yangu
mkononi kashika kikombe, akanisogelea akanipa
kikombe hicho ambacho ndani yake kulikuwa na
divai nyekundu lakini cha kushangaza mlikuwa na
risasi ndani yake, akanambia
‘Kunywa’, nikasita akanambia kuwa ‘yakupasa
unywe’, nilikiangalia kikombe kile, mwsho nilikitwaa
na kunywa, nilipomaliza tu nilihisi kizunguzungu na
kuanguka kutoka juu ya mnara ule kuelekea chini,
lakini kabla sijafika chini nilishtuka kutoka
usingizini.
Mara moja niliitafakari ile ndoto lakini sikupata
maana yake, nikapiga magoti kusali, wakati nasali
niakaanza kusikia kelele za mlango wa Sakristia
ukifunguliwa, kelele zile zilikuwa kubwa mno hata
kuyasumbua masikio yangu, nilinyanyuka na kuitwaa
kanzu yangu kisha nikaja chumbani kwako
nikakukuta umelala, nikakuacha na kwenda kungalia
nini kinachotukia huko, lo! Fr Frederick alijishika
kifuani na kukumbuka ahadi yake na yule jambazi
‘ibaki kuwa siri yetu’…”
“Oh Bill, aaaah, uuuuh” sauti ya kimahaba
iliyoashiria kuwa viumbe hao wapo kwenye
ulimwengu mwingine zilitawala chumba kimojawapo
katika hotel kubwa inayojulikana kama Plazza Hotel
iliyopo katikati ya jiji la Nairobi.
Bill, mtu mnene alikuwa kitandani akipewa raha na
msichana wa Kikikuyu kutoka North Kinangop, binti
huyo alihakikisha anampagawisha mzee huyo
mpaka ammalize kabisa, na hivyo ndivyo ilivyokuwa,
Bill alikuwa nyang’anyang’a kwa penzi alilopewa na
msichana huyo aliyembeba usiku uliopita katika
mtaa wa Koinange hapo hapo Nairobi kwa dau la
kulipana dola za kimarekani, alimfurahia jinsi
alivyomkatia kiuno kwa mitindo ya ajabu hata
akafanywa kusahau adhma ya kumtaka msichana
huyo kimapenzi.
Rosemary Wangui alihakikisha anamkamua Bill mtu
mnene mpaka tone la mwisho akiwa na lengo moja
tu la kuchota madola yake yaliyojaa katika mkoba
maalumu wa ngozi.
Penzi la uongo na muda mfupi liliendelea katika
kitanda cha hotel hiyo, hakuna aliyekiogopa kifo,
baada ya kuona hawafaidi utamu wa maumbile yao
ndipo walipokubaliana kutokutumia kinga ili kutiana
hasara roho, hapo sasa ndipo mtu mnene alipoahidi
donge nono kwa shughuli aliyopewa na msichana
huyo aliahidi kufanya lolote kwa jinsi
alivyopagawisha na mtu mnene, Bill.
“Rose, you are so sweet baby!” Bill alitamka
maneno hayo huku akijifunga taulo kuelekea
maliwato.
“Same to you my cock” Rose alimsindikiza Bill kwa
macho wakati akielekea maliwatoni huku moyo
wake ukimuenda mbio kwa kuuona ule mkoba wa
Bill ulioshiba manoti. Dakika chache baadae Bill
alitoka maliwato na kuketi juu ya kitanda na
kuruhusu minyama ya mwili wake kutikisika kwa
jinsi alivyojitupa hapo.
“Rose!” Bill aliita
“Yes, Sir!” Rose aliitika kwa adabu ya uongo.
“Unauona ule mkoba wenye pesa?” Bill alimtupia
swali Rose
“Yeah nauona, vipi?”
“Nitakupa ule mkoba kama ulivyo, na pesa yake
ndani” Bill alizungumza hayo na kumwangalia Rose
usoni, Rose hakuamini anayoyasikia kutoka mtu
mnene, tabasamu pana lilichanua usoni mwa
mrembo huyu, tabasamu la kuuaga umasikini,
tabasamu la utajiri wa dharula.
“Sijaelewa darling” Rose alisema kuonesha kuwa
hajaelewa aliloambiwa.
“Nini hujaelewa? Kwenye ule mkoba kuna dola za
kimarekani nyingi tu, nahitaji kukupa wewe pamoja
na mkoba wake kama ulivyo”. Rose alibaki kimya,
kisha akafungua kinywa chake na kumwambia mtu
mnene “Asante,” akamkumbatia na kukutanisha
ndimi zao ambazo zilichukua muda kidogo kila
moja kuonja ladha ya nyingine. Kisha Bill akamtoa
Rose kinywani mwake.
“Sikia, hakuna ujira usiyo na kazi kwanza” Bill
aliongea, akainua glass yake ya pombe ya kirusia
‘Pushkin’ akapiga funda moja na kumtupia jicho
Rose aliyejilaza kitandani na kuegamia upande wa
mbele wa kitanda hicho kwa kutumia mto wa
kulalia.
“Nakusikiliza” Rose alimwambia Bill mtu mnene.
“Unamjua huyu?” Bill alimuuliza Rose na kumpa
picha ndogo iliyoonekana kwenye kioo cha simu
yake kubwa, Rose aliipokea na kuiangalia kwa
makini sana kisha akatikisa kichwa kuashiria
ameifahamu.
“Mmh! Namfahamu, kafanyaje?”
“Namtaka huyu mtu nizungumze nae kirefu, na
wewe nataka unifanikishie hilo”
Rose alibaki midomo wazi, alimwangalia Bill mtu
mnene hakummaliza
“Kivipi?” akauliza
“Nataka ufanye kila hila ya kike, umlete mahali
halafu vijana wangu watawateka wote wawili ila
wewe watakuacha nay eye tutamchukua kwa kuwa
tuna shida naye” Bill alimueleza kinagaubaga, Rose
alionesha woga sana katika hilo, alijifikiria kwa kina,
pesa anazitamani, kulitekeleza hilo ni vigumu,
ugomvi mkubwa kati ya nafsi yeke ulizuka haikuwa
rahisi kwake kuuamua, alinyanyuaka kutoka pale
kitandani alipokaa na kuvuta hatua chache kuelekea
maliwato alipita mbele ya Bill akiwa mtupu kama
alivyozaliwa, Bill alibaki hoi na kushuhudia jogoo
lake likiinua taulo kuashiria network imerudi.
3
SAJENT Maria na koplo Othorong’ong’o walibaki
kutazamana hawakuwa na jibu sahihi juu ya mauaji
yale, waliperuzi kwa pamoja faili lile
walilokabidhiwa na Inspekta Simon Saitoti
“Kwa maelezo ya Fr Joe, yule paroko, nafikiri
tuifanyie kazi hiyo taarifa tuliyopewa” koplo
Othorong’ong’o alimueleza sajent Maria aliyekuwa
ameketi kwenye benchi huku akiwa na redio call
yake mkononi.
“Uko sahihi, lakini haya maelezo yangekuwa timilifu
sana kama tungeonana na marehemu lakini haikuwa
hivyo” sajenti Maria alionesha ugumu wa kazi ulipo.
“Sajenti, hivi tukifanya uchunguzi kwenye mitaa ya
vibaka kama Kawangware kule hatuwezi kupata
habari yoyote ya huyu Cheetah, ili tupate kwa
kuanzia?” koplo Othorong’ong’o aliuliza.
“Unafikiri Cheetah kwa hadhi yake atakuwa anjificha
kule ambako kila mara tunaenda kwa msako, kule
wamejaa wahamiaji haramu koplo” sajenti Maria
alimjibu koplo Othorong’ong’o, kisha kimya kifupi
kikatawala.
“Nafikiri litakuwa jambo la busara sana tukijaribu
njia hiyo, ila twende kiraia zaidi ili tuchangamane
nao kisha tuweze kupata habari yoyote inayoweza
kutuanzishia game hii.” Walikubaliana kuingia mtaa
huo jioni ya siku hiyo kujichanganya ili kupata lolote
la kuanzia katika kesi hiyo iliyoonekana kuwatoa
kijasho kidogo.’
Walikubaliana kukutana baada ya muda kidogo wa
mapumziko ambapo kila mmoja wao aliutumia kwa
jinsi anavyojua yeye.
‘A Catholic priest murdered after returning from
Rome’. Kilikuwa ni kichwa cha habari kilichosomeka
juu kabisa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la
Daily Nation la siku hiyo, mwandishi wa gazeti hilo
alieleza kwa kina habari hiyo aliyoifanyia uchunguzi
wa kutosha na wa kuridhisha. Sajenti Maria
alilishusha gazeti lile lililokuwa limeuficha uso wake
na kulitua magotini pake na kuruhusu wazo moja
lipite kidogo kisha akaendelea tena kuisoma habari
ile iliyomsisimua sana kama riwaya tamu za Richard
Mwambe, alipojiridhisha na habari hiyo aliandika
vitu fulani katika kijitabu chake cha kumbukumbu
kisha akalifunga na kuingia ofisini kwake ambako
alimkuta koplo Otho’ amesinzia kitini, akamshtua na
kumueleza juu ya gazeti lile kwa jinsi lilivyoandika
kwa kina juu ya habari.
“Sajenti, turudi kwa Fr Joe kwa mahojiano kidogo ili
tujue kwa undani juu ya safari yake ya Roma na
kama kulikuwa na uadui wowote na mtu,”
“Positive, koplo” Maria alijibu na mara moja
wakaelekea katika kanisa kuu la Familia takatifu
kwa kazi hiyo.
§§§§§
“Marehemu Fr Gichuru hakuwa na mazoea ya
kuhifadhi kumbukumbu sehemu? Ama kwa
maandishi au njia yoyote ile?” lilikuwa ni swali
kutoka kwa koplo Otho’
“Yeah, alikuwa anaandika sana, daima alikuwa na
diary yake” Fr Joe alijibu hukua akinyanyuka na
kuingia kwenye chumba cha marehemu Fr Gichuru,
kisha akarudi na diary ndogo mkononi mwake na
kuiweka mezani, sajenti Maria aliichukua mikononi
mwake
“Fr, samahani kwa kukusumbua mara kwa mara
lakini nafikiri ndani ya diary hii tunaweza kupata
chochote kitakachotusaidia, kama unaturuhusu
tuondoke nayo ili kuendelea na upelelezi”
“Oh ninyi mpo kazini, usijali mama, nenda nayo
ukimaliza kazi nayo uirejeshe kwa kumbukumbu
hapa” Fr Joe aliwakabidhi ile diary na kuagana nao,
akawasindikiza mpaka getini, walipokuwa
wanaagana pale getini, mwanamke mmoja mnene
lakini aliyeonekana ana mwili wa mazoezi akiwa
kavalia sketi nyeusi, iliyobeba blauzi nyeupe na juu
yake ikafunikwa na kijikoti cheusi, aliingia getini na
kuwapita sajenti Maria na koplo Otho’ wakati
wakiagana na Fr Joe. Jicho la sajenti Maria
halikuondoka kwa yule dada aliyekuwa akitembea
kwa mwendo wa wastani akielekea kanisani
kulikokuwa kukiendelea na maombolezo. Baada ya
maagano yale, sajenti Maria alirudi garini pamoja na
koplo Otho’
“Koplo, umemuona yule dada aliyetupita pale?”
Maria aliuliza
“Nimemuona, halafu sura yake si ngeni kichwani
mwangu” koplo Otho’ alijibu na kuongezea. Sajenti
Maria alitulia kwa nukta kadhaa, akavuta kijidroo
cha dashboard ya gari na kutoa kamera ndogo
ambayo unaivaa kama saa mkononi, akateremka
garini.
“Nakuja koplo, Linda mkia wangu tafadhali” Maria
alitamka hayo huku akiurudishia mlango wa gari ile
na kurudi kule kanisani kwa kutumia njia ile
aliyopita yule dada wakati huo akiivaa ile camera
mkononi mwake. Ilikuwa ni hatua chache tu
alimuona yule dada akiwa katikati ya watu
akijipenyeza ili kupata eneo zuri la kumuezesha
kujua kinachojir katika kanisa hilo ambalo lilijawa
na waumini waliokuwa wakiomboleza kwa nyimbo
na zaburi. Sajent Maria aliendelea kumuangalia kwa
makini, alimuona akitoa simu yake na kuandika kitu
kama ujumbe mfupi kisha kuirudisha kotini, na
muda huohuo alijipenyeza tena kuelekea upande
mwingine ndipo alipogongana kikumbo na sajenti
Maria ambaye kwa uzoefu wake wa kazi ya kipolisi
alikuwa tayari amekwisha mpekua kwa
kumgusagusa.
“Dada, we vipi? Mbona unagonga watu ovyo, huoni
njia?” yule dada aliuliza
“Samahani nilikuwa nasoma saa hata sikukuona,
samahani sana” sajenti Maria aliomba radhi, kila
mtu aliyekuwa pale aliawaangalia wanawake hawa.
Sajenti Maria alikua amehisi kitu kigumu katika
ubavu wa kushoto wa mwanadada yule na kwa
uzoefu wake aligundua kuwa yule dada amehifadhi
bastola katika ubavu wake, aliishusha saa yake
machoni na kutazama kama picha aliyoipiga
imetoka vizuri, akaridhika nayo kisha akajiondoa na
kurudi garini.
“Vipi?” koplo Otho’ aliuliza
“Ah, clear, nina wasiwasi na yule dada, kwanza
inaonekana ana bastola kiunoni mwake” Maria
alijibu
“Tumsubiri?”
“Haina haja lumsubiri, huyo hapo anakuja, hakikisha
hatumpotezi kwenye sight yetu.”
Yule mwanadada alitoka getini na kupinda kushoto
kwenye maegesho ya magari na kuingia kwenye
moja ya magari yaliyopo hapo, na gari ile taratibu
iliyaacha maegesho yale kuingia barabarani
kuelekea upande wa Westland. Koplo Otho’ naye
aliiondosha gari yao aina ya Peugeot 308, gari ya
kisasa kutoka Uingereza, baada ya dakika kadhaa
waikuwa kwenye foleni kubwa za Nairobi lakini
macho yao yalikuwa makini kuitazama gari
aliyopanda mwanadada yule isipotee. Kwa mwendo
wa taratibu walikuwa katika barabara ya Mombasa
kisha wakaiacha ile iendayo Nairobi central na wao
kuifuata ile gari aliyokuwa sasa imekamata barabara
ya Waiyaki kuelekea Westland, baada ya mwendo
kidogo ile gari ilikunja kulia na kufuata barabara ya
vumbi iliyoingia katikati ya nyumba zilizojengwa kwa
mpangilio mahsusi kama quarter za shirika Fulani,
Otho’ nae aliingia na gari yake kuifuata, sasa ailibaki
gari mbili tu mbele aliyopanda yule dada na nyuma
ya kina koplo Otho’ na sajenti Maria…
Otho’ aliegesha gari yake mbele kidogo karibu na
duka kubwa lililokuwa likiuza bidhaa muhimu kwa
binadamu. Sajenti Maria alishuka kutoka katika gari
na kutembea taratibu kuelekea kule aliko yule
mwanadada, Otho’ alibaki kwenye gari akiangalia
kwa mbali tukio hilo. Yule mwanadada aliongeza
mwendo kidogo alipogundua kuwa anafuatwa,
alitembea huku akitoa simu yake ya mkononi na
kuongea na mtu Fulani, sajenti Maria aliona tayari
kagundulika kama anamfuata huyo mwanadada, na
yeye alitoa simu yake na kwasiliana na Otho’ ili
amlinde katika hilo. Otho’ aliiacha gari pale dukani
na kufuata ule mtaa kama mtu aliye na shughuli
nyingine kabisa, kwa mbali alimuona sajenti Maria
kasimama akitazamana na yule mwanadada, kati
yao kulikuwa na nafasi kama ya mita mia moja hivi,
Otho’ alimpita sajent Maria na kumsalimu kama
hamjui huku akiendelea upande ule aliko yule
mwanadada na alipomfikia alimsalimu vilevile na
kuendelea na safari yake na kumpita yule
mwanadada, baada ya mwendo kama wa mita
hamsini alikunja kona na kusimama kuona nini
kinaendelea.
Sajenti Maria alibaki akitazamana na yule
mwanadada kila mmoja akiwa na simu mkononi,
mara nyuma ya Sajenti Maria ulisikika mlio wa
pikipiki, Sajenti Maria alipogeuka nyuma kuipisha
pikipiki ile alichelewa, dereva wa ile pikipiki
alimgonga Maria na kumuangusha chini, sajenti
Maria alijaribu kujiinua lakini kabla hajakamilisha
zoezi hilo aligongwa tena eneo la mbavu na
kuanguka chini, kisha yule muendesha pikipiki
aliteremka na kuiegesha ile pikipiki huku ikiwa
inanguruma na taratibu alimfuata sajenti Maria pale
chini, alimtazama kwa dharau na kupandisha juu kile
kioo cha kofia ngumu aliyoivaa.
“Wewe ndiyo unajua kufatilia nyendo za watu siyo?”
alimuuliza huku akimsogele karibu zaidi. Sajenti
Maria alimwangalia kwa hasira mpaka uso wake
ulipoteza kabisa ile haiba ya uanamke, yule jamaa
alipomkaribia alichuchumaa ili kumsaili vizuri sajenti
Maria, kwa kushtukiza sajenti Maria alirusha teke la
nguvu lililotua katikati ya mapaja ya yule jamaa na
kupiga sawasawa sehemu zake za siri, yule jamaa
kabla hajajielewa teke lingine lilitua upande wa kulia
wa shingo yake na kumpeleka chini, sajenti Maria
alijiinua kwa haraka na kusimama kidete na
kumuacha yule jamaa akiwa chini. Yule mwanadada
alipoona mchezo ule wa kiufundi kutoka kwa sajenti
Maria aligeuka ili apotee eneo lile, lakini hamad
alijikuta akitazamana uso kwa uso na bastola ya
Othorong’ong’o, alisimama ghafla na kujikuta hana
la kufanya, Otho’ akatoa pingu zilizokuwa mifukoni
mwake ili kumfunga yule mwanadada.
“Weka mikono yako nyuma!” alimuamuru ili
amfunge pingu hizo, yule mwanadada
akaishikanisha mikono yake nyuma ya mgongo
akiwa anatazamana na Otho.
“Geuka” Otho alimuamuru, na yule mwanadada
aligeuka na mkononi mwake tayari alikuwa na
bastola amabayo aliificha upande wa nyuma kwenye
sketi yake, aligeuka na kufyatua risasi iliyoenda na
kupiga mguu wa Otho, yowe la maumivu lilimtoka
Otho huku akiiachia bastola yake ikidondoka chini,
sajenti Maria alichanganyikiwa afanye nini akiwa
bado katika kuhamaki pikipiki nyingine ilitokea
nyuma ya Otho na yule mwanadada akaidandia
katika kiti cha nyuma, sajenti Maria alirusha risasi
kwa bastola yake lakini hakuweza kupata shabaha
nzuri kwani ile pikipiki ilikuwa imekwishakunja kona
na kumuacha Otho akiwa chini mguu ukivuja damu,
aligeuka kumwangalia yule mwenye pikipiki ya
kwanza lakini hakumuona pale badala yake watu
walianza kujaa eneo lile, sajenti Maria akavua shati
lake alilovaa juu na kumfunga koplo Otho jeraha
lake ili kuzifanya damu zisiendelee kumwagika
kisha akajitahidi kumyanyua kutoka pale chini
akisaidiwa na watu wachache walifanikiwa
kumfikisha kwenye gari, sajenti Maria aliwasha gari
na kuondoka eneo lile.
Siku mbili
kabla ya mauaji ya Fr Gichuru
MTAWA wa kike alikuwa amesimama katika kituo
cha matatu akisubiri usafiri kuelekea mjini, kila mara
alionekana akiiangalia simu yake, huku akiwa na
kikapu mkononi alionekana kama anayekwenda
sokoni. Mara gari moja Land Rover Defender ilikuwa
ikitoka katika geti la kanisa hilo na kukunja kulia
kuelekea mjini, ikasimama jirani kabisa na mtawa
yule.
“Sista, twende nikusaidie” ilikuwa ni sauti ya Fr
Gichuru akimpa lifti yule mtawa, alipokwishakuketi
sawia kitini waliondoka kuelekea upande wa mjini
na Fr gichuru alianzisha maongezi.
“Sista safari ya wapi saa hii?”
“Nakwenda Kileleshwa estate, kusalimia jamaa
kwani leo nina ruhusa kutoka kwa mama mkuu”
yule mtawa alijibu.
“Ooh, vizuri kuwatembelea ndugu siku mojamoja” Fr
Gichuru alimueleza huku akiwa anakaribia katikati ya
jiji la Nairobi
“Ila kwanza nataka kwenda pale shule ya msingi
Nairobi, ningeshukuru kama unganisaidia kufika pale
maana usafiri wa kwenda kule ni mgumu” yule
mtawa aliomba huku akimlegezea macho Fr
Gichuru. Siku zote kumnyima mwanamke ombi lake
siyo rahisi sana, Fr Gichuru aliiacha barabara kubwa
na kuufuata barabara ndogo inayopita katika
majumba ya watu kuelekea huko shule ya msingi,
alipoyamaliza majumba na kuteremka kibonde
kidogo kuliendea daraja ili kuvuka na kutokea
upande wa pili, alikuta mtu aliyeanguka na pikipiki.
“Oh God!” yule sista alihamaki, Fr Gichuru
akasimamisha gari akataka kushuka kwenda
kumsaidia yule jamaa aliyeanguka.
“No usiende Fr ni hatari, huwezi jua nini kilichopo
huko chini” Sista alimbembeleza Fr Gichuru, lakini
haikuwa rahisi kwani moyo wa huruma wa kikasisi
ulimsukuma kushuka.
“Hapo hapo ulipo tulia” sauti ilitoka nyuma ya gari
yake, alipogeuka alikutana na mtu aliyeshika
bastola akimnyooshea yeye.
“Nini tena jamani? Mbona sielewi kinachoendelea?”
Fr Gichuru alilalamika
“Tulikuwa tunakusubiri wewe na tunashukuru huyo
sista wako amekuleta mahali pema peponi” yule
jambazi alizungumza, “Haya haraka ingia katika gari
iyohiyo siti ya nyuma” aliamuriwa, na bila kubisha
alijipakia ndani yake na nyuma ya usukani yule
mtawa aliyepewa lifti alikuwa tayari nyuma ya
usukani kwa kuondoka.
“Ha! Sista!” Fr Gichuru alipigwa na mshangao
alipomkuta yule sista tayari ameketi kwenye
usukani.
“Aliyekwambia mi sista ni nani!?” alijibu yule mtawa
huku akitoa kilemba chake kichwani na kuruhusu
rasta zake ndefu kumwagika mabegani “Mimi
nilikuwa nakutafuta wewe, naitwa kahaba Rose”
alijitambulisha. Fr Gichuru alivalishwa soksi usoni ili
asione anapopelekwa na safari ilianza. Mwendo wa
muda kadhaa waliisimamisha ile gari na kumshusha
Fr Gichuru kisha wakachukua gari nyingine na
kuitelekeza ile ya mission palepale eneo la
Madaraka estate pembeni mwa barabara ya
Mbagathy, kisha wao wakaendelea na safari yao
kuelekea barabara ya Mombasa na mpaka karibu na
kiwanda cha saruji cha Bamburi na kupinda kushoto
kuelekea kwenye eneo la viwanda, moja kwa moja
waliingia kwenye godown kubwa na kumteremsha
Fr Gichuru. Ndani ya chumba kidogo chenye
vikorokoro vingi walimuhifadhi akiwa amefungwa
kamba kwa nyuma.
Yule mwanamke aliyejifanya mtawa alimvua ile
soksi usoni na kumuacha huru akiweza kuona kwa
mbali kutokana na giza lililotanda ndani humo
ITAENDELEA....
 
SEHEMU YA 4
.
§§§§§
“Kazi uliyonituma nimeimaliza, nipe changu” Rose
alimwambia mtu mnene walipokutana tena katika
chumba chao kilekile katika Plazza Hotel.
“Usijali, mzigo wako upon a asante kwa kazi nzuri,
lakini ole wako uitoe siri hii, nakuua” Bill mtu
mnene alimpatia pesa nyingi kahaba Rose na
kuagana nae.
“Asante Bill” alishukuru huku akitoa machozi,
machozi yenye pande mbili, furaha ya kukamata
pesa nyingi ambazo hajawahi kuzishika maishani,
na uchungu wa kumsaliti kasisi asiye na hatia.
Alitoka na kubamiza mlango nyuma yake, moja kwa
moja akaiendea lifti na kuteremka chini kabla ya
kupotelea mitaani.
Bill akiwa na swahiba zake waliingia katika gari aina
ya hammer na kuelekea kumuona mateka wao
mioyoni mwao wakijua kazi imekwisha.
Ukimya ulitawala katika lile godown isipokuwa
kweny kijichumba kimoja kimoja tu ambako Fr
Gichuru alikuwa akisali kwa kilatini kwa sauti tulivu
ambayo kama ungekuwa karibu na dirisha lake
ungeisikia vizuri tu.
Mara mlango ulifunguliwa kwa ghafla na watu sita
waliingia ndani ya kijichumba kile. Fr Gichuru
aliendelea na sala yake kana kwamba hakuna mtu
aliyeingia humo ndani.
“Mmmh Sali sana tu mpaka milango ifunguke!”
sauti hiyo ilimshtua Fr Gichuru na kuinua macho
yake juu na kugongana na yale ya ya Bill mtu
mnene
“Bill!” aliita kwa mshangao
“Unashangaa nini? Habari za Roma?” Bill alimuuliza
Fr Gichuru
“Nzuri tu, habari za ulikokwenda”
“Salama tu Fr, leo tumeonana tena, sina
mazungumzo mengi na wewe leo ila ninachohitaji ni
ile Monstrance, tuambie ilipo tukaichukue usiku huu
kisha tutakuachia huru, mimi sipendi kumwaga
damu isiyo na hatia kama yako Reverent Father
Frederick Gichuru” Bill aliongea kwa pozi huku
akiruhusu pumzi zake kumtoka kwa shida. Fr
Gichuru alimtazama mtu huyu mnene na kisha
kuwatazama wale wengine watano, mara moja
akamtambua Gichui, yule jambazi waliyekutana naye
kanisani akipekuwa makabati.
“Muulizeni huyu kama ameiona” alimueleza Bill huku
akimtazama Gichui, “Ile ni mali ya kanisa ninyi
mnaitakia nini?” akawauliza. Wote wakatazamana.
“Gichuru, kama hutaki kutueleza utataulazimisha
kufanya kitu tusichokitaka, haya mi natoka
nawaacha vijana wangu utawaelekeza” Bill mtu
mnene alizungumza na kutoka katika kile chumba
akifuatiwa na wengine wawili, pale ndani wakabaki
watatu. Cheetah na wenzake walimuadhibu vikali Fr
Gichuru kwa mapigo makali sana kumlazimisha
aseme, lakini Fr Gichuru hakufungua mdomo wake
badala yake alikuwa akisali kwa kilatini ambacho
wale jamaa hawakuelewa kitu. Mateke ya tumboni,
mbavuni, mikanda ya kijeshi vyote vilikuwa ni
masluub kwa Fr Gichuru.
Lakini baada ya kumtesa kwa zaidi ya lisaa limoja
Fr Gichuru alipoteza fahamu kabisa na kulala kama
mfu.
“Amekufa?” Mellina aliuliza
“Hajafa huyu kazirai tu, lete maji baridi” Wambugu
alimueleza Mellina, ndoo ya maji ikafika na
kummwagia mwilini Fr Gichuru, akashtuka na
kuhema kwa nguvu, akawatazama wale watesi wake
mmoja baada ya mwingine.
“Baba uwasamehe maana hawajui watendalo” baada
ya kusema maneno hayo alianguka na kupoteza
fahamu kwa mara nyingine…
Kwa mbali alisikia mlango ukifunguliwa, ilikuwa ni
ndoto tamu iliyomfariji moyo, alimuona Malaika
akija pale alipolala na kumfungua zile kamba.
Haikuwa ndoto kiuhalisia, mlinzi wa godown lile
aliingia kwa kunyata ndani ya kile chumba kidogo
alimfungua kamba na kumbeba mabegani mwake
Fr Gichuru aliyekuwa hana fahamu na kujaribu
kutoroka nae, alipita kandokando ya magari mabovu
ili walinzi wenzake wasimuone kasha kwa kutumia
kijimlango kidogo cha nyuma alitoka nje huku akiwa
kambeba fr Gichuru kwa mtindo ule ule, baada ya
mwendo mfupi alimuhifadhi katika nyumba ndogo
jirani tu na eneo hilo, kasha yeye akaenda zake tena
lindoni kwake, hakuna mtu aliyemgundu kwa hicho
alichokifanya aliingia tena kimyakimya na kuendelea
na majukumu yake kama kawaida.
Baada ya masaa machache Fr Gichuru alirudiwa na
fahamu zake na kujikuta mahali tofauti na mwanzo,
alijitazama na kujikuta hana zile kamba mikononi,
yuko huru isipokuwa maumivu makali katika
maeneo ya tumbo na mbavu yalikuwa
yakimsumbua, hakujua ni jinsi gani amefika eneo
lile, alijaribu kuinuka kutoka pale alipokuwa amelala,
akaketi na kuegemea kabati kuukuu lililokuwa ndani
ya kijichumba hicho na kushusha pumzi ndefu
alipogundua kuwa hapo kwa vyovyote ni mahali
salama. Akiwa katika tafakari hiyo alisikia nyayo za
mtu zilizokuwa zikipitapita huku na huko upande wa
nje, akajituliza kimya na kubaki kusubiri kuona ni
nani huyo; mara kelele za mlango ambao bawaba
zake zimekosa mafuta zilisikika na mlango ule
uliacha kijinafasi cha kupenya mtu mwembamba, na
punde tu mtu mmoja alijipenyeza na kuurudishia
huo mlango nyuma yake.
Kutoka ndani ya koti lake alitoa mfuko wa plastiki
uliondikwa UCHUMI na kuuvirigua kisha akatoa
kachombo ka plastiki na kufungua mfuniko wake.
“Father, kula chakula, najua una njaa sana” yule mtu
alimwambia Fr Gichuru. Ndani ya kichombo kile
kulikuwa na chakula aina ya mokimo
(mchanganyiko wa maharage, mahindi na viazi
kisha husongwa kama ugali), Fr Gichuru alikula na
kunywa maji yaliyokuwa jirani hapo bila kuangalia
yana hali gani.
Baada ya kumaliza kile chakula, akajiweka vizuri na
kumtazama yule mtu, sasa akagundua kuwa alikuwa
ni mzee sana lakini bado likuwa na nguvu zake.
“Wewe ni nani?” Fr Gichuru alimuuliza
“Mimi ni bwana Melchior Ndege, mtu wa huko
Iriyamurahi”
“Hapa nimefikaje na ni wapi?”
“Tangu unafikishwa pale godown mimi nilikuona na
sura yako si ngeni kwangu, nakufahamu sana, wewe
ni Fr Gichuru wa kanisa kuu siyo?”
“Sawa kabisa! Zaidi ya hapo wewe ni Malaika
kwangu, hakika Mungu amekutuma”
“Napenda tuzungumze kidogo” yule mzee
alimwambia Fr Gichuru. Fr Gichuru alimwangalia
kwa makini yule mzee aliyekaa mbele yake juu ya
kiti kidogo cha miguu mitatu.
“Father, kwa nini hawa jamaa wamekuteka wewe?
Maana kama hela huna!”
“Bwana Ndege, hii ni hadithi ndefu sana” Fr Gichuru
akatulia kidogo kisha akaanza kumueleza kila kitu
mzee yule, hakumficha hata jambo moja, kuanzia
safari yake ya Roma mpaka aliporudi, mpaka
alivyotekwa na jinsi ilivyokuwa. Mzee Melchior
Ndege alitulia tuli kama maji ya mtungini,
alimwangalia yule kasisi asiye na kosa kisha
akakohoa kidogo.
“Father, mimi ndiyo niliyekuleta humu ndani, ndiye
niliyekutoa kule, wala si mbali ni mtaa wa tatu tu
hapo, nimekufuatilia kwa muda mrefu sana na hata
mpango wa wewe kutekwa mi niliujua mapema.”
Maelezo yale yalimshtua sana Fr Gichuru, alishindwa
kuelewa inakuwaje mzee huyo kumfuatilia na kujua
hata kutekwa kwake.
“Sijakuelewa bado bwana Melchior!” Fr Gichuru
aliuliza kwa mshangao
“Na hiyo nayo ni hadithi ndefu father Gichuru,
nitakwambia jiweke tayari” akachukua chupa yake
ya maji na kupiga mafunda kadhaa kisha akaiweka
chini na kuendelea, “Bill, ni mtu anayetafutwa sana
kila kona ya dunia hii, ni jasusi la kutisha la
kimataifa linalotumiwa na makundi mengi kuekeleza
mauaji au wizi wa kimataifa, hapa ninavyokwambia
tayari FBI wameshafika Kenya kwa ajili ya kumnasa
mtu huyu, Bill hawezi kuja hapa kwa kuitaka hiyo
monstrance tu kama alivyosema, ama kuna kitu
kingine nyuma yake au hiyo monstrance ina jambo
lingine ambalo ninyi hamlijui, mimi hapa usinione
mzee, mi siyo mzee” yule mzee aliposema hayo
aliingiza mkono wake ndani ya kofia aliyojifunika
ambayo ilikuwa imeunganishwa na jacket lake na
kwa kutumia nguvu alivua kitu kama gozi nene
usoni mwake na kulitupa chini kisha akajifuta vizuri
na kumtazama Fr Gichuru ambaye alikuwa
amepigwa na butwaa akmtazama kijana huyo
mtanashati kwa sura, kumbe alivaa sura bandia.
Siku chache zilizopita
SIMU ya mezani kwa Melchior Ndege iliita, mara
moja aliacha kazi aliyokuwa akiifanya na kuitazama
simu hiyo alisita kidogo kuipokea, lakini kelele za
simu ile zilimfanya aipokee
“Hello!” aliita
“…aa! Ok, sawa (…) sasa hivi nashughulikia”
Melchior aliinuka kwenye kiti chake na kuingia
kwenye lift iliyompeleka juu kama ghorofa tano hivi
katika jengo la KICC, aliuendea mlango Fulani na
kuufungua kisha kuingia ndani
“Karibu sana Ndege, keti, maana kwa jinsi
unavyohema itakuwa unahabari nzito” Gallus
Shikuku alimkaribisha Ndege ofisini kwake.
“Nimepata simu kutoka ofisi ndogo ya uwanja wa
ndege” Melchior alianza kuzungumza
“Mh niambie kijana!” alijiweka vizuri kitini na
kuiegemea meza yake kubwa akimtazama Melchior
Ndege.
“Mtu tunayentafuta kwa udi na uvumba ameingia
nchini, Bill”
Gallus Shikuku hakuamini anachokisikia kwa kijana
huyo alimkazia macho na kumuuliza tena swali
lilelile, naye akapata jibu lilelile.
“Bill…” Gallus Shikuku alilirudia jina hilo, “Kaja
kufanya nini tena? Kajileta mwenyewe” aliongea
peke yake.
“Ok! Ndege nimeisikia hiyo habari, sasa vijana
kazini, naomba umchunguze Bill anavyoketi na
anvyosimama na wakati huo mimi nawasiliana na
vyombo vyote vinavyomsaka ili tupate usaidizi
maana huyu mtu ni wa hatari sana na tukienda
vibaya anatumaliza.”
Melchior alitoka ofisini kwa boss wake bwana
Gallus Shikuku na kurudi ofisini kwake kujipanga
kwa kazi aliyopewa. Bwana Gallus Shikuku alijishika
kichwa na kuzunguka kutoka huku na huku, aliiona
sasa bahati imekuja kwao ya kumtia mkononi
mkorofi huyu, Bill, aliyeshindikana, FBI wanamtafuta,
Interpool wanamsaka kila kona ya dunia, lakini jinsi
anavyowatoroka ni utata mtupu, wengine wakadiriki
kusema ni mchawi lakini haikuwa hivyo.
Gallus Shikuku aliketi kitini na kuvuta laptop yake
na kufungua sehemu ya kuandika ujumbe, baada ya
kuhakikishiwa kuwa aliyeonekana ni Bill na watu
wake walio uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta
kumtumia picha za haraka na yeye kuzifikisha katika
kitengo maalumu cha utambuzi, picha hizo zilitoa
jibu lilelile, Bill Van Getgand. Shikuku alitoa taarifa
kwa vyombo husika vya usalama ambavyo tayari
vilisambaza habari na picha ya jasusi huyo popote
duniani atakapoonekana basi mara moja wataarifiwe
ili atiwe nguvuni.
Melchior Ndege aliondoka na kuliacha jengo la KICC
na kujichanganya mjini kadiri ya maelekezo
aliyopewa na watu wanaomfuatilia Bill, ili kujua ni
wapi amefikia. Haikuwa kazi kwani alimuaona mtu
huyu mnene akiwa na ile fimbo yake ya kutembelea,
mara hii Ndege alishtuka kidogo, hakuambiwa kuwa
huyu jamaa anatembea kwa msaada wa fimbo,
alichukua kamera yake kubwa aina ya Cannon
Cibershot na kumpiga picha kadhaa akiwa pale nje
ya Plazza Hotel akilipana na muendesha tax, mara
moja zile picha aliziingiza katika computer yake
ndogo na kuzituma kwa bosi wake na maelezo
machache.
Bill Van Getgand alipanga chumba namba 207
katika hotel hiyo, akiwa kaja Nairobi kwa kazi moja
tu ndogo ya kuhakikisha anaipata monstrance
aliyotumwa na tajiri wake kutoka Ujerumani, Don
Andreas, kwa pesa nyingi sana.
Melchior Ndege, aliweka vijana eneo lile kuhakikisha
wanapata nyendo zote za Bill mchana huo ili wajue
jinsi ya kumtega.
§§§§§
Melchior Ndege aliendelea kubaki pale nje ya hotel
hiyo akifuatilia kujua ni wakati gani bwana Bill
atatoka ili na yeye afanye kazi yake, alilolisubiri
likatimia, muda kama wa saa nne usiku hivi Bill
alitoka na kwenda kusikojulikana, alipopotelea na
gari hilo alilolikodi, Melchior alitoka katika gari yake
na kuchukua vifaa vyake vichache na kuelekea katika
hoteli ile, moja kwa moja hakupitia katika ofisi ya
mapokezi, aliingia katika lifti na kupanda mpaka
ghorofa ya pili, alikitafuta chumba namba 7,
haikuchukua muda alikipata, kwa kutumia funguo
zake maalum alicheza na kitasa kile na mlango ule
ukafunguka, akaingia na kuurudisha nyuma yake.
Akatazama kile chumba kwa macho ya kiintelijensia
kisha akakiendea kile kitanda kikubwa na kuivuta
droo ya kitanda hicho kisha kwa upande wa chini
akabandika kidubwasha maalum kisha akafanya
hima kutoka katika chumba hicho.
Alipofika chini, pale alipoegesha gari lake aliingia na
kuketi ndani, kisha akawasha chombo Fulani kama
simu na kuweka vidubwasha Fulani masikioni
mwake alibonyabonya vitu Fulani na kutulia,
haikuchukua muda Bill alirudi na mwanamke fulani
wakikokotana na kuingia ndani ya hotel hiyo.
Melchior aliwasha kile kidude chake na kujiwek
tayari kisha akalaza kiti cha gari yake na kusubiri,
mara baada ya sekunde kadhaa akaanza kusikia
mazungumzo ya mahaba yaliyokuwa yakitoka katika
chumba hicho, mara alisikia mikoromo ya raha za
dunia, akabonyeza kitufe cha kurekodi kila
kinachozungumzwa kisha yeye akajitupa katika
usingizi akiwa ndani ya gari hiyo.
Katikati ya usiku melchior ndege alishtuka kwa
simu iliyomuita ndani ya gari, aliitazama saa yake
ilikuwa tayari imetimu saa tisa kasoro robo usiku,
aliwasha mashine yake na kusikiliza machache
yaliyoongelewa chumbani humo, Melchior alipata
habari nyingi ambazo Bill alimshirikisha yule kahaba
Rose na kumshawishi aweze kumfanyia kwa malipo
ya pesa nyingi za kigeni. Mazungumzo yote
melchior alikuwa ameyapata katika chombo chake
kile. Alipogundua kuwa tayari ulikuwa ni usiku sana
aliamua kuondoka eneo lile.
Asubuhi siku iliyofuata aliwasilisha ripoti kwa boss
wake Bw Shikuku na kwa pamoja waliisikiliza kwa
makini na kupanga mikakati ya kazi ikiwamo
Melchior kusafiri katika ndege ambayo Fr Gichuru
angeitumia kwenda Roma kwani huyo bwana Bill
naye alipanga kusafiri kwa ndege hiyo ikiwa ni moja
ya njama zake za kujiweka karibu na kasisi huyo.
Mpango ukasukwa na kila kitu kikawa sawa kabisa,
Melchior Ndege akawa tayari kwa safari hiyo.
Akiwa ujerumani aliweza kumfuatilia vizuri sana mtu
mnene Bill nyendo zake zote na kujua ni nini na ni
nani aliyekuwa akionana nae mara kwa mara na kwa
nia gani, alipolijua na kuhakikisha kuwa hapo cha
kuhitaji, Melchior Ndege alichukua ndege na
kuelekea Roma Italy ambako alijichanganya na
watalii mbalimbali katika viwanja vya Vatican lakini
yeye akiwa na lengo tofauti kabisa, alipopata nafasi
ya kuingia ndani ya jengo hilo la kihistoria alijariu
kutafuta kama anaweza kuona muhusika yoyote
labda angemuuliza habari fulani fulani juu ya hiyo
Monstrance ambapo sasa ndicho alichogundua
kuwa Bill, mtu mnene ndicho hasa kilichomleta.
§§§§§
Yule mzee aliyekuwa sasa kijana alimtazama Fr
Gichuru aliyekuwa amepigwa na butwaa kwa habari
hiyo ambayo kwake ilikuwa kama riwaya nzuri
masikioni mwake, alimtazama kijana huyu na
kumuona hakika ni Malaika kwake.
“Na kuhusu kutekwa kwangu we ulijuaje?” Fr Gichuru
alimtupia swali yule kijana.
“Ndiyo maana nakwambia ni stori ndefu sana, mimi
nilijua kila kitu mpaka mpango wa wewe kuletwa
hapa, anyway, hatuwezi kumaliza yote hapa maana
muda nao unatuacha, mpango uliopo sasa kwanza,
tunataka tumnase huyu mtu mnene kwani yeye ni
jasusi linalotafutwa kila kona ya ulimwengu, kisha
wewe tukuweke kwenye usalama, hivyo basi mimi
na wewe tutatoka hapa na nitakupeleka sehemu
ambayo utakaa huko mpaka amri nyingine
itakapotolewa” Melchior Ndege alimaliza
kuzungumza na kuinuka pale alipoketi kisha
kujikung’uta vumbi katika zile nguo kuukuu.
“Sasa, unajua mimi ni Kasisi, hata kama nakwenda
huko lazima viongozi wangu wajue na kuna zana
ambazo ni muhimu kuondoka nazo kutokana na
mfumo wa maisha yangu” Fr Gichuru alitoa ombi.
“Yeah, najua sana juu ya hilo, lakini kwa sasa kama
wameshakuteka ujue hawatashindwa kukuua, kwa
hiyo wewe twende na taarifa kwa viongozi wako sisi
tutazipeleka kwa njia tunayoijua, maana kwa sasa
hatuamini mtu” Melchior aliendelea. Japokuwa
alijaribu kumbembeleza fr Gichuru lakini alikataa
katakata, alipendekeza arudi kwanza parokiani
kwake ndipo afanye taratibu kama hizo. Melchior
Ndege hakuona haja ya kupoteza muda, alimchukua
fr Gichuru na kupita nae katika vichocjoro kadhaa
kisha wakafika nyuma ya jingo moja kubwa,
kulikuwako hapo kituka kibanda lakini
kilichofunikwa na manyasi marefu yaliyorundikwa
baada ya kukatwa.
Ndege akapekua pekua na ndani yake kulikuwa na
pikipiki kubwa iliyofichwa hapo, akaitoa na
kuwasha, muungurumo wake ulieleweka kabisa
kuwa pikipiki hilo ni bidhaa ya Mjerumani BMW.
Wote wawili wakakaa juu yake na Melchior Ndege
akaliongoza kuelekea mjini. Moja kwa moja walifika
mbele ya kanisa kuu la familia takatifu, Nirobi mjini
na kumuacha hapo,
“Sasa, ukiwa tayari unifahamishe maana tunataka
usalama wako fr,” Melchior Ndege alimuasa.
“Sawa Melchior, na Mungu akubariki sana katika
hili,” alimalizia fr Gichuru na kuingia ndani ya wigo
wa kanisa hilo, wakati Melchior Ndege akiondoka
eneo lile na kurudi katika majukumu yake.
§§§§§
Kijua cha asubuhi kilianza kuchomoka katika
maeneo ya viwanda ya Nairobi kandokando ya
barabara ya Mombasa, walinzi waliopewa kazi ya
kumchunga Fr Gichuru walikwenda kumtazama ili
kuhakikisha kuwa yupo salama, walipofika
hawakuamini wanachokiona, mlango ulikuwa wazi
katika mtindo uleule kama Maria Magdalena
alipofika katika kaburi la Yesu alfajiri.
Wakatazamana, hawakuwa na lakufanya, wakatoa
taarifa haraka kwa wakubwa waliomleta mateka
huyo.
“Yaani aisee msilete ujinga, tunakuja sasa hivi”
ilikuwa ni sauti ya Blach Cheetah kwenye simu hiyo,
na mara simu ile ikakatwa.
Dakika kumi na tano, Black Cheetah, Mellina
Wanjiku na Bwana Gichui walifika pale godown na
kushuhudia hali hiyo, waliwaita walinzi wote pale
laikini mmoja hakuonekana,
“Mwenzenu yuko wapi?” lilikuwa swali kutoka kwa
Gichui kwenda kwa wale walinzi, hawakuwa na jibu,
walibaki kutazamana tu, “Nawauliza ninyi, walinzi
gain mpo hapa na mtu anatoroka? Ninyi mmekula
njama,” aliongeza kisha akawasukumia wote
kwenye kile kichumba na kuufunga mlango kwa nje.
Taarifa za kutoweka kwa fr Gichuru hazikumfurahish
a Bill mtu mnene hata kidogo, alihisi kuwa hiyo ni
njama na hasa kwa kuwa mlinzi mmoja
hakuonekana kati ya hao.
Pamoja na adhabu walizowapa walinzi wale lakini
hakuna kilichozaa matunda.
Bill aliwaita vijana wa kazi katika kivhumba kidogo
ndani ya godown hilo na kuwapa kazi ya kumsaka
popote alipo Fr Gichuru na atakapoonekana hakuna
cha kusubiri ni kumuondoa uhai tu na mambo
mengine yatafuatia.
“Sasa tukimuua ndiyo tutapata hiyo monstrance?”
Mellina aliuliza.
Bill alibaki kimya kwa swali hilo kisha akamtazama
Cheetah na Gichui, akimaanisha watoe wazo hapo
cha kufanya.
“Sikia, yule Gichuru ameshajua mengi juu yetu, sasa
tukimuacha atatoa siri polisi, halafu mission
itashindikana. Hivyo tunamuua kisha tunavamia
kanisa ki-ambush na kuchukua tunachokitaka” Black
Cheetah aliwaeleza wanzake.
“Safi!” Bill mtu mnene alimpongeza.
Baada ya kikao hicho kifupi, walitawanyika na
kuanza kazi ya kumsaka kasisi huyo.
Alfajiri ya siku iliyofuata…
“Baba, mimi leo sijisikii vizuri, mwili wote unaniuma
sana, naomba unisaidie kigangoni kwa misa mimi
nitabaki hapa” fr Gichuru alimuomba paroko wake fr
Joe Simith
“Kwa kweli fr inabidi ubaki, kwani hawa maharamia
wanaweza kukukamata njiani, ubaki hapa mimi
nitakwenda kigangoni”. Baada ya makubaliano hayo
fr Joe alichukua gari ya mission na kuondoka zake
na kumuacha Fr Gichuru akisubiri muda wa ibada
saa kumi na mbili kamili asubuhi.
Fr Gichuru alivalia kanzu yake nyeusi na kofia ya
kikasisi nyeusi yenye nyoya jeusi katikati, mkononi
akiwa na rozali yake aliterenka ngazi taratibu ili
apate muda wa kusali alfajiri hiyo kabla hajaingi
katika misa. ‘Moyo wangu una huzuni kiasi cha
kufa’ alijiwazia wakati amesimama kwenye ngazi za
nyumba yao, kisha kwa hatua za taratibu aliteremka
na kukanyaga uwanja wa kanisa hilo kongwe, ‘Baba
ikiwezekana kikombe hiki kinipitie mbali,’ aliendelea
kupata tafakari hii ya uchungu, hatua chache
alisimama, ‘ Lakini si kwa mapenzi yangu bali yako
yatimizwe.’
Subaru ya kijivu ilikuwa imesimama karibu kabisa
na barabara ipitayo mbele ya kanisa hilo kubwa,
hata fr Joe alipopita hapo aliiona lakini hakuitilia
maanani. Nadni ya gari hiyo kulikuwa na watu
watatu, awili wanaume na mmoja mwanamke.
Black Cheetah aliitazama saa katika dashboard ya
gari hiyo, ilikuwa tayari ni saa kumi na moja alfajiri
akamwambia Gicui aliyekuwa nyuma ya usukani
huo, “Twende sasa, mlinzi atafungua tu huu muda ni
sawa,” kwa mwendo wa taratibu Gichui aliielekea
geti kuu na alipofika getini kwa mbali aliona vivuli
kama vya watu, akawasha taa katika mtindo wa full
na kuwamulika, alikuwa ni sista na fr, akawasha
tena taa mara kadhaa katika mtindo huo. Yule
kasisi akalisogelea geti kutazama kulikoni, alifika
getini na kusimama akilitazama gari hilo. Milango
ikafunguliwa, Black Cheetah akatoka akiwa ndani ya
koti lake jeusi na kulielekea geti, sasa uso kwa uso
na fr Gichuru.
“Kwa kosa ulilolifanya la kututoroka, jua la leo si
halali wewe kuliona” Black cheetah, alimueleza fr
Gichuru huku akiondoa usalama wa bastola yake na
kuruhusu risasi niingie katika chemba, fr Gichuru
aliutazama mdomo wa bastola ile,
“Si kwa mapenzi yangu, bali yako yatimizwe” Fr
Gichuru alisema mara hii kwa sauti iliyoweza
kusikiwa na Black Cheetah pekee, mkono wa
jambazi huyo ulikuwa ukitetemeka hata kutaka
kupoteza nguvu.
“Black Cheetah, unachelewaaa!” ilikuwa sauti ya
Mellina ikimstua Black Cheetah na bila ajizi vidole
vyake vikapata nguvu na kufyatua trigger ya ile
bastola, risasi mbili zilipenye katika kifua cha kasisi
huyo na kumnyayua kabla ya kumbwaga chini chali
na mifereji ya damu kuanza kuchuruzika kutoka
mgongoni alaikolalia.
Kwa mwendo wa kasi ile Subaru iliondolewa mahali
pale na kusababisha kelele za tairi pindi ilipoingia
barabarani.
Fr Gichuru hakuwa na nafasi hata ya kuomba maji,
“Yametimia, Baba mikononi mwako naiweka roho
yangu” alitamka maneno hayo kwa shida huku damu
nyingine zikitoka kinywani na kisha kichwa chake
kikaelemea uapnde wa kushoto na kukata roho.
4
INSPEKTA Saitoti alikuwa akigongagonga kalamu
yake mezani kwake huku akionekana wazi kuwa
kichwa chake kilikuwa na mambo mengi sana
ambayo kwa namna moja au nyingine
yalimchanganya kichwa., mara alivuta kabrasha hili
mara lile lakini hakujua anachotaka kufanya kwa
muda huo, akiwa katika hali hiyo aligutushwa na
hodi iliyogongwa mlangoni mwake kisha
mwanamama mmoja aliyevalia kiraia aliingia kwa
ukakamavu na kubana miguu yote miwili kuonesha
nidhamu ya kijeshi.
“Jambo afande?” Inspekta asitoti alisabahi
“Jambo!” alijibu yule mwanamke au kana
anavyojullkana Sargeant Maria, “Afande natoa taarifa
ya kuumia afande Otho’ katika mapano na moja kati
ya majambazi tunayoyatafuta”
“Oh! Pole sana afande, nieleze kwa kina,” Inspekta
Saitoti aliomba aelezwe huku akimpa ishara ya
kuketi kitini sergeant Maria.
Alipokwishakueleza kinagaubaga kila kilichojiri,
alitulia kitini kimya akisubiri amri ya boss wake
itasema nini, mara Inspekta Saitoti alikohoa
kuashiria kuuvunja ukimya ule.
“Ok! Sasa kutokana na hilo, naomba afande Otho
nimuondoe kwenye operesheni hii na nikupe kijana
mwingine machachri wa kukusaidia, koplo Kariithi,
au we unasemaje?” alimuuliza huku akimkazia
macho,
“Sina neno afande, kijana yupo kamili na anaweza
kazi,” Maria alijibu kwa sauti ya ukakamavu hasa.
“Ok basi nitampa taarifa na mara moja ataungana
na wewe katika hili, hakikisheni tunawatia mbaroni
wauaji ili sheria ichukue mkondo wake,” sergeant
Maria alisimama na kubana miguu yake sawia,
“Sawa afande!” alijibu, akageuka na kutoka nje.
Inspekta Saitoti alibaki tena peke yake mle ofisini,
sasa hakuwa anagongagonga ile peni tena pale
mezani bali alikuwa akibofya namba za simu yake
ya mezani na kuweka kile kisikilizio sikioni mwake
kusubiri sauti ya upande wa pili iongee lolote.
Alipokwisha kuongea na mtu wa upande wa pili
alitulia tena kitini na kufungua runinga yake ndogo
iliyowekwa ofisini humo na kufuatilia habari za
kimataifa. Mara mlango uligongwa na
alipomkaribisha mgongaji, aliingia kijana wa
makamo, mwenye kadiri ya miaka kama ishirini na
minane hivi, mwenye siha nzuri ya kuvutia,
aliyejengeka kimazoezi, alisimama mbele ya
Inspekta kikakamavu, Inspekta Saitoti alimtazama
kijana huyu, kisha akavuta motto wa meza na kutoa
bahasha ya khaki akamkabidhi, na maneno
machache yakafuatia ya kumpa majukumu ya
afande Otho ambaye kwa kipindi hicho alikuwa
hospitalini akiuguza jeraha lake. Kariithi alirudi
nyuma hatua mbili na kupiga mguu chini kisha
akageuka kikakamavu na kutoka nje ya ofisi ile.
§§§§§
Sergeant Maria alikuwa akimuelekeza mambo Fulani
Fulani koplo Kariithi juu ya wapi wameishia na nini
cha kufanya juu ya sakata hilo la mauaji ya Kasisi.
“Ok, mi nafikiri sasa cha kufanya ni kufuatilia
nyendo za hawa jamaa ili tuweze kuwatia mkononi”
Kariithi alitoa ushauri.
“Ni sawa, lakini bado hatujajua adui yetu anapenda
kuonekana wapi,” Maria alieleza dukuduku lake
katika hilo.
“Nimekuelewa afande, hapa kuna sehemu kubwa
nne za kufanya doria, Dagoreti Corner, Kawangware,
Korogocho na Uthiru Kenoo, nafikiri tukifanya doria
kali pande hizo tunaweza kama si kuwatia mkononi
basi kupata japo harufu yao” koplo Kariithi alieleza
kwa kujiamini na mkakati ukapangwa wa kufanya
doria ya kimyakimya maeneo hayo yote.
Ulikuwa ni usiku wa balaa katika mitaa hiyo, hakuna
aliyekamatwa kwa maana polisi hao waliwajua
wanaowatafuta, hawakufanya kamatakamata kama
za huku kwetu Bongo.
Uthiru Kenoo…
“Leo hii lazima tumalize kazi!” Cheetah aliwaambia
wenzake huku aking’ata pande kubwa la mutura na
kulishushia na tusker, akabeua na kuwatazama
wenzake kwa zamu, “Maisha hayana guarantee, hasa
haya yetu, Bill atatulipa pesa nyingi sana ukizingatia
pesa tu aliyomlipa yule kahaba Rose ni ndefu
itakuwaje kwetu sisi?”
Mellina alionekana kuwa mbali kabisa kimawazo,
walipomgutusha wenzake alionekana kama mtu
aliyetoka katika usingizi,
“We vipi? Mbona hauko nasi kabisa?” Wambugu
alimuuliza
“Ah! Nafsi yangu inanisuta sana, hivi kwa nini
tunafanya unyama huu kwa sababu ya pesa?
Tumemuua kasisi wa watu bila kosa,” Mellina
alionekana kusikitika sana.
“Aaa ha ha ha ha Mellina, wewe ni jambazi wa kike,
muuaji ambaye hata Mungu hana muda wa
kukusamehe, leo hii ujutie kifo cha mtu mmoja, mtu
asiye na faida, hana watu wanaomtegemea wala
nini, pesa pesa Mellina, hata Yuda Iskariote alimtoa
Yesu auawe kwa vipande thelathini vya fedha, nini
wewe!!!” Cheetah aliongea huku akiwa amesimama
akigonga meza yake kwa ngumi, tayari pombe
ilikuwa imekwishafanya kazi yake kichwani, alihema
kwa nguvu na kuwatazama tena kwa zamu,
“Ninawaamini sana vijana wangu, kwa kuwa Mellina
ameonesha mashaka sasa nabadili program, leo hii
tunaenda kuibeba hiyo Mostrance, lazima ipatikane,
kwa udi na uvumba, kama jina la riwaya ya Innocent
Ndayanse, leo hii ili kesho Bill atupe dolari zetu na
kila mtu atawanyike kivyake, kama kukamatwa na
akamatwe kivyake,” amakweli pombe mwana
haramu, Cheetah alitoa bastola yake na kuifutafuta
vumbi hakujali kama watu walikuwa wakimwangalia,
Wambugu akainuka na kumnyang’anya ile bastola
kisha kumvutia nje na kumuingiza kwenye gari,
alishaona kuwa sasa Cheetah hakuwa yeye.
Mellina alikaa nyuma ya usukani na kutaka kuiondoa
gari ile lakini alikuta mbele yake kuna watu wawili
wamesimama wakimtazama, ‘Polisi’ alijiwazia huku
akikanyaga clutch na kutumbukiza gia ya kwanza,
alipoanza kukanyaga accelerator wale polisi
wakatoa bastola zao tayri kwa mashambulizi,
“Shiiittt!” Mellina alikanyaga mafuta kwa nguvu na
huku bado mguu haujatoka sawasawa katika clutch
na kuuzungusha usukani, norinda iliyotokea hapo
haikuwa ya kawaida, vumbi lilitimka usiku huo na
watu walio jirani walisikika wakipiga mayoe ya
woga, Cheetah na Wambugu tayri bastola mikononi
wakishambulia upande ule walipo wale askari, lakini
umahiri wa Mellina katika usukani uliwafanya
wakose shabaha, ile Subaru iliizunguka na kuingia
barabarni kisha Mellina akatumbukiza gia ya pili
mara ya tatu na kuwaacha watu midomo wazi.
Mwendo haukuwa wa kawaida kuelekea mjini huku
baadhi ya gari ya polisi zikifuata nyuma kwa kupiga
ving’ora ili kupisha njia kumbe kwa jinsi hiyo
walimpa mwanya Mellina kuchanja mbuga, dakika
kama tano kulikuwa na pengo kubwa kati ya polisi
na Mellina.
“Weka gari pembeni,” aliamuru Cheetah kisha
akafungua mlango na kuwaamuru wenzake
kumfuata, wote walitoka na moja kwa moja
wakaenda katika maegesho ya NAKUMATT
supermarket maeneo ya Westland na kuingi kwenye
Toyota Prado, kwa kutumia funguo za bandia
waliiwasha ile prado na kuitoa pale maegeshoni na
kuileta barabara kubwa, waliyaacha mafgari ya
polisi yapite kisha wao wakaingia nyuma yao na
kufuata taratibu.
“Sasa tunakwenda moja kwa moja kuchukua ile
Mostrance sasa” Cheetah aliamuru na kila mmoja
akajiweka sawa kwa hilo, bastola zilizoshindiliwa
risasi za kutosha zilikuwa tayari mikononi na viunoni
mwao.
§§§§§
“Ah!” koplo Kariithi alitikisa kichwa kwa kuchelewa
kufika eneo la tukio,
“Vipi koplo?” sergeant Maria alimuuliza huku
akiweka vizuri jacket lake.
“Yaani ningewapata hawa leo, nakuhakikishia afande
ungeijua shabaha yangu leo” Kariithi alimueleza
huku akivuta hatua fupifupi kuwaelekea wale polisi
wawili waliokuwa pale kwa doria ambao ndiyo
waliwapigi redio ili wafike hapo.
“Siku yao ipo! Usiku huu halali mtu mpaka tuwatie
mkononi kwa gharama yoyote ile” sergeant Maria
alimueleza koplo Kariithi. Kishapo wote wakaingia
garini na akabla hawajatoka eneo lile walipata
taarifa kuwa gari aina ya Subaru forester iliyotumiwa
na majambazi hao imeonekana maeneo ya
Westaland imetelekezwa, nao wote wakaenda hapo
kuiona, kama walivyoambiwa waliikuta pale
imetulia.
“Koplo, tunapambana na watu makini, tujiweke
vyema” Maria alimtahadaharisha Kariithi.
Wakiwa wanajiandaa kuondoka wakati huohuo polisi
wakifanya mchakato wa kuiwekea mtego ile gari
labda watarudi kuichukua, mara walikatishwa na
kelele kutoka katika maegesho ya supermarket hiyo.
“Oooh my car my car” (Oooh gari yangu, gari
yangu), Sergeant Maria alitega sikio na kushuka
katika gari yao kisha akaelekea kule kwenye ile
kelele, mama mmoja wa kizungu alikuwa akilia kwa
uchungu kuwa gari yake imeibwa, sergeant Maria
alimtuliza na kumuuliza maswali machache kisha
akamchukua na kwenda nae kituo cha karibu kwa
ajili ya kuanza uchunguzi, alipokwishamkabidhi kwa
wahusika, akarudi garini na kumkuta Kariithi akiwa
bize kusikiliza muziki uliokuwa ukipigwa ndani ya
gari hiyo, aliingia na kujifungia mlango.
“Koplo, kwa vyovyote Cheetah na wenzake wameiba
ile gari,”
“Nilikuwa nafikiri hivyo pia, afande huu lazima uwe
usiku wa kazi” Kariithi alisisitiza.
“Endesha gari!” Maria aliagiza
“Twende wapi afande?”
“Twende tukabane karibu na kanisa kuu kwa muda
kidogo tukisubiri taarifa nyingine, labda tutaokota
kitu huko.” Kariithi akaitoa ile gari kujiunga na
magari mengine kuelekea katikati ya mji. Ilikuwa
imetimu saa nne usiku, bado foleni ilikuwa kubwa
ya magari katika jiji la Nairobi.
ITAENDELEA....
:::: UKIITAKA RIWAYA HII IPATE KWA 3000
TU!:::::::
:::: KUJIUNGA NA WHATSAPP GROUP NI SH 2000
TU NA ADA YA 500 KILA MWEZI ::::::::
NITAFUTE WASAP AU SMS 0766974865
 
Ngumi ya hasira ilitua juu ya meza ya chuma katika
chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya
Nairobi, huku akiuma meno aliuangalia mwili wa Fr
Gichuru uliolala kwenye kitanda hicho ukiwa ndani
ya mfuko maalum wa plastiki.
“Bill, Bill, Billllllllll !!!!! lazima ulipe kifo hiki kwa
gharama yoyote,” Melchior Ndege alijikuta akiongea
peke yake mle ndani ya chumba kile kidogo cha
kuhifadhia maiti.
Hali ya utulivu ilitawala nje ya eneo la jingo hilo
kubwa, watu waliokaa kwa utulivu kwenye vibenchi
vidogo vilivyowekwa maalumu kwa kazi hiyo.
Melchior Ndege alitoka akiwa kama mtu
asiyejielewa na moja kwa moja aliingia kwenye gari
yake na kuliacha eneo hilo kurudi ofisini.
Aliketi na kutulia akiwa na mawazo mengi sana juu
ya hili sakata, sasa aliona kuwa kazi inaanza rasmi,
kumsaka Bill na genge lake, kujua ni nani yuko
nyuma ya Bill katika hili.
Mlio wa simu ulimshtua Melchior mawazoni,
akaitazama simu ile iliyokuwa ikipiga kelele bila
kunyamaza, akainyanyua na kuiweka sikioni,
hakuongea kitu bali alijaribu kusikiliza sauti ya
upande wa pili, nako kulikuwa kimya, walitegeana.
Zaidi ya kusikia pumzi inayopanda na kushuka
kutoka upande wa pili, melchior hakuna alichosikia
kutoka kwa mpiga simu, akaitua taratibu na
kuiweka mezani bila kuirudisha kwenye kitako
chake na kuifanya iendelee kuwa hewani, zaidi ya
hilo alibofya kitufe cha kuruhusu sauti isikike kwa
nguvu ‘loud speaker’ kisha akajituliza kitini.
Akishika hiki na kile juu ya meza yake mara mlango
uligongwa na kufunguliwa na mgongaji aliyejitoma
ndani bila kukaribishwa, hakuwa mwingine ni yule
boss wake bwana Shikuku aliyeingia akiwa amefura
kwa hasira ambayo ilimtisha hata Melchior,
akajitupa kwenye kiti cha upande wa pili na
kushusha pumzi ndefu,
“Mr Ndege, FBI wapo hapa” alimwambia Melchior
ambaye alionekana kushtushwa kidogo kwa taarifa
hiyo
“Oh shit, wataharibu mipango yetu” Ndege alimjibu
huku akiiweka kalamu yake mezani na mkono
kuuelekeza shavuni.
“Sio wataharibu, wameshaharibu,” bwana Shikuku
alitamka hayo huku akitikisa kichwa, kisha
akamuangalia melchior na kumwambia,
“Wameshatuomba tujitoe kwenye huu mkakati ili
wao wafanye kazi ya kumnasa bwana Bill,
wameniuzi”
“What?!” bwana Ndege aliuliza kwa mshangao
mkuu.
“Ndiyo hivyo,” Shikuku akajibu kwa mkato huku
akiangalia pembeni.
“Bill hawezi kuondoka mikononi mwetu kijingajinga
wakati tunajua wazi jinsi alivyoendesha mambo ya
kijasusi katika Afrika Mashariki, na sasa yupo kwetu
tena, kule Tanzania alitoroka hatukuweza kumtia
mkononi kwa sababu hizi hizi, sasa na leo tena
haiwezekani,” Melchior aliongea kwa uchungu, kisha
akatulia na baadaye kumtazama boss wake, “Bill
nitamtia mkononi kabla ya wao kufanikisha hilo”
alimwambia boss wake huku akifungafunga vitabu
vyake, akasita kidogo na kusema, “Lazima tujue
nyuma ya mauaji ya kasisi kuna nini, mpaka Bill
ahusike, tusipompata Bill hatutaweza kutatua juu ya
kifo hiki cha utata, mimi nina mwanzo wa mkasa na
Bill ana hatima ya mkasa, lazima nimpate mimi na
siyo FBI.
5
DAR ES SALAAM
TANZANIA
MVUA kubwa iliendelea kunyesha katikati ya jiji la
Dar es salaam, maji yalizijaza barabar zote na
kufanya ugumu wa watembea kwa miguu kuonekana
dhahiri, akina mama viatu mkono wakizikunja nguo
zao kwa juu huku mifuko ya plastiki ikiwa imefunika
vichwa vyao ili kuokoa nywele za gharama
zisiharibike, magari nayo yalipita shida kwa namna
moja au nyingine, yakitumbukia kwenye mashimo ya
liyojitengeneza kutokana na mvua hiyo, basi jiji lote
lilikuwa vururuvururu. Kila mtu alionekana kuchukia
hali ile ambayo serikali inaifumbia macho mara
zote, shida kubwa ikawa kwa wale waishio
mabondeni waliokuwa wakifukuzwa kila siku tangu
enzi za mheshimiwa Makamba lakini waling’ang’ana
utafikiri walizaliwa hapo, huyu akisonya, yule
akimkashifu kiongozi Fulani wa chama na serikali.
“Bora tuwachague wapinzani mwaka ujao”
mwingine alisikika akisema hayo huku akiwa juu ya
moarobaini uliokuwa ndani ya maji nusu nzima.
Ilhali anasahau kuwa mvua hizo ni mabadiliko ya
tabia nchi ambayo mimi na wewe ndio visababishi.
“Ila mi Mabwepande ndio siendi” alijibiwa na yule
aliyekuwa juu ya paa lanyumba iliyochoka ambayo
kwayo uhai wake ulifika tamati, alisahau kabisa
kuwa haikomoi serikali bali anawaumiza watoto
wake ambao hakuhusika katika kuchagua eneo la
kuishi.
Wakati upande mwingine watu wakiwa wamejazana
katika daraja kubwa la Tabata Matumbi wakivumilia
harufu kali ambayo ilisemekana ni ya mwili wa
binadamu uliokwama katika maji yam to Msimbazi
huku jeshi la polisi likisaidi kazi hiyo, wengine
walikuwa wakichanganya vichwa, akili na mawazo
yao vikiwa tofauti na matakwa ya mioyo yao.
Ndani ya jengo la JM MALL, ghorofa ya saba
mlango namba 705 ni watu wawili tu mwanamke na
mwanaume walikuwa wameketi wakitazamana
mmoja akishindwa kuamua na mwingine akishindwa
kushauri nini cha kuamua. Wakiwa bado katika
kushangaana wawili hawa mara mlango ulifunguliwa
na bibi mmoja wa makamo ambaye nywele zake
zilishahitilafiana na weusi wake wa asili na kuubeba
weupe ambao wengi hupenda kuuita mvi, aliingia
moja kwa moja na kuketi kwenye kiti kikubwa
ambacho kilikuwa pembeni kidogo ya meza ile safi
iliyozungukwa na mapambo murua ambayo ukiketi
basi yatakupa burudani ya macho na kuondosha ile
ambayo muandishi wa kitabu cha SHIDA, Ndyanao
Balisidya aliita ‘kiwi cha macho’.
“Karibu Madam S” Kamanda Amata alisimama na
kupeana mkono na mwanamama huyu aliyebobea
kwenye kazi za kikachero tangu usichana wake.
“Nimekaribia Kamanda” akajibu huku akijiweka
vizuri pale kochini ambapo aliweza kuonana na
mrembo aliyemkuta ofisini humo. Mara baada ya
kujiweka sawa alimtzama Amata na kumpa bahasha
moja ya khaki ambayo juu yake imeandikwa
maandishi yanayoitambulisha kuwa ni mali ya
serikali, akaitupia mezani na Kamanda Amata
akaichukua na kuifungua, baada ya kuisoma
akaitupia mezani,
“Nairobi tena! Kuna nini madam?” Kamanda Amata
aliuliza
“Mauaji ya Kasisi, jasusi Bill Van Getgand yuko
Nairobi, FBI na taasisi nyingine za kikachero
zimetuma watu wao kumnasa, lakini sifikiri kama ni
vyema wakamchukua ndani ya ardhi yetu wenyewe,
huyu ameshatekeleza mambo Fulani ya kijasusi
katika nchi yetu na zingine za Afrika Mashariki”
madam S alikuwa akiongea bila mapumziko
akionekana wazi amehamanika kwa hilo.
“Madam, mi niko safarini,” kamanda Amata alitoka
katika meza yake na kuchukua vifaa vyake vichache
vya kiofisi, akamwita Gina na kumpa maagizo
Fulani Fulani ya kiofisi kisha akatoka na madam S,
boss wake wa miaka mingi na kuondoka zake.
§§§§§
BOEING 737 ilishuka katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta. Ilikuwa alasiri tulivu
uwanjani hapo palipoonekana kuwa na ulinzi mkali
wa polisi na ule wa vyombo binafsi vya ulinzi.
Baada ya itifaki zote kukamilika, kamanda Amata
alitoka nje na kukamata tax moja kabla ya kuamua
wapi anataka kwenda mchana huo. Alijiweka katika
saiti ya nyuma na kumwambia dereva ampeleke
katika hoteli kubwa ya nyota tano katikati ya jiji hilo
la Nairobi.
Kamanda Amata alifika katika Hotel Intercontinental,
katika mtaa wa Posta na kuweka kambi yake hapo
akiwa naa kazi moja tu aliyotumwa na serikali yake
ama kumkamata Bill ili ajibu kwa yale aliyoyafanya
siku za nyuma au uhai wake ubaki Afrika Mashariki
na mwili wake urudi kwao, ilikuwa ni moja kati ya
hayo lililotakiwa kutekelezwa. Amata alitupia begi
lake kitandani na kuchukua kifaa chake maalum
kilichoweza kung’amua kama humo ndani kuna aina
yoyote ya mlipuko au chombo chochote
kitakachoweza kuhatarisha maisha yake, aliporidhika
na usalama wake, akalisogelea dirisha kubwa na
kuvuta kidogo pazia lake na kutupa macho yake nje
upande wa chini ambako pilikapilika za wakazi wa
Nairobi waliokuwa wakirudi majumbani kutokea
makazini zilikuwa kubwa, kana kwamba hakuridhika
na kile alichokua akikitazama alivuta kibegi chake
na kutoa kiona mbali na kukisogeza karibu na
macho yake, naam kile alichokiangali kilikuwa
kikionekana kwa uzuri wa hali ya juu, vijana
waliokuwa wakijidunga madawa ya kulevya katika
moja ya mitaa hiyo ulioonekana wazi kuwa haukuwa
ukitumika na wapita njia, alitazama kwa makini
vijana wale walivyojidunga mpaka kuanza kusinzia
pale chini, Amata alitikisa kichwa kwa masikitiko,
‘Nguvu kazi ya taifa inatoweka’. Akiwa katika
kutafakari hayo mara alisikia ving’ora vya polisi na
kufuatiwa na gari mbili zilizopita kwa kasi kuelekea
upande wa pili wa eneo hilo, ‘Shughuli za kiusalama
hizo’, alijiwazia kwa mara nyingine na kutoka pale
dirishani kisha kuketi katika kochi moja lililopo pale
chumbani. ‘Bill Van Getgand, umekuja tena, sasa
hakika hutoponyoka kwenye mikono hii,’ akaivuta
laptop yake na kuanza kuperuzi habari mbalimbali
za jasusi huyo, akirejea hasa yale matukio
yaliyofanywa na mtu huyu pale Dar es salaam …
Miaka mitano iliyopita
Kilimanjaro Hotel
KAMANDA Amata aliuangalia mwili usiokuwa na
uhai uliokuwa ukielea katika bwawa la kuogelea la
hoteli hiyo kubwa ya kimataifa iliyopo pembezozi
mwa bahari ya Hindi. Watu kadhaa walizunguka
eneo hilo wote wakiwa wametokwa na hamu ya
kujiburudisha kwa maji hayo ambayo sasa yalikuwa
mekundu kwa damu ya mtu huyo aliyeonekana kuwa
na asili ya America. Akiwa amepiga goti moja pale
katika ukingo wa bwawa hilo, kamanda Amata
aliinua kichwa chake na kutazama uelekeo ambao
labda muuaji alikuwapo, kwa maana mtu huyo
aliuawa kwa risasi iliyotoka katika bunduki aina ya
Sniper Rifle ya Kimarekani, naam macho yake
yalitua mahali sawia, dirisha moja lililokuwa katikati
kama ghorofa ya nane hivi katika jingo lililokuwa na
benki ya Meridian Biao enzi hizo. Alipotuiliza macho
yake alishuhudia pazia la dirisha hilo likifungwa
ghafla kana kwamba aliyekuwa hapo dirishani
alikuwa akimtazama Amata pia. Ili asimpoteze
maboya mtu huyo Kamanda Amata kwa kutumia
simu yake maalum iliyounganishwa na saa ya
mkononi alipeleka ujumbe wa sauti kwa Madam S
aliyekuwa upande wa pili wa jingo hilo, nae bila
kusita alituma kikosi cha watu wanne kwenda
kufanya uchunguzi katika ghorofa hiyo.
Hisia za Amata hazikuwa bure, jasusi Bill Van
Getgand lilikamilisha kazi yake kupitia ofisi ya mtu
Fulani ndani ya jingo hilo kwa kutumia bunduki ya
Sniper Rifle, wakati vijana wale wakigawana
majukumu mmoja apande kwa lift, mwingine kwa
ngazi ya kawaida na wengine wabaki nje kutazama
kinachoendelea, ndipo yule aliyepanda kwa ngazi
alipopishana na Bill aliyekuwa akishuka huku
akitanguliwa na mwanadada mmoja mwenye umbo
dogo aliyekuwa amebeba koba kubwa la kuhifadhia
guitar lakini akiwa kwenye hali ya kutojiamini, yule
afisa usalama alitulia kidogo na kuwaangali huku
akipishana nao na mara hiyo akatoa taarifa kwa
walio nje kumwafuatilia watu hao bila kuwapoteza.
Kwa uchunguzi wa muda mfupi uliofanyika katika
chumba kilekile ambacho Amata alikihisi tangu
mwanzo liliokotwa ganda moja la risasi ambayo ni
ile iliyotumika kumuua bwana yule.
Kamnda Amata alilitazama ganda lile na kutikisa
kichwa kukubali hisia zake.
“Mnasema mmeweka watu wawafuatilie hao
mnaowahisi?” aliwauliza wale vijana chipukizi katika
kazi hiyo.
“Ndiyo na tunatumaini bado wanawafuatilia” alijibu
mmoja wao. Kamanda Amata akainua simu yake ya
upepo na kuwauliza vijana wale waliopewa kazi,
“Ndiyo, tupo hapa Red Carpet Upanga, wameingia
ndani na bado hawajatoka, gari yao ipo hapa nje
inawasubiri,” jibu lilimridhisha Amata, aliingia garini
na mara moja kuelekea Upanga, akawakuta vijana
wake wakiwa wametega pa si kuwaona watu hao,
masaa mawili yalikuwa yamepita, Amata aliteremka
na kuzunguka lile jingo la ghorofa mbili na alipofika
nyuma yake alitikisa kichwa kwa kuugundua
upumbavu wa vijana hao waliobaki ndani ya gari
wakati nyuma ya jingo kuna ngazi zinazoweza
kumtoa mtu yoyote aliye ndani ya jingo hilo, akarudi
mpaka mbele na kuwapa taarifa hiyo ambayo
iliwafanya wafadahaike sana kwa ujinga
walioufanya.
Hakika Bill Van Getgand alikuwa ametokea upande
wa pili pamoja na yule mwanadada na kuchukua tax
iliyokuwa imeegeshwa huko nyuma na kuondoka
zao mpaka uwanja wa ndege ambako walichukua
ndege na kuelekea Nairobi.
Baada ya kumsukasuka yule dereva wa tax
aliyewabeba Bill na yule mwanadada hakuna jibu la
maana walilopata zaidi ya kubaki na lile koba la
gitaa ambalo ndani yake kulikuwa na bunduki
kubwa iliyotumika kwa mauaji yale lakini hakukuwa
na guitar, baada ya uchunguzi wa hali ya juu
kufanyika uliohusisha vyombo mbalimbali vya
kiintelijensia ilionekana Bill amehusika na mauaji
hayo na si sehemu moja tu basil maeneo
mbalimbali duniani, nah ii iliifanya nchi yetu kuingia
kwenye matatizo ya kimahusiano na nchi husika ya
mrehemu yule kwani iligundulika alikuwa ni mtu
muhimu serikalini ambaye alikuja kwa shughuli za
kiserikali na kufikia hapo hoteli ya Kilimanjaro.
Rejea Nairobi Intercontinental Hotel…
Kamanda Amata aliishusha picha ndogo ya Bill
aliyokuwa akitumbulia macho na kuirudisha kwenye
kikoba maalum. Mara kengele ya mlango wa
chumba chake ikagongwa, akanyanyuka taratibu na
kuuendea mlango huo huku bastola yake ndogo
ikiwa mkononi mwake, akiwa kaificha kwa nyuma
alimruhusu mtu huyo kuufungua mlango.
Mwanadada mwembamba, mrefu wa wastani
aliupenyeza mwili wake ndani ya chumba cha
Amata, Amata alimeza mate ya uchu hasa
alipokutana macho na paja mwororo la mwanadada
huyo ambalo lilibaki wazi baada ya sketi yake
iliyofungwa kwa vifungo upande wa kulia kulipa
nafasi paja hilo kuonekana, kiuno chake kidogo
kilibeba kajiumbo ka wastani, si kanene sana, lakini
kenye mvuto mahsusi kwa mwanaume yoyote rijali,
mikono ya Amata ilipoteza nguvu na kuiruhusu ile
bastola yake kurudi mfukoni bila kutarajia, macho
yake yalikuwa yakitalii kifua cha mwanadada huyo
ambapo blauzi aliyoivaa yenye vifungo vichache
mbele iliruhusu nusu ya titi lake ambalo
halikuhifadhiwa kwa sidiria kuonekana na kumfanya
kamanda kuinuka kutoka pale alipoketi na
kumjongelea mwanadada huyu, kabla hajamfikia,
yule msichana aliweka magazeti aliyokuwa nayo
mkononi juu ya meza ya kioo iliyokuwa hapo ndani.
“Wakati unasubiri kuonana na mwenyeji wako,
usome magazeti haya!” sauti tamu ya yule dada
iliyapenya masikio ya Kamanda Amata. Baada ya
kuyaweka magazeti hayo pale mezani, aligeuka na
kutoka nje huku macho ya Amata yakimsindikiza
kwa kila hatua aliyoivuta, alitoka na kuurudishia
mlango nyuma yake. Amata alibaki kapigwa na
bumbuwazi, ‘Mwenyeji, mwenyeji wangu,’ alijiuliaza,
kengele za hatari zikalia kichwani mwake, akainama
kuchukua yale magazeti lakini kabla hajayachukua
kutoka pale mezani, akasita, akatazama saa yake,
muda ulikuwa umekwenda sana, akaachana nay ale
magazeti na kujiandaa kwenda kuoga.
Dakika chache zilimpita akiwa maliwato na
alipomaliza, aakaufungua mlango, akasimama
ghafla, akatupa macho yake juu ya kitanda kikubwa
kilichopo katika chumba hicho hakuamini
anachokiona, akafikicha macho kana kwamba
anachokiona ni kiini macho.
“Come to me boy..” sauti ya msichana yule
aliyekuja na magazeti ilimfikia tena Amata
masikioni, akamtazama kwa makini msichana huyu
mrembo aliyejilaza kitandani na kujifunika shuka
mpaka maeneo ya kifuani na kuishika kwa mkono
mmoja huku mwingine ukifanya ishara ya kumuita
Amata kitandani. Lilikuwa ni jicho baya na kali la
Amata lililomfanya yule msichana kuurudisha
mkono wake chini na kupatwa na sura ya woga.
Amata akautazama mlango ambao yeye aliufunga
lakini alishangaa huyu msichana kapita vipi mpaka
kujitoma ndani ya chumba hicho, kisha akarudisha
macho yake pale kitandani, “Toka!” alimuamuru
yule msichana, lakini hakuonekana kuitii amri hiyo,
“Mmmm boy, kwa nini unanifukuza wakati nimekuja
kukuburudisha?” alianza kutumia silaha ya sauti
yake kumlainisha Amata, “Tokaaaa!” Amata
aling’aka kwa hasira huku akimfuata yule msichana
pale kitandani, yule msichana akanyanyuka haraka
na kukiacha kitanda kile, akasimama pembeni akiwa
uchi wa mnyama, akachukua nguo zake na kuzivaa
kisha akaufungua mlango na kutoka nje. Kamanda
Amata akakiendea kioo cha ukutani na kujitazama
kisha akaanza kuvaa suti yake nadhifu aliyoichagua
kwa siku hiyo. Akiwa pale kiooni alihisi mlango
ukifunguliwa kwa mara nyingine, kabla hajageuka
aksikia sauti kutoka nyuma yake, “Tulia hivyohivyo,
ukijifanya mjuzi, tunaondoka na pumzi yako,” Amata
akaona sasa mambo si mambo, akaendelea
kujiandaa huku mtutu wa bastola yenye kiwambo
cha sauti ikimtazama.
“Ok, umependeza, sasa utaondoka na sisi, bwana
Bill anataka kukukona usiku huu kwa maana hana
uhakika kama jua la kesho utaliona,” yule jamaa
alimwambia Amata huku akimruhusu kutangulia
mlangoni ambapo palikuwa na watu wengine wawili,
hamna ujanja. Kamanda Amata aliongoza taratibu
nje ya chumba kile na kuifikia korido ndefu, mbele
yake kulikuwa na mtu mmoja, nyuma yake kulikuwa
na mwingine yule mwenye bastola ambayo sasa
alikuwa ameifunika kwa koti lake la suti kiasi
kwamba kwa mtu mwingine hasingeweza kujua
kama mkoni hapo kuna mguu wa kuku. Waliingi
ndani ya lifti kwa mtindo huo huo, hakuna
aliyeongea kati yao, wakateremka mpaka chini na
kuongoza kwenye gari moja la kifahari aina ya
Cardilac, gari ya kifahari na gharama ya hali ya juu,
Amata alitangulizwa kuingia ndani kiti cha nyuma
kisha wawili kati ya wale watatu wakaingia mmoja
huku na mwingine kule, yule mwenye bastola akiwa
mmoja wao, mwingine wa tatu akaingia siti ya
mbele.
“Karibu sana Amata,” ilikuwa sauti ile tamu ya
mrembo aliyeongea huku akigeuka nyuma na
kumtolea tabasamu pana Kamanda. Taratibu
waliyaacha maegesho ya hotele ile na kutokomea
mjini, barabara chache na foleni za hapa na pale
katika jiji hilo la Nairobi ziliwafanya wachukue muda
kidogo kufika wanapopakusudia, mwanadada yule
aliyekuwa akiendesha gari hiyo kwa umahiri mkubwa
alikatiza kwatika vichochoro mbalimbali na kutimiza
kusudio lake.
Mguu wa kulia wa mwanadada yule ulihama kutoka
katika pedeli ya mafuta na kukanyaga ile ya breki
huku mikono yake ikiuzungusha usukani kwa kidole
kimoja kuingia katika maegesho ya hoteli ya Safari
Park.
Wote wakashuka na yule mwanadada alitangulia
kuelekea ndani ya hotel ile akifuatiwa na wale
wengine wakati Kamanda Amata alikuwa katikati ya
wote, wakaingia na kupita mapokezi kisha kuingia
upande mwingine na kuchukua lifti kushuka ghorofa
moja chini, walipotoka walikaribishwa na maandishi
makubwa ya kuwakawaka yaliyosomeka, Safari Park
Casino, casino ya kisasa iliyojengwa chini ya ardhi
katika hotel hiyo, mlangoni walisimama wazaume
wawili waliovalia suti nyeusi na kuonekana
wameshiba kimazoezi, walikuwa wamesimama
mithili ya sanamu ya bismini.
“Clean!” mmoja wa wale waliomtangulia Amata
alitamka neon hilo akimaanisha hakuna shida, mara
mlango wa kioo ukafunguka na wote wakaingia
ndani. Taa za rangi mbali mbali ziliujaza ukumbi
huo ambao ulionekana kuwa na shughuli nyingi,
wanaocheza kamali walikuwapo, wacheza uchi nao
walilipamba jukwaa wakicheza miziki yao michafu,
waliokuwa wakinyonyana ndimi hadharani nao
hawakukosa, wale waliokana jinsia zo hawakuwa
mbali, ilimradi tu dhambi zote zilihifadhiwa ndani ya
casino hilo.
“Huku tafadhali,” Amata alielekezwa ngazi ndefu
zilizokuwa zikipanda juu, akazifuata bila ubishi
mpaka juu, pale wale wasindikizaji wakamuacha na
kupokelewa na wengine kisha akaingizwa ndani ya
chumba safi na nadhifu kilichoja samani za
gharama ya hali ya juu, mbele yake kulikuwa na mtu
mnene amaye alisimama na kuja kumlaki kwa
bashasha, “Oooh Kamnda Amata, karibu sana,
nisingefurahi kama nisingeonana nawe leo hii,
karibu sana,” Bill alimkaribisha Amata na
kumuongoza kitini, kisha akampatia glass yenye
kinywaji na kuketi katika mtindo wa kutazamana.
§§§§§
Akiwa kwa mwendo wa miguu huku akipiga mruzi
usiku huo, Melchior Ndege alikuwa akipita mbele ya
hotel hiyo ya Safari Park, mara akapitwa na gari
moja ya kupendeza inayovutia macho, akasimama
kuitazama gari ile, Cardillac ya bluu nyeusi,
iliyokwenda na kuegeshwa kwa utulivu. Lakini
alipata mshtuko baada ya kuwaona wale walioshuka
kutoka garini, aliwatazama kwa makini na kuoamua
kubadili uelekeo wa safari yake. Melchior aliyaamini
macho yake yaliyomwambia kuwa umuonaye ndiye
Kamanda Amata, ‘Shiiit, amefika lini?’ alijiuliza na
kusukuti kwa sekunde chache kabla kuruhusu miguu
yake kuamriwa na ubongo juu ya lile linalopaswa
kutendwa kwa wakati huo. Alipotazama vizuri, kwa
macho yake ya kipelelezi akajua wazi kuwa
Kamanda alikuwa kwenye hatari, akavuka
kijibarabara kidogo na kuelekea mlango mkubwa wa
hotel ile kisha akaingia ndani, alipofika mapokezi
hakutaka kupoteza muda kwani aliwaona wapi
wameingilia, akafuata, wakati wao wakifunga
mlango wa lifti kuteremka chini yeye akazifuata
ngazi zinazoelekea hukohuko chini. Alizuiliwa
mlangoni na kupekuliwa, “Haturuhusu kuingia na
silaha, weak pale unapotoka utaichukua.” Melchior
alisogea kwenye meza ndogo ambayo ilikaliwa na
mwanadada mrembo akaichukua bastola ya
Melchior na kumpatia kadi maalum ya
kumbukumbu. Akaelekea kaunta na kuketi juu ya kiti
kimoja kirefu mbele ya kaunta hiyo. Akiwa
anakunywa kinywaji chake taratibu huku macho yake
akiwa kayaongoa kule wlikopelekwa Kamanda
Amata, ambapo palitenganishwa na ukumbi
mkubwa kwa vioo maalum vinavyoruhusu mtu wa
ndani kuweza kuona kinachoendelea ukumbini lakini
yule wa ukumbini asiweze kujua nini kinaendendele
ndani ya chumba kile. Melchior akatoa miwani yake
maalumu na kuipachika usoni, miwani hii ilikuwa na
madini ambayo yaliweza kupenya kwenye kioo cha
aina yoyote pia yaliweza kukuruhusu kuona mtu
kama amebeba silaha au vipi, maana iliruhusu
kuona vitu vigumu tu vilivyo mwilini mwa mtu.
Alimuona Kamnda Amata akiwa na Bill
wakizungumza, lakini hakuweza kujua
wanazungumza nini, aliwatazama walinzi wa mlango
wakuingia kule juu aliwaona wakiwa na bastola
mbili kila mmoja, kisha akawatazama wafanyakazi
wa casino hiyo na kuona kila mmoja alivyoipachika
silaha yake, kisha akayarudisha macho yake na
kuyatuliza kule aliko Kamanda Amata na kuendelea
kuona kinachojiri, huku akiendelea kunywa kinywaji
chake. Mara alihisi, akipapaswa kwa nyuma
maeneo ya kiunoni, akageuka na kukutana macho
na mwanamke mshumami, aliyejiremba
akarembeka, yule mwanamka aliyeonekana ana kila
dalili ya ulevi machoni mwake alizunguka na
kusimama mbela ya Melchior, akamrembulia
macho, Melchior hakuonesha hata kumjali kwani
yeye alitaka kujua tu nini kitatokea kule ndani,
“Mwanamke unataka nini? Kama kinywaji chukua
uende, mi sihitaji mwanamke saa hii,” Melchior
alimwambia yule mwanamke, akamnunulia kinywaji
kisha kwa akapewa shukrani ya sonyo kali na refu,
“Go fish!” yule mwanamke alimwambia Melchior.
§§§§§
 
SEHEMU YA 6
“Bado mnanifuata Kamanda!” Bill alimwambia
Amata huku akimimina kinywaji katika glass yake.
“Kwanza nashangaa kukuona huku, umekuja kufanya
nini?” Amata alimuuliza Bill, cheko kali lilimtoka
mpaka walinzi wake waligeuka kutazama ndani.
“Kamanda Amata, mimi si motto mdogo au
punguani, najua ninachofanya na ninajua kila
anayeingia katia wigo wangu popote pale katika
pepo zote nne za dunia,” Bill aliongea kwa
kujiamini, “Nina macho Kamanda, siyo haya mawili,
mengi tu, na nilijuwa kuwa utakuja, maana una kiu
na mimi, lakini ujue hata mimi nina kiu na wewe,
umeshaniharibia mambo mengi sana,” akapiga
fuinda moja kinywaji chote kikaishia tumboni
mwake, akabeua kwa shibe ya kinywaji.
“Bill Van Getgand, unajua unachokizungumza?
Nimekuja Nairobi, nashangaa naambiwa wewe
unanihitaji, nisingeshindwa kuwararua hawa nyau
wako hata kama wangekuwa hamsini, lakini kwa
heshima yako nikawaacha na kuwatii kwa kuwa
umeniita, na ungependa kuniona kabla ya jua la
kesho kwa kuwa unajua kuwa jua la kesho sitaliona,
ok, niambie ulichotaka kuniambia, unataka kunipa
deal?” Kamanda Amata aliuliza.
“Oh, Kamanda, mi nipo hapa takribani wiki mbili
sasa, nimekuja kibiashara, lakini nilijuwa safari yako
ya kuja hapa Nairobi, nikajua wazi kuwa wewe ni
mgeni wangu, ndo maana nikakukaribisha uje
tustarehe, lakini nataka uniambie umekuja kufanya
nini hapa Nairobi,” Bill alihoji kijanja.
“Bill, maswala yangu ya kikazi siwezi kukwambia
wewe kuwa nimekuja kufanya nini, kama hilo ndilo
uliloniitia basi hutopata jibu,”
“Hivi unajua kuwa upo mikononi mwangu?” Bill
aliuliza
“Hata kama, lakini huwezi kunilazimisha nikwambie
nimekuja kufanya nini,”
Bill akachomoa bastola yake na kumnyooshea
Amata, “Utaniambia tu, maana hata nikikuua hapa
hakuna atakayejua kama umekufa zaidi ya mimi na
wewe mwenyewe,”
“Sitishiki na hiyo bastola ya Kirussi Bill,” Amata
alijibu kijeuri, lakini kabla hajakaa vizuri, bastola ya
Bill ikafyatuliwa, risasi ikapenye katikati ya paja na
paja la Amata, ile sofa ikatimua vinyoya kidogo,
Amata alitetemeak ka hofu, kijasho chembachemba
kikamtiririka, akaona kuwa kumbe hapo hakuna
usalama wala mzaha, hakuna urafiki kama upo basi
ni wa mashaka.
“Usifikiri nakutania, nataka unieleze lile lililokuleta,
na ukijifanya mjanja nakuua,” Bill aliongea huku
akimlenga na ile bastola yake iliyoonekana wazi iko
tayari muda wowote kufanya itakachoamuliwa, kabla
hajajaibu, Bill alifyatua risasi kadhaa, moja katikati
ya mapaja ya Amata, ya pili upande wake wa
kushoto nay a tatau upande wa kulia, hali ile
ilimfanya Amata aweweseke na kushindwa kujua
atfanye nini, alibaki kutetemeka na kulowa jasho
mwili mzima, akabana meno kwa hasira, “Nimekuja
kukufuata wewe hayawani, na nakupa muda
mchache tu utakuwa mikononi mwangu, Bill, ndipo
dunia itakapojua kuwa roho moja dhalimu
imeondoka duniani.”
“Aaaaaaa ha ha ha ha ha!” Cheko la Bill lilipasua
anga la chumba kile, “Kamanda Amata, Tanzania
Secret Agency, hapa mmefika, nitawaacha hapa na
mi nitaondoka na kile kilichonileta. Kama hauamini
hujiulizi nimejuaje kuwa huko hapa! Ujue kuwa
muda wowote nitaitwaa roho yako kabla ya jua la
asubuhi inayofuata.” Bill akamalaiza risala yake na
kugugumia tena glass nyingine ya kinywaji kikali,
“Nimefurahi kukuona!” alimalizia na kuichukua
fimbo yake ya kutembelea kisha kuondoka eneo
lile.
“Tutaonana tena soon,” Amata alijibu kijeuri na
kunyanyuka kuelekea mlango, kabla hajatoka
mlangoni alisimama na kugeuka nyuma akagongana
macho na Bill, wakatazamana, “Siku yetu inakuja,”
alimwambia na mara wale walinzi wakamvuta
kumtoa katika mlango ule alioutumia kuingilia na
kwenye ngazi alikutana na yule mwanadada
aliyemjia chumbani akiwa ameweka pozi akitazama
yanayoendelea ukumbini mle, wakatazamana kwa
sekunde, “Unahitaji lifti yangu?” yule mwanadada
alimuuliza Amata huku tayari akiongozana nae
kumsindikiza, mara simu ya yule mwanadada ikaita,
“Yes Boss…” aliitika, sauti ya upande wa pili ilisikika
vizuri masikioni mwa Amata japo ilikuwa ndogo,
“Nakupa usiku huu tu ukamstareheshe Kamanda,
maana ana msongo wa mawazo, kisha urudi kabla
jua alijachomoza,”
“Sawa boss, umesomeka,” alijibu kisha
akamwangalia Amata, “Leo mimi na wewe mpaka
kuchee, boss ameruhusu,” kisha akamshika mkono
Amata na kujichnganya nae katikati ya watu ndani ya
casino ile.
§§§§§
Nyimbo za masifu ya jioni zilikuwa zikirindima
katika masikio ya walio jirani na eneo hilo la kanisa
la Holy Family, masista waliokuwa kanisani mida
hiyo walikuwa wakimalizia sala zao za jioni kabla ya
kwenda kulala, kusubiri siku inayofuatia, ikiwa ni
siku chache tu tangua mazishi ya Fr Gichuru
yamalizike, bado mioyo yao ilikuwa imejawa na
huzuni ukizingatia kwao kasisi huyo alikuwa ni mtu
wa pekee sana, mwenye karama ya uponyaji ya hali
ya juu, mpole, mcheshi, mwenye upendo na mcha
Mungu.
Ibada ilimalizika na watawa hao wa kike walianza
kutoka kuelekea nyumbani kwao, nyumba iliyo
umbali wa kama mita mia mbili kutoka kanisa hilo,
taa za nje zenye mwanga wa njano zilipendezesha
eneo hilo, maua na miti michache ilifanya kabaridi
kawe kakali kiasi. Masista wote walimalizika
isipokuwa sista Rose ambaye alikuwa akimalizia
kupanga vitu vya ibada itakayofuatia, kisha afunge
sakristia. Haikumchukua muda alimaliza na kujianda
kutoka ndani ya jengo hilo ili akaungane na
wenzake. Alipoukaribia mlango tu alijikuta akibanwa
na mkono wenye nguvu, uliombana barabara katika
shingo yake hata akajikuta anakosa pumzi na mwili
wake kukosa nguvu, mkono ule ulilegezwa kidogo
na kumruhusu sista Rose kuweza kufurukuta kidogo,
akataka kupiga kelele lakini alibadili mawazo ghafla
baada ya kukutana na bisu kubwa na kali
lililoshikwa na mkono wa mwanamke, Mellina
alimkazia macho mwanamke mwenzake kana
kwamba anamwangalia kuku au sungura.
“Monstrance! Onesha haraka iliko,” ilikuwa sauti ya
Mellina ikimtoka huku mkononi bado kalishikilia lile
jisu lake tena akiwa kalinyooshea kwa sista Rose.
Ilikuwa ni wakati mgumu sana kwa mtawa yule wa
kike, hakuwa na ujanja, hatari zote zilimkabiri,
“Tuoneshe ilipo monstrance, tunaitaka monstrance
sasa hivi, ukileta ujuaji nakutumbua na hili bisu,”
Mellina alimwambia Sista Rose huku akiwa bisu
lake kaliegesha nchaye katika ziwa moja la mtawa
yule aliyekuwa akitetemeka kwa hofu kuu huku
akilisukuma kama anayetaka kutoboa.
“Utaonesha au tukumalize kama yule kasisi wenu?
Maana na ye alikuwa mbishi kama wewe” Cheetah
alimuuliza kutoka nyuma yake, ndipo yule sista
akajua kuwa aliyemkaba alikuwa ni mwanaume. “Ni
ni nitawaonesha!” alijibu yule sista. Kisha wote kwa
pamoja wakaongozana kuelekea milango mingine
iliyotengenezwa vizuri kabisa ndani ya vyumba hivo
vya kanisa hilo kubwa. Baada ya kupita milango
kadhaa mara waliteremka ngazi kuelekea chini na
huko walikuta stoo kubwa lakininzuri yenye vitu vingi
tena vya thamani kubwa, sista Rose akawaonesha
kabati moja kubwa lililofungwa ukutani, Mellina
akaliendea na kufungua milango yake, “Waoh!”
alijisemea kwa sauti ambayo kila mmoja alisiikia.
“Nini Mellina?” Cheetah aliuliza, alipokaza macho
yake alishuhudia monstrance kubwa ya dhahabu safi
ikiwa imetulia kabatini, akamuacha yule mtawa na
kuliendea kabati akainyanyua ile monstrance kwa
umakini wa hali ya juu na kuiweka mikononi mwake,
kisha kwenye begi walilokuja nalo maalumu kwa
kazi hiyo. Sista Rose alikuwa akitetemeka sana
akiangalia walivyokuwa wanaichuku bila heshima
yoyote kwa chombo hicho kitakatifu.
“Tafadhali muiache hiyo monstrance,” sista Rose
aliwasihi Cheetah na Mellina.
“Acha ujinga wako,” alijibiwa na mellina huku
akipata pigo moja la ubapa wa kile kisu kikubwa.
Sista Rose akabaki kimya huku machozi yakimtoka
baada ya pigo lile, walipohakikisha wameiweka
sawa katika begi lile la ngozi, Cheetah akalibeba na
kumtazama sista Rose, akacheka cheko la dharau,
“Kazi yetu imekwisha, kwa heri msalimie paroko,”
Cheetah alimwambia sista Rose huku akimpita na
kuuelekea mlango waliouingilia. Pigo moja la judo
lilitua mwilini mwa sista Rose, akapepesuka, kabla
hajajitambua, mellina akampa pigo lingine
lililompoteza akili na kumbwaga chini kama mzigo,
kisha guu nene la Mellina lilikanyaga koromeo la
sista yule kwa sekunde kadhaa likimkandamiza
chini na kumfanya kurusharusha miguu na mikono
huku na kule na kuzimika. Ilikuwa tabu kuujua
mlango waliongilia, kila walipoufungua huu walijikuta
eneo lingine kabisa, walipojaribu huu hali ilikuwa
ileile, Cheetah alionekana kuchanganyikiwa maana
alipoingia aliona milango michache lakini sasa
anaona milango mingi kuliko ile ya kwanza,
iliwachukua dakika nyingi kuutafuta mlango ule bila
mafanikio.
§§§§§
Melchior Ndege, aliendelea kupepesa macho yake
maangavu ndani ya casino lile lililosheheni watu wa
kila aina, muda ulivyozidi kwenda ndivyo watu
walivyoongezeka ndani yake, alihakikisha hampotezi
Amata machoni pake, na liona wazi jinsi alivyokuwa
amegandwa na mwanadada yule. Melchior alijaribu
kuvuta kumbukumbu ni wapi amekwisha wahi
kumuona yule mwanadada lakini jibu hakulipata
kirahisi japokuwa sura ilikuwa ikimjia.
Alimuona Kamanda Amata akiwa anakunywa kinyaji
kikali huku mwanamke yule akiwa pembeni yake na
akionekana kumhamasisha, mara amsike kiunoni
mara ambusu mara ampapase hapa na pale, kisha
aliwaona wakikokotana kutoka nje ya casino ile.
Melchior alishusha glass yake taratibu na kuiweka
katia meza ya kaunta kisha akateremka kutoka
katika kile kiti kirefu na kuuendea mlango wa casino
kutoka nje, akachukua bastola zake pale mlangoni
nakuiendea lift iliyompandisha hadi juu na kutoka
mlango mkubwa wa hoteli. Katika maegesho ya
magari alimuona Amata akiwa na yule mwanamke,
sasa ilionekana wazi kuwa mapenzi yanachukua
nafasi yake, akajifanya anapiga simu, ili kupoteza
muda ajue kitachoendelea. Muda si mrefu,
ikasimama gari pembeni yao, Jeep Cherokee ya
kibuluu hivi, yule mwanamke akamvutia ndani
Amata na gari ile ikatoweka. Melchior alitazama
hapa na pale na kuona gari nyingi zilizokuwa
zimeegeshwa na wamiliki wake walikuwa wakila
starehe ndani ya hoteli ile, akaiendea moja wapo,
Toyota Celica, akatoa funguo yake, wengi huiita
Malaya, funguo inayoweza kufungua takribani lock
zaidi elfu kumi za magari bila shida achana na
switch zake. Alizungusha mara mbili tu mult lock
zikaachia akaingia nyuma ya usukani na kulitekenya
nalo likacheka, taratibu akaingia barabarani na
kuifuata ile Jeep Cherokee, alikanyaga mafuta na
kuhakikisha haiachi mbali gari ile, kati yake aliacha
gari kama mbili hivi na kuendelea kuifuata, baada ya
barabara tatu nne na vichochoro kadhaa ilianza
kuuacha mji na kuchukua barabara ya kuelekea
Thika, Melchior aliendelea kuwafuata na
walipokaribia maeneo ya Kalimoni, akaona hapana,
akaongeza mwendo na kuifikia ile Jeep, akaipita na
kukaa mbele yao. Kila dereva wa ile jeep
alipoijitahidi kuipita ile gari ya Ndege haikuwa rahisi,
Melchior akaongeza kasi na kuiacha kama mita
ishirini hivi kisha akafunga breki kali sana na ile
jeep ilikuja na kuigonga ile Toyota kwa nyuma,
kutoka katika ile jeep, mtu mmoja akateremka na
kuifuata ile Toyota akaangalia ndani lakini hakuona
dalili ya mtu, alitazama huku na kulea asione kitu,
akarudi garini mwake na kuingia, alipofunga mlango
tu alihisi kitu cha baridi kikigusa shingo yake, “Tulia
hivyohivyo,” sauti ilimwambia, kisha Ndege
akaunyoosha mkono wake na kuichomoa bastola ya
yule dereva, wakati huo tayari kipigo cha haraka
kilishampa usingizi wa muda yule mwanamke
aliykuwa na Amata, “Toa gari barabarani, weka
kando ile,” Melchior Ndege aliamuru na amri
ikafuatwa, mbele kabla ya mahali alipoambiwa
aiegeshe gari ile palikuwa na daraja kubwa sana la
mpishano wa barabara, wao sasa walikuwa barabara
ya juu, yule dereva akafanya hila kwa kugongesha
ile gari katika ukingo wa daraja, ile gari ikayumba
kidogo, Melchior, mle ndani ya gari akaangukia
upande wa pili na kumpa nafasi yule dereva kufanya
lolote, lakini kabla hajafanya hivyo, maana Melchior
alimuona akichomoa bastola nyingine sehemu
Fulani ya dashboard yake, kitendo bila kuchelewa,
kwa kutumia miguu yake miwili alimbana kabali
njema, gari iliyumba lakini Melchior hakujali, mara
akasikia kishindo kikubwa, ile gari ilijipiga kwenye
ukingo wa daraja, ikahamia upande wa pili
ikakutana na Toyota prado na kujibamiza kisha
akaangukia nje ya barabara. Kamanda Amata akiwa
hajui lolote linaloendelea kutokana na usingizi mzito
alioulala mara tu baada ya kuingia mle garini,
alijigonga kichwa kwenye muhimo wa dirisha,
akshtuka na kuanza kushangaashangaa, huku damu
zikimtiririka kutoka kwenye jeraha dogo lililotokea
katika kichwa chake baada ya kujigonga kule.
Melchior alitoka kwa shida kidogo katika gari ile
baada ya kuvunja kioo cha mbele, kisha akamsaidia
Kamanda Amata kutoka nje, bado Kamanda alikuwa
hajarudiwa na akili sawasawa alikuwa kama zezeta
hivi, Melchior akamshika mkono na kutembea nae
kuelekea pale alipoiacha ile gari alioichukua kule
hotelini, aliwakuta polisi wawili akiitazama ile gari
huku wakiwa na wanaandikaandika vitu Fulani
wakisaidiwa na taa za barabarani. Melchior
aliufungua mlango wa mbele na kumtumbukiza
Kamanda kiti cha kushoto kisha yeye akazunguka
kiti cha kulia, “Halo, vipi, mbona unakuwa kama
hauheshimu mamlaka?” mmoja wa wale askari
akauliza, Melchior akawasha gari huku
akimwangalia yule askari, “Nenda pale karibu na
njia panda utakuta ajali ya gari aina ya Jeep
Cherokee, hiyo ndiyo ukaipime, hii sio ajali,” kisha
akaondoka kwa kasi mpaka kwenye mzunguko
mkubwa na kuhama njia kuchukua njia inayorudi
mjini, kwa mwendo uleule wa kasi ya ajabu.
AGA KHAN HOSPITALI
Parkland Avenue-Nairobi
MELCHIOR ndege aliegesha gari katika lango la
hospitali ile na daktari mmoja alikuwa pale tayari na
kitannda cha magurudumu, akisaidiwa na manesi
wawilli walimlaza kamnda Amata na kuingia naye
ndani, moja kwa moja wakamuweka kitandani
kwemye chumba cha peke yake, wodi maalumu,
daktari alipomuangalia vizuri aliona wazi hali yake si
nzuri, hivyo akaamuru awekewe drip ya glucose ili
iweze kumrejeshea nguvu japo kidogo. Wale
wauguzi wakafanya hivyo lakini pia walicheki
mapigo ya moyo na kuweka kumbukumnbu zake
kati faili maalumu lililokuwa pale, Kamanda Amata
alilala kimya akiwa hajitambui tena, jeraha lake
lilishonwa na kuwekwa katika hali ya usafi.
Melchior Ndege, alipekuwa kwenye mifuko ya
Amata lakini hakuona chochote, akabaki kumtazama
pale kitandani alipozungukwa na mitambo tiba ya
kisasa ambayo ilikuwa inaangalia mwenendo wa
mwili kwa ujumla kama mapigo ya moyo na
mambo mengine. Melchior Ndege alitoka nje na
kufunga mlango mkubwa kioo kisha kurudi ofisini
kwa daktari.
“Rafiki yako inaonekana amepewa sumu kali sana
ambayo imempotezea fahamu na kuathiri mfumo
wa urendaji kazi wa mwili wake, itamchukua masaa
mengi sana kuirudia hali yake ya kawaida,” Daktari
alimweleza Melchior Ndege, haikuwa rahisi
kulielewa swala hilo, lakini aligundua kuwa Bill
alidhamiria kummaliza Amata. Akashusa pumzi
ndefu na kumtazama daktari.
“Huyu ni mtu wetu, katoka Tanzania,” akamwambia
kwa kifupi, daktari akatikisa kichwa kuashiria kuwa
ameelewa, kisha Melchior akampa habari nzima
jinsi alivyomuona kuanzia pale hotel ya Safari park
mpaka kule kwenye ajali.
Hasira zilizidi kumtawala Melchior na moyoni
akaapa lazima Bill alipe yote ayafanyayo, hapo
akagundua kuwa Bill ni jasusi la kimataifa lenye
mbinu za kuua bila kutumia silaha na kuwafanya
watu kutojua ni nini chanzo cha kifo. Aliagana na
daktari na kuomba kurudi baadaye kidogo lakini
apewe taarifa ya kila kinachoendelea.
Safari yake na gari ile ya kukodi iliishia katika mtaa
wa Riara, akashuka na kuilipa tax hiyo kisha
akaliendea geti kubwa jeusi lilofungwa sawia,
akabofya kengele, mara likafunguka naye akajitoma
ndani, “Karibu sana kijana!” alikaribishwa na sauti ya
boss wake bwana Shikuku, “Vipi mbona usiku
sana ?” akaongeza swali, ndipo Melchior alipoinua
mkono wake kuitazama ile saa yake iliyomuonesha
kuwa ni saa nane kasoro robo usiku. Wakaingia
sebuleni na kuzungumza machache, Melchior
alimpa habari yote ya Kamanda Amata. Shikuku
alisikitishwa sana na habari hiyo, kisha wote wawili
usiku huo wakatoka na kuelekea kule hospitali
kumuona Kamanda, walimkuta katika hali ileile
isipokuwa sasa ilikuwa mbaya zaidi kwani mapigo
ua moyo yalishuka sana, hata daktari alikuwa na
wasi wasi juu ya hilo maana hayakuonekana kupata
unafuu wowote.
“Shiiiittt!!!!” aliinua simu yake na kubofya namba
Fulani kisha kusikiliza sauti ya upande wa pili,
baada ya mazungumzo mafupi aliikata na kuiweka
mezani, akajishika kichwa kwa masikitiko, mara
simu yake ikapata uhai na kujitikisatikisa pale
mezani, aliinyakuwa na kusikiliza, “Yeah… ndiyo…
ee. Fanyeni haraka tafadhali,” akakata simu na
kuitia mfukoni.
“Vipi, ni nani hao?” Ndge alimuuliza bosi wake.
“Nilikuwa nawapa taarifa juu ya mtu wao huko
Tanzania, ili wajue ni nini watafanya, sasa
wamesema wayanijibu haraka iwezekanavyo,”
Shikuku alijibu.
“Hivi Bill amedhamiria haswa kufanya mauaji ya
mtindo huu sivyo?” Ndege alimuuliza Shikuku.
“Yule ni shetani, sio binadamu, hivi umesema yuko
wapi saa hii?” Shikuku aliuliza swali kwa Ndege.
“Niliwaacha, Safari Park casino, lakini sidhani kama
bado wako hapo, ngoja tufatilie wale watu wa
kwenye ile gari ili tujue kwa undani juu ya sakata hili
na nini kipo nyuma yake, simpendi kabisa Bill, na
aombe Kamnda Amata asiamke milele, lakini
Shikuku nakuhakikishia, Kamanda akiamka atavunja
mpaka miiko ya kazi yake ili amtafute huyu
hayawani na kwanza atamuua kisha amuulize
maswali anayoyataka,” melchior Ndege aliongea
kwa hasira na kutoka nje ya chumba cha daktari.
Mkono wa bwana Shikuku ulimshika bega Melchior
Ndege pale alipokuwa ameegemea ukuta akiwa
amewaka hasira zilizojaa uchungu.
“Malchior, punguza jazba, pamoja na FBI kuwa
hapa, isiturudishe nyuma, ingia kazini, mimi
nakuamuru, kama kuna swali mi nitajibu; Kamanda
atapona tu, najua walimuwahi katika namna ambayo
hakuitegemea,” yalikuwa ni maneno ya Shikuku kwa
Melchior, akageuka kumtazama mtu huyo mwenye
mwili mkubwa, mkuu wa idara ya usalama wa Taifa
hapo Kenya, Melchior alitabasamu kwa bashasha
baada ya kuambiwa ‘Ingia kazini’, alitoka pale alipo
na kuelekea tena chumba cha daktari kisha akaingia
kumuona Kamanda, alimutoa alama ya saluti ya
heshima, na kumuhakikishia Kamnda kuwa sasa
analipiza kisasi kwa ajili yake, kishapo akatoka nje
na kuagana na Shikuku.
DAR ES SALAAM
Saa 9:15 Usiku
KELELE za simu ya mezani ya Madam S ilipiga
kelele usiku huo, mlio wa dharula ulimshtua kutoka
katika usingizi mzito, “Aaaa nini tena saa hizi?”
aliongea kwa sauti ya hasira na kuinyakua ile simu
masikioni mwake, “Hallo nini saa hii?” aliipokea na
kutupa swali hilo; huku akisikiliza sauti ya upande
wa pili, “Madam, kuna taarifa kutoka Nairobi kuhusu
Kamanda Amata, hali yake ni mbaya sana yuko
kufani,” sauti hiyo iliongea kwa upole, ilikuwa ni
simu kutoka ofisi ya usalama wa Taifa ikimpa
taarifa hiyo Madam, mkuu wa kitengo maalum
chenye watu wachache makini wanaofanya kazi za
umakini kwa umakini wa kimakini. Aliishika ile simu
bila kuongea. “Unasemaje?” akauliza, akajibiwa tena
jibu lilelile. Madam S alishikwa na kigugumizi,
midomo ilimchezacheza, hakuamini anachoambiwa,
ni jana tu mchana alipoagana na Kamanda wake
pale JNIA na kumpa usia wa nguvu, Madam alibaki
kimya na simu ikiwa hewani nab ado hajaishusha
kutoka sikioni mwake, akashusha pumzi kisha
akafungua kinywa chake, “OK, asante kwa taarifa,
fanya kila kinachowezekana Kamanda afike hapa
mara moja,” akakata simu na kurudisha mkono
wake mahali pake, “Uuuuhhhhh!!!!” akashusha pumzi
nzito kwa mara nyingine, akajilaza kitandani kwake
huku mawazo lukuki yakiwa yamemtawala kichwani
mwake. Akafikiri la kufanya na kumpigia daktari
wao pale Muhimbili, ushauri aliopewa aliuona una
maana sana, yule daktari alimshauri ikodiwe ndege
ya haraka kutoka Nairobi imlete Dar, badala ya
kukodi kutoka Dar. Utaratibu ukaandaliwa haraka
kwa ushirikiano na Bwana Shikuku kule Kenya.
Usingizi haukuja tena kwa Madam S, akaifungua
kompyuta yake ya kazini ambayo imeunganishwa
moja kwa moja katika kitanda chake, alipojaribu
kuingiza password yake, ikagoma, haikufuka,
akajaribu tena na tena, wapi. Alipoona
imeshindikana, akampigia simu Chiba, mtaalamu wa
ICT wa kitengo chao, naye akajaribu kuifungua lakini
ikawa ngumu, akatumia mbinu zote kuitafuta maana
alishajua kuwa wajanja wameiiba kimtandao, na
kwa maana hiyo siri zote za usalama wa Tanzania
ziko hatarini kuvuja, kijasho kilimtoka Chiba, usingizi
ulikatika, akiwa mezani kwake alikuwa akishindana
na mtandao kuloitatua tatizo hilo huku Madam S
akimuahidi kufika hapo mapema ili kujua kulikoni.
Majibu yalikuja na kugundua kuwa kompyuta ya
Madam S imekuwa ‘Hiked’ sehemu Fulani huko
Nairobi, mchezo ukaanza kunoga, sasa mapigano ya
kimtandao, Chiba hakukubali, alifanya juu chini
kuinusuru, ‘Kamanda Amata wanataka kumuua na
mtandao wanataka kuukamata, shiit,” alijiwazia
kisha akaiacha kompyuta yake na kuelekea kwenye
kabati lake, akavaa nguo haraka haraka na kuibeba
ile kompyuta kisha kuchukua gari yake haraka
akawahi katika ofisi ya mawasiliano ya Usalamawa
Taifa, pale kuna kompyuta kubwa zaidi inayoweza
kujua vizuri sana, ni wapi na ni nani aliyefanya hivyo,
haikuchukua muda aliinasa, na kuifunga kabisa kwa
namba ambazo mwingine asingeweza kuzifungua.
Akasimama na kumtazama kijana aliyekuwa
akisaidiana naye kazi hiyo, Frank Masai.
“Dah, hatujui ni kiasi gani wamepata siri zetu,” Chiba
alimueleza Frank Masai aliyekuwa kasimama karibu
na meza kubwa yenye screen kubwa sana ya
kompyuta inayoweza kuzileta kompyuta nyingi za
ulimwenguni na kutafuta kila wanachokitaka.
“Sasa Bro, cha kufanya ni kiunguza kabisa hiyo
kompyuta yao waliyotumia kutu ‘hike’,” Frank
alisema.
“Tutafanyaje, maana inabidi tupate namba ya BIOS,”
Chiba alisema
“Ah no, siku hizi huwezi kuua kompyuta kwa
kuiharibu BIOS maana technolojia imepanda kaka,
Operating System za sasa zina uwezo wa kutest kila
hardware na software zilizopo kati kompyuta bila
kupitia kwenye BIOS, cha kufanya hapa tufuondoe
taarifa zetu kisha mi nitaweka kirusi kibaya sana
kwa jina la faili moja, najua kwa vyovyote
watafungua tena, maana kwa sasa wanaonekana
wapo offline, kisha huyo kirusi atavuruga system
yote ya kompyuta yao,” Frank Masai alijibu kwa
kujiamini, kijana mwenye elimu ya ICT kutoka chuo
kikuu cha Dar es salaam.
“Ok, fanya hivyo wakati mi nafanya mengine,” Chiba
alimalizia. Kijana Frank Masai alikaa makini kwenye
laptop yake akitengeneza shetani hilo alilolipa jina
TOP SECRET, kazi iliyochukuwa kama lisaa limoja
hivi na kuifanikisha akiwa kachoka sana. Kisha
akamwendea Chiba na kumwambia kazi tayari ili
apate ruhusa ya kufanya mlipuko huo, akakubaliwa,
kazi ndogo, akaingiza kile kirusi kwenye mfumo wa
kompyuta ya Madam S na kukiacha hapo, wakati
document zingine zote akiwa zimebanwa na Chiba
kwa pin ngumu.
§§§§§
REJEA NAIROBI… kanisa la familia Takatifu…
Ilikuwa ni kazi ngumu kwa Black Cheetah na Mellina
kutoka ndani ya wigo wa kanisa maana tayari
sergeant Maria na koplo Kariithi walikuwa pale na
wengine wanne wenye silaha, walitanda kila upande
kuhakikisha majambazi hao hawatoki bila kuacha
roho zao.
Gichui, aliyekua akiendesha gari siku hiyo aliwapa
taarifa kwa simu kuwa jamaa wamejipanga vipi
huko nje, wakamuamuru, aanzishe show kwa kupiga
risasi za hewani. Naye akafanya hivyo, mlio wa
risasi zile ukawafanya wale askari kuchanganyikiwa
kidogo, Black Cheetah alitoka katika mlango
mkubwa akiwa na lile begi na kukimbilia upande wa
pili wa ukuta huo ambako ndiko waliokoingilia, huku
Mellina akitambaa mwendo wa nyoka kulifuata geti
kubwa akiwa na bastola yake aina ya revolver
mkononi mwake.
Gichui alipiga norinda na kutimua vumbi
liliwachanganya Mellina na Kariithi ambao walikuwa
tayari kujibu mashambulizi, Sargeant Mellina
alijitupa chini na kubingirika kwa usatadi mpaka
kwenye ukuta wa wigo wa kanisa hilo huku
akishuhudia vijana wake wakijiweka tayari,
“Freeze!!!!!!” sauti ya askari mmoja lisikika upande
wa pili, Kariithi bado alikuwa akijaribu kuona afanye
nini, akajitoa na kukimbilia upande wa sauti ile
ilipotokea, akiwa anakata kona ya ule ukuta alisikia
mlio wa risasi na kushuhudia mwili wa yule askari
ukijibwaga chini kama kiroba, “Shiittt!” akng’aka
kwa hasira, alimuona Cheetah, aliyeifanya kazi hiyo
akiishia gizani, akajaribu kulenga na kufyatua risasi
mbili lakini hakumpata, mara ile gari yao ilipita kwa
kasi na kuelekea upande ule alipo Cheetah,
haikuhitaji kusimama, kawani Cheeta alirusha begi
ndani ya gari na kujirusha kupitia dirishani, lakini
kabla hajamalizi miguu risasi moja ilipita katikati ya
mguu wake na kufumua mifupa ya ugoko, Gichui
aliizungusha gari kwa ustadi na kumfanya Cheetah
kutumbukia ndani, “Aaaaaaaaiiiiggggghhhhhh!!!!”
ulikuwa ukelele wa maumivu kutoka kwa Cheetah.
“Vipi brother?” Gichui aliuliza huku akiizungusha
tena ile gari na kumgonga askari mwingine, sasa
alikuwa akilielekea geti kuu la kanisa lile.
“They have shot me, bastards!” wamenipiga
wanaharamu alimwambia Gichui, huku akiiweka
tayari bastola yake. Sergeant Maria akiwa pale chini
aliilenga sawia ile gari na kabla hajapiga risasi
alihisi kama kitu kimenguka pale alipolala kwa
nyuma yake alipogeuka aliona mwanamke kibonge
akitua juu ardhi kavu na bastola mkononi, akiwa
pale chini alijigeuza na kupiga mtama mmoja
maridadi, Mellina alilipokea pigo hilo na kubwagwa
chini, alijitahidi kujiinua kisarakasi lakini kabla
hajawa wima mtama mwingine wa Mellina
ulimrudisha chini na kumfanya hoi pale ardhini, sasa
alishindwa kujiiunua. Bastola ya Mellina ilicheua na
risasi ikapita mililmita chache kwenye uso wa Maria
aliyekuwa pale chini, teke moja kali la afande Maria
lilipeperusha bastola ile kutoka mikono ya Mellina
ikapaa juu, kisha aliushusha mguu wake na kuutuza
juu ya uso wa Mellina.
Koplo Kariithi alijitoa mhanga na kucukua ile SMG
ya askari ambaye aliku marehemu, kuilenga gari ya
Gichui, ‘nice shot’ risasi moja alipiga tairi ya nyuma
na kuipotezea muelekeo ile gari, ikayumba na
kuyumba lakini ikakaa tena barabarani, risasi ya pili
kutoka kwa Kariithi ikakishusha kioo cha nyuma na
bila kukosea ikafumua kisogo cha Gichui na ile gari
ikayumba myumbo mkuu na kugonga mti. Wakati
Kariithi akiifuta, ghafla nyuma yake kulitokea gari
aina ya BMW kwa kasi ya ajabu ikafunga breki kali
karibu kabisa na ule mti ilipogonga ile gari ya
Gichui, kwa haraka watu wawili walishuka na
kuifungua milango wakamtoa Cheetah na kulibeba
begi kisha kurudi ndani, ile gari nayo ikazungushwa
kwa mtindo wa U turn na risasi moja iliyotoka ndani
ya gari ile ilimpata koplo kariithi mkononi, na
ukelele wa maumivu, ulimchanganya sergeant Maria,
akamsahau Mellina na kumkimbilia Kariithi,
“Soldier!!!” Askari, sergeant Maria aliita kwa sauti na
askari wote wakaja eneo hilo na kumbeba mwenzao
wakimpakia kwenye gari, wengine wakabaki kufanya
utaratibu wa kumuondoa Gichui ambaye alikuwa
hana maisha tena na kichwa chake kikiwa
kimevurugika kwa risasi ya Kariithi, moja kwa moja
walimfikisha katika hospitali ya taifa ya Nairobi.
ITAENDELEA HAPA HAPA
 
“Soldier!!!” Askari, sergeant Maria aliita kwa sauti na
askari wote wakaja eneo hilo na kumbeba mwenzao
wakimpakia kwenye gari, wengine wakabaki kufanya
utaratibu wa kumuondoa Gichui ambaye alikuwa
hana maisha tena na kichwa chake kikiwa
kimevurugika kwa risasi ya Kariithi, moja kwa moja
walimfikisha katika hospitali ya taifa ya Nairobi.
SEEMU YA 7
6
MADAM S alisimama kwenye mlango maalum wa
kioo akimtazama Kamanda Amata aliyekuwa
amelala kitandani akiwa ndani ya mitambotiba, sasa
alikuwa ameamka baada ya kazi kubwa ya daktari
wa muhimbili ya kumtoa sumu mwilini, alifumbua
macho, aliweza kuongea japo kwa shida, alikutana
macho na bosi wake, akamtazama, “Karibu Nairobi
Madam,” Kamanda alimkaribisha madam S.
“Aliyekwambia hapa Nairobi ni nani?” Madam
alimuuliza Kamanda.
“What?” akajiinua na kuketi, “Niko wapi?” akauliza.
“Upo Muhimbili, karibu sana Dar es salaam,
Kamanda umefanya mambo ya kijinga sana
Kamanda, siwezi kukuvumilia hata kidogo, tumekaa
kikao na kuona kukutoa wewe katika cheo chako
cha TSA 1 na kumpa mtu mwingine,” Madam S
akameza mate, “Kila mara nakuonya na wanawake
wako hutaki kunisikia, kwa nini? Sasa wlitaka
kukuua, mshukuru bwana Shikuku na kijana wake
Ndege, ulikuwa marehemu tayari, na sasa
tungekuwa tunautafuta mwili wako. Kamanda huna
maana tena kwetu na kwa serikali kwa ujumla,
tunaandaa utaratibu wa kukustahafisha hasa kwa
uzembe unaouonesha, unajua wewe ni kama roho ya
serikali, wakikubana wewe watakuwa wamepata kila
kitu, kila siri, na sumu waliyokupa si ajabu
imekufanya utoe siri nyingi bila kujijua.” Madam
akageuka na kuondoka zake na kufunga milango
nyuma yake, Kamanda Amata akabaki kajiinamia
kisha akajitupa kitandani kwa hasira, “Biiiiiilllllll
lllllllll !!!!!!!” alipiga ukelele wa nguvu kisha
akapoteza fahamu. Ilikuwa ni zamu ya madaktari na
wauguzi kuhakikisha wanaokoa maisha ya Kamanda
Amata katika dakika hizo, haikuwa rahisi maana
ilionekana mapigo ya moyo yakishuka zaidi,
walijaribu mbinu zote za kitaalamu lakini bado hali
ilikuwa tete, baada ya kuhangaika kwa muda refu,
kidogo hali yake ilianza kurudi na mapigo ya moyo
yalirejea kwenye hali ya kawaida ingawaje bado
alikuwa katika usingizi mzito uliogubikwa na taswira
ya Bill kama mtu wa kutisha na hatari, aliyetaka
kuyakatisha maisha ya Kamanda kwa mtindo ambao
hakuutegemea, wauguzi na madaktari walishusha
pumzi wakiwa wamekizunguka kitanda cha Amata,
walifarijika zaidi walipomshuhudia akiwa
amefumbua macho akiwaangalia mmoja baada ya
mwingine, “Kuna nini?” aliuliza, “Mbona
mmenizunguka hivyo?”
“Kamanda! Ulikuwa katika hali mbaya sana, kiasi
kwamba bila jitihada za hawa wote tungekukosa,”
Daktari alimueleza akiwa amemuinamia. Ilikuwa
kama hali ya mshangao kwa Amata, alijitazama
kama mtu aliyerukwa na akili, “Yuko wapi Bill?”
aliuliza. “Bill?! Bill ni nani?” aliulizwa na daktari,
Amata alizungusha shingo yake na kuona wauguzi
tu na madaktari, akajilaza kitandani kwa mara
nyingine. “Ok, tumuache apumzike sasa,” ilikuwa ni
kauli ya daktari akiwaambia wale wauguzi pamoja
na wasaidizi wake, wote wakakiacha kile chumba na
kurudi katika idara zao. Akili ya Kamanda Amata
haikutulia, muda wote ilimuwaza Bill, hasira
zikaanza kuuteka moyo wake, maneno ya Madam S
yakamvunja nguvu, ‘Bill anataka kunisababishia
kushushwa cheo na kustahafishwa kabisa,’
alijiwazia; ‘Haiwezekani,’ alinyanyuka katika kile
kitanda alichokilalia, akajichomoa drip iliyokuwa
ikiendelea kuingia mwilini mwake, akatazama huku
na kule hakuona nguo yake yoyote zaidi ya yale
mavazi aliyovaa, mavazi ya hospitalini, hakujali,
akauendea mlango na kutoka, huku na kule, hakuna
mtu, akatoka mlango wa pili na mpaka ule wa nje,
akiwa pale nje alikutana na watu mbalimbali hakujali
wala kushangaa, alipita eneo la walinzi na kufikia
maegesho ya tax, akajichagulia moja, “Wapi mzee?”
dereva Tax alimuuliza, “Kinondoni, mkabala na
Leaders Club,” akampa maelekezo, wakatokomea
kutoka hapo.
“Una simu hapo?” Amata alimuuliza yule dereva tax.
“Ndiyo braza,” akajibiwa.
“Niazime nipige mahali, pia niambie ni shilingi
ngapi,”
“Haina shida, hapa utanipa shilingi elfu thelethini,”
lilikuwa ni jibu lingine la dereva tax.
Kamanda Amata alichukua simu na kubofya namba
Fulani, kisha kuweka sikioni, “Baada tu ya kukata
simu hii, naomba uingize shilingi elfu hamsini
katika namba hii, (…) niangalizie kama kuna ndege
inayoondoka mida hii kupitia Nairobi, iwe inaelekea
hapo au inapita hapo, niandalie safari tafadhari, nina
dharula, call aborted” Akakata simu na kumrudishia,
dedreva tax, akamuamuru kusimama, akashuka na
kuagana nae baada ya kumpa maelekezo kuwa hela
yake itaingia kwa simu.
§§§§§
“Pamoja na maumivu ulonayo, nitakupa malipo yako
ya mwisho, umenifanyia kazi kubwa sana Cheetah,”
Bill Van Getgand alikua akimuangalia Cheetah kwa
jicho la uchungu sana hasa pale kijana huyo
alipokuwa akiugulia kwa maumivu ya jeraha lake,
hakuweza kwenda hospitali kwa kuhofia polisi, hivyo
alijificha katika moja ya magheto yake katika mji
mdogo wa Kinangop ya kaskazini. Bill akatoa bunda
la noti na kumpatia, “Ugawane na Mellina, lakini
usisahau kumnunulia sanda Gichui,” akanyanyuka na
kulitwaa lile begi la ngozi na kumpa Wambugu
kisha kwa kutumia ile fimbo yake akaujongelea
mlango wa kutokea nje ya ghto hilo, akasimama na
kugeuka nyuma, akawa akitazamana na Cheetah.
“Asante braza, nitafanya hilo, wewe ni mwema sana,
maana mwingine angeshapata mzigo wake na
kutoroka hata asingekumbuka kazi kubwa
aliyofanyiwa na swahiba zake,” Cheetah aliongea
kwa tabu kidogo, akionekana wazi ni mwenye
maumivu makali katika jeraha lake. “Nami na
shukuru kwa kazi njema mliyonifanyia, nasikitika
sana juu ya Gichui lakini naamini Mellina mtaonana
usiku huu, lazima akufuate. Kwa kuwa mimi
sijakudhulumu haki yako basi naomba na wewe
usimdhulumu Mellina haki yake. Cheetah lazima
ujue hata waovu wana aina ya wema uliobaki
mioyoni mwao,” Bill akanyanyua ile fimbo yake ya
kutembelea, akaongea huku akiwa ameiyooshea
kwa Cheetah pale kitandani, akitoa maneno ya
faraja na kumshukuru, mkono wake wa kulia
ulioishika ile fimbo ukafyatua kibati Fulani karibu
kabisa na kwa kushikia, ukakibonyeza tena ka
namna nyingine, mara kitu kama msumari
kikachomoka kwa kasi kutoka katika ncha ya fimbo
ile na kuzama moyoni mwa Cheetah, macho
yakamtoka Cheetah, akabaki akimtazama Bill, damu
ilitiririka na kuichafua fulana yake, akalegea na
kudondokea kifuani, “Asta la Vista baby,” Bill
alitamka maneno hayo na kuchukua tena lile bunda
la noti akaligawanya nusu, nusu akaiacha pale
kitandani na nusu akatoka nayo.
“Kuna watu ninaohitajia pumzi zao leo kabla
sijaondoka,” Bill alimwambia Wambugu wakiwa
ndani ya gari yao.
“Mi nilijua ushamaliza kazi kaka,” Wambugu aliijibu
kauli ya Bill
“Hapana, lazima tusafishe makandokando
yanayoweza kutuletea shida wakati wa kula bata,”
Bill aliendelea.
“Kwa hiyo unasemaje?”
“Nina muda mchache sana wa kupotea hapa mjini,
najua natafutwa, nimeshawaona, FBI
ninaowafahamu, watu wa MOSSAD wapo mjini,
ukiachana na wana usalama wa hapa Kenya,
nafurahi tu kuwa Kamnda Amata popote alipo
lazima apoteze uhai, sumu niliyompa ni mbaya
sana,” akakohoa, “Wambugu!” akaita na kumtazama
kijana huyu wa Kikuyu, “nataka roho ya Mellina na
Kahaba Rose ndani ya masaa machache yajayo.”
Ilikuwa ni kauli iliyotaka kumfanya Wambugu
ashindwe kuendesha gari lakini alijikaza kisabuni
nyuma ya usukani na kumeza mate maana alihisi
koo limekauka kau.
“Mi nilifikiri hao hawana maana,” Wambugu aliongea
kwa upole.
“Wakishakufa niulize kwa nini nimewaua
nitakwambia sababu ambayo hata wewe ungewaua,
cheetah tayri nimeshamuua,” Bill alisema huku
akiwasha sigara yake kuvuta akizitupia nywele zake
ndefu mgongoni.
“Simamisha gari pale karibu na ile Subaru,” Bill
aliamuru na Wambugu akasimamsiha kama
alivyoagizwa, Bill akashuka na kulichukua lile begi,
akasimama na kumwangalia Wambugu, “Sikia,
kama unataka maisha yako basi ufunge mdomo,
hakuna ajuaye undani wa sakata hili zaidi zaidi yaw
ewe, Mellina na kahaba Rose. Naomba uchunge
mdomo wako, ila kazi moja ukanifanyie, hakikisha
unamuua Rose na Mellina kabla hujajiua
mwenyewe,” Bill aliongea huku akimrushia kile
kibunda cha pesa Wambugu kupitia dirisha la ile
gari, akakidaka na kukiweka kitini. “Nitakupigia
simu baada ya masaa matatu ili nijue kazi yangu
imefikia wapi, elewa kuwa hauko peke yako,”
akageuka na kuliendea lile gari aina ya Subaru na
kulitupia lile begi kiti cha nyuma kisha yeye akakaa
nyuma ya usukani wa gari ile na kutokomea
akiifuata barabara ya Uganda.
§§§§§
Haikuwa rahisi kwa Madam S kuelewa kile
anachoambiwa na dakatari kuwa Kamnda Amata
ametoroka hospitalini, alibaki kimya huku akiwa
anashindwa kuchanganyikiwa, akizunguka kutoka
upande mmoja kwenda mwingine wa ofisi ile,
akasimama katikati na kumtazama daktari kwa
makini, “Hebu nambie, katoroka au katekwa?”
“Kweli Madam katika hilo siwezi kujibu, mi nimerudi
sikumkuta kila niliyemuuliza anadai hakumuona,”
alimjibu.
Madam S alitoka kwa daktari bila kuaga na
kuielekea gari yake, akaketi ndani na kuitia ufunguo,
switch on, kisha akabonya bonya mahali Fulani.
Skrini ndogo ikachomoza na kujifungua katia ile
dashboard ya gari, akaminya mahali Fulani katika
skrini hio mara ramani kubwa ikatokea, akaingiza
namba Fulani ambazo hutumia kumpata Kamanda
Amata, kwa kujua mahali alipo lakini haikuwa rahisi
kupatikana, alijishika kichwa hajui la kufanya,
akawasha gari na kurudi ofisini.
Mawazo yalimtawala hakujua la kufanya, alishika
hiki mara kile, alijaribu mbinu zote za kitaalam
kupata Kamanda, haikuwa rahisi. Akapata wazo,
akampa kazi Chiba amsake mpka amtie mkononi.
Gina aliegesha gari yake katika maegesho ya uwanja
wa ndege wa Dar es salaam,
“Mtu awaye yote akikuuliza juu yangu mwambie
nipo katika majukumu ya kiserikali, najua Madam S
atakutafuta jioneshe kuwa hata hujui wapi nilipo
zaidi ya Nairobi, kwa heri mpenzi tutaonana tena,”
Kamanda Amata alimkumbatia Gina kumuaga, Gina
alikuwa akitokwa na machozi ya upendo.
“Kamanda, najua hauko sawa sana, lakini
nakuombea urudi salama, mambo yakiwa magumu
basi nipe taarifa nije kukusaidia kwa lolote,” Gina
aliongea sikioni mwa Amata wakiwa bado
wamekumbatiana, kisha wakaachana na Kamanda
akaelekea katika chumba cha wasafiri, huko
haikumchukua muda, akaondoka zake na ndege ya
shirika la ndege la Kenya na kurudi katika jiji la
Nairobi, sasa akiwa binafsi zaidi, hakuna aliyejua
kama yupo huko zaidi ya Gina, katibu muhtasi
wake.
Masaa machache yalimchukua hewani na baadae
kuikanyaga tena ardhi ya Kenya, moja kwa moja
alirudi palepale katika hoteli ya Intercontinental
maana alijua wazi kuwa si pengine pa kuanzia kazi
zaidi ya hapo. Ni masaa ishirini na nne na kidogo
alikuwa mahali hapa, aliingia chumbani kwake na
kukagua harakaharaka kwa macho, akaona jinsi
chumba kilivyopekuliwa kitaalamu lakini zile alama
ndogondogo alizoziweka alikuta haziko vile
kutokana na upekuzi huo, alijaribu kuangalia kama
kuna kitu chochote chenye hatari kwake, lakini
hakukuwako, alipojiridhisha akaweka vitu vyake
sawa na kuketi kitini akiwa tayari na bastola yake
mkononi, alijuwa wazi kwa vyovyote lazima wapo
wanaojua juu ya ujio wake hivyo kuna uwezekano wa
kuja usiku huo, alizima taa na kuketi macho kodo
katika kiti kilichopo kwenye moja ya kona ya
chumba hicho.
Kamanda Amata hakukosea, katikati ya usiku alihisi
mlango ukifunguliwa, akajiweka sawa tayari bastola
yake iliyofungwa kiwambo cha sauti ikiwa mkononi
mwake. Taratibuuuuu mlango ukasukumiwa ndani,
na huyo mtu akajaribu kuwasha taa ya ndani lakini
haikuwakam akachezesha mara kadhaaa ile switch
lakini bado taa haikuwaka. Akavuta hatua chache
ndani na kuingia kisha akarudisha mlango nyuma
yake, kabla hajafanya lolote alijikuta akimulikwa na
mwanga mdogo mwekundu katika kifua chake,
akachangayikiwa hajui la kufanya, mara taa ya
mezani ikawaka kwa mwanga hafifu.
“Tulia hivyo hivyo,” sauti ya Kamanda Amata alitua
katika masikio ya mtu Yule, kama alikuwa hajawahi
kukutana na mtu huyu sasa ilikuwa zamu yake,
miguu ilimchezacheza, alitamani kukimbia lakini
haikuwa hivyo.
“WE nani?” Yule mtu aliuliza.
“Kwani we umekuja kumfuata nani?” Amata alijibu
kwa swali. Risasi ya kwanza ikavunja mguu wa mtu
Yule kabla hajajiweka vizuri pale chini alipokuwa
akiugulia kwa maumivu tayari Kamanda Amata
alikuwa amemfikia na kumkanyaga kwenye jeraha
hilo lililokuwa likivuja damu mbichi.
“Jibu maswali yangu, nikuache hai,” Kamanda
alianza namna hiyo, “Nani amekutuma?” akaanza
namna hiyo.
“Mimetumwa na boss kaka,”
“Sawa, nitajie jina lake,”
“Mi simjui kaka, simjui kabisa,” alijibu huku akilia
kwa maumivu.
“Sikiliza wewe bwege, ukilia utasumbua watu
kwenye vyumba vingine, jibu maswali kwa ufasaha,
sawa?!” Kamanda aliuliza kwa ukali huku bado
akikandamiza lile jeraha la Yule mtu.
“Basi kaka nasema, nasema, usiniumize nasema,”
akameza mate, kisha akaendelea, “Tumetumwa na
mtu mmoja anaitwa Wambugu”
“Kawatuma nini?” lilikuwa swali lingine kutoka kwa
Amata.
“Begi na nyaraka nyingine za muhimu kama zipo,”
“Ok, nay eye yuko wapi?”
“Kuna kazi nyingine anafanya huko mjini,” alipojibu
hayo mara simu yake ya mkononi ikaita kutoka
katika mfuko wa jeans, Amata akainyakuwa na
kusoma jina lililopo hapo juu ‘Moriyo’, “Moriyo ndo
nani?” Amata aliuliza tena.
“Ni mwenzangu yuko hapo chini ananisubiri,
tumeambiwa tupeleke haraka hilo begi,” Kamanda
Amata hakupenda kupoteza muda, alimuwekea ile
bastola katika sikio lake la kuume, “Usiniue kaka,
nina watoto mimi watalelewa na nani?” alilia kwa
uchungu.
“Ungekuwa na watoto unaowajali, ungefanya kazi za
kishetani kama hizi, sikuui lakini lazima uwe
mlemavu ili siku zote za maisha yako umkumbuke
Kamanda Amata,” alipotamka jina hilo, akamuona
Yule jamaa akishituka na kuguna kama aliyekutana
na jinamizi.
“Umesema we nani?” aliliza hata akawa amesahau
kama ana jeraha baya la risasi katika goti lake,
“Amata, Kamanda Amata, na siyo mzimu ni mimi
mwenyewe halisi, namtaka huyo Wambugu na
mwenzake Bill,” Yule jamaa bado aliduwaa
akimkodolea macho Amata, “WE umeshakufa kaka,”
Yule jamaa aliongea kwa unyonge.
“Ni sawa, na sasa nimefufuka kutoa wafu kama
nilivyosema,” kabla hajaendelea na lolote, Kamanda
Amata alimshuhudia Yule jamaa akitapatapa
akirusha miguu huku na kule, alipomtazama vizuri,
aligundua tundu la risasi kifuani mwake, risasi
imepigwa wakati gani, kitendawili. Alichosikia yeye
ni mvumo hafifu wa kitu kama nyigu kumbe tayari
chuma hicho kilishatumwa kutoa uhai wa mtu.
Amata alitazama huku na kule bado ukimya
ulitawala, mara akasikia nyayo za mtu zikitembea
harakaharaka kwenye korido, akatoka haraka na
kuufungua mlango , akashuhudia mtu akiishia
kwenye lifti ya jingo hilo, haraka akakimbia na
kuziwahi ngazi za kushukia chini na kuteremka nazo.
Kamanda Amata alfika chini na kushsudia Yule mtu
akiwahi kuingia katika gari Fulani, lakini kabla
hajaisjia garini, tayari shabaha isiyo na chembe ya
uongo kutoka katika mikono makini ya Kamanda
Amata, Tanzania Secret Agency ilikuwa
imeshafumua ubongo wa kiumbe huyo na kumfanya
alalie kiti cha dereva bila uhai huku miguu ake bado
ikiwa nje ya gari hiyo, kazi imeanza. Hakumjali
marehemu wa ndani wala nje, aliichukua ile simu
aliyokuwa ameichukua kwa Yule jamaa wa kule
ndani na kuifungua, haikuwa na namba hata moja,
akenda kwenye meseji pale mwili ulimsisimka hata
nywele alihisi zina simama baada ya kukutana na
ujumbe uliondikwa,
‘Hakikisha kahaba Rose anauawa kabla ya jua la
asubuhi, kisha nitakupa kazi ingine,’
‘Kahaba Rose,’ Kamanda Amata alilirudia jina hilo
akilini mwake mara kwa mara, akiwa amesimama
kwenye kiambaza cha ukuta aliendelea kusukuti juu
ya kahaba huyo kamanahusika na lolote katika
sakata hili, lakini muunganiko wa matukio haukuwa
sawa kwake, alimfikiria Yule mwanamke aliyepewa
kumstarehesha kama ndiye lakini haikuwa hivyo,
nwuisho alimua la kuamua, kumsaka kahaba ni kazi
ndogo sana, aliweka bastola yake mfukoni na
kuiendea simu iliyokuwa jirani, ‘simu ya jamii’
akukwanyua mkono kutoka katika kikalio chake na
kubofya namba yenye tarakimu tatu na kusikiliza
upande wa pili.
“Yes hallo tukusaidie nini?” ilikuwa ni sauti ya polisi
wa kikenya, ambayo ilitaka kumfanya Amata
kucheka lakini hakufanya hivyo.
“Intercontinental hotel, kuna mauaji yametokea na
pia kwenye maegesho ya gari ya hoteli iyo hiyo pia
kuna mauaji mengine yametokea,” kisha akakta
simu, halafu akacheka kutokana nay eye kuiga
lafudhi ile ya kikenya. Alitoka eneo lile na kubana
sehemu nyingine, muda kidogo alishuhudia gari
mbili za polisi waliofika eneo hilo na kuivamia
hoteli hiyo, alipoona hilo kwake limewezekana,
akabaki na kazi yingine ngumu ya kumpata kahaba
Rose na vipi awe ahusiki na hili, lilikuwa swali
linguine, akasonya na kuingia mtaani akiacha
hekaheka za wale askari zikiendelea.
§§§§§
Jua change la Nairobi lilianza kuikwea anga tulivu la
jiji hilo, watu huku na huko walikuwa wakiwahi
makazini, wengien kwenye matatu na wengine kwa
miuu yao wenyewe, ilimradi tu ilionekana asubuhi
tulivu.
Lakini hali haikuwa hivo katika kanisa kuu la Familia
takatifu, wakiwa bado hawajaondokewa na majonzi
ya kifo cha Fr Gichuru, asubuhi hii wanaamka na
kupotelewa na monstrance ambayo ililetwa kutoka
Vaticna, maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya
jubilee ya miaka mia moja ya ukristu nchini hapo.
‘Kwa nini wameichukua?’ lilikuwa ni swaligumu
kidogo kwa maana hakuna aliyejua lolote juu
yachombo hicho zaidi ya yeye anayekitafuta.
“Tutaieleza nini Vatican?” sauti ya masikitiko
ilimtoka mhashamu askofu Njue iliyotoka kwa tabu
kidogo kutokana na uzee uliokuwa ukipiga hodi kwa
kasi ya ajabu iliwafikia makasisi wachache
waliokuwa wameketi pamoja nae katika meza yake
kubwa anayoitumia kwa mikutano na wasaidizi
wake hao, wakiwa katika hali ya ukimya hakuna
aliyekuwa na jibu sahihi juu ya swali hilo lililoulizwa
na baba Askofu.
Habari ya kuibiwa kwa Monstrance hiyo ilitapakaa
kama upepo wa pwani, kila mtu alisema lile ambalo
kwake lilikuwa ni sahihi. Mapigano ya polisi na
majambazi usiku uliotangulia lilikuwa gumzo
linginem kukutwa kwa mwili wa Cheetah katika
ghetto ilikuwa ndiyo habari ya kuvutia zaidi kwani
jmbazi hilo sugu limetingisha sehemu mbalimbali
lakini hakuna watu walioweza kumtia mbaroni, kila
mtu hakuna aliyejua, jambazi huyo amekufaje,
wengine walionekana kufurahia kifo hicho lakini
wengine walisikitika ‘kwa nini hawakumkamata hai’
basi ilimradi ni mazungumzo mchanganyiko.
Hakuna aliyezungumzia mauaji ya kasisi ambayo ni
wiki moja tu imepita bali kila mtu alikuwa anavytiwa
na vifo vya majambazi hao wawili na kuibiwa kile
chombo kitakatifu. Magazeti hayakuwa mbali
kupamba kurasa za mbele kwa picha na habari
moto moto.
Ni sergeant Maria tu aliyesimama katika uwanja wa
kanisa hilo akiwa hana furaha sana, akiwa na askari
wawili wenye furaha, walionekana wakizungumza
jambo Fulani na paroko wa kanisa hilo Fr Joh
Smith, wakipeana maelekezo ya hapa na pale,
wakitazama hiki na kile, baada ya mazungumzo
marefu waliagana na kuahidi kurudi tena kwa
uchunguzi wa kina.
“Afande,” mmoja wale askari aliita, Sargeant Maria
akageuka kumtazama kwa jicho lake kali,
“Inaonekana hauna furaha, nini tatizo zaidi?”
“Furaha yangu ingekuwa kubwa kama Cheetah,
angepatikana na roho yake, lakini haikuwa hivyo,
kwa desturi ya majambazi lazima wamegeukana
katika malipo,” Sargeant Mari alijibu huku akijiingiza
kwenye gari ake.
“Itakuwa Mellina kamgeuka Cheetah, hilo
linawezekana? Maana aliyebaki hai ni yeye tu na
hapa amekimbia,” Yule askari aliongeza maswali,
Sargeant Maria Litulia kwa muda kisha akainua uso
wake na kumwangalia kija huyu, “Umenipa wazo
jipya, Mellina anaweza asiwe aliyemuua Cheetah,
uko sawa, sasa nani? Wambugu au Bill!! Kazi bado
ngumu, twendeni kituoni,” aliamuru huku akiwa
anatoa kalamu na kijitabu chake akaandika mambo
Fulani Fulani humo.
Sergeant Maria akiwa tayari akili yaje imekaa vyema
alimuru vijana wake waanze msako kumsaka
Mellina popote atakapopatikana na aletwe akiwa hai
ili aeleze kisha chote kabisa na sababu ya wao
kufanya hayo yote. Jeshi la polisi likajipanga
kuhakikisha ile monstrance inapatikana na Mellina
anatiwa nguvuni wakati huohuo idara kubwa za
usalamaa zimejipanga kumtia nguvu Bill Van
Vetgand, wakiwa hata hawana habari ya ujambazi
huo wakiuona kwao ni matukio ya kipolisi ya kila
siku, wakiwa hawajui kuwa kuna muungano mkubwa
katika hayo yote mawili, wao walikaza jicho lao kwa
jasusi Bill pekee, wakiwa wamemtega kila upande
kwa kila mtindo lakini walishangaa Bill hakuonekana
mjini kote, ametoweka. Hali hii iliwafanya
kuchanganyikiwa zaidi, atatowekeaje wakati njia zote
za kutokea nje ya Nairobi zimefungwa na
wanausalama? Hii iliwapa moyo FBI na vyombo
vinine kuwa mtu huyu hatari bado yupo Nairobi,
hivyo waliongeza msako tuli, msako usiyo na fujo.
Siku hiyo asubuhi, kikao kifupi cha maafisa wa
polisi kilikuwa kikiendelea katika ofisi ya mkuu wa
polisi mkoa wa kati, Inspekta Saitoti.
“Sargeant Maria, nahitaji hizo tafutishi haraka,
Mellina kama nilivyokuagiza, namhitaji hapa, hiyo
Monstrance lazima ipatikane kwa udi na uvumba,
pia nahitaji uchunguzi wa kina juu ya mauaji pale
hotelini ili tujue kama vina uhusiano au la,” Saitoti
alizungumza kwa ukali huku akiirekebisha kofis yake
kichwani mwake.
“Sawa afande, opereshen inaendelea na kikosi kipo
kazini, ripoti itakuja jioni afande,” Maria alijibu
kiaskari.
“Nakuaminia sana, piga kazi,” alimalizia Saitoti.
Sargeant Maria alitoka ofisini akionekana kusawajika
uso wake kwa mawazo lukuki, akapita kaunta na
kuzunguka nyuma ya kituo hicho ambapo kuna
mgahawa mdogo na kuketi ndani yake, kisha
akaagiza sturungi (Sturungi ni chai ya rangi) ili
imchangamshe kidogo. Akiwa katika meza hiyo
pamoja na maafande wengine, mara kijana mmoja
mchafu sana aliingia kwenye mgahawa huo na
kuketi mbele ya sergeant Maria, wakatazamana
macho, maria akakunja sura yake kuonesha
hakuridhika kwa kijana huyo kuketi hapo.
“Afande, nna njaa, ninunulie japo chai kisha
nitakutatulia tatizo lako linalokuumiza kichwa,” yule
kijana akajieleza, Maria alimwangalia tena na tena.
“Niambie kwanza!” Maria alidai lakini yule kijana
akawa kimya akimtazama afande huyo wa kike
aliyeshupaa kwa misuli kama mwanaume.
Sergeant Maria akamuagizia chai Yule kijana na
kumpatia, naye akaanza kunywa kwa fujo bila kujali
kama chai hiyo ni ya moto, alionekana hasa ana
njaa kali asubuhi hiyo. Maria alitazama saa yake na
kuona tayari asubuhi imepamba moto anahitaji
kwenda katika majukumu mengine.
“Naona una haraka ya kuondoka, subiri kwanza,”
Yule kijana akamueleza Maria, naye akavuta subira,
akatulia kitini na kuanza kusoma gazeti la Daily
Nation. Yule kijana alipomaliza kunywa ile chai
akamshukuru sana sergeant Maria aliyekuwa
ameketi mbele yake.
“Afande, usione mi nimevaa hivi labda ukafikiri ni
kichaa au mvuta bangi, hapana, nina akili na ni
mzima kabisa, hii ni moja tu ya miondoko ya mji
mkubwa kama huu” akameza mate na kuendelea na
hab ari yake ambayo sergeant Maria aliona kama
anapotezewa muda, “Najua unaona kama
nakupotezea muda, lakini kazi unayoenda kuifanya
mimi ndio nitakupa msaada mkubwa sana, sikia,
hiyo kesi unayoifuatilia ya Mauaji ya kasisi ni kesi
pan asana kuliko wewe na wenzako
mnavyoichukulia, ninyi mnatazama mauaji ya Fr
Gichuru, na kumsaka muuaji na monstrance
iliyopotea, lakini hali sivyo ilivyo, kwa uwezo wenu
nyie lazima mtaishia katikati kwani katika kesi hiyo
kuna mkono wa kimataifa, mkono nambao pambano
lake lazima liwe la kimataifa vilevile,” kabla
hajaendelea, sergeant Maria alimkatisha,
“Unasemaje wewe?” Yule kijana akarudia
kumwambia yale yote aliyokwisha sema, “Mimi
nilishuhudia Fr Gichuru alivyotekwa, alivyofungwa na
kupewa mateso makali, lakini usiku huo akatoweka
pale alipofungwa, nilikuwa mlinzi katika godown
moja ambalo huyo marehemu alifungwa, na tulipata
shida sana baada ya kutoweka kwake, na wale
waliomteka waliapa kumuua pindi tu
watakapomuona, na ndivyo ilivyokuwa”
Sasa sergeant Maria alionekana kuvutiwa na simulizi
hii tamu ambayo iliifanya damu yake kuchemka
kikazi, “Nambie kwa nini unasema ya kimataifa?”
akamuuliza.
“Nasema ya kimataifa kwa kuwa kati ya watu
waliomleta kulikuwa na bosi wao ambaye kwa
mazungumzo yao ya harakaharaka anatoka nje ya
nchi na ndiye aliyewatuma hawa majambazi na
aliwaahidi pesa nyingi sana,” Yule kijana akaeleza.
Sergeant Maria akavuta kumbukumbu na
kukumbuka kuwa walipoikuta maiti ya Cheetah
kulikuwa na burungutu la hela, hela nyingi kuliko
unavyofikiria zikiwa zimetupwa juu ya mwili huo,
akatikisa kichwa juu chini kuonesha kuwa ameliafiki
hilo.
“Ok, hebu nambie, hao waliomleta au kumteka
hasahasa walikuwa wanataka nini kwake?” Maria
alitupa swali linguine.
“Walikuwa wanadai awaoneshe monstrance, lakini
yeye alikataa kata kata ndiyo maana walimtesa sana
hata kuzimia mara nyingi kwa kipigo,” Yule kijana
alijibu.
“Na alitoweka vipi?” Maria aliuliza, huku akindiki vitu
Fulani katika kijitabu chake.
“Hapo ndipo utata unapojitokeza, maana asubuhi
mimi na mwenzangu tulipoenda kumtazama
hatukumkuta, lakini miongoni mwetu mlinzi mmoja
pia hakuonekana mpaka baada ya siku mbili
tulipogundua mwili wake katika pipa la takataka
ukiwa hauna uhai, tukateswa sana tuseme ni wapi
ametorokea mateka wao lakini hatukujua, ndipo
name nilipotoroka na kujificha huko Korogocho,
najua kuwa sakata hili halijaisha ipo siku hata mi
nitakuwa mikononi mwa wanaharamu wale, najua
wataniua kwani ninalijua hili, nikaapa kumtafuta Yule
atakayekuwa ameishika kesi hii ndipo nilipojua ni
wewe nikakutafuta,” Yule kijana alimaliza maelezo
yake.
“Sasa wewe unanisaidiaje katika hili?” sergeant
Maria aliuliza.
“Sina msaada afande zaidi ni kukuambia tu,
usiumize kichwa, ukilifuatilia hili hakika utakufa,
waache wakubwa wafanye yao,” Yule kijana sasa
aliongea kwa msisitizo kidogo. Sergeant Maria
alikuwa akimuangalia kwa kugeuzageuza kichwa
chake kana kwamba haelewi analoambiwa,
akainama chini kufikiri kitu Fulani alipoiunua kichwa
chake kumtazama Yule mtu, hakumuona pale
alipokaa, badala yake kiti kile kilikuwa kimekaliwa
na askari mwingine wa kike, wakasaliamiana lakini
Mria alionekana kuchanganyikiwa kwa hilo, “Afande,
aliyekaa hapa yuko wapi?” aliuliza. “Mbona hapa
hapakuwa na mtu afande!” lile jibu likazidi
kumdidimiza katia shimo la mawazo, akanyanyuka
haraka na kutoka nje ya mgahawa huo, akatazama
huku na huku asione mtu, akazunguka upande wa
pili hali hiyo hiyo, akajishika kiuno na kufikiria mara
mbili kama alikuwa amekaa na mzimu au binadamu
wa kweli. Lakini katia yote hayo bado hali ilikuwa
ileile kuwa Yule mtu hayupo pale.
ITAENDELEA.....
 
SEHEMU YA 8
§§§§§
“Baby, mbona hivyo? Unaniumiza mwenzio,
umenitafuta usiku wenye baridi kali nije nikuliwaze
lakini tuko kitandani, mwenzangu huoneshi
ushirikiano, mmm sweet nambie shida nini?”
Kahaba Rose alikuwa akinung’unika kitandani
alipokuwa amelala na Kamanda Amata usiku huo,
baada ya Amata kumtafuta kahaba huyo kati viunga
vyote vya mji wa Nairobi, ndipo alipoambiwa na
mmoja wa makahaba katika mtaa wa Koinange
kuwa Rose alipata ‘Big Deal’ hivyo ni siku kadhaa
hayupo barabarani, lakini kwa msaada
walimuelekeza wapi anaishia naye kamanda
akamfungia safari mpaka nyumbani kwake na
kumkuta, akamchukua na kumueleza shida yake
kuwa anataka huduma yake usiku huo, kwa kuwa
Rose alikuwa hana kaziingine usiku huo alikubaliana
naye na kutoka mpaka kwenye hoteli moja isiyo na
jina katika mitaa ya Mathare na kuchukua chumba
hapo.
Kamanda Amata hakutaka penzi la kahaba huyo bali
alikuwa na yake moyoni, alimtazama Yule kahaba
na kutingisha kichwa, alikuwa mwanamke mzuri wa
sura, mtamu wa umbo, mwenye miguu minene ya
kuridhisha, hips zilizojaa, macho ambayo
yakikutazama utaona jinsi mwili wako unavyolegea
mbele yake, hakika alikuwa mrembo.
“Sikia mrembo,” Amata alinguruma, “Yes Baby,”
Rose alijibu huku akijisogeza na kujilaza juu ya kifua
cha Amata, “nimekutafuta sana leo siku ya saba,
ulikuwa wapi? Maana sifa za urembo wako
zimenifikia nikiwa Kongo,” uongo ukaanza kuchukua
nafasi, Rose akatabasamu na vibonyo viwili
vikajitokeza katika mashavu yake.
“Nilipata kazi ya wiki mbili kwa tajiri mmoja wa
kizungu, ana pesa kama matundu ya neti, lakini
hatujamaliza kazi yetu, simuoni tangu juzi na simu
zake hazipatikani, kwangu si shida maadamu
kanilipa parefu,” Rose alieleza kwa sauti yake tamu
ya kumtoa nyoka pangoni.
“Hongera motto mzuri, huyo tajiri ni nani anayeiacha
starehe tamu kama yako na kutokomea?” Kamanda
Amata alitupa swali. “Aaaa si unajua tena wenye
pesa wanafanya lolote, muda wowote wanapoamua,
anaitwa Mr Bill, lakini tusiongelee habari za
mwanaume mwingine, tuongee yetu,” Rose alijibu.
“Sawa, lakini mimi nataka nimuone Bill,
amenidhulumu pesa yangu, kuna kazi alinipa
nimemfanyia kwa ukamilifu lakini hajanilipa,” Amata
aliendelea.
“We Bill unamjua?” Rose akauliza kwa mshangao na
kujitoa katika kifua cha Kamanda Amata. Amata
akatoa picha ndogo na kumuonesha, “Huyu siyo?”
akamuuliza na kumpa ile picha.
“Ni yeye,” Rose alijibu huku akimrudishia ile picha,
“Pole sana nafikiri itakuwa mmedhulumiana na si
kakudhulumu, mbona ni mtu poa sana huyu!”
aliendelea. “Lazima awe poa kwako lakini si
kwangu, Bill alikupa deal gani mrembo?” alijibu hoja
ya Rose na kumuunganishia na swali.
“Aaa, starehe za ngono na kazi binafsi za kukutana
na watu wake anaowataka,” Rose akaanza
kumpapasa Amata maeneo ya kitovuni mara
akaanza kukinyonya kitovu hicho huku mkono wake
mmoja ukiwa safarini kuelekea ndani ya boxer ya
Kamanda, hali ikawa tete kidogo kwani macho ya
Kamanda yalipotua katika kiunno cha binti huyo
alikuwa katika mtindo wa kifudifudi na kulifanya
shuka llililomsiti kuangukia upande wa pili,
alishuhudia kiuno kicho kutangulia na makalio yenye
kuvutia, mkono wake ulitamani kuyaminyaminya
lakini akajikataza kwani bado alikuwa hajakamilisha
analotaka kwanza.
“Baby, nipe cha asubuhi,” Rose alilalamika huku
akijiinua na kupiga magoti huku akiiweka kati ya
mapaja yake miguu ya Amata, mokono wake ukiwa
tayari umeshachoropoa ndungula ya Kamanda na
kuiweka nje.
“Rose, najua na nitakupa subiri kidogo.” Akamtoa
pale alipo na kuliendea dirisha kisha akamuita Rose
pale dirishani, “Tazama,” akamuambia, “Nini?” Rose
akauliza, Kamanda Amata akamgeukia Kahaba Rose
na kumtazama usoni, “Leo hii usingeyaona haya
yote kwa maana ulitakiwa kuuawa kabla ya mawio,”
Rose alishtuka kwa kauli hiyo, Kamanda akaendelea,
“Nilikuja kwako nikuokoe kwa hilo na siyo mapenzi,
rafiki yako Bill alitaka kutekeleza mauaji hayo kwa
kutumia vijana wake,” alipomaliza kumwambia hilo
akaichukua ile simu ya Yule marehemu na
kumuonesha ile meseji, Rose akajitupa kitandani na
kulia kwa uchungu
§§§§§
Wambugu alijikuta anashindwa kuchanganyikiwa
baada kujua kuwa viajana wake wameuawa kule
hotelini, na Kahaba Rose hayupo nyumbani kwake,
alibaki kajifungia ndani akiogopa hata kutoka nje,
macho yake yote yakiwa kwenye TV na simu yake.
Hakuna akili nyingine iliyokuwa kichwani mwake
zaidi ya kutoroka nje ya nchi, lakini kila
alipomuwaza Bill alijikuta anaishiwa nguvu na
kurejea kitini, maji yamezidi unga!
‘Nitagundulika,’ alijiwazia. Lakini bado maswali
mengi yalikuja juu ya nani aliyetekeleza mauaji ya
vijana wake pale hotelini, hakupata jibu. ‘Bill
kaniachia msala, kanitoroka,’ alijiwazia mara kwa
mara, lakini hakupata muda wa kujijibu, mara
mlango wake ukagongwa, akashtuka nusu ya
kuanguka ijapokuwa alikuwa ameketi kitini, taratiibu
akaufuata mlango na kuufungua kwa woga, ‘Polisi?!’
alijiwazia, alipoufungua akakutana uso kwa uso na
mwanamke kibonge alijitumbukiza kwenye baibui
jeusi lililoruhusu macho tu kuonekana, kabla
hajamkaribisha Yule mwanamke akapitiliza ndani na
kuubamiza mlango nyuma yake.
“Unatetemeka nini mwanaume?” Yule mwanamke
akauliza, Wambugu akabaki ameduwaa kwa sauti
hiyo aliyoitambua vyema, “Nyie ni washenzi, wewe
na Yule nguruwe wako, Bill,” ilikuwa ni sauti kavu ya
Mellina ikimueleza hayo Wambugu ambaye
alionekana hana la kufanya, Mellina akaendelea,
“Ujio wangu hapa unapopaona wewe mafichoni, ni
kuchukua pesa yangu, nataka kusepa leo hii, mji
ushachafuka, njagu kila kona, haya fanya fasta”
“Mbona pesa zako tulimpa Cheetah,” Wambugu
akajibu.
“Cheetah!? Msinifanye mi mjinga, Bill kamuua
Cheetah na nimeiona hiyo action kwa macho yangu
kwa taarifa yako, sasa sema napata pesa sipati? Mi
sina muda wa kupoteza,” Mellina alifoka.
“Pesa nakupa Mellina, lakini naomba jambo moja,”
Wambugu akatulia kidogo, kisha akendelea, “Mimi
hapa nilikuwa nataka kutoroka na kiukweli Bill
alishasema wewe uuawe, ila sioni umaana wa hilo,
tufanye mpango tutoroke pamoja, unasemaje?”
Mellina alitulia kimya kwa sekunde kadhaa, kisha
akanyanyua uso wake kumtazama Wambugu,
“Sikuamini hata kidogo,” Mellina alimwambia
Wambugu, akatulia kidogo na kuendelea, “Nipe
pesa kwanza mengine tutaongea.” Wambugu
akavuta begi lake na kuingiza mkono ndani yake,
alipoutoa akaibuka na donge nono la pesa, mellina
akatabasamu alipokuwa anapokea pesa yake,
akaitia ndani ya baibui lake na kugeuka kuondoka,
“Kila mtu afe na dhambi zake,” alitamka maneno
hayo akiwa ameshika kitasa tayari kutoka nje, mara
nyuma yake akasikia mlio hafifu wa kilinda usalama
cha bastola, kabla hajageuka, chuma baridi
kikamgusa kisogoni, “Ha ha ha ha ha, huwezi
kutoka hapa ukiwa hai, never” sauti ya Wambugu
ilisikika nyuma yake …
Mellina alisimama ghafla, akameza funda la mate
lililokuwa kinywani mwake, hakugeuka haraka kwa
kuwa hakujua adui yake sasa amejiandaa vipi.
“Kwa hiyo ndio hila zako sio?” Mellina akamuuliza
Wambugu huku bado akiwa anaangalia mbele.
“Nilishapewa kazi na Bill nikumalize ili kuondoa
ushahidi wowote usio na tija,” Wambugu alijibu
kijeuri.
“Kwa hiyo katika orodha uliyopewa, umeshaua
wangapi?” Mellina aliuliza, alitumia mbinu ya
kuongea ikiwa ni moja ya kumzubaisha Wambugu
kabla hajapanga ni nini cha kufanya katika hali
kama hiyo amabayo kwayo hakuna masikhara kwani
maisha yako yapo kwa adui yako.
“Bill alishamaliza kazi yake, na alishapata kile
anachokitaka, hivyo basi ninyi mlioshiriki ambao
mnaweza mkatoa siri hii lazima msiwepo katika uso
wa dunia, Gichui amekwenda, Cheetah hayupo,
umebaki wewe na Kahaba Rose ambaye muda si
mrefu roho yake itakuwa mikononi mwangu,”
Wambugu aliongea kwa pozi, wakati Mellina alikuwa
akifikiri juu ya shambulizi linalofuata, shambulizi la
ghafla ambalo akili yake ilikuwa ikiushawishi mwili
nini cha kufanya ambacho madhara yake yatakuwa
kwa adui.
“Na katika hao wanaojua hiyo siri, wanaotakiwa
kuuawa, unafikiri wewe haumo?” Mellina
alimwambia Wambugu kauli ambayo ilimfanya
kustuka kidogo, na kukumbuka kuwa kumbe hata
yeye mwenyewe yupo kati ya wanaojua, akiwa katika
kiutafakari hayo mara Mellina aligeuka kwa ghafla
na mkono wake wa kulia ukakamata korodani za
Wambugu.
“Aaaaaaaaiiiiggghhhh!!!!!” yowe la uchungu
likamtoka Wambugu na kuitoa ile bastola kichwani
mwa Mellina. Sasa Mellina na Wambugu walikuwa
wakitazamana, sura ya Mellina iliyogeuka kutoka
katika uzuri wa kike na kuwa ya kikatili kama
mnyama ilikuwa imekaza macho kwa Wambugu
aliyekuwa akilia kwa maumivu.\
“Sikia wewe mwanaume mjinga, Bill anataka kukuua
na wewe vilevile, sasa kabla hajakuua yeye mimi
naanza,” Mellina aliunguruma huku akizidi kuziminya
korodani za Wambugu na kuzizungusha, maumivu
makali yalikuwa yakimpata Wambugu kabla
hajatulia, Mellina alimpiga kichwa kimoja cha nguvu
na kumuachia Wambugu alipepesuka na kudondoke
kwenye kijimeza kidogo kilichokuwa ndani ya
chumba hicho hukun ile bastola ikiwa chini
sakafuni, Mellina akaiokota, kulichukua lile koba
lenye fedha na kuanza kuondoka.
“Mellinaaaaaa!” Wambugu alipiga kelele hasa
alipoona Mellina amenyanyua koba la fedha, Mellina
aligeuka na ile bastola mkononi, “Kelele wewe
kubwa jinga,” alimtuliza kwa mtindo huo huku
akifyatua risasi kadhaa pembeni kabisa mwa pale
alipoangukia Wambugu na kuchimba sakafu na
ukuta kuacha mashimo, akatoa sonyo refu na
kumuacha Wambugu hoi katota kwa mkojo.
Mellina akaubamiza mlango nyuma yake na
kukamata tax iliyokuwa ikipita hapo muda huo na
kutokomea zake. Huku nyuma Wambugu alipopata
akili alinyanyuka haraka na kukimbilia mlangoni
hakuna alichoshuhudia zaidi ya vumbi jekundu
lililobakisha hapo na ile gari, Wambugu alilikimbiza
kwa miguu lakini hakufanikiwa alianguka chini na
kuanza kulia akijigalagaza kama motto na mwili
wote kuwa mwekundu kwa lile vumbi.
“Bingo!” Mellina alijikuta akitamka neon hilo
alipokuwa katika siti ya nyuma ya ile tax baada ya
kupekuwa na kukuta maburungutu kadhaa ya pesa,
“Wapi dada?” ilikuwa sauti ya dereva tax ikimuuliza
Mellina, ndipo Mellina alipokumbuka kuwa yupo
kwenye tax, “Nipeleke Nakuru,” Mellina alijibu. Yule
dreva tax alikuwa kama kichaa vile, akakanyaga
mafuta na kuchukua barabara ya kuelekea Nakuru,”
§§§§§
Madam S alikuwa amesimama karibu na dirisha la
ofisi yake, dirisha kubwa lililokuwa likikupa
mandhari nzuri ya bahari ya Hindi, alitazama upande
huo wa bahari, alipotosheka akageuka na kurudi
kitini kwake pale ambapo aliwaacha wageni wake
wameketi.
“Ndio Madam, unaonekana mtu mwenye mawazo
sana,” mmoja wao alianzisha mazungumzo.
“Yeah na ndilo swala hasa ambalo nimekuitieni
hapa,” Madam S alijibu, akainua bilauri yake yenye
maji na kunywa kisha akaitua mezani, “Kamanda
Amata ametoweka hospitalini na haijulikani wapi
alipo, mkiwa kama wanaintelijensia nataka mnipe
maelezo ya kina labda nini mnakihisi kimetokea,
maana leo ni karibu siku ya tatu, na hatuna maelezo
yakutosha, hapa ninavyokuambieni mzee katuma fax
na inabidi ifanyiwe kazi haraka. Nyote mnajua
umuhimu wa Amata, kichwa chake kimejaa siri
asilimia 99 za serikali, hivyo haiwezekani apotee tu
namna hii,” Madam S alianza kuzungumza
akionekana wazi kuwa swala hilo limemuumiza
kichwa kuliko maelezo. Aliwatazama wale vijana
wanne waliokuwa mbele yake waliotulia kama
vinyago vya mmakonde maana hawakuwa wakitisika
wala kupepesa macho.
“Madam, Kamanda ni mtu wa kisasi sana
asiyekubali kushindwa, je hatokuwa amerudi Nairobi
kumsaka mbaya wake?” mmoja wao aliuliza.
Madam S alionekana akiandika vitu Fulani kati
kijidaftari chake cha kumbukumbu, kisha akainua
uso na kumwangalia yule aliyeuliza, “Yote
yanawezekana, tumetoa taarifa ofisi husika ya
usalama pale Nairobi, nao wanajaribu kumwangalia
kama yupo huko lakini bado hawajatupa jibu, ila
sijui kwa maana hata yule msichana wake hakuna
anachojua juu ya hili na hii si kawaida.” Alijibu
Madam S.
“Ukicheki namba zake za siri kwenye mtandao vipi
hazionekani?” mwingine aliuliza.
“Namba zake nazo hazioneshi chochote, maana
nimempa hiyo kazi Chiba lakini mpaka sasa
anasema hamuoni kwa namba zake, akijaribu
juelekeo wa simu anasema pia hazisomi kwa
maana simu zake zote zilizimwa juzi pale airport na
ndio signal ya mwisho inasoma hapo,” Madam S
alishusha pumzi ndefu na kujiweka sawa kitini,
“Dah, Kamanda!’ alijiwazia huku akifikicha jicho lake.
“Kwa hiyo Madam unasemaje?” yule watatu aliuliza
“Nataka mfanye kila njia mumtafute na hakikisheni
mmempata kisha mniambie yuko wapi,” Madam S
alimjibu, akawapa kazi ya kumsaka Amata kwa
kuwa yeye hatakiwi kupotea mbele ya macho ya
wakubwa wake kutokana na kazi na cheo
alichonacho.
Siku tatu nyuma…
TAARIFA za kushushwa cheo kwa Kamanda Amata
hazikumfurahisha hata kidogo, baada ya Madam S
kutoka pale hospitali, Amata alitafakari sana na
kuumia moyoni, alijikuta anamchukia kila mtu.
Alipogundua kuwa wauguai wote wametoka na yuko
peke yake katika kile chumba akatoka kitandani na
kutorokea upande wa nyuma ambako alipitia katika
dirisha kubwa la alluminium. Akachukua tax na
moja kwa moja alielekea nyumbani kwake maeneo
ya Kinondoni.
Akiwa nyumbani kwake alijua wazi kuwa lazima
atatafutwa kwa mtindo wowote ule, alijaribu
kuangalia kila kitu ambacho kingemfanya ajulikane
alipo, simu, saa ya mkononi, headphone set na kila
kitu, kitu kimoja alitaka kukisahau ‘micro chip’ ya
kielektroniki ambayo alipandikizwa katika kwapa
lake la kushoto ambayo inawasiliana na satellite
moja kwa moja hivyo kutoka ofisi ya mawasiliano
ya kitengo chao wanaweza kumuona muda wote
kwa namba maalum ambazo zinamtambulisha.
Kamanda Amata alijua wazi kuwa hiyo chip sasa
ndiyo inayomweza kumuharibia, akaona isiwe tabu,
alijaribu kuminyaminya katika kwapa lake na
kugundua wapi ipo kutokana na umbo lake la
mcheduara lenye ukubwa kama punje ya mchele,
akavuta mtoto wa meza na kutoa kisu kidogo
pamoja na forceps, akiwa anajiangalia katika kioo
kikubwa kilicho mbele yake alinynyua mkono na
kujichana pale alipohisi chip ile imewekwa,
hakukosea, kwa kutumia ile forceps akakibana
sawia na kukichomoa, damu zilimwagika lakini
alidhibiti hali hiyo kwa shashi iliyokuwa hapo ndani
kwake na kutia dawa kidogo aina ya Iodini au wengi
tunaaita dawa ya joto, aliichukua ile chip na kuitia
moto ikateketea kabisa, kisha akajipanga kwa
safari. Gina alimfuata na kumpeleka uwanja wa
ndege ambako alichukua ndege na kurudi Nairobi
kwa kificho bila mtu kujua. Aliapa kumtia mkononi
kila aliye jirani na Bill mpaka ampate Bill ili kazi
yake aiache kwa heshima na si kwa dharau. Ndipo
aliporudi Nairobi kwa hasira ya kumsaka Bill na
vibaraka wake.
Nairobi
GARI aina ya Vogue iliegeshwa nje ya kanisa la
Familia takatifu, kijana mmoja aliyevalia nadhifu,
suti nyeusi iliyotanguliwa na kaba shingo la rangi ya
cream aliteremka na kuufunga mlango wa gari hiyo
kwa madaha, kisha akaingiza mkono wake mfukoni
na kutoa miwani myeusi akaipachika usoni mwake,
naam, ushababi wake ulijitokeza waziwazi,
akazunguka upande wa pili na kufungua mlango.
Mwanamke mwenye umbo la wastani, lililojaa vizuri,
anayevutia ukimwangali kuanzia kifuani mbala chini
ya kiuno mashaalah taarabu ipo ya kuvutia, akiwa
ndani ya suti ya kike ya kijivu, na uso wake
ameuficha kwa miwani safi ya rangi ya udongo.
Haikuwa rahisi kugundua kuwa huyu ni Kahaba Rose
ambaye akiwa pale mtaa wa Koinange huvalia
kijisketi kifupi kilichobana na chepesi ambacho
huuacha mwili wake sehemu kubwa wazi. Alishikana
mkono na kijana huyo kisha wakavuka geti mpaka
kwenye kibanda cha mlinzi na kuomba kuonana na
Paroko kama yupo, baada ya itifaki zote kufanyika
ikiwa kutazamwa kama wana silaha yoyote
kukamilika waliruhusiwa.
Kati ya viti sita ni vitatu vilikaliwa, upande huu
Kahaba Rose na Kamanda Amata na upande
mwingine ni Fr Joe Smith, babu.
“Karibuni sana, mumekuja kuandikisha ndoa?”
alianza kuuliza yule kasisi.
“Hapana, tumekuja kwa maswala ya kikazi,
tunahitaji kuongea machache juu ya tukio zima la Fr
Gichuru,” Amata alitonesha kidonda cha kasisi huyo
mzee raia wa Marekani.
“Mimi nimechoka na kuulizwa maswali kila wakati
na wala sioni maendelea yake, mara Kenya Polisi,
mara FBI, Mara MOSSAD, mara sijui nini, ah,
nihurumieni jamani, kama kazi imeshindikana basi
acheni mbona Gichuru amekwishakufa hawezi
kufufuka hapa duniani tena, haya niambie na wewe
unatoka wapi?” Fr Joe alilalama na mwisho kuomba
utambulisho.
“Naitwa Kamanda Amata, kutoka Tanzania.”
Akampa na kitambulisho kidogo cha plastiki, yule
kasisi mzee alionekana kama kupigwa na shock
baada ya kusikia kuwa aliye mbele yake ni Kamnda
Amata, mara nyingi alimsikia mtu huyu tu na
kusoma baadhi ya visa vyake ambavyo vingine
vimeandikwa kama riwaya, hakuawahi kufikiri kama
bonadamu huyu yupo kweli au ni hadithi tu, sasa
mbele ya macho yake anakutana na kiumbe huyu,
alimkazia macho kana kwamba sijui kakutana na
Malaika Gabrieli.
“Wewe ni Kamanda Amata?” aliuliza huku
akimnyoshea kidole na kumrudishia kile
kitambulisho chake.
“Ndiyo ni mimi,” Amata alijibu huku akikiweka
kitambulisho chake katika mfuko wake maalumu
ndani ya koti lake.
“Kamanda Amata karibu sana,” alimkaribisha.
“Asante sana nafurahi kukutana na wewe, sasa
kilichonileta hapa ni juu ya mauaji ya kasisi, Fr
Gichuru. Ningependa kujua juu yake kwa kifupi ili
nijue wapi pa kuanzia,” Amata alianzisha
mazungumzo ya kikazi. Fr Joe Smith, alimueleza
Amata kila kitu kuanzi asafari yake ya Roma
kwenda kuchukua ile monstrance mpaka aliporudi,
na mazingira ambayo kifo chake kilitokea,
akamueleza pia juu ya kupotea kwa Gichuru kwa
takribani masaa 24 na yote yaliyotukia. Kamanda
Amata alitulia kitini akisikiliza kwa makini huku
akiandika vitu Fulani katika kijitabu chake kidogo.
“Umesema majambazi hao wamechukua
Monstrance, unafikiri kuna nini katika chombo
hicho?” Amata aliuliza.
“Kwa kweli sijui labda kwa sababu ya malighafi
iliyotengenezewa, kwa maana ile monstrance
imetengenezwa kwa dhahabu tupu na ni ya gharama
sana pia ni ya kihistoria sana katika kanisa,” Fr Joe
alieleza.
“Baada ya mauaji ya Kasisi, umesema siku chache
baadae mlivamiwa na majambazi ambao sasa ndio
walikuja kuichukua hiyo Monstrance, siku ya tukio
wewe ulikuwepo?”
“Nilikuwepo, nilijificha huku juu ghorofani, niliangalia
mapambano malali sana ya polisi na majambazi,
lakini mwisho wa yote ile gari ya majambazi
iligonga mti hapo nje na gari nyingine ikaja na
kuchuku lile begi kisha wakaondoka, sasa hapo
sijaelewa nini kimefanyika,” alijibu kwa ufasaha.
“umesema siku ya mauaji mtawa wa kike Rose
alishuhudia na pia umesema siku ya kuibwa hiyo
monstrance mtawa huyohuyo alishuhudia, je huoni
kuwa kuna uhusiano kati ya matuklio haya?
Nikimaanisha kuwa Rose anahusika moja kwa moja,
na yeye anaweza kutufungua masikio katika hili,”
Amata alimshtua kidogo Fr Joe na kumuacha akiwa
na bumbuwazi, aliporudiwa na fahamu alijibu.
“Hapana, ni bahati tu labda niseme, mtawa Rose
yeye anahudumu huko kanisani ndiyo maana haya
yote yamemkuta huko, lakini kuhusika yeye sina
uhakika na hilo,” Fr Joe alijibu kwa upole.
“Naweza kumuona Sr Rose?” Kamanda Amata
aliuliza, na bila kuchelewa alivuta simu yake na
kupiga kwa masista, akongea maneno machache na
kukata simu ile.
“Kamanda Amata, tunahitaji kupata hii Monstrance,
Vatican haitatuelewa kabisa, mimi naumia sana,” Fr
Joe aliongea huku akitoa machozi.
“Usijali father, itapatikana tu endapo mtanipa
ushirikiano wa karibu,” Kamanda Amata alipokuwa
akisema hayo mara mlango ukafunguliwa na mtawa
Rose aliingia ndani ya ofisi ile na kuwakuwa watu
hao wawili pamoja na Fr Joe, akakribishwa kiti na
kuketi upande ule wa Fr Joe, akatulia na
kutazamana na Amata.
“Ahusiki tangu machoni pake,” Kamanda Amata
alitamka hayo, kawa kuwa alitazamana macho na
mtawa yule na kuyasoma kitaalamu na kugundua
kuwa hana hatia, kwani mwenye hatia usomeka
tangun machoni na katika pua zake.
“Pole sana Sr Rose kwa mikasa iliyokukumba, tupo
hapa katika kuona ni jinsi gani ambayo itatusaidia ili
kupatikana kwa ile monstrance, nikuulize swali moja
ulipopelekwa polisi kwa mahojiano ulihojiwa na
askari gani, unaweza kumjua kwa jina?” Kamanda
Amata aliuliza kitu ambacho hakuna kati yao
aliwaza.
“Anaitwa Sargean Maria,” Rose alijibu.
“Ok, asante, nilitaka kujua hilo tu, sasa kuanzia sasa
hutakiwi kumueleza mtu yoyote habari hii isipokuwa
mimi tu kama nikihitaji,” Amata alisistiza, “Fr Joe,
mimi nimekuja kufanya kazi hii kwa siri sana ,
hakuna anyejua uwepo wangu hapa Nairobi, naomba
usimueleze mtu yoyote juu ya uwepo wangu hapa
kwako na Nairobi kwa ujumla, mimi nitawasiliana
na wewe kwa jinsi ninayoijua mimi tu, sawa father?”
“Sawa, usijali Kamanda,” Fr Joe alijibu.
“lakini kabla sijaondoka, naweza kutembelea
chumba cha marehemu? Nahitaji kujua kama
naweza kupata chochote cha kunisaidia katika kazi
yangu,” Amata aliomba, Fr Joe akamchukua na
kumpeleka katika chumba hicho kidogo chenye
kitanda cha futi tatu na nusu, kilikuwa chumba cha
kimasikini hasa, meza moja ya mbao ilibeba vitabu
vichache na kitabu kimoja cha kumbukumbu,
ukutani palikuwa na kanzu zilizoning’inizwa, bila
shaka zilikuwa za marehemu, Kamanda Amata
akavuta hatua fupi mpaka pale mezani na kunyanyua
kile kijitabu cha kumbukumbu, akafungua kurasa
moja baada ya nyingine, kijitabu hicho kikamvutia
sana, akamtazama Fr Joe akaona yuko mbali
kimawazo, akakitia katika mfuko wa ndani wa koti
lake, kisha wakarudi mpaka pale ofisini na
kauagana, akamchukua Kahaba Rose na kuondoka
akiahidi kurudi tena muda wowote.
Dakika chache baadae kahaba Rose na Kamanda
Amata walikuwa tayari barabarani kuelekea mjini,
mbele kidogo baada ya kuvuka eneo la St Paul
kuelekea Westland hakuna aliyekuwa akiongea na
mwenzake katika gari, Kamanda Amata alipinda
kushoto na kuingiza gari katika maegesho ya
supermarket ya Nakumatt.
“Nawataka watu wawili kwanza,” alimueleza kahaba
Rose
“Nani na nani na wa nini?” Rose aliuliza
“Mellina na Wambugu, hawa watanipa ramani nzuri
ya wapi alipo Bill,”
“Utawapata wapi? Kwa vyovyote kila mmoja yuko
mafichoni mwake saa hii,” Rose alieleza
“Mimi najua pa kuwapata na wewe unajua jinsi ya
kuwapata,” Kamanda aliongea kwa kujiamini kama
ilivyo kawaida yake, “Ok mpango utakuwa hivi,
wewe utarudi nyumbani kwako, kwa kuwa wale
jamaa wanakutafuta wakuue mimi nitakuwa pale ili
niwashughulikie na wanipe ramani ya wapi Bill
alipo.”
Kahaba Rose hakuwa na la kupinga hoja hiyo
alitikisa kichwa juu chini kuashiria kuwa ameelewa
vyema mpango mkakati huo jinsi ulivyo. Rose
aliinua mkono wake wenye saa na kuitazama.
“Vipi, Saa ngapi?” Amata aliuliza.
“Saa nane kasoro,” Rose alijibu huku akishusha
mkono wake.
“Ok, twende tupate chakula cha mchana kisha
tuanze shughuli yetu,” kamanda alieleza huku
akifungua mlango wa gari kushuka nje, naye Rose
akafanya vivyo hivyo. Kati ya viti vingi vilivyo mbele
yao wawili hawa walichagua viwili vilivyowafaa na
kuketi kabla hawajaagiza juice wakati wakisubiri
chakula cha mchana.
Kamanda Amata alijitahidi kutupa jicho huku na kule
kuchunguza lolote ambalo linaweza kumsaidia
katika sakata lake hilo lakini hakuna kitu, ila mara
kadhaa alitabasamu kwa kumuona kijana mmoja
teja jinsi alivyokuwa akirandaranda kwa mwendo wa
madaha katika maeneo huyo bila kuchoka kuomba
pesa ndogondogo kwa wateja wa eneo hilo, ilikuwa
kero kwa kiasi Fulani kwa waliopo eneo hilo kila
askari walipokuwa wakimtoa yeye alirudi kwa njia
nyingine.
“Vipi mbona unamshangaa huyo teja?” Rose aliuliza
“Ah huwa napenda wanavyotembea,” Amata alijibu.
“Kweli hauna kazi.” Rose alimkebehi Amata
“Hata hii ya kumwangalia ni kazi pia,” Amata alijibu
huku akitoa tabasamu lake la nadra mbele za watu.
Wakiwa katika mazungumzo na Kahaba Rose mara
Yule teja akaja mpaka pale katika meza waliyoketi
Amata na Rose, huku udenda ukimtoka. Rose
alijaribu kumfukuza na kuita askari wa ulinzi, lakini
Kamanda Amata alizuia Yule kijana asiondolewe
pale.
“Muacheni, ni mgeni wangu huyu, mpeni juice
tafadhali na biskuti kadhaa,” Kamanda Amata
aliamuru na amri ikatekelezwa haraka. Kamanda
Amata alitazamana uso kwa uso na kijana Yule
‘teja’ macho yao yaligongana na kuangaliana kwa
kina, Yule kijana alikuwa akipepesa macho kwa
mtindo wa ajabu sana, harakaharaka, akaifumba na
kufumbua kwa mitindo tofauti, akigeuzageuza
mboni zake kwa hali ya kupendeza, naye Amata
alikuwa akimfanyia vivyo hivyo kwa kupeana muda,
pembeni Rose alikuwa akifa kwa kucheke alipokuwa
akiangalia wawili hao walipokuwa katika huo
mchezo wa ajabu, mchezo wa macho. Baada ya
kumaliza juice yake Yule kijana alinyanyuka akatoa
ishara ya kuishukuru, Amata akampa shilingi mia ya
Kenya na kumruhusu aende.
“Mh, duniani kuna mambo” Rose alisema, Amata
akageuka kumtazama Rose, “Kwa nini wasema
hivo?” Amata aliuliza.
“Si kama hivi, kijana Yule madawa yamemuharibu
kabisa, ona sasa hata wazazi wake wamepata
hasara ya kulea,” Rose alilalama.
“Usiseme hivo, hawa ni watu wa kuwapenda tu,
katika kupenda usibague maana leo kesho hujui ni
katika mazingira gani utahitaji msaada wa nani.”
Kamanda alimueleza Rose kwa upole.
“Ok, sasa amekaa hapa anachekacheka tu na ndio
mlikuwa mnafanya nini na macho?” Rose aliuliza.
“Aaah hawa huwa hawapendi kuongea wao ni
kuchekacheka tu kama ulivyoona na kuchezesha
macho vile ni jambo wanalolipenda sana,” Amata
alieleza. Alitupa jicho nje ya wigo wa supermarket
ile na kumuona Yule teja akipotelea mitaani.
ITAENDELEA ....
 
SEHEMU YA 9
§§§§§
“Vipi afande mbona una mawazo mengi sana?”
afande Otholong’ong’o alimtupia swali Sargeant
Maria aliyekuwa amesawajika uso kwa mawazo na
macho yake yakiwa yametopea kwa uchovu, aliinua
uso na kumwangalia askari huyu kijana ambaye
katika mapambano yao na majambazi aliumizwa
mguu kwa risasi, sasa alikuwa amerudi nyumbani
baada ya matibabu kukamilika. Alikuwa nyumbani
kwake maeneo ya Kasarani kwa mapumziko
akiuguza jeraha lake.
“Nimepambana na kazi nyingi za upelelezi lakini hii
inanitoa jasho afande,” Marina alieleza, “Kwa nini?
Mbona kama imeisha maana wale wawili wamekufa
bado huyo Mellina, na kumpata sio tabu, unafikiri
atakuwa amekimbia?” Otho aliuliza.
“Kukimbia sidhani., lakini hata hivyo pia anweza
kuwa hayuko nchini, hali akijua kuwa swahiba zake
wameuawa,” Marina alieleza.
“Kazi ndogo afande, anzisha msako wa kwenye
mabasi yote ya abiria, treni na hata ndege ili
kumbaini kama bado yupo ao kakimbia, sambaza
na picha zake kwenye maeneo husika,” Otho
aliongea, huku akijaribu kuinuka pale kitini.
“Otho! Ni point ambayo sikuwaza kichwani yangu,
umenipa wazo, sasa lazima nimtie mkononi,” Maria
alieleza lakini sauti kavu ya Otho ilimpa tena swali
ambalo lilimrudisha Maria katika lindi la mawazo,
“Na baada ya kumpata Mellina, nini kitafuata? Na
hicho chombo kilichoibwa kanisani tutyakipataje?”
lilikuwa swali gumu lililoulizwa na Otho. Maria
alitulia kimya huku akichezea simu yake, akikosa
jibu la moja kwa moja la kumpa Otho aliyeonekana
akilisubiri kwa hamu sana, “Tumpate kwanza
Mellina, yeye ndiye atatupatia picha nzima ya nini
kilitokea na nani anahusika katika hilo, kishapo
tutajua hicho chombo kipo wapi na jinsi ya kukipata,
lakini Otho, kesi hii ina mambo ya ajabu mengi
sana” Maria alimsimulia Otho juu ya Yule kichaa na
maneno tata aliyomueleza na pia jinsi
alivyomtoweka kimiujiza. Otho alimsikiliza bosi
wake mpaka alipomalizia mkasa huo.
“Ila majamazi sio watu aisee, kinachonichanganya
wakati wa mapambano yetu, kuna gari nyingine
ilikuja na kumchukua cheetah na hilo begi kisha
wakaondoka zao, kwa akili ya haraka haraka
inaonekana hapa kuna makundi mawili katika
mchezo mmoja,” Maria aliongea kwa nhisia kali,
“Kama ni hivyo bado shughuli ni pevu, apatikane
Mellina kwanza kisha yeye atatupa mpango mzima
kwa kibano cha nguvu,” Otho aliongezea.
Mazungumzo kati yao yaliendelea yakilenga kazi na
mambo mengi kwa ujumla. Walipokamilisha
mazungumzo yao ndipo Maria aliporudi kazini na
kutekeleza yale aliyoyaongea na Otho ya jinsi ya
kumnasa Mellina, mchana uohuo shughuli hiyo
mpya ilianza kwa kasi katika kila chombo cha
usafiriu kinachotoka ndani ya Nairobi. Sergeant
Maria alikuwa akisubiri kwa hamu aambiwe tu kuwa
wapi Mellina kaonekana ili akamchukue na afunge
kabrasha hilo la ‘Mauaji ya Kasisi’, lakini bado
ilikuwa haijazaa matunda mpaka muda huo.
§§§§§
Kamanda Amata aliegesha gari yake mbele ya
nyumba ya kahaba Rose, na kukubaliana nae
kuonana jioni ya siku hiyo ili kupeana raha kama
kawaida yao, kazi na dawa. Rose alimwangalia sana
Amata wakati alipokuwa tayari nje ya gari hiyo
akainua mkono na kumpungia ishara ya kwa heri
naye Amata alijibu kwa mtindo huohuo kisha akatia
moto gari na kuondoka eneo hilo kurudi katika
hoteli aliyofikia.
Mara moja aliingia na kuoga harakaharaka kisha
akabadilisha nguo lakini leo alitoka tofauti kidogo si
kama tulivyomzoea, fulana moja nzuri ilitulia mwilini
mwake iliyobeba maandishi madogomadogo katika
upande wa kushoto wa kifua chake yaliyosomeka
‘lacoste’, na chini akiwa na jeans nyeusi ya bei
mbaya na kiatu cha mtindo ule ule wa lacoste.
Alipohakikisha kuwa sasa yuko tayari katika
miondoko hiyo ya ujana, alijitokeza hadharani na
kujichanganya mjini huku gari yake akiwa kaiacha
palepale maegeshoni.
Alipita mtaa wa kwanza na kuvuka ule wa pili,
aliendelea kutembea kwa mguu mpaka mahali hasa
alipopataka, kimvua cha rasharasha kilikuwa
kikiendelea katika jiji la Nairobi, Kamanda Amata
aliendelea kutembea kwa harakaharaka na kupita
hapa na pale mpaka mahali hasa alipopatakam
akachukua tax na kuondoka haraka, dakika kadhaa
mbele alikuwa katika lango la kuingia sehemu
ambayo waamini wa madhehebu ya Kikatoliki huja
mara nyingi kufanya sala na tafakari eneo hilo,
bustani ya ufufuko, ilijulikana kwa jina hilo. Akaingia
langoni na kusimama kidogo kisha akafnya ishara
ya msalaba na kuingia hatua tatu mbele akasimama
tena, mara mtu mwingine akaungana naye palepale
aliposimama, Kamanda Amata hakuonekana
kumtilia maanani mtu huyo, aliyevalia suti nyeusi
mwenye uso ulikunjanakunjana kama mtu aliyewahi
kumwagikiwa na tindikali. Walisimama sambamba
wote wakikaza macho kutazama mbele kila mmoja
akiwa na rozali yake mkononi.
“Kamanda Amata,” Yule mtu aliita kwa sauti ya
kunong’ona bila kumwangalia Amata.
“Unasomeka,” Amata alijibu
“Umekuja kufanya nini huku ilhali maisha yako yapo
hatarini?” Yule mtu akauliza
“Hatari ndiyo chai ya asubuhi kwangu na kifo ni
chakula cha jioni, achilia mbali mlo wa mchana
ambao ni maumivu na mateso makali, nimezoea,”
Amata alijibu.
“Wewe ni jeuri, jibu swali langu, umekuja kufanya
nini? Watakuua mara hii, wapo wengi pande tofauti,”
Yule mtu alisema tena kwa mtindo uleule.
“Mtu kama mimi siogopi kufa wala simuogopi
muuaji, nipe ripoti kama inastahili,” Amata alijibu.
“Usijali, mawingu ni mengi, yote yanakuzunguka,
dhambi zako ni Mungu tu anayezijua na si mwingine
awaye yote, unatakiwa kutubu kabla ya kifo chako
leo hii,” Yule mtu akakohoa kidogo kisha
akaendelea, “Usichelewe, dakika kumi zijazo
hakikisha upo katika kitubio ndani ya kikanisa kile
pale mbele yako,” Yule mtu alipomaliza kusema
hayo akainamisha kichwa na kutoka nje.
Kamanda Amata alisimama kwa sekunde kadhaa
akitafakari yote, kisha akazunguka hapa na pale na
kupotelea nje, alipofika upande wa pili wa bustani
hiyo aliona kile kikanisa kikiwa wazi na watu
wakiingia na kutoka, akatazama saa yake ilikuwa
tayari dakika kumi zimefika. Akavuta hatua na
kupanda ngazi mpaka ndani akageuka huku na huku
na kukiona kile kisanduku maalumu cha kufanyia
maungamo akakijongelea na kufungua pazia lake
kisha akajitoma ndani na kupiga magoti akitazama
katika kile kidirisha kikuukuu kinachomtengenisha
muumini na kasisi, sauti kavu ikatokea upande wa
pili, haikuwa sauti ngeni bali ni ileile aliyoisikia kule
bustanini.
“Nilijua utarudi Nairobi, na nimefurahi kukuona, ujio
wako niliutambua mara moja tu kwa mauaji ya wale
jamaa wawili pale Plazza Hotel katika chumba
chako cha mwanzo,” ile sauti ilimwambia Amata,
bumbuwazi lilichukua nafasi katika uso wa Kamanda
Amata, alijiuliza ni vipi amekwishagundulika uwepo
wake katika jiji hilo, alikaa kimya kidogo kisha
akafungua kinywa chake, “ Wewe ni nani?” aliuliza.
“Unataka kunijua mimi?” ileh sauti iliuliza
“Ndiyo,” Amata alijibu.
“Mimi ndiye niliyekuokoa katika mikono ya Bill pale
Safari Park casino,” akajibiwa.
‘Safari Park casino,’ Amata alijiwazia sana juu ya
sehemu hiyo, alijaribu kuvuta kumbukumbu ya siku
ile lakini hakujua ni nani alimuokoa na kivipi, akili
yake ilirandaranda huku na huko kuoanisha matukio
lakini hajkupata jibu la uhakika katika hilo.
“Hakuna kitu kama hicho, hakuna aliyeniokoa katika
lile, jioneshe sura yako tafadhali,” Kamanda Amata
alizungumza kwa kusita kisha akamuamuru mtu
huyo kujionesha wazi na si kuendelea na ngonjera
zake hizo.
“Utaniona tu. Amata ulikuwa umelala kwa sumu
ulopewa na Bill, ulipochukuliwa na gari
hukujitambua ndipo mimi nilipokufuatilia kwa
nyuma mpaka eneo amb alo nilitumia kukuokoa,
nikakuleta mpaka hospitalini kwa matibabu, Bill
alitaka kukuua na hata sasa nafikiri anaamini hivo,”
ile sauti iliendelea.
Kamanda Amata kwa maneno yale alituliza moyo
kidogo akajua kuwa kumbe anayeongea naye
alikuwa ni mmoja kati ya wale walio upande wake,
Amata hakujua kabisa nini kilitokea nyuma baada ya
pale Safari Park, alitikisa kichwa kama mtu
aliyeingiwa na sisimizi sikioni, “Sasa Bill yuko
wapi?” Amata akauliza.
“Hilo swali gumu sana, maana Bill si mtu wa
kuonekana hovyo na sijui yuko wapi,” ile sauti
iliendelea.
“Nimekuja kwa kazi binafsi, nahitaji kichwa cha Bill
nikakipambe nyumbani kwangu,” Amata aliongea
kwa hasira sana.
“Punguza hasira, mtumie yuleyule Malaya uliyekuwa
naye pale atakuonesha Bill, Yule anajua kila kitu
asikudanganye kwa lolote, Yule ni mwanamke wa
Bill, na kitendo cha wewe kuiwa naye ujue Bill
anakusoma kila hatua ufanyayo kupitia Yule
mwanamke,” ile saiuti ilikuwa kama inayomgutusha
Amata usingizini, akajiuliza mara kadhaa juu ya
ujinga aliyoufanya kwa kuongea mengi na Rose
kumbe alikuwa akipelelezwa, mwe, kweli muwinda
huwindwa.
Hasira zikakamata moyo wa Amata, “Unasema
kweli?” aliiuliza ile sauti ya mtu asiyemjua.
“Nikikudanganya itanisaidia nini mimi? Ujue kuwa
muda wowote watakuua maana wameshakujua
vilivyo kupitia Yule mwanamke Malaya. Sasa nenda
kambane yuleyule, yeye ndiye atakupa kila kitu juu
ya Bill mpaka alipojificha atakwambia,” Ile sauti
ilizidi kusisitiza, Amata alibaki hajielewi kwa
analolisikia, “Hakikisha saa tatu kamili usiku wa leo
tunakutana pale KICC kwenye mgahawa wa juu
kabisa Nairobi super café, kwa heri.” Ile sauti
ikaaga. Amata akajinyanyua, na kutoka kwenye kile
kiboksi ndipo alipogundua kuwa ni giza
limeshaingia, harakaharaka akatpoka nje na
kuelekea barabarani, tax ya kwanza aliidaka na
kujitupia siti ya nyuma, akampa maelekezo dereva,
tayari Kamanda Amata damu ilikuwa inachemka,
anamuwahi Rose ili amchukue na huko
atakakokwenda naye basi akambane vyema ili
amueleze siri yote ya Bill.
Dakika thelathini, ile tax ilikuwa imeegeshwa mbele
ya nyumba ya Rose, lakini kabla hawajaifikia
nyumba ile aliona gari ndogo ya kijivu ikitoka katika
egesho la nyumba hiyo na kuondoka kwa kasi,
Kamanda Amata aliitazama ile gari lakini hakuitilia
maanani ijapokuwa wasiwasi ulimuingia.
Alimlipa dereva tax na kumuacha aende zake,
aliliendea geti la nyumba ya Rose na kulisukuma
lilikuwa wazi, akapita moja kwa moja mpaka
mlango wa kuingia katika sebule, aligonga kengele
lakini hakukuwa na majibu, aligonga tena kwa tena
lakini wapi, kengele za hatari zikalia kichwani
mwake, akaichomoa bastola yake na kuiweka tayari
kisha kwa mkono wake wa kushoto akanyonga
kitaza kilichoiuachia mlango wazi. Kwa hatua za
taratibu Kamanda Amata alisoge mpaka katika
korido ya kuelekea vyumbani, aliitazama sebule ile
iliyoonekana wazi kuwa kulikuwa na vurugu Fulani
iliyotokea muda si mrefu, akaendelea kufungua
mlango mmoja baada ya mwingine, akakifikia
chumba cha Rose, kabla hata hajaingia ndani
alikaribishwa na michirizi ya damu iliyokuwa
imetoka chumbani humo na kuelekea mahali Fulani,
aliitaza lakini hakujuwa wapi ilitoka na wapi
ilielekea, moja kwa moja akaenda zake mpaka stoo
ambako alikuta damu nyingi zimetapakaa, akajua
kwa vyovyote kila kitu kipo chumbani, akawahi
chumbani, alipofungua mlango tu aliakaribishwa na
damu nyingi, damu bichi ambayo ndio kwanza bado
ilikuwa ikizidi kumwagila kutoka katika kiwilikiwili
kilicholazwa hapo kitandani, Kamanda amata
aliirudisha bastola yake kiunoni na kukisogelea kile
kiwilikiwili pale kitandani, akatema mate chini baada
ya kujisikia kichefuchefu cha ghafla. Kitanda kilibeba
mwili usio na kichwa, Amata akautazama ule mwili
na kusikitika sana, akajikuta akitokwa na machozi,
akavuta hatua kuondoka lakini akasimama
mlangoni, ‘Je kama si mwili wa Rose!’ alijiuliza,
akarudi kuukagua mwili huo, akaufunua taratibu
nguo katika eneo la paja Rose alijichora tattoo ya
nnge, kweli ni yeye, alijiridhisha na kuondoka eneo
lile haraka kabla watu wa usalama hawajamkuta.
Kamanda Amata aliingia hotelini mwake na
kujifungia chumbani akitafakari, kichwa chake
kilichanganywa kwa mawazo hakujua ni nini
kinatokea, alimkumbuka Yule mtu kule kanisani
aliyemwambia kuwa Rose anajua kila kitu juu ya
Bill, kwa nini amwambie, na yeye anafika kwa Rose
anakuta ameuawa, alijaribu kuunganisha picha lakini
hakupata jibu, sasa aliona wazi kazi inakuwa
ngumu, kama alijuwa kuwa kwa Rose ndiko atapata
jibu basi haikuwa hivyo, utata, utata wenye utata.
Dakika ishirini na tano zilimpita Amata akiwa
kasimama mbele ya kioo kikubwa akijiangalia lakini
hakujiona, akiwa amegubikwa na mawazo, hasira na
chuki kwa mtu asiyemjua, aliona wazi kuwa mtu
huyo amekwamisha harakati zake zote.
KICC – NAIROBI
MEZA MOJA iliyokuwa mbele ya kijana mtanashati,
Melchior Ndege, ilibeba bia aina ya tusker na
vitafunwa kadhaa. Kijana huyu aliyekuwa akinywa
bia yake taratibu kana kwamba hana haraka katika
hilo alionekana akipepesa macho yake huku na kule
kuona kama Yule anayemsubiri amefika au la.
Pembeni kukiwa na wateja wengine lakini yeye
halikumfanya kujali hali hiyo, aliendelea taratibu
kubarizi kwa macho akina dada warembo
wanaojipitisha mbele yake, wakizani kuwa labda
wangeitwa lakini wapi, hakukuwa na muito wala
mruzi. Muda ulizidi kwenda, Ndege hakumuona
mgeni wake, akili ikaanza kumzunguka, nini
kimetokea maana muda wa ahadi yao ulishapita
kwa dakika arobaini na tano na zaidi.
§§§§§
Mwanamke mmoja wa makamo kidogo aliteremka
kwenye tax hatua chache kutoka katika jingo la
mikutano la Kenyatta (KICC), alipokwishamlipa
dereva tax alivuta hatua chache kulielekea jingo hilo,
akaingia ndani na kutazama huku na kule, usalama
ulikuwepo, akaiendea lifti na kubofya kitufe Fulani,
dakika moja baadae mlango ule wa alluminium
ulifunguka na Yule mwanamama kujitoma ndani,
kidole chake cha kati kilichobeba pete kubwa ya
haja, kikabonyeza namba 5 na 0 yaani 50, ile lifti
ikamnyanyua na kumfikisha ghorofa ya juu kabisa,
akashuka na kuiendea kaunta.
“Tusker tafadhali,” aliitisha tusker ambayo ilikuja
maramoja na kuanza kuimiminia tumboni mwake,
huku akiangalia kwa makini Yule mwenyeji wake
asiyemjua. Hapa na pale alianza kumuhisi kijana
mmoja aliyeketi pembeni kabisa katika meza ya
peke yake, akashuka na kuielekea ile meza huku
akimuambia mhudumu amletee bia yake pale.
“Naweza kujiunga nawe? Maana naona u mpweke
sana,” Yule mwanamama alimueleza Ndege.
Melchior alimtazama Yule mwanamama kwa makini,
macho yake yalipanda na kushuka mpaka kifuani
ambako hakuona matiti ya asili isipokuwa ya
kuchonga, akacheka na kutikisa kichwa, “Kamanda
Amata, salute kwako. Jinsin ulivyojiweka
sikukutambua kabisa, hakika hakuna anyeweza
kukutega kwa ubaya maana unajua jinsi ya
kukwepana na kifo,” Ndege alimueleza Kamanda
Amata ambaye alijitupia ndani ya vazi maridadi la
kike na kuonekana wazi kuwa ni mwanamke, akiwa
ameondoa ndevu zote kidevuni mwake, vipodozi na
mekap alizojipaka zilimfanya aonekane mmoja kati
ya wanamama mashangigi wa kutoka Mombasa.
“Wewe ni nani?” Amata aliuliza sasa kwa sauti yake
ya kawaida, huku mkono wake wa kulia ukiwa ndani
ya pochi ambayo ililazwa mezani. Melchior Ndege
alielewa ishara hiyo alijua wazi kuwa Kamanda
Amata ndani ya pochi hilo amekamata bastola
tayari kwa lolote, alimtazama macho yake na
kuyaona hayana masihara hata kidogo.
“Melchior Ndege, idara ya usalama wa taifa Kenya,”
Ndege alijibu.
“Umenifahamia wapi?” Amata aliuliza
“Kamanda, tulikutana Arusha kwenye kozi ya
kiintelijensia pamoja na watu wa Cuba na USA”
Ndege alijieleza.
“Sasa naanza kukumbuka, kijana wa Bwana Shikuku,
siyo?”
“Hapo umenena,”
“Inaonekana umekuwa ukinifuatilia sana, kwa nini?”
Amata aliuliza.
“Hapana, sikufuatilii, ila nilikuona mara moja katika
hali ambayo nilijua wazi upo katika hatari, tangu
hapo nikaanza kukulinda kuhakikisha hushuriki na
nilijua wazi kuwa umekuja kwa ajili ya Bill Van
Getgand,” Ndege alipoeleza hayo, Amata alikunja
sura kidogo kwa mshangao.
“Wapi?” Amata akauliza.
“Ujio wako kamnda ulijulikana tangu ukiwa JNIA
pale Dar es salaam, watu wa Bill ambao
walitapakaa kila kona iliyotia wasiwasi walikuona na
kutoa taarifa huku kwa Bill, mpaka unatua JKIA
hapa Nairobi walikuwa wamekuweka kwenye target
yao, hawakupenda kukumaliza ila walitaka wajue
hasa kuna nini ulichokifuata, watu wangu niliowatega
pale uwanja wa ndege wa Jommo Kenyatta walinipa
taarifa kuwa watu wa Bill wapo pale na inaonekana
kuna mtu wanamsubiri, bahati mbaya
hawakufahamu wewe. Hivyo nilifika na kuwafuata
kwa nyuma, nilitazama ratiba ya ndege kujua ndege
ile ilikuwa ikitoka wapi, nikaambiwa ni kutoka Dar
es salaam, hisia zikaanza kunicheza juu yako.
Ulipoingia hotelini pale Plazza wale jamaa walibaki
nje wakisubiri labda kukuvamia au sijui kufanya nini,
mimi niliondoka kwa kuwa niliitwa ofisini ambako
nilipewa taarifa iliyonikosesha raha kabisa.” Ndege
alitulia na kupiga funda moja la bia.
“Taarifa gani?” kamanda aliuliza
“Niliambiwa na Bwana Shikuku kuwa FBI
wamesema sisi tuachane na Bill, wao ndio
watakaofanya kazi ya kumnasa, nilihuzunika sana,
nikaamua kuondoka zangu kwenda kutafuta sehemu
ya kutuliza mawazo kwa muda, ndipo nilipopita pale
Safari Park Hotel, na kukuona wewe pamoja na wale
jamaa wane na mwanamke mmoja, kwa jinsi
walivyojipanga tu nilielewa umetekwa, nikabadili
mawazo nikaingia hotelini humo mpaka casino
walipokupeleka na kufuatilia kila kitu. Pole sana
Kamanda, Bill alidhamiria kukuua, hakukupa sumu
kwenye pombe kwa maana nyote mlikunywa chupa
moja, bali sumu ilikuwa kenye vipodozi vya Yule
mwanamke aliyekupa akustareheshe, vuta
kumbukumbu Kamanda, nilikuwa nafuatilia kila kitu,
kila hatua na kila kipengele. ”
Kamanda Amata alitulia kwa muda, akavuta
kumbukumbu ya tukio hilo akakukumbuka kitu,
Ilivyokuwa…
Muziki laini ulikuwa ukipigwa katika casino ile, watu
walikuwa wakiendelea kucheza kamali na michezo
mbalimbali inayofanana na hiyo. Alipepesa macho
na kushuhudia tu dhambi mbalimbali zilizokuwa
zikiendelea katika jumba hilo. Kamanda Amata
hakuwa na linguine alijivuta taratibu kuelekea kaunta,
hakuweza kutoka nje wala kufanya nini, kwa maana
Bill alimuwekea ulinzi wa nguvu, Amata alijuwa wazi
kuwa yupo mtegoni. Mara Yule mwanamke
aliyemfuata chumbani akaja kwake na
kumkumbatia, “Mmm Sweetie, fanya haraka
tukalale, Bill amesema nikakuburudishe usiku wa
leo,” Yule mwanamke alimueleza Amata ambaye
hakuonekana kuwa na hari ile iliyozoeleka, kichwa
chake kilikuwa kimevurugika kikitafuta njia ya
kujinasua. Alimkumbati Yule mwanamke kwa
mkono mmoja na kumvutia mlango wa kutokea nje,
“Tunywe kidogo hubby” Yule mwanamke aliendelea
kumbembabemba Amata, akaingiza mfukoni mwake
mkono na kutoka na pafyumu iliyoandikwa ‘Sunset’
kwenye kopo lake.
“Nini hiyo?” Amata aliuliza.
“Pafyumu, beibi, inanukia vizuri sana, check” baada
ya Yule mwanamke kumueleza hayo aliifyatua ile
pafyumu na kumpulizia usoni kiasi. Kisha
akajipulizia kwapani huku nakule na kuirudisha
pochini, akatoka na Amata na kuelekekea kwenye
gari huku nyuma akifuatiwa na mtu mwingine.
Wakaingia garini na kuondoka, Kamanda Amata
alishangaa badala ya kuelekea hotelini ile gari
ilikuwa ikichukua barabara ya kuelekea Embu,
akawauliza wakamwambia kuna mzigo wanafuata
kisha watarudi, mara akaona nguvu zinamuishia,
mwili unachokia, macho yanakuwa mazito, kila
alipojaribu kupambana na hali ile alishindwa kabisa,
aliwaona wale jamaa kama madudu ya kutisha
mbele yake, mpaka alipokutana na usingizi mzito
wa kutokujitambua kabisa…
Rejea KICC …
“Niliwafuatilia kwa gari niliyoiba pale hotelini kwa
mwendo mrefu mpaka nilipoona panafaa ndipo
nikasababisha ajali ya makusudi na kukuokoa, lakini
nilikukuta ukiwa na hali mbaya, povu zito likikutoka
puani na mdomoni, nikakuwahisha klatika hospitali
yetu pale Nairobi, kwa matibabu, ndipo bwana
Shikuku akamtafuata boss wako Madam S na
kumpa taarifa. Ofisi yako ilikodi ndege hapa Nairobi
na kukuchukua mpaka Dar es salaam,” Ndge alitulia
akimtazama Amata, kisha akafungua kinywa chake
na kumwambia, “Ni mimi nilikutana nawe pale
Nakumatt, Westland kama mbwia unga, ni mimi
tulikutana pale kwenye bustani ya ufufuko ndani
chumba cha kitubio, najua unamsaka Bill lakini Bill
ametoweka, hayupo Nairobi na hajulikani alipo, ila
Rose anajua kila kitu.”
“Ndege, Rose ameuawa kikatili,” Amata alimwambia
kwa kifupi. Ndege alishtuka sana kwa habari hiyo,
“Unasema Rose ameuawa? Lini na wapi?” aliuliza.
“Rose ameuawa nyumbani kwake, jioni hii, baada ya
kukutana na wewe pale kwenye bustani ya ufufuko
na kuniambia nikamuulize Rose kuwa anajua habari
za Bill nikakuta kauawa kwa kukatwa kichwa ndani
ya nyumba yake mwenyewe. Sikumkuta aliyemuua
lakini nishuhudia gari iliyotoka hapo nje kwa kasi
ilikuwa ya rangi ya kijivu, sikuweza kuisoma namba,
lakini pia sikuona haja ya kuifuata,”
“Dah! Rose, hivi nilikuwa nasubiri upate habari toka
kwake kisha tuone tunafanya nini, bwana Shikuku
amenambia nifanya kazi hii kwa siri sana.” Ndege
aliongea kwa masikitiko.
“Ok! Kuna watu wawili, Wambugu na Mellina,
nawahitaji sana, kutoka kwao nitajua wapi pa
kuanzia, lakini kifo cha Rose kimenikwamisha kwa
mengi sana, watu wengi wanajua mi ni Malaya sana
lakini svyo, kutoka kwa wanawake ndio mara nyingi
tunapata habari za wahalifu tunaowafuata lakini pia
tunaweza kuwakamata kwa urahisi wahalifu kwa
kuwatumia wanawake hawa, Masikini Rose, lazima
niilipe damu yake kwa damu.” Amata aliongea kwa
masikitiko.
“Usijali kaka, nilikujengea mazingira bila kujua,
twende kwa Rose sasa hivi, mengine tutaongea
mbele,” Ndege alimwambia Amata.
“Ok, sawa, sikia Ndege, nimekuja hapa mimi
binafsi, najua ofisi inanitafuta lakini usimwambie
mtu kama niko hapa hata bosi wako usimwambie.”
Amata alimsihi Ndege,
“Dah! Samahani sana kaka, nilishamwambia Shikuku
kama upo hapa,”
Kamanda Amata alimtazama Ndege kwa jicho bay
asana, “Tuyaache, hukuwa unajua, ila usimwambie
mtu mwingine, na leo hii lazima tuonane na Shikuku
tulidhibiti hilo haraka,” Kamanda Amata aliufungua
mlango wa gari na kuketi upande wa kushoto, Ndge
akaukalia usukani na kuondoka zao.
“Imekuwaje ukavaa kama mwanamke leo?” Ndege
aliuliza
“Na we ilikuwaje ukajifanya teja au kasisi?” Amata
nae aliuliza
“Ah ah ah ah!!! Trust no one kaka,” Ndege alijibu.
“Umeona ee? Muwinda huwindwa!”.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 10
Kwanza kabisa walifika hotelini mwa Kamanda
Amata, kamanda akabadilisha nguo na kuingia
ndani ya suti kama kawaida yake kisha wote wawili
wakionekana vijana nadhifu wakarudi kwenye gari
yao na Ndege akatulia nyuma ya usukani
wakaendelea na safari.
“Wewe unamtaka Bill? Lakini kuna kesi nyingine
hapa inaungana nay a Bill. Kiasi kwamba lazima na
hiyo uifanyie kazi ili upate picha kamili,” ndege
alimwambia Kamanda.
“Yeah, ya mauaji ya kasisi?” Kamanda aliuliza
kupata uhakika.
“Ndiyo hiyo, kwa sababu inaonekana Bill anahusika
kwa namna moja au nyingine,”
“Nimeshaanza kuifatilia ila nataka nimfahamu mtu
anayeitwa sergeant Maria kwa kuwa yeye nasikia
ndio kashika hiyo kesi,” Kamanda alimuelezea
Ndege.
“Usijali, kumpata Maria si kazi ngumu,” Ndege
akajibu huku akiizungusha gari kwenye mzunguko
wa Dagoreti corner, mtaa wa kwanza, wa pili,
nyumba ya tano, Ndege alipita kama hataki
kusimama mahali hapo na mbele alikunja kona na
kuegesha gari karibu na duka noja kubwa la bidhaa
mbalimbali, wakateremka, kwanza Ndege akaingia
dukani na kununua jojo mbili wakagawana na
kutembea taratibu wakiielekea nyumba ya Rose,
walipofika mlangoni wakashangaa mlango uko wazi,
Ndege akachomoa bastola yake na Kamanda
akafanya vivyo hivyo, kisha kwa mwendo wa
kunyata wakapita na kuingia ndani, chumba kwa
chumba huyu upande huu na huyu upande ule,
wakafika chumba cha maraehemu, kamanda
alipotupa jicho kitandani hakuna ule mwili,
akatazama huku na kule baadae kidogo Ndege
akaungana nae, wote wakabaki hawana la kusema,
mwili umeenda wapi hakuna jibu.
“Ndege, nilinde tafadhali,” kamanda Amata
alimwambia Ndege na kuirudisha bastola yake
kiunoni mwake kisha akakijongea kitanda kile
alichokuwa amelazwa marehemu, akatazama kwa
makini ni mashuka yaleyale tu, alipokuwa anatoka,
akaona kikaratasi kidogo chini karibu na kitanda,
akakiokota, namba ya simu, akakitia mfukoni, mara
wakasikia mlango ukifunguliwa na watu
wakibishana, Kamanda na Ndege, wakajificha.
“Mi nina uhakika ni humu humu maana pale si
uliinama!” sauti moja ilimwambia mwingine
“Hapa mi sina uhakika unajua,” ingine iliijibu ile ya
kwanza
“Tutakuwa tumecheza blanda kweli yaani, sasa tajiri
tutampataje? Maana kasema yeye tumpate kwa
simu na ye atatulipa kwa simu, hataki tuonane kwa
sura.” Ile sauti ya kwanza ilisema.
“Dah huu utata sasa, any way ngoja tuone, fasta
basi wasije kutukuta,”
Wale watu wakaingia ndani na kuelekea chumba kile
kilichokuwa na ule mwili, wakapekua hapa na pale
hawakuona kitu, kasha wakarudi mpaka chooni
ambako walianzia kazia ile. Kamanda Amata
aliyekuwa katika ficho lake akapata wazo haraka,
akatoa peni yake na kijikaratasi kingine kasha
akaandika namba yake ya simu anayotumia pale
Kenya akachana katika mtindo uleule na kukitupa
chini kwenye korido kasha akajificha tena.
“Ah, we, hiki huku,” mmoja wa wale jamaa akakiona
na kuikiokota kasha wote wakatoka nje na kuchukua
gari yao wakatokome. Ndege na Kamanda wakatoka
mafichoni mwao, “Dah, Kamanda kwa nini ulinizuia
nisiwashambulie wale jamaa? Tungepata majibu ya
maswali yetu,” Ndege alimlaumu Amata.
“Hapana, tunayemtaka sana ni Bill, na Bill mtu
mwingine anayejua siri yake kama si Mellina basi ni
Wambugu, unajua walikuwa wanatafuta nini?”
Kamanda aliuliza
“Sikuwaelewa,” Ndege alijibu. Kamanda Amata
akatoa kijikaratasi na kumuonesha, namba ya simu.
“Sasa mbona walisema wamekipata? Sielewi hapo!”
Ndege alibaki njia panda.
“Sikia ndege, ukisikia TSA namba 1, ndio mimi,
nacheza na akli yako nakutangulia sekunde kadhaa
mbele ndiyo maana ya Intelijensia, mi niliokota hii
karatasi kabla yao, baadae nikaandika nyingine
nikaweka namba zangu ndiyo ile walioiokota wao,”
Kamanda Amata akamueleza Ndege.
“Dah! We mkali kaka, sasa inakuwaje?” Ndege
aliuliza
“Tutafute sehemu tukae tusubiri watatupigia kasha
tunawanasa na watatuambia tajiri wao yuko wapi,”
Amata alijibu.
“Lakini tufanye kitu Fulani, twende kwenye shirika la
simu hii, tukaombe information zote za namba hii,
miito iliyofanya kwa sauti na ujumbe ili tumtafute
mtu huyu yuko wapi nan i nani,” Ndege alitoa
ushauri, Amata akatikisa kichwa nan a kumpigapiga
mgongoni kuashiria kuwa wazo zuri alilotoa.
Wakatoka ndani ya nyumba ile na kuzunguka kule
walikoacha gari yao, kwa haraka sana Kamanda
Amata aliona ile gari yao haina upepo tairi moja,
walipoikabia Kamanda Amata akamshika mkono
Ndege na kupita naye wakaiacha ile gari yao pale
na kuchukua tax kisha wakaondoka, wakamwambia
dreva akawaache barabara ya Waiyaki maeneo ya
Westland, wakamlipa nao wakaongoza kuelekea
pale makao makuu ya kampuni ya simu ya Kenyatta
Telecom, wakafika na kujitambulisha kasha
wakapata kuonana na mhusika, mtu wa ICT, baada
ya kujitambulisha na kusema shida yao, Yule kijana
akafanya kazi hiyo kwa haraka na kuwakabidhi CD
moja yenye kila kitu.
“Hii ni MP3 ina audio, data na sms zote,”
aliwaeleza. Kamanda Amata na Ndege walitazamana
na kumshukuru wakimuachia shilingi za Kenya 5000
wakaondoka zao.
Ndani ya ofisi ya Ndege pale katika jengo la KICC,
kamanda Amata na Ndege walikuwa wawili tu
ofisini humo wakiwa wameiweka CD ile katika
chombo maalum na kuchambua simu zote
zilizotoka na kuingia, meseji zote walisoma mpaka
wakachoka, lakini hawakukata tamaa, simu a
mapenzi ziliwafanya wacheke sana, meseji za
nguoni zilizowaacha midomo wazi, wakiwa
wamekata tama kabisa kuona kwamba katika
namba ile hakuna wanachokiitaji, ndipo walipoona
simu moja iliyowashtua, sauti ya mtu mwenye
lafudhi ya kizungu, wakajua kwa vyovyote ataku Bill,
walisikiliza ujumbe ule mpaka mwisho
wakatazamana, haukua mbaya wala haukuwa mzuri,
bali ulimtaka mwenye namba ile ajifiche na
asionekane nje kwa usalama wake kwani kwa
kufanya hivyo atahatarisha maisha yake. Waliinakili
ile namba waliyoiona kwenye vitabu vya
kumbukumbu vya kila mmoja kisha wakaamua
kuondoka zao. Wakiwa njiani simu ya Amata ikaita
na kawaida simu hiyo ilikuwa ikipigwa na Rose tu,
akainyanyua akitabasamu, akabadilisha sauti na
kuongea Kiswahili cha Kenya.
“Sasa mkubwa, kazi imekamilika,” sauti ya upande
wa pili ikasema.
“Oh vizuri sana sana sana, sasa kwa kazi
mliyofanya, nimeona pia tuonane niwapongeze
kidogo, kama mpo radhi tuonane mahali pa utulivu,”
Kamanda Amata alisema. Kimya kidogo kikatawala
kati yao, “Sawa Boss, tukuone wapi?” ile sauti
ikauliza.
“Tuonane Dagoreti Corner the super pub saa mbili
kamili usiku.”
“Sawa boss,” ile sauti ilijibu. Ndegeakamtazama
Kamanda Amata wakati akikata ile simu.
“Bingo!” Ndege akatamka, akainua mkono na
kutazama saa yake, saa kumi na mbili jioni.
§§§§§
Basi la Eldoreti, lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea
kampala Uganda lilifika eneo la Kisumu, askari wa
usalama barabarani katika kituo cha ukaguzi usiku
huo wakalisimamisha. Mlango ukafunguliwa na
mmoja wao akaingia na kuwatazama abiria,
wengine walilala na wengine walikuwa wakiangalia
filamu ya Kinigeria iliyokuwa ikiendelea ndani ya
basi hilo.
“Haya wote weka vipande yenu juu, tunataka kagua,”
askari Yule aliyetangulia aliwaambia abiri, waliolala
wakaamka na kila mmoja akatoa kitambulisho
chake na kunyoosha juu, ukaguzi ukaanza.
Karibu kabisa na mlango pale mbele alikuwapo
mwanamke aliyevaa baibui jeusi na kuruhusu macho
tu kuonekana. Askari aliyekuwa aikagua, akaichukua
passport yake, Jamila Babiker, ilikuwa ni jina
lililondikwa juu ya hati ile, Yule askari aliitazama
kwa makini na kuigeuzageuza, akamtazama na Yule
mwanamke kwa vizuri, kasha akashuka na ile hati
mpaka kwenye ofisi yao ndogo iliyopo hapo, aikiwa
na mwenzake waliendelea kuikagua na walipoona
hawaridhiki katika hilo, wakamshusha Yule
mwanamke na kumleta katika kile kiofisi.
“Mamaa, hii hati yako mbona inatutia wasiwasi?”
askari mmoja aliuliza
“Kwa nini wasema hivo na kila siku natumia hiyo
hiyo?” alijibu Yule mwanamke.
“Ok, una uhakika na hilo? Sema ukweli kama ni feki
tuelewane hapahapa tukuache uende,” askari
mwingine alidakia. Wazo hilo likamfanya Yule
mwanamke ababaike kujibu. “Hapana hiyo ni halali
kabisa, ni hati yangu ninayotumia kila niendako.
Yule askari akavuta simu yake na kupiga simu
mahali Fulani, baada ya muda kidogo akatuka zile
namba za ile hati ambayo alikuwa nayo pale
mkononi mwake. Baada ya muda kidogo ile simu
iliita tena na Yule askari akainyanyua, Yule
mwanamke akajua sasa mambo yanaharibika
maana anajua wazi alichokifanya katika ile hati.
Baada ya Yule askari kumaliza kuongea na simu,
akamtazama Yule mwanamke.
“Unatufanya sisi wajinga sio?” Yule askari
akamuuliza. Yule mwanamke akawa amejishika
kiuno mkono wa kushoto na ule wa kulia
ameuingiza kwenye mfuko wa lile baibui lake.
“Wamesema ya nani kama si yangu?” aliuliza kwa
jeuri.
“Hii ni hati ya Elizabeth Wangari Joseph” Yule
askari alijibu huku akiinuka na pingu mkononi,
askari wa nyuma yake alikuwa akija kumkamata kwa
nyuma, Yule mwanamke kwa wepesi wa ajabu,
alipiga teke la nyuma ambalo lilitua sawia katika
tumbo la Yule askari wa nyuma na kumsukuma
mpaka kwenye lile basi akajibamiza mgongo na
kuanguka chini, wakati huo Yule mwanamke akutoa
mkono wake wa kulia ukiwa na bastola moja kwa
moja akafyatua na kumpiga Yule askari wa mbele
kifuani, akarushwa na kujibamiza kwenye ukuta wa
ile ofisi, Yule mwanamke akageuka nyuma kwa kasi
na bastola mkononi, risasi ya pili ilitua kichwani
kwa Yule askari aliyeangukia kwenye basi.
“Leo mtamjua Mellina, nyau nyinyi,” alitamka Yule
mwanamke.
“Mikono juu weka silaha chini!” askari mwingine
aliyekuwa upande wa pili wa basi. Mellina
alijiangusha chini na kuviringika kupita uvunguni
mwa basi akatokea upande wa pili, aliposimama na
kutazama nyuma alipaishwa juu kwa risasi ya askari
aliyekuwa ndani ya gari, alilenga shabaha hiyo ya
haraka kupitia dirisha la basi, Mellina alianguka
chini na kutoa yowe la maumivu, aligalagala damu
ikimmwagika kutoka katika bega lake la kulia,
walea skari wakamfiki na kumtia pingu huku jeraha
lake bado likivuja damu.
“Mfunge kitambaa kwenye jeraha, asije akatufia
njiani,” askari mmoja alipiga kelele, wakamfunga
vyema, na kumchukua mzobemzobe wakisaidiwa na
wananchi waliokuwa kwenye basi, wale wenye moyo
mgumu, maana kelele zilitawala eneo hilo.
Mellina hakuwa na ujanja, hakika, mbio za sakafuni
huishia ukingoni.
Taarifa hiyo ya kupendeza ilimfikia Sargeant Maria,
tangu sakata hilo lianze, kwa mara ya kwanza Maria
alitabasamu kwa bashasha, akainuka na kumfuata
Inspekta Saitoti ofisini kwake.
“Ndiyo afande,” Saitoti aliitikia hata kama hakuitwa,
baada ya kupokea saluti ya utii. Maria akampa
taarifa hiyo tamu ambayo ilimfanya ashibe hata
kama hajala. Mara moja inspekta Saitoti akaamuru
gari ya plisi kutoka kuelekea Kisumu kumleta huyo
anayeitwa Mellina. Safari ikaanza, Sargeant maria
akiwa katika cabin ya gari na askari kadhaa wakiwa
nyuma, mwendo wa kasi wa gari hiyo ulifanya kila
aliye barabarani kupisha.
Upande mwingine, jeshi la polisi mkoa wa Kisumu
lilikuwa katika masikitiko makubwa kwa kupoteza
askari wao wawili katika tukio hilo. Haikuwa kazi
rahisi kukubali lililotokea lakini bado hali ilikuwa
hivyo ilivyo.
Baada ya masaa kadhaa gari ya polisi kutoka
Nairobi iliingia katika uwanja wa Hospitali ya
Avenue pale Kisumu. Sergeant Maria alikuwa wa
kwanza kushuka na hakuuliza chochote moja kwa
moja aliingia ndani ya hospitali hiyo na kuelekea
katika wodi aliyoambiwa huku nyuma akifuatiwa na
vijana wake waliovalia kishari kabisa na bunduki zao
mgongoni. Mellina alikuwa hoi, drip ya maji ikiwa
inaendelea kuingia mwilini mwake, Maria alisimama
mbela ya kitanda hicho na kwa jicho la hasira huku
akiuma meno alimtazama Mellina.
“Ulifikiri utafika wapi wewe kiumbe?” Sergeant Maria
alimuuliza Mellina. Mellina alimsonya Maria, na
Maria aktabasamau na kuendelea kumwambia, “Huu
ni mkono wa dola, haukimbiliki, haya nimekuja
kukuchukua na dhambi zako utaenda kutubu Nairobi,
ila lazima kitanzi kiitafune shingo yako,
mwanaharamu wewe!” kisha Maria akaondoka na
Mellina akabebwa katika kitanda maalum,
akawekwa ndani ya gari la wagonjwa, kasha safari
ikaanza kurudi Nairobi chini ya ulinzi mkali.
§§§§§
Ndani ya Dagoreti corner super pub, Kamanda
Amata aliketi karibu kabisa na kaunta wakati Ndege
alibana kule kunako mlango wa kuiingilia wateja
wote. Mbinu hiyo ilitegwa mahsus kuwakamata
wale waliomuua Rose Kahaba, Amata na Ndege
walijiua wazi kuwa katika sakata hilo nguvu ya watu
wawili ingetosha ilimradi tua mnajipanga kitaalamu.
Kamanda Amata alitembea taratibu kuelekea mbele
kabisa ya pub ile, akavuta kiti na kuketi. Mhudumu
alipokuja alimkuita Amata amekwishaketi.
“Nikusaidiwe nini kaka?” Mhudumu huyu mwenye
lafudhi ya Kimombasa alimuuliza Kamnada Amata
pale alipoketi.
“Nipe Tusker light,” Amata alijibu, alipokwisha
letewa alimsubiri yule aliyemhitaji katika pub hiyo.
Melchior Ndege aliketi meza ya mlangoni kabidsa
akisubiri aone kile kitakachoendelea kwa kamanda
na hao wageni wake.
Ndege aliiona Toyota Spacio moja ikiegeshwa
mbele tu ya pub hiyo , akaikazia macho sana na
kuwaangalia watu wanaoshuka kuingia ndani ya pub
hiyo. Vijana wawili mashababi, wakateremka na
kuongeza mambo machache kasha wakaingia ndani
na kuelekea moja kwa moja sehemu walioelekezwa,
Kamanda Amata akawapa ishara aliyowaambia,
wakamfuata na kuketi pembeni yake. Mhudumu wa
puba hiyo akaja, vikaagizwa vinywaji na nyama
choma za kufa mtu.
“Niambieni kazi ilikuwaje?” Amata alianzisha
mazungumzo
“Ah boss, kazi ilikuwa easy tu, tulimkuta anaoga
tukammalizia huko huko!” mmoja alijjibu
“Hamkupata upinzani wowote?” kamanda aliendelea
“Hatukupata boss, ila boss mwanamke mzuri kama
Yule kwa nini ulitutuma tukatishe maisha yake
kinyama vile?” mwingine aliuliza swali lisilo na tija.
Kamanda Amata alimtazama kwa jicho kali.
“We unaijua kazi yako?” alamwuliza. “Ndiyo,” naye
akajibu
“Yule mwanamke mzuri kwa sura lakini si mzuri
kwa roho, kama mlimuua bila kumbaka basi
mmekosa utamu alionao,” Amata aliposema hayo
wote wakacheka.
“Ilo muhimu boss,” Yule wa kwanza akasema.
“Dah! Aisee nyi mna dhambi kweli yaani
mmembaka hivihivi halafu ndo mkamuua, au kwa
sababu alikuwa anaoga mkamtamani?” kamanda
Amata alizidi kuwafurahisha wale vijana.
“Sasa Boss, si hatutaki kukaa sana si unajua
Nairobi imechafuka sasa hivi,” jamaa alimwambia
Amata.
“Usijali, nataka mnipeleke mlipomfukia Yule Malaya,
malipo yenu nayafanya sasa hivi kama ifuatavyo,”
Kamanda Amata akavuta briefcase yake ndogo na
kuifungua, akavuta bulungutu moja la pesa na
kumpa kila mmoja la kwake, “Sina haja ya
kuhesabu kwani najua kazi mloifanya ni kubwa,”
aliwaambia. Vinywaji vilizidi kuteketea kati yao, na
walipomaliza. Walijipanga kuondoka.
Melchior Ndege, alikuwa kwenye meza moja karibu
kabisa na mlango wa kutokea nje, alimuona
Kamanda Amata akinyanyuka na wale vijana, alijua
wapi wanaelekeakea kwani mazungumzo yao yote
alikuwa akiyasikia kupitia earphone zake ndogo
alizopachika sikioni zikiongozwa na kinasa sauti
ambacho Kamanda Amata alikipachika kama moja
ya kifungo cha shati, haikuwa rahisi kwa mtu wa
kawaida kugundua hilo mara moja. Akawatazama
walipokuwa wakija taratibu huku wakiongea
akawaruhusu wapiti pale alipoketi na kuilekea ile
Toyota Spacio.
Mara simu ya mmoja wapo ikaita, akaitoa mfukoni
na kuitazama kiooni, private number, akaipokea na
kuongeza na mtu wa upande wa pili.
“Yeah, nimewapa kazi mbona hamnijulishi
kinachoendelea?” sauti ya mtu wa upande wa pili
iliuliza
“We ni nani, na kazi gani ulitupatia?” Yule kijana
akauliza. Kamanda Amata alishajua nini kinaendelea
katika majibizano hayo, akajiandaa kwa
litakalofuata, huku Ndege akiwa bado ameketi
kataika kiti kilekile alikuwa akiangalia nini
kitaendelea.
Baada ya kuongeza na ile simu, akashusha mkono
wake na kumgeukia Amata, akiwa mekunja sura
kama mtu aliekula pilipili pa si kutarajia, alifyatua
ngumi kumuelekea Amata, lakini akamkosa kwa
kuwa Amata aliepa kwa ustadi sana.
“Nini kijana mbona unarusha ngumi bila taarifa?”
Amata aliuliza.
“Bastard! Unajifanya wewe ndo ulotupa kazi kumbe
sio?” alilalama Yule jambazi.
“Kama si mimi kwa nini nimewalipa? Basi twendeni
kwa huyo anayesema yeye ndo kawapa kazi,
mtakuja kukamatwa na polisi bure,” Amata
aliwaambia, wale jamaa wakabaki wamrchanganyiki
wa hawajui lipi la kufanya, nani boss nani tajiri,
wakatazamana, “Samahani Boss” mwingine
aliyekuiwa kasimama pembeni akajibu. Kisha
wakaingia kwenye gari pamoja na Amata, safari
ikaanza.
Baada ya kukata mitaa kadhaa wakaliacha jiji la
Nairobi na kuchukua barabara ya kuelekea Kisumu
mpaka njia panda ya Kinangop, wakapita Soko
mjinga na kusonga mbele kama kilomita tano hivi,
wakachepuka na kuingia kushoto barabara ya vumbi
mwendo mfupi wakasimama, “Aisee, mmemzika
mbali hivi?” Amata aliuliza, “Ah boss, umesahau
kama ulituagiza tumlete huku,” akajibu mmoja wao.
“Ah, nshasahau aisee,!” Amata alijibu baada ya
kujigundua kuwa amejisahau. Wakafika eneo lile
walilomfukia Rose, Amata alinyamaza kimya mara
wakasikia majani yakitaikisika na mtu mmoja
akaibuka kama ninja.
“Hapo hapo mlipo, mikono juu,” Yule mtu aliamuru.
Hawakuwa na ujanja walikubaliana na hilo wote
wakaweka mikono yao juu.
“Tunawatafuita sana wauaji kama ninyi, fukua hapo!”
aliamuru Yule mtu, kamanda Amata akiwa mikono
yake iko hewani alijua wazi kila kinachoendelea,
akatulia kimya, wale vijana wakaonekana jinsi
wanavyotetemeka. Mara taa za gari zikamulika
upande ule zikimaanisha kuna gari ambayo ilikuwa
inakuja pale walipo. Polisi watatu waliteremka
wakiwa na pingu mkononi mwao, wakawafunga
wote pamoja na Kamanda Amata, kasha
wakawapakia katika Land cruiser yao wakawapakia,
Yule aliyewakamata kwanza akavua soksi aliyoivaa
kichwani na kuruhusu sura yake kuonekana,
Melchior Ndege alikuwa kasimama mbele yao.
“Fukua hapa,” Ndege akawaamuru vijana waliokuja
na gari ya polisi, wakafanya hivyo na kuukuta mwili
wa mwanamke kwenye mfuko mkubwa wa plastiki,
‘Ukatili gani huu,’ Ndege alijiuliza kichwani mwake.
§§§§§
Wambugu, alibaki kujiuliza maswali mengi, vijana
aliowapa kazi walikuwa hawajarudi kumpa taarifa,
alipowapigia akagundua wazi kuwa hakuna
uelewano kati yao. Aliendelea kuketi pale kitandani
akijiuliza la kufanya, tayari alikwishajua kuwa kuna
mchezo umechezwa kati yake na vijana wake.
Akinuka na kulisogelea dirisha, moyo wake haukuwa
na amani hata kidogo, aliona siku zinavyozidi
kwenda ndivyo hali inavyozidi kuwa mbaya, alihaha,
sasa alibaini wazi kuwa Bill alikuwa msaliti mbaya
kuliko msaliti wa kawaida. Akachukua rimoti na
kuwasha tv, habari ya saa mbili usiku ilikuwa ipo
katikati lakini alibaki mdomo wazi kwa habari
aliyokuwa anaiona mbele yake, habari ya
kukamatwa kwa jamabazi sugu la kike
lililowasumbua polisi kwa miaka mingi, Mellina.
Wambugu hakuamini anachokiona mbele yake,
‘Mellina katika mkono wa dola’ alijiwazia akiwa
kasimama huku kajishika kiuno, ‘bass hapa usalama
hakuna tena usalama,’ akazidi kugubikwa na
mawazo. Wambugu akaamua kutoroka maana
alijuwa wazi kuwa endapo Mellina atabanwa vya
kutosha lazima atataja, alifunga kibegi chake
harakaharaka akaweka kila anachoona kinafaa katika
kibegi chake akakiweka mgongoni, bastola yake
akaipachika kiunoni na ikafunikwa kwa jacket
alilokuwa amelivaa, akauacha mlango na kutoka nje
ya gesti hiyo a,liyopanga na kutokomea mtaani.
Gari moja nyeupe ilisimama kando mwa gest hiyo,
kijana mmoja shababi, akashuka na kuiendea kaunta
ya nyumba hiyo, “Mwenyeji wangu yuko chumba
namba saba,” alimwambia Yule mhudumu pale
kaunta.
“Chumba namba saba leo hakina mtu, tayari ame-
check out,” Yule dada alijibu.
“Amecheck out? Lini?” Kamanda Amata akauliza.
“Yaani hata masaa mawili hayajaisha,” Yule dada
akamueleza, Amata alipita kwenye korido mpaka
katika kile chumba na kumkuta mtu wa usafi
akifanya kazi yake. Akarudi kaunta, hana la kusema,
akarudi kwenye gari. “Vipi?” Ndege akamuuliza.
“Jamaa kaondoka, hayupo hapa, tena wanasema
kuwa ni kama masaa mawili yaliyopita” Amata na
Ndege walikuwa hawana la kufanya.
“Ningempata huyu mshenzi leo, ndo angenipa
uelekeo wa Bill yuko wapi!” Kamanda Amata
alimwambia Ndege.
“Usikate tamaa braza, tutampata ndani ya masaa
ishirini na nne, mimi ndiyo ninayoijua Nairobi na
Kenya yangu,” Ndege alijibu huku akigeuza gari na
kutrudi mjini.
7
“MADAM S, Kamanda Amata yupo Nairobi, kwa
habari tulizozipata kutoka kwa watu wetu huko,”
Chiba alimwambia Madam. Madam S alitikisa
kichwa kutokana na kujua hilo kwa kuwa tangu
muda mrefu alihisi kwa vyovyote atakuwa huko.
“Vizuri sana Chiba, sasa mpelekee taarifa mwambie
namhitaji haraka sana ofisini.” Madam S alitoa amri.
Ilikuwa ni usiku ambao Madam S alibanwa na kazi
nyingi, akikumbuka kikao chake cha machana na
watu wengine wa idara ya usalama wa taifa alihisi
jambo jipya hasa kutokana na kutoroka kwa Amata
hospitali na kwenda kusikojulikana. Walimtuhumu
kuwa ni mtovu wa nidhamu, asiyejali yale
anayoambiwa na wakubwa wake, wote kwa sauti
moja wakaona Kamanda Amata anyang’anywe cheo
chake hasa kutokana na uzembe anaouonesha
kwenye kazi za maana kama hizo. Ijapokuwa
mvutano ulikuwa mkubwa sana kati ya wana kikao,
lakini mtu mmoja alionekana kushikia bango sana
kamanda ashushwe cheo, kwa kuwa hafai tena,
lakini kabl;a ya yote atafutwe, arudishwe kasha
apewe barua ya kushushwa cheo na abadilishiwe
idara.
Kichwa kilizunguka, Madam S alibaki njia panda,
hoja imepitishwa lakini bado moyoni mwake
anamhitaji sana maana alijua wazi kuwa hakuna mtu
anayeweza kushika nafasi hiyo ngumu. Atafanyaje,
lazima afuate maamuzi ya kikao, Madam S alianza
kuwaza kustahafu kazi endapo Kamanda Amata
atashushwa cheo, amtetee vipi? Aliumiza kichwa
kwa hilo. Alipoona hapati jibu kwa hilo, aliamua
kuachana nalo, ataona wakati ukifika, alijipanga kwa
safari ya Nairobi ili akakutane na Kamanda,
waongee wamalizane hukohuko, aliamua kufanya
safari hiyo kwa siri sana, asijue mtu yeyote.
Akafunga ofisi na kuondoka zake kujipumzisha
nyumbani kwake Masaki. Hakuwa na muda wa
kupoteza, alipotoka tu ofisini aliwasiliana na watu
wa uwanja wa ndege akapata ndege yashirika la
Swiss ambayo ilikuwa iondoke saa nne usiku huo
kuelekea Zurich, kwa kuna watu waliokuwa
wapandie Nairobi, kwa heshima yake alipatiwa siti
moja kwa bei ya kawaida yenye punguzo la asilimia
25. Aliweka kibegi chake cha mgongoni tayari, nguo
chache na vitu muhimu, bila kusahau kikoba cha
vipodozi. Bastola zake mbili aliziandaa tayari kwa
safari hiyo, alipohakikisha yuko poa alijiswafi kidogo
kisha akajitupia jeans moja kali na fulana nyeuzi
kichwani nakavaa kapelo nyekundu iliyomrudisha
katika ujana kwa kila atakayekutana naye.
Saa nne kasoro robo ilimkuta uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere, akaegesha gari yake
mahala pa usalama ndani ya uzio wa uwanja huo
kwa kibali maalumu kisha akingia ndani katika eneo
la kuondokea wasafiri. Akatoa hati zake na
kumkabidhi mwanadada aliyekuwa hapo kwa kazi
hiyo.
“Ooh, karibu sana, tulikuwa tunakusubiri wewe tu,
watu wote wako tayari kwenye ndege,” alizungumza
Yule mwanadada aliyevalia nadhifu kabisa
alimkaribisha Madam S na kuingia nae ndani moja
kwa moja kwenye ndege hiyo ya kisasa kabisa,
alimuonesha siti yake na Madam akaketi tayari kwa
safari, baada tu ya yeye kuwa ameingia, ndege ile
ilijitoa katika vizuiz vyake ikisukumwa na gari kubwa
kuipeleka barabarni.
ITAENDELEA
:::: KITABU CHA MAUAJI YA KASISI, KITAKUWA
SOKONI MWEZI JULAI. WEKA ODA YAKO SASA
KUPITIA SMS 0766974865. PIA WAWEZA KULIPIA
MAPEMA ILI KUJIAKIKISHIA KUWA UNACHO:::::
 
“Ooh, karibu sana, tulikuwa tunakusubiri wewe tu,
watu wote wako tayari kwenye ndege,” alizungumza
Yule mwanadada aliyevalia nadhifu kabisa
alimkaribisha Madam S na kuingia nae ndani moja
kwa moja kwenye ndege hiyo ya kisasa kabisa,
alimuonesha siti yake na Madam akaketi tayari kwa
safari, baada tu ya yeye kuwa ameingia, ndege ile
ilijitoa katika vizuiz vyake ikisukumwa na gari kubwa
kuipeleka barabarni.
§§§§§
NDEGE na Kamanda Amata walikuwa wameegesha
gari yao pembezoni mwa jengo la Posta katika mji
wa Nairobi, wakijadiliana hili na lile jinsi ya
kumnasa Wambugu. Kamanda Amata alichukua
simu ya Wambugu, simu ya kisasa kabisa
akaigeuzageuza na kumtazama Wambugu, “Unamjua
Wambugu kwa sura?” akamuuliza.
“Hapana, sijawahi hata kumuona, hata hilo jina ni
geni sana kwangu,” Ndege alijibu. Kamanda Amata
akaichukua namba ya Wambugu na kuiingiza katika
simu hiyo, akaiunga kwenye mtandao wa internet,
kisha akaingiza nambari Fulani Fulani na kufungu
mtandao wa usalama wa Tanzania, akaingiza ile
namba pamoja na jina Wambugu katika na kujaribu
kufananisha vitu hivyo. Haikumchukua muda mrefu
simu hiyo ilimpa majibu, namba, jina na picha vyote
vitatu vilionekana kwa wakati mmoja na maelezo
mengine kedekede.
“Ndege!” Amata aliita na kumpa ile simu, “Unahisi
huyu anaweza kuwa ndiye?” akamuuliza, Nege
akaitazama ile picha kwa makini sana akatikisa
kichwa.
“Naijua sura hii vizuri, ni moja kati ya wahalifu
wanaoisumbua serikali,” Ndege alijibu huku
akiirudhisha ile simu kwa Kamanda, kamanda
Amata akaihifadhi ile picha katika sehemu maalumu
kwa kazi hiyo ndani ya simu ile. Kisha akafunga ule
mtandao na kurudisha simu katika hali ya kawaida,
hakuishia hapo, “Ndege, piga simu kwa jamaa yako
wa kampuni ya simu, atuambie simu tatu za
mwisho za Wambugu zinasemaje tunaweza kupata
majibu ya shaka letu.” Ndege akaichukua ile simu
na kufanya hivyo kisha wakasubiri jibu
watakaloletewa. Haikuchukua muda ukatumwa
ujumbe wa sauti katika simu hiyo, Ndege
akaufungua na kusikiliza, hawakukosea, ilikuwa sauti
ya Bill ikimtaka Wambugu aende Iryamurahi
akajifiche huko.
“… najua kuwa una mahangaiko makuu, najua kuwa
Mellina amekamatwa, sasa sikiliza, na husijibu simu
hii bali tekeleza unaloambiwa, ondoka haraka
Nairobi kwa njia za siri unazozijua wewe, njoo
Iryamurahi utanikuta hapa, kisha tupange mpango
kabambe wa kuondoka katika nchi hii, nakusubiri,
ukifika hapa mjini nitakupigia…”
Ilikuwa ni mwisho wa ujumbe ule wa sauti.
“Ina maana Bill yupo Iryamurahi?” Ndge aliuliza kwa
mashaka, huku akiwasha gari na kuliingiza
barabarani kuchukua barabar ya kueleka Embu.
“Ndege, Bill ni jasusi la kimataifa, hawezi kukaa
nchini kwako wakati kazi aliyopewa imekwisha,”
Amata alimjibu Ndege, akaichukua tena simu ya
Ndege nakuanza kufanya utundu mwingine wa
kupata uelekeo ambao Wambugu atakuwepo kwa
wakati huo.
“Unafanya nini?” Ndege akauliza.
“Natafuta uelekeo wa Wambugu atakuwa wapi,
kama katoka Nairobi au bado hajatoka tusije
tukapoteza muda,” Kamanda Amata alijibu.
“Hiyo kazi ndogo Kamanda, piga simu kwa huyo
jamaa atatuambia point gani alipigia simu mara ya
mwisho na sasa atakuwa maeneo gani kadiri ya
signal inavoonesha,” Ndege alimuelekeza Kamanda.
“Ndege acha kutumia njia za kianalogia hizo, sasa
hivi namtafuta kwa GPS na nitakwambia alipo,”
Kamanda Amata akaiweka simu katika program ya
GPS akajaribu kuingiza namba za Wambugu na
kuitafuta simu anayoitumia, jibu likaja, ikatumwa
namba ya IMEI ya simu ambayo kwa wakati ule
ilikuwa imebeba sim card ile, akaendelea na utundu
wake mpaka akaweza kuunganisha mtandao huo,
taraytibu ramani ya Nairobi na vitongoji vyake
ikaonekana katika kioo cha simu hiyo, kidoti
chekundu kikatua katika maeneo ya Juja. Kamanda
Amata alicheka kwa ushindi huo.
“Wambugu hayupo mbali sana,” Amata alimwambia
Ndege, akamtajia na vpimo vya ardhini kabla
hajamaliza Ndege akamwambia hilo ni eneo gani.
Gari ikaongeza moto kuelekea barabar ya Embu
kumuwahi Wambugu, “Tusifanye lolote, twende nae
mpaka Iryamurai tukaone kuna nini,” Kamanda
Amata alimwambia Ndege aliyekuwa katika usukani
akiendesha gari hiyo kwa kasi ya ajabu.
“Kamanda, kimpata Bill utamfanyan nini?” Ndge
aliuliza swali la kizushi.
“Sijui, ila shetani anajua maana nina hasira nae, na
nitamfuata popote alipo katika dunia hii, mpaka
nimtie mkononi,” Amata alijibu. Wakati huo walipita
maeneo ya Kasarani na kuendelea kuikanyaga lami
kusonga mbele.
§§§§§
Saa sita usiku, ndege ya Swiss ilikanyaga ardhi ya
Nairobi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta. Madam S alikuwa ni mtu pekee
aliyeshuka katika ndege hiyo, aliwashukuru
wafanyakazi kwa ukarimu wao na kuzishuka ngazi
hizo kwa fujo. Alipomaliza itifaki zote, alitoka nje
lutafuta usafiri wa kwenda mjini.
“Karibu Madam, karibu sana Nairobi,” ilikuwa ni
sauti ya kiume iliyotokea kwa nyuma yake, madam
alisita kwa kuwa hakutegemea kupata ukaribisho wa
aina yoyote hapo Nairobi, mkono mmoja ukiwa
ndani ya jacket aliloliva muda mfupi uliopita katika
kukabiliana na baridi ya Nairobi, aligeuka nyuma na
kumuona kijana huyo mwembamba mrefu, sura
yake haikuwa ngeni sana machoni, alimtazama tena
na tena kisha akamkubuka, “Mashaka?” alimuuliza.
“Ndiyo, Mashaka, kutoka ubalozi wa Tanzania,”
alijibu Yule kijana ambaye jina lake ni Mashaka,
alietumwa miaka kadhaa nyuma kufanya kazi za
idara ya usalama katika ofisi za ubalozi wa Tanzania
huko Kenya.
“Kwangu?” Madam aliuliza.
“Ndiyo,” Yule kijana akajibu, kisha madam
akaondoka eneo lile na kuelekea kunakoegeshwa
tax, akaingia na kuketi ndani, Yule kijana akarudi na
kuingia kwenye gari binafsi nyingine. Dereva wa tax
hiyo akageuka nyuma na kumtazama Madam S,
kabla hajaongea chochote Madam S alimwambia,
“Safari Park Hotel,” kisha akampa noti tatu za
shilingi elfu moja moja za Kenya, safari ikaanza.
Kwa kuwa ni usiku haikuwa tabu na wala
haikuchukua muda kwao kufika katika hotel hiyo.
Akiwa ameketi katika gari hiyo mara alihisi mfinyo
katika mkono wake wa kushoto, akauinua na
kuitazama saa yake kisha akabofya kitufe Fulani,
mara mkanda mwembamba ukatoka kwa chini
ukiwa na maadishi Fulani, akausoma na kuukata
kisha akautia kwenye mfuko wa suruali.
‘…Kamanda Amata yupo Nairobi, kwa sasa yupo
barabara iendayo Embu akielekea upande wa
kaskazini, nimemnasa pindi alipotumia mtandao
wetu wa usalama kwa kupitia nywila yako. Chiba…’
Ulikuwa ni ujumbe uliokuwa katika kijimkanda
hicho. Madam S alikunja sura, ‘mshenzi kabisa
Amata, kaipata wapi password yangu?’ alijiuliza.
Ilimbidi Kamanda Amata kutumia password ya
Madam S baada ya kugundua kuwa ile yak wake
ilikuwa imefungwa hivyo hakuweza kuingia kwenye
mtandao wa usalama wa Tanzania, alijaribu kuibuni
password ya Madam S mara mbili, mara mbili ya
tatu akaipata na kuingia kwa kutumia jina hilo,
baada ya kumaliza kazi hiyo ndipo Chiba alipojua
kuwa kamanda Amata yupo Nairobi kwa jinsi
alivyokuwa akichukua data ambazo zinaendana na
kazi aliyotumwa tangu mwanzo huko Nairobi.
Ubalozi wa Tanzania huko Kenya kupitia mtaalamu
wa mawasiliano aliyepelekwa kwa ajili ya kublock
password zilizoibwa na Bill, Frank Masai aligundua
kuwa muingiliano huo uliotokea Nairobi kwa
vyovyote madam S alikuwapo hapo, alipowapa
taarifa hiyo wengine wakafanya uchunguzi wa haraka
na kugundua kuwa Madam S yupo njiani kuja hapo
Nairobi, hivyo wakamtuma Mashaka kumuwekea
ulinzi kutokana na hali halisi ilivyo katika jiji hilo.
Madam S aliweka kambi katika hotel ya Safari park,
alihakikisha kila kitu kipo salama, na kupanga jinsi
ya kumsaka Kamanda Amata kwa udi na uvumba.
Aliifungua laptop yake ndogo na kuingia kwenye
mtandao wa idara ya usalama, kwanza akaangalia ni
nini Kamanda Amata alikuwa akifanya katika
mtandao huo, akasoma maelezo ya Wambugu na
kuitazama picha yake, akaangalia na maelekezo
mengine mengi, akaichukua namba ya simu
iliyojitokeza hapo ambayo Amata aliitumia kuchukua
maelezo hayo, akatabasamu na kumsifu Amata
kimoyomoyo kwa jinsi alivyokuwa mtundu wa
kufikiri pindi anapohitaji maelezo Fulani.
Alikumbuka jinsi anavyoweza kuiga sauti na saini za
watu pindi anapohitaji kufanya hivyo, hakushangaa
kusikia kuwa ameweza kupenya mtandaoni kwa
kutumia password yake. Alijiuliza mwenyewe, nani
anaweza kukaa katika cheo cha Kamanda Amata na
akatosha katika kila idara, mapambano ya mikono,
utumiaji wa silaha za aina na aina, lugha za kutumia,
utundu wa kuendesha vyombo vya ardhini, majini na
angani, utundu wa kuiga sauti za watu, saini za watu,
vyote hivi nani angeweza, kama isingehitajika watu
wawili au zidi kufanya kazi ya mtu mmoja. Jambo
moja tu lililomuuzi ni wanawake, Kamanda Amata
alikuwa mdhaifu sana mbele ya mwanamke, na adui
zake wengi walimuweza kwa hilo tu, walimkamata
kwa hilo tu. Lakini bado walipokuja kuona jinsi na
njia aliyotumia kutoroka walibaki hoi. ‘Kamanda
atabaki kuwa Kamanda tu,’ Madam S alijisemea
huku akiifunga laptop ile ndogo na kuirudisha
mahala pake.
EMBU – KENYA
EMBU, mji uliopo kilomita takribani 120 kutoka
Nairobi, upande wa Kaskazini mashariki kuelekea
mlima Kenya. Ukifika miezi ya kumi na kumi na
moja utafurahi kuona barabara na viunga vyake
vilivyopambwa kwa maua ya rangi ya zambarau
kutoka katika miti ya Jacaranda.
SAA 4:15 USIKU
MAINA HIGHWAY HOTEL
KWA KUTUMIA mwendo wa miguu, Wambugu
alivuta hatu kuelekea katika hoteli hiyo iliyopo
katikati ya mji katika mtaa ya Haille Selasie, moyoni
mwake alikuwa na amani sana kuwa sasa
kafanikiwa kulitoka jiji la Nairobi. Akitegemea
kukutana na mtu wake, Bill siku inayofuata huko
Iryamurai, kabla hajaifikia kaunta ya hotel hiyo simu
yake ikatikisika mfukoni mwake, akaitoa na
kuitazama, private call, ilijiandika, hakuipokea
akaenda kaunta na kuchukua chumba.
Akiwa ndani ya chumba chake Wambugu aliiona
tena simu yake ikiita, akainyakua na kupoke,
“Wambugu, nikipiga simu upokee mara moja,
unafuatwa, hapo mahali si salama, ondoka mara
moja, nenda utafute sehemu salama,”
Ile simu ikakatika, Wambugu akabaki ameduwaa,
hajui la kuamua, ‘Nani ananifuata?’ alijiuliza, ‘Bill
amejuaje?’, ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa
Wambugu kufanya uamuzi, kwa kuwa alikuwa
akijiandaa kuoga, ilibidi aahirishe zoezi hilo na
kujipanga kutoka katika hoteli hiyo, alirudi kaunta
akiwa kaweka mkono wake mfukoni, kashikilia
bastola tayari kwa lolote ambalo litatokea.
Alikabidha funguo na kuaga kuwa atarudi muda si
mrefu. Alitoka na kuzishuka ngazi kadhaa za
mlango huo na kupotelea kwenye kichochoro Fulani
ambacho kilimleta katika maduka na mchanganyiko
wa watu, ‘niende wapi?’ akajiuliza, hakupata jibu,
usiku ulizidi kuwa mnene, kichwa kikimuuma,
mawazo yake yakivurugika, mipango ikigoma
kupangika, ulikuwa wakati mgumu. Wambugu
alivuta hatua ndogo ndogo kuelekea kituo cha tax,
pale alizikuta tax chache zinazongoja abiria wa
usiku, akiwa kutahamaki hivyo mara gari moja aina
ya Jeep Cherokee ilisimama ghafla miguuni mwake,
mlango ukafunguliwa kwa haraka na Kamanda
Amata akatoka bastola mkononi, Wambugu akajua
hapo kazi nzito, alipiga risasi moja kwenye kioo cha
dereva, wakati Kamanda Amata anazunguka gari
kiufundi ili kumfiikia Wambugu, kumbe mwenzake
alishaliona hilo, akalala chini na kupita uvungu wa
gari akatokea upande wa pili kisha risasi mbili
zilifumua matairi nay a tatu ikalenga tank la mafuta.
Kamanda Amata alipogeuka nyuma alishuhudia ile
gari ikipaishwa juu kwa mlipuko huo, akajishika
kichwa kwa sekunde kadhaa kisha akaikimbilia ile
gari na bila kujali, alifungua kwa taabu mlango wa
dereva, na kumtoa Ndege ambaye alipigwa risasi
begani na Wambugu, akamvuta na kumtoa nje, hali
ya Ndege haikuwa nzuri kwani jeraha la risasi na ule
moto almanusura vimmalize. Haikuwa na aja ya
kumtafuta Wambugu aliomba msaada wa wananchi
na kumkimbiza hospitali ya Agha Khan.
Wambugu baada ya kuona kafanikisha hilo,
alikimbilia kwenye viunga vya mji na kutokomea
mbali kidogo na mji. Alitembea polepole na
kutafuta mahali pa kujihifadhi usiku huo maana
aliona sasa hakuna sehemu yanye usalama kwake.
Polisi wa Embu, walifika katika hospitali hiyo na
kukutana na Kamanda Amata aliyekuwa pembeni
mwa kitanda cha Ndege wakati mwenyewe akiwa
katika chumba cha upasuaji.
“Tunataka tujue ni nani jambazi na nina
mwanausalama?” askari mmoja alieonekana kuwa
ndio mwenye sauti aliuliza. Kamanda Amata
alimtazama kwa tuo askari huyu aliyeonekana
anajua sana kuongea. Akamuonesha kitambulisho
chake, lo, Yule askari alilowa ghafla na kutoa
salamu ya kiaskari kwa ukakamavu wa hali ya juu.
“Sasa sikia, kuna jambazi hili hapa,” akachukua
simu ya Ndege na kumuonesha ile picha, Yule polisi
akashtuka kidogo na kushangaa akiwa kakunja ndita
si kitoto, “Huyu, kafika hapa, ni mtu hatari sana
tunamtafuta nchi nzima mpaka nje ya mipaka, ok
sasa kama unaruhusu nianze doria usiku huu,” Yule
polisi alimueleza Kamanda Amata, baada ya kufikiri
kidogo, akaona hiyo ni njia nzuri ya kujua ni wapi
huyo mtu anaweza kuwapo. “Ok, hakikisheni
mnampata akiwa hai maana kuna maelezo nayataka
kutoka kwake,” Yule askari alipopokea hiyo amri,
akapiga saluti na kuondoka.
Usiku huo mchakamchaka ulianza, kila kona kila
mtaa ni gari za polisi kumsaka Wambugu. Kila
nyumba ya wageni ilipekuliwa usiku huo na akila
aliyefanana alibebwa na kupekwa kituoni.
Melchior Ndege alirudishwa wodini baada ya lisaa
limoja kwa oparesheni iliyofanikiwa sana ya kuitoa
risasi iliyokwama katika mifupa ya bega lake la
kulia, majeraha ya moto hayakuwa mabaya sana,
aliweza kuongea kama kawaida japo chupa ya damu
ilikuwa ikiendelea kuingia mwilini mwake.
“Kamanda! Siwezi tena,” alimwambia kamanda
Amata kwa sauti ya chini kidogo, wakati huo
Kamanda Amata alikuwa ameketi kwenye kiti jirani
kabisa ya kitanda kile, “Kwa nini kaka? Tupo pamoja
usijali,” Amata alijibu. “Sikia, nina hasira sana na
Wambugu kama wewe ulivyo na hasira na Bill,
nenda kamsake popote alipo, nitapona tu nikisikia
kuwa umempata na umemtoa roho, nenda Kamanda
kamalize kazi kabla hawajajua kuwa tuko pamoja,”
Ndege alimueleza maneno hayo Amata. Wakapeana
mikono, Kamanda Amata akatoka pale hospitali na
mlangoni wakakutana na Yule polisi, “Vipi?”
alimuuliza, lakini Yule polisi hakujibu kitu, nyuma
yake kulikuwa na polisi wengine watatu, “Kamanda
Amata, upo chini ya ulinzi kwa kuwa unaifanya kazi
hii kinyume cha sheria,” Yule polisi mkubwa
akasema hayo, “Nani aliyekwambia?” Kamanda
Amata akauliza, “Tumepata taarifa kutoka makao
makuu ya polisi Nairobi kwa uthibitisho kutoka
katika ofisi yako huko Tanzania, twende kituoni,”
Yule askari alimuamuru Kamanda. Kamanda Amata
hakuwa na ubishi, alitii sheria bila shuruti,
akapakiwa katika gari na kuondolea hospitalini
hapo.
Wambugu alipoona hali si nzuri, polisi kila upande
alijua kuwa sasa mambo yameharibika, alichomoka
kutoka maficho yake na kutega barabara kuu kuona
kama kuna gari litakalotokea. Mara akaona pikipiki
ikija upande wa kulia kwake akaokota jiwe na
kumpiga nalo Yule mwendesha pikipiki, kisha
akajitokeza barabarani na kuokota ile pikipiki,
akakaa juu yake na kuitia moto, akaondoka kwa
kasi kubwa. Gari iliyokuwa imemchukua Kamanda
Amata ilikuwa ikipita barabara hiyo na mara
wakaiona ile pikipiki ikija kwa kasi sana, dereva
akapunguza mwendo kuona ni nani huyo,
“Msimamishe tafadhali,” Yule mkuu akamwambia
polisi mwingine, ambaye kwa haraka aliruka chini na
kutua barabarni kisha akasimama katikati ya barabar
kumsimamisha jamaa huyo, lakini akiwa katika hali
hiyo, mlio wa risasi ukasikika na mara Yule polisi
akawa chali barabarani, Kamanda Amata akatzama
huku na huku akishuhudia Yule dereva akishuka
kumsaidia mwenzake, akaruka upande wa mbele
kwa dereva na kuigeuza gari kwa fujo kuifuata ile
pikipiki, mwendo uliokuwa ikiendeshwa hiyo land
cruiser haikuwa ya kitoto, Kamanda Amata
alikanyaga mafuta kwa ustadi wa hali ya juu,
akaiona ile pikipiki ikikata kushoto na kuingia
barabara nyingine nae alipofika pale vivyo hivyo
akakunja kuelekea kushoto akiendelea kuifuata ile
pikipiki.
§§§§§
Usiku wa manane, Madam S alipata taarifa ya
kukamatwa kwa Kamanda Amata, taarifa zilitoka
katika ofisi za ubalozi usiku huo, likaandaliwa gari
kwa ajili ya kwenda Embu kutoka ubalozini kwa
minajiri ya kumchukua Kamanda na kumrudisha
Tanzania. Aliamka kwa kusuasua, na kujiandaa,
alipokuwa tayari aliteremka kwa lifti mpaka chini
ambako aliikuta gari hiyo ikimsubiri, akaketi kiti cha
mbele na kuanza safari na watu wengine wawiliyaani
dereva na Mashaka, Yule kijana waliekutana pale
uwanja wa ndege.
Upande mwingine bwana Shikuku alishtushwa na
taarifa za kijana wake Ndege kupigwa risasi na
Wambugu pia kupata ajali ya moto uliosababishwa
na mtu huyo huyo, moyo ulimchafuka na usiku huo
akapanga safari yake ya kwenda Embu kujua nini
kinaendelea. Akiwa njiani alikuwa akijaribu
kuwasiliana na watu wa usalama upande huo kujua
hali kwa ujumla ikoje, na kama ni chuki basi hakuna
mtu aliyemchukia wakati huo kama Wambugu,
aliapa moyoni lazima amtie nguvuni na atumikie
kifungo chake kwa mateso makali.
Kwa ujumla usiku huo kila mtu alikuwa akiwaza
yake juu ya Wambugu. Madam S alikuwa ametulia
kitini haongei chochote, aliwaacha dereva na
Mashaka waongee.
Haikuwachukua muda mrefu usiku huo, masaa
mawili na nusu tu tayari walikuwa Embu na moja
kwa moja walienda katika kituo kikuu cha polisi na
kukutana na mkuu wa polisi wa kituo hicho. Madam
S alijitambulisha kwao na kuonesha kitambulisho
chake.
“Tunasikitika kuwa kijana wako ametoroka,” ilikuwa
kauli ya mkuu Yule. Mashaka akamtazama Madam
S ambaye alikuwa ameketi bila kuongea neno lolote,
“Na isitoshe ametoroka na gari ya polisi,”
akaongeza tena Yule mkuu wa polisi. Madam S
alikuwa akitikisa kichwa tu kuashiria kuwa
ameelewa anachoambiwa.
“Atarudi tu, msiwe na shaka,” madam S akajibu kwa
kifupi, kisha akanyanyuka na kumuamuru dereva
waelekee hospitali ya Agha Khan ili akamuone
bwana Ndege aliyejeruhiwa katika sakata hilo.
Alipofika tu pale hospitali alikutana na Bwana
Shikuku, kila mmoja alimkumbuka mwenzie,
waksalimiana kwa bashasha kwa kuwa ni miaka
mingi hawajaonana. Baada ya hapo wote wawili
wakaelekea ndani ya hospitali hiyo kumuona Ndege
aliyekuwa amelala usingizi.
“Kwa nini usimrudishe Nairobi kwa matibabu?”
Madam S akauliza.
“Amesema hatotoka hapa mpaka amuone Kamanda
Amata,” Shikuku alijibu.
“Ok, wameivana hawa. Ulikuwa unajua kama AmaTa
yuko hapa?” madam S aliuliza tena.
“Ndio kwanza nafahamu sasa kuwa yuko hapa siku
nzote sikuwa najua,” Shikuku alidanganya, wakati
Ndege alishamwambia kuwa kamanda Amata yupo
Nairobi kwa shughuli hiyo ila si kiofisi.
Madam S alitulia kimya akitafakari jambo Fulani,
alionekana wazi kukosa raha usiku huo, aliitazama
saa yake ilikuwa tayari ni saa kumi alfajiri.
§§§§§
Kamanda Amata alikunja kona kali kuingia ile
barabara ambayo ile pikipiki iliingia, alipoenda
kama mwendo wa mita mia hivi hakuiona ile
pikipiki wala dalili zake, akajua kwa vyovyote huyu
jamaa atakuwa mitaa, akasimamisha gari na
kushuka bastola yake mkononi, akawa anashangaa
akitafuta huku na kule akizungukazunguka kwa
hadhari kubwa sana, alipokuwa tayari kukata tama
alisikia mnguruno wa pikipiki kwenye vichaka,
akawahi na kuiona ikitokomea porini, akainu bastola
yake na kufyatua risasi ya kwanza haikua na
shabaha ila ya pili alipiga tairi na kulitoa upepo, ile
pikipiki ikaanguka, na Wambugu akawa chini,
Kamanda Amata akafika eneo lile na kumkuta
Wambugu amekwishasimama na amejiandaa kwa
mapigano, Kamanda Amata alitaka kufyatua risasi
lakini akakuta zimemuishia, aliirusha ile bastola
kumpiga nayo Wambugu, Wambugu aliruka hewani
kama ninja na kuipiga tik tak ile bastola ikapotelea
kwenye vichaka, wakati huo tayari Amata alifika pale
kabla hajajiweka sawa, mguu wa nguvu ulimshukia
Amata begani, akayumba upande na Wambugu
akasimama kwa mguu mmoja kisha akaushusha ule
mwingine taratibu kwa madaha, “Siku zote mnajua
kuwa kila mtu ni bwege, kama ulikuwa hujui basi
mimi ni Sempai,” Wambugu alijisifu huku
akisimama katika pozi la kungfu, Kamanda Amata
akaona hapo ndo penyewe, “Huwa sijibishani na
wahalifu kabla sijawafundisha adabu,” Kamanda
Amata alizungumza kwa gadhabu, akaruka hewani
kiufundi na kuimshia mapigo makali Wambugu,
lakini mapigo yote aliyapangua vizuri sana, kisha
akaanza yeye kupeleka mashambulizi ya mikono
kwa Kamanda Amata, ambaye naye alikuwa
akiyapangua kiufundi sana mpaka Wambugu
akamaliza mapigo yote, Kamanda Amata
alipomuona sasa hana ujanja mwingine ndipo
alipombadilishia staili kutoka kungfu kwenda kick
boxing. Teke la kwanza lilitua mbavuni kabla
hajakaa sawa lapili likatu shingoni kisha zikafuata
ngumi mfululiozo kama ishirini na tano
zilizomuacha Wambugu hoi akigalagala, “Nyanyuka
juu Sempai, upambane na mwanaume wa shoka,
hayo mapigo niliyokupa niliagizwa na Melchior
Ndege sasa naanza ya kwangu,” Kamanda Amata
alipomaliza maneno hayo, alijivuta kwa hatua ndefu
amgfikie Wambugu, lo, Wambugu akamzidi ujanja,
alijirusha kutoka pale alipolala akasimama kisha
akajibinua na miguu yake yote miwili ikatua tumboni
mwa Amata na kumfanya ateme damu, hasira za
Amata zikawaka ghafla, aligeuka nyuma kwa kasi na
kumchota ngwala Wambugu lakini jamaa akaruka
na ule mguu ukapita chini kisha Wambugu
akashusha pigo moja la karate lililotua sawia
kwenya shingo ya Amata na kumpeleka chini mzima
mzima. Kamanda Amata alitambaa kama motto,
damu zikimvuja puani na mdomoni, akaona wazi
asipofanya makeke anaweza akazimishwa na watu
wasiione maiti yake.
“Ha ha ha ha Tanzania Secret Agency namba 1 ndio
wewe!!? Unatambaa kama motto, nyanyuka
upambane na jabali la chuma linalotisha kama kifo,
Kenya yote wananijua na hapa kila goti linapigwa,”
Wambugu akasema hayo kwa kujitamba
akijipigapiga kifuani. Maneno hayo yalimuuma sana
Amata, akanyanyuka kwa kasi na kugeuka
akitazamana na Wambugu ambaye mkononi mwake
alikuwa ameokota gongo, akaliinu na kumpiga nalo
Kamanda lakini Kamanda akalidaka kwa mkono
mmoja, akatazamana na macho mabaya ya
Wambugu.
Taswira za mauaji ya kikatili ya kahaba Rose
ikamjia na kumtia hasira, taswira ya Ndege
akiungua moto ikamjia na kumuongezea hasira,
kauli ya kushushwa cheo ikamaliza kila kitu akilini
mwake.
Kamanda Amata akiwa kalishika lile gongo kwa
mkono mmoja alinyanyua mguu wake na
kulikanyaga kwa juu akalivunja kwa mtindo huo
kisha akabaki na kipande, kwa hasira na visasi
akamchoma nacho Wambugu tumboni, yowe la
uchungu lilimtoka akaanguka chini, Amata
akamuendea palepale alipo na kumvua kibegi chake
kisha akakivaa yeye mgongoni, akamnyang’anya
simu yake na kuitia mfukoni kisha akamkamata
ukosi wa jacket lake na kumburuza mpaka kwenye
kibarabara, akampigiza sura yake chini kwa nguvu,
“Bill yuko wapi?” akamuuliza kabla hajajibu
akampigiza tena kwa nguvu na kuvunja mfupa wa
pua. “Sasa ukiniua ndio ntasema?” Wambugu alijibu
kwa uchungu. “Nambie haraka, Bill yuko wapi?”
Kamanda aliuliza kwa kelele maana hasira ilikuwa
bado imetawala kichwa chake. Wambugu alinyanyua
uso wake na kutema mabonge ya damu, “Kuna
binadamu ambao hamtakiwi kuzaliwa kabisa, kama
wewe na Bill, nakuuliza mara ya mwisho kabla
sijakutenganisha na roho yako, Bill yuko wapi?”
Kamanda aliendelea kuhoji, “Mi si si si sssjui,”
Wambugu alijibu kwa tabu sana. Kamanda Amata
akamburuza mpaka aliposimamisha gari na
kumuinua akamsimamisha wima akimuegemezea
katika bodi la gari. “Wambugu! Nakuua,” Amata
alimwambia, “Niue braza, kwa maana ukiniacha hai
nitateseka sana na mkono wa sheria,” Wambugu
akajibu. “Niambie Bill yuko wapi?” akauliza tena,
“Braza utanitesa utaniua lakini mimi sijui Bill yuko
wapi alishatoroka hapa muda mrefu,” kamanda
Amata alishikwa na hasira akampiga kichwa kimoja
maridadi na kumuachia akianguka chini kama
mzigo.
Mara taa za gari mbili zikawamulika kutoka
barabara kuu, na zile gari zikaja mpaka pale,
walikuwa ni polisi, wakateremka haraka na
kumuweka Kamanda Amata chini ya ulinzi. Kamanda
Amata akanyosha mikono juu, wale polisi wakaja na
kumtia pingu, nyuma yao akaja mtu mnene kiasi
aliyeonekana kuwa na sura ya kikatili isiyo na
chembe ya huruma, akamuendea Kamanda Amata,
akamtazama usoni, juu mpaka chini, “Hey, askari!”
akaita, “Mfungue pingu Kamanda, mpe na begi
lake,” wale askari wakafanya hivyo, kamanda Amata
akapokea lile begin a kulitupia mgongoni. “Mzima
au amekufa?” Yule bwana akamuuliza Kamanda.
“Mzima huyo hawezi kufa kirahisi,” Amata akajibu.
Yule bwana akatoa amri ya kupakiwa Wambugu
garini kisha yeye na Kamanda Amata wakaingia
katika gari ndogo ya polisi na kurudi mjini.
“Kamanda Amata, umetusaidia kazi moja ngumu
sana ambayo jeshi la polisi la Kenya na vyombo
vingine vya usalama imetusumbua kwa miaka
takribani kumi kumpata huyu mtu, asante sana
kijana” akamshukuru Kamanda na safari ikaendelea
mpaka kituo cha polisi cha Embu.
Madam S na Mashaka walikuwa hapo kituoni pia
wakimsubiri Kamanda Amata, walimuona alipokuwa
akishuka katika ile gari na waziwazi alikuwa
ameumia sana kwa jinsi alivyokuwa akitembea,
wakakutana uso kwa uso na Amata, wakatazamana.
“Madam, kijana wako huyo wapo, sisi hatuna deni
nae!” alisema Yule bwana mwenye mwili mnene,
kisha akapita kwenda ndani ya kituo hicho,
ijapokuwa ilikuwa alfajiri lakini watu walijazana
kutaka kuhakikisha kama kweli jambazi sugu
Wambugu limekamatwa, jambazi lililowanyima
usingizi Wakenya wengi kwa miaka mingi.
Kamanda Amata, Madam S na Mashaka waliingia
kwenye gari yao na kuondopka eneo lile, moja kwa
moja mpaka hospitali ya Agha Khan ili kwanza
apate huduma ya kwanza. Ndani ya nusu saa
alikuwa tayari amefanyiwa check up ya nguvu na
kutibiwa palipohusika, Mashaka akamuendea Amata
katika chumba alichokuwapo kisha akamkabidhi
begi jeusi mpano wa briefcase, alkipofungua ndani
akakuta suti mpya, saa ya kisasa kwa kazi yake na
bastola ndogo.
“Umerudi katika hali yako Kamanda,” Madam S
alimwambia walipokutana mara tu Kamanda
alipotoka kule ndani, “Yeah, lakini bado kitu
kimoja,” kamanda alisema, “Nini?”
“Nataka kumuona Ndege,” akajibu. Wote watatu
wakaingia wodini alikolazwa Ndege na kumkuta
tayari amewekwa katika kitanda cha magurudumu,
amefungwa mikanda sawia na chupa ya
majiiliyowekwa baada ya ile ya damu ikiendelea
kwenda, “Melchior Ndege,” Kamanda alimwita huku
akwa amemuinamia pale kitandani, “Amekufa au
amekimbia?” Ndege aliuliza kwa shauku, “Hali yake
ilivyo hawezi kuiona jioni, yuko katika mikono ya
polisi,” Amata alimwambia Ndege ambaye
alionekana wazi kuifurahia habari hiyo. “Asante
Kamanda,” Ndege alishukuru, “Asante na wewe”
Kamanda akamalizia.
§§§§§
Kama kuna habari iliyomfurahisha Sargeant Maria,
basi ni hii ya kupatikana kwa Wambugu, kwa
sababu baada ya kumbana sana Mellina kwa kipigo
na mateso makali alitaja washirika wote akiwamo
Wambugu. Sargeant Maria na wenzake waliishiwa
nguvu kusikia kuwa Wambugu anahusika na mauaji
ya Kasisi, swali lilikuwa, tutampataje? Lakini ghafla
alfajiri hiyo wanaambiwa kuwa Wambugu kapatikana
huko Embu karibu na msitu wa Njukiri baada ya
vyombo vya usalama kupambana nae vilivyo, baada
ya kutaka kujua zaidi ndipo Sargeant Maria
aliposikia juu ya Kamanda Amata ambaye yeye siku
zote alijua ni mtu wa kwenye riwaya tu, hakujua
kuwa ni burudani ya waandishi kuandika visa vyake
kila amalizapo kimoja na kuanza kingine. Ulikuwa ni
ushindi mkubwa, mkubwa sana, Maria alijiuliza,
Mellina tumemkamata, Cheetah, kauawa, Wambui
kauawa, Wambugu ndio huyu hapa, sasa ile
Mostrance ambayo ndicho chanzi cha kazi nzima
haijapatikana, bado kuna kazi mbele.
ITAENDELEA....
::: KITABU CHA RIWAYA HII KITAKUWA SOKONI
MWEZI JULAI. HAKIKISHA UNAPATA NAKALA
YAKO.::::
 
Alichomoa memorycard kutoka katika ile darubini
akaipachika katika kompyuta yake kisha akatuma
zile picha kwa Chiba Tanzania, acheki kama zina
lolote. ‘Nimuueje Bill?’ alijiuliza, ‘Uso kwa uso au
nimdungue kwa mbali?’ bado alikuwa akishindana
na nafsi yake katika kuamua juu ya hilo,
‘Kumdungua ni kumuogopa, nitapambana nae,’
alikata shauri.
§§§§§
BILL hakuamini anchosikia kutoka kwa mmoja
wafuasi wake, kuwa Kamanda Amata yupo Aachen
na tayari ameshawajeruhi vibaya walinzi wa nje wa
Andreas waliokuwa wakimfuatilia kule makaburini.
“Nani aliwaambia yule mtu anafuatwa namna hiyo
mliyofanya nyie?” Bill aliwauliza wale vibaraka wake.
Baada ya kumaliza mazungumzo yake na watu
wake, hakuna kilichokuja akilini mwake zaidi ya
kukimbia mji huo na kujificha sehemu nyingine,
‘Lakini nitaonekana nimemuogopa, nitapambana nae
hapahapa. Bill alitoka mchana huo na kuelekea
mjini ambako baada ya pitapita zake akaingia
katika kanisa kuu la mji huo, akiwa sasa
medhamiria na ameamua kumsaka Amata kwa njia
yoyote ile. Alikuta watoto wakicheza cheza katika
ngazi za kanisa hilo, mara mbele yake gari oja
ilikuwa ikija pale aliposimama, Bill akaisimamisha,
alikuwa ni Fr Frank, akitoka kwenda mjini kutafuta
mahitaji, Bill aliiendea ile gari na kufungua mlango
akaingia na kuketi kiti cha pembeni bastola
mkononi, “Unahifadhi wanausalama sio?”
alimuuliza Fr Frank ambaye alionekana kutetemeka
mwili mzima. “Hapana, hapana,” akamjibu. “Huyo
kasisi wenu mweusi ni nani? Si Kamanda Amata?”
swali lingine lilitua sikioni mwa Fr Frank. Kisha Bill
akamuamuru Fr Frank kuendesha gari mpaka
maeneo anayoyajua yeye. Lilikuwa ni shamba
kubwa ambalo lilikuwa na aina mbalimbali ya miti
na mazao, Bill alimshusha Fr Frank na kumuongoza
katika banda Fulani, akaingia, alichokifanya ni
kumfunga kamba kisha kuanza kumpa mateso
makali ili amueleze kama ni kweli wamemficha
Kamanda Amata ndani ya nyumba yao, Fr Frank
hakujibu kabisa swala hilo.
“Unajifanya jeuri siyo, basi yatakupata yaliyompata
Fr Gichuru kule Nairobi,” Bill alimwambia Fr Frank
huku akimpa kipigo kikali kwa kutumia mkanda wa
kijeshi.
Kisha akamuacha ndani ya banda hilo nay eye
akaondoka kurudi mjini. Breki yake ilikuwa moja
kwa moja ofisini kwa Andreas, kumpa habari hiyo
nyeti. Andreas hakuonekana kuumiza kichwa kwa
swala hilo. “Bill, nimeshakwambia fanya nunaloweza
umuue bas, sitaki habari nyingine,” Andreas
alisisitiza. Kabla hajajibu kitu, Andreas akamwambia
Bill, “Ila leo jioni tukutane pale nyumbani kuna tafrija
fupi kwa ajili ya kijupongeza kwa kukamilisha hili
swala, na Fr Gustav atakuwepo maana tayari yuko
njiani.” Bill aliupokea mualiko huo na akawa tayari
kujumuika na wageni watakaokuwepo siku hiyo.
Fr Frank alibaki kule bandani peke yake, mwili wake
ukiwa hoi kwa maumivu makali ya kipigo
alichokipata kwa Bill, kwa kutumia ujanja alionao
alijua jinsi ya kujinasua katika kifungio hicho,
akafanya makeke yake na baada ya dakika kumi na
tano alikuwa huru, sasa kilichomsumbua ni kupata
funguo ya kutokea nje. Fr Frank alitafuta mahali
pazuri kwa kujificha ndani ya banda lile akapapata,
akajificha na kutulia tuli akisubiri yeyote atakayekuja
aelewane nae. Fr Frank hakuwa mjinga katika
mapigano iwe ya mikono au ya silaha, alikumbuka
sana alipokuwa jeshini mara baada ya kuhitimu
masomo yake huko Austria, alipokuwa akijifunza
karate na kungfu akiwa seminari, alimstahi Bill kwa
kuwa alihisi labda kuna kitu atakachokigundua
mahali hapo. Fr Frank aliajiriwa na FBI kisirisiri na
alikuwa hapoa Aachen kwa kazi moja tu ya
kumnasa Bill na kupeleka taarifa zote huko
Marekani ili wajue jinsi ya kumnasa na kumuweka
chini ya ulinzi. Hakutaka kujionesha juu ya hilo hivo
alikuwa makini sana katika kulifanya. Ni miezi
mitatu sasa tangu ahamishiwe katika kanisa hilo
kuendelea na uchunguzi wake, na alikuwa akiju kila
ktu kilichotokea kule Nairobi. Akiwa katika mawazo
kule katika maficho yake alisikia mlio wa gari ikija
maeneo yale akatulia na kusubiria watu hao ambao
walikuwa wakizungumza wao kwa wao,
harakaharaka alielewa kuwa watu hao wa[po watatu.
Mara mlango ulifunguliwa na wale jamaa wakaingia
ndani wakashangaa kukuta kiti wazi, hayupo Fr
Frank.
Mmoja wao akainua redio yake na kutoa taarifa kwa
waliowatuma kuwa mtu wao katoroka, akiwa tayari
kamaliza kuongea na simu hiyo, aliirudisha mahala
pake na kwaamuru wake wenzake kumfuata, lakini
kabla hajafika mbaliki lilikuwa ni t eke zito lililotua
nyuma ya sjingo yake, kisha akajiviringa na
kusimama upande wa pili, wale wawili nao wakaja
kwa pamoja Fr Frank akaruka juu nakuitawanya
miguu yake na kumpiga kila mmoja kwa mguu
wake, mmoja alijibamiza vibaya katika nguzo
iliyokuwa katika banda hilo na kupasuka sehemu ya
nyuma ya kichwa chake. Akajibwaga chini akiwa
tayari hana uhai, wakati mmoja akiwa tayari katoka
nje mwingine aliendelea kumkabili Fr Frank, alirusha
ngumi ikakwepwa, akarusha nyingine ikakwepwa
tena kwa mtindo uleule, kabla hajakaa sawa Yule
jamaa akapigwa teke hafifi katika kanyagio la mguu
wake, aliposhusha sura kuangali chini, alijikuta
anachezea makonde yasiyo na idadi ambayo
yalimpeleka chini sakafuni akiwa hajiwezi, akiwa
anatambaa alipigwa teke moja la nguvu mbavuni na
akalala chini bila kipingamizi.
Fr Frank alimwangalia Yule jamaa akigalagala pale
chini, mara akakumbuka kuwa kuna aliyetoka nje,
akaichomoa bastola katika mfuko wake na kuvuta
hatua chache kuuelekea mlango, mara akasikia
nyuma yake mlio wa kiondoa usalama cha bastola,
kwa kazi ya ajabu aligeuka na tayari kidole kilikuwa
kwenye trigger, aligeuka huku akiwa anaenda chini
kupiga goti moja akachezesha kidole na risasi mbili
zikamtwanga Yule jamaa kifuani, akatoa yowe la
maumivu nay eye akajiunga na wenzake pale
sakafuni.
“Mwambe Bill, sina shida nae, na hsinifuate fuate,”
alimwambia Yule aliyekuwa hai bado lakini hali yake
ilikuwa mbaya kwani alimvunja mbavu mbili.
Akatoka nje ya ile nyumba na kuingia katika gari
yake iliyotumika kumleta pale akapotelea mjini
kama kawaida, akarudi mpaka misheni, akaegesha
gari palepale, na kuingia ndani.
§§§§§
KAMANDA Amata hakuamini anachokiona katika
darubini yake, mmoja wa wahudumu wa misheni,
aliyempokea siku alipofika alikuwa akiongea na
watu Fulani katika jumba la Don Andreas, Kamanda
Amata akagundua hapo kuwa kumbe siri zingine za
yeye kufika pale ijapokuwa ilikuwa kwa njia ya siri
ni yeye aliyeipeleka kwa watu hao, akatoka na
kuelekea jikoni, pale aliwakuta wafanyakazi wengine
wakiandaa chakula cha jioni, hakuongea na mtu,
akakiendea kibao kinachoonesha zamu za
wafanyakazi, kweli siku hiyo Yule mfanyakazi
alikuwa off, akaondoka akarudi ndani kila mtu mle
jikoni alikuwa akimwangalia mtu huyu mweusi,
walimdharau kwa rangi yake lakini yeye hakujali.
Alirudi tena chumbani kwake mara hii hakumuona
Yule mtumishi pale alipokuwa mwanzo.
Akatembeza tena darubini yake na kunasa dirisha
linguine lakini hakuwaona wale watu waliokuwa
wakiongea na Yule mhudumu. ‘Msaliti’ alijisemea,
na mara mlango wake ukagongwa, akauendea na
kuufungua taratibu, alikuwa Fr Frank, akaingia na
moja kwa moja akasimama mbele ya Kamanda,
“Bill ameshajua kama tuko hapa?” Frank alisema,
Kamanda Amata akatulia kumwangalia, hakuielewa
kauli yake, “Uko hapa na nani?” akauliza. Fr Frank
akagundua kuwa ametereza katika maongezi yake,
akamtazama Amata, akakutana na sura ilijikunja
kuwa sasa haina utani hata kama na askofu,
Kamanda Amata akatoa bastola yake na
kumnyooshea Fr Frank, “Niko na nani?” akauliza
tena, “Mmeamua kunicheza shere sio? Mpishi wenu
anatoa siri za mimi kuwapo kwa Bill sivyo, kumbe
mnajua kila kitu, niambie niko na nani?” akazidi
kuuliza.
Fr Frank hakuwa na la kujibu, “Usihofu Kamanda,
mimi si mbaya kwako,” akasema huku akitetemeka.
“Ninyi wote ni wasaliti humu ndani,” Kamanda
Amata bhakuonesha kabisa masihara katika hilo,
uso wake uliloa jasho la hasira. Fr Frank
akamtazama tena Kamanda,
“Mimi niko upande wako Kamanda,” akamwambia.
“Naitwa Frank Edson, kutoka FBI, idara ya upelelezi
ya Marekani, nipo hapa kwa kazi maalumu lakini
hakuna anayejua,” akajieleza.
“Lete kitambulisho,” kamanda akaomba, Fr Frank
aktoa kitambulisho katika mfuko wake wa ndani na
kumpa Amata akakisoma, ni sahihi kabisa.
§§§§§
Frank Edson, mpelelezi kutoka shirika la kipelelezi
la Marekani FBI, alikuwa amepewa kazi maalum na
ofisi yake, kazi ya kumfuatili Bill ili amtie mkononi
na kumpeleka Marekani akajibu mashitaka yake.
Frank kama alivyo alikuwa kasisi katika kanisa la
Katoliki huko Texas Marekani, ijapokuwa alikuwa
akifanya kazi hiyo kwa siri kubwa sana lakini
viongozi wake wa juu walilifahamu hilo.
Katika harakati za kumsaka Bill kama jasusi
linaloendesha shughuli zake kwa kukodiwa kwa nia
mbaya na matajiri mbalimbali duniani, Marekani
ilianza kumsaka tangu pale alipotekeleza mauaji ya
balozi wao kule Iraq miaka kadhaa nyuma.
Walimsaka kila kona bila mafanikio. Bill akaibuka
tena katika sakata hilo la Nairobi, kwa kuwa wale
waliokuwa wametumwa Kenya walishindwa
kumnasa Bill, Frank alitumwa muda mrefu huko
Ujerumani kabla Bill hajaenda Nairobi, hivyo
akapewa kazi ya kuhakikisha anamtia mkononi
hukohuko.
Frank alifika Aachen kama kasisi aliyekuja kwa kazi
maalum na kufikia katika kanisa kuu la Aachen.
Hivyo alijua kila kitu kinachoendelea juu ya Bill, hata
Kamanda ASmata alipokuwa anakuja, Frank alikuwa
akimfuatilia tangu akiwa Nairobi hivyo alijuwa wazi
kuwa lazima atafika kwa kazi hiyo. Ili asilete
Madhara, kwa kuwa yeye alitakiwa ampfikishe Bill
akiwa hai huko Marekani, alijua kuwa Kamanda
Amata kaja kwa mawili kummaliza. Hivyo
alimpokea Amata kwa maelekzo toka ubalozi wa
Tanzania, wakijifanya kuwa kanisa linataka
kushirikiana na Tanzania katika sakata hilo hasa
kwa kuwa walikuwa wanaitaka monstrance yao
kumbe sivyo.
Bill alimjua vyema Frank Edson, na alipewa taarifa
kuwa yuko hapo kitambo na mmoja wa
mashushushu wake ambaye ni mfanyakazi wa
misheni hiyo. Frank Edson, siku zote hakugundua
kuwa ndani ya misheni hiyo kuna mamluki mpaka
alipokuja kupewa siri hiyo na Kamanda Amata.
§§§§§
Fr Frank akamuonesha Kamanda Amata beji yake
maalum ya FBI iliyobanwa vizuri katika loop ya
suruali yake. Kamanda Amata akashusha bastola
yake na kuirudisha kiunoni. “Samahani, si unajua
hizi kazi zetu hakuna kuaminiana,” akamwambia
Frank, “Hamna shida hata ningekuwa mimi
ingekuwa hivyohivyo,” akajibu Frank, kisha wote
wakasogea pale dirishani.
“Sikiliza, unamjua huyu?” kamanda akamuuliza na
kumuonesha baadhi ya picha zilizopigwa na ile
camera yake aliyoiunganisha na ile darubini pale
dirishani, Frank alipigwa na bumbuwazi akabaki
midomo ikimchezacheza, “Kaka ungeshakufa muda
mrefu sema tu huo ukasisi wako umekulinda, la
tayrai mauaji ya kasisi yangeshafanyika hapa
Aachen,” Kamanda alimwambia Frank huku
akimpigapiga kifuani kwa ngumi yake.
“Sasa Kamanda, hapa mambo yameshaharibika
inaonekana huyu mpishi anajua na ameshawapa kila
habari zetu, ndo maana walikufuata kule makaburini.
Bill huwa hatoki ovyo lakini alinifuata leo hapa,”
Frank akmwambia Kamanda. Habari hiyo ilimfanya
Kamanda kushtuka, “Unasema Bill alikuja hapa?!”
kamanda akauliza.
“Ndiyo, Bill kaja akaniteka hapa leo asubuhi na
kunipeleka huko kwenye maficho yao,” Frank
akaeleza. “Sasa nani kakuokoa?” lilikuwa swali la
Kamanda.
“Si nimekwambia mi ni FBI yaani Federal Beureau
of Investigation, sishindwi kujiokoa kwa watu dhaifu
kama hawa,” Frank alitamba, sasa akiwa amevua ile
kanzu ya kikasisi. “Laiti ningepata hiyo nafasi
ningemmaliza huyo mtu palepale, maana sihitaji
mahojiano naye, nimetumwa kuirudisha roho yake
kwa muumba wake, bas,” Kamanda akamwambia
Frank. “No Kamanda, sikiliza, unatakiwa unisaidie
tumpate Bill akiwa hai, serikali ya Washington
inamtaka akiwa hai ili akaungane na wenzake kule
Guantanamo bay,” Frank akamwambia Amata.
“Hamna shida, mimi serikali ya Dodoma imenituma
niitenganishe roho na mwili wake, so tutagawana,
wewe utamchukua akiwa hai na mi nitamtoa roho
yake,” Kamanda Amata alimwambia Frank, kisha
wakatazamana si kirafiki tena sasa kiadui zaidi. “Na
hapa siwezi kuishi, hapanifai, kwa heri ya kuonana,”
Amata akamalizia, kisha akamuacha Frank bado
amesimama akitweta kwa hasira wakati yeye
anaifungua ile darubini yake pale dirishani.
Saa moja baadae, Kamanda Amata alikuwa nje ya
uwanja wa misheni hiyo, hakuna aliyejua kuondoka
kwake, akiwa kava kofia kubwa aina ya pama na
miwani myeusi akasimamisha tax iliyokuwa ikipita
mbele yake, “Novotel tafadhali,” Kamanda
alimwambia Yule dereva, naye bila kushangaa
alipiga gia na kusonga mbele, dakika chache
walikuwa mbele ya hotel hiyo, “Deutsche Mark 75
tafadhali,” Yule dereva alimwambia Amata, “Bado
unatumia hiyo pesa ya kizamani? Hapa nina Euro na
Dollar,” Kamanda akmwambia yule dereva, “Ok, US
Dolar 65” akabadilisha, Kamanda Amata akampatia
pesa yake kisha akaiendea kaunta ya bhotel ile.
“Nikusaidie boss,” mmoja wa wahudumu alichukua
suitcase ya Amata na kutangulia Kaunta kisha
akasubiri pembeni.
“Jina tafadhali,” sauti ya mhudumu mrembo kama
Malaika ikamuuliza Kamanda Amata. Kama
unavyojua ugonjwa wa kamanda Amata, warembo,
akatabasamu, “Fransisco Kintu,” akajitambulisha
kwa jina bandia. Yule mhudumu akaandika kwenye
kompyuta yake, “Passport yako au kitambulisho
tafadhali,” Yule mhudumu akaomba vitu hivyo
kimojawapo. Kwa kuwa Kamanda daima alikuwa
habahatishi, alivuta wallet yake na kuchomoa moja
ya kitambulisho akampa, ‘Fransisco C. Kintu –
Utaifa: Uganda – Kazi: Muandishi wa habari UBC.’
Maelezo hayo yalionekana juu ya kitambulisho.
Baada ya kuingiza maelezo hayo katika kompyuta
yake, akamrudishia kile kitambulisho.
Kamanda Amata akauliza bei kwa siku, akatajiwa
akahesabu fedha ya siku mbili akampa Yule dada,
“Oh samahani bwana Fransisco, tuhitaji Maestro
card au Visa card kama hauna basi kadi yoyote ya
malipo,” Yule mhudumu alimwambia Amata, akili ya
Kamanda ikafanya kazi haraka, “Samahani situmii
hivyo vitu, ninalipa cash, kama haiwezekani basi.”
“Ok, nitakusaidia kwa leo, lakini mara nyingine ukija
Ulaya hatulipi kwa cash, sawa bwana?” Yule
mhudumu akamwambia Kamanda kwa lugha safi ya
kiingereza.
“Ich danke Ihnen” (nakushukuru) Kamanda Amata
alishukuru kwa Kijerumani msaada huo.
“Danke, gleichfalls!” (nakushukuru pia) Yule
mhudumu naye akajibu, huku akisimama na kelekea
sehemu Fulani, akaja na kadi mkononi akampatia,
Kamanda Amata akaitazama, kisha akatoa kadi
yake ya kibiashara na kumuwekea mezani,
akaondoka pale kaunta na kuelekea ghorofa ya juu
kwa kutumia lift.
175 ilikuwa ni namba iliyosomeka mlangoni mwa
chumba hicho, Kamanda Amata kama kawaida yake
aliingia ndani na kukikagua chumba hicho kwa staili
ileile aliyoizoea kuona kama kuna chochote cha
kufanya ajulikane uwepo wake.
9
CHAKULA cha jioni kilikuwa tayari, simu ikapigwa
chumbani kwa Amata kutoka pale kwenye chumba
cha chakula ambapo Fr Frank na wageni wengine
walitumia. Simu iliita kwa muda mrefu haikujibiwa,
ikarudiwa na kurudiwa lakini wapi. Ikabidi Fr Frank
aende chumbani kwa Kamanda Amata
akamwangalie, alipogonga mlango hakuna jibu
lililotoka ndani, akanyonga kitasa na mlango
ukafunguka, alipoingia ndani hakukuta mtu, chumba
kilikuwa tupu, kitanda kilitandikwa vizuri kana
kwamba hakukuwa na mtu aliyekuwa akikitumia
chumba hicho.
Akili ikamzunguka Fr Frank, akaona sasa kazi yake
inakuwa ngumu ya kumpata Bill akiwa hai kutokana
na kutoweka kwa Kamanda Amata.
Fr Frank alirudi mezani akiwa na hasira, “Mgeni
wetu hayupo, kaondoka bila kuaga,” wale
wahudumu wakashangaa kapitia wapi kwa kuwa
hawakumuona kupita hata katika mlango wa
kutokea nje. Fr Frank ndipo alipoelewa maneno
aliyoambiwa tangu mwanzo na wakuu wake wa kazi,
‘Mtazame sana Kamanda Amata, ni mjanja zaidi ya
CIA, huyo ni TSA no 1 ana uwezo wa kujigeuza
hewa,’ Fr Frank alipokumbuka maneno hayo
akaanza kucheka mwenyewe, kisha akaketi na
kuendelea kula huku akifikiri zaidi juu ya Amata,
kama alitaka kufanya kazi aliyopewa kwa muda
mrefu basi sasa ilimlazimu kubadili utaratibu huo
kwani Kamanda Amata alitaka kuifanya kwa muda
mfupi zaidi, kasheshe.
§§§§§
NOVOTEL AACHEN – CASINO
KAMA ILIKUWA ni siku ya bahati kwa Kamanda
Amata basi hiyo ilikuwa mojawapo kati ya chache
katika maisha yake. Alipotoka kaunta alipewa
kijikaratasi kama brosure ndogo, hakuwa na muda
wa kuifungua ndani, baada ya kujiweka sawa,
alipomaliza kuoga na kuchagua suti safi kati ya zile
alizozikuta ndani ya kabati hilo, akaijonge meza
yake na kukinyanyua kile kijikaratasi kilichopambwa
kwa rangi za dhahabu za kuvutia, akakifungua na
kukisoma, kilikuwa ni juu ya shindano la kamali
ambalo lingefanyika siku hiyo saa 3:30 usiku katika
casino iliyopo katika hotel hiyo, matajiri wengi
walialikwa, hakuamini kabisa kama katika
walioalikwa alikuwemo Don Andreas.
Akajua hapo kuwa Don Andreas ni mcheza kamali
maarufu sana kwa jinsi alivyoelezewa pale katika
hiyo karatasi, pia matajiri wengine wengi walialikwa,
hivyo hata yeye alipewa nafasi kama angependa
kushiriki, ama kwa kutazama shindano hilo au kwa
kushindana kama ana uwezo. Tabasamu pana
likaupamba uso wa kijana shababi, Amata. Katika
ile karatasi ya mualiko kulikuwa na namba za
kupiga kama utahitaji kushiriki kucheza, akavuta
simu ya mezani na kupiga hizo namba kisha
akaongea na mchezweshaji wa huo mchezo na
kusajiliwa. Kamanda Amata akasubiri muda ufike ili
aweze kushiriki mchezo huo na pia kuonana na Don
Andreas ana kwa ana.
SAA 3:00 USIKU
POKER POINT
WAGENI walianza kuingia katika ukumbi huo
mkubwa wenye kila aina ya starehe, huku kukiwa na
muziki wa jukwaani ukipigwa na mwanamama
mkongwe aliyealikwa siku hiyo Tina Turner kutoka
Marekani. Watu walikuwa wengi na kila mmoja
alionekana akiwa ametingwa na shughuli zake ama
kunywa pombe na wapenzi wao au wakicheza
michezo kama roulette, slots machine, lucky wheel
na mingineyo mingi.
Ni meza moja kubwa sana ilibaki wazi hakuna mtu
aliyeketi kwenye viti vilivyozunguka meza hiyo, viti
kumi na nne, saba kwenye mstari wa mbele
uliopakana na meza hiyo yan kijani yenye michoro
kadhaa na saba vingine vilikuwa nyuma yake, lundo
la karata maalum zisizochoka lilikuwa limewekwa
hapo juu, taa angavu kabisa isiyokusumbua macho
ilikuwa ikiwaka na kumulika eneo lile nyeti kwa watu
nyeti. Mmoja baada ya mwingine waliingia eneo lile
wakisindikizwa na akina dada warembo kabisa na
kuwapanga vitini kwa namba. Baada ya kutimia
vilibaki viti viwili, kimoja cha mbele na cha nyuma
cha mpambe.
Wote walishangaa kumuona mtu anayeletwa na
mwanadada mrembo, kijana mweusi, aliyependeza
kwenye suti nyeusi iliyotanguliwa na shati jeupe na
tai ndogo ya kubana shingo (neck tie), akakribishwa
na kuketi katika kile kiti kimoja, akawatazama
mmoja baada ya mwingine kisha mchezo
ukafunguliwa na mchezeshaji akiwataka wachezaji
kujitambulisha mmoja baada ya mwingine. Kila
mmoja alijitambulisha na Kamanda Amata
alijitambulisha kwa jina lile la bandia akijisema
kuwa yeye ni mwanahabari lakini ni mcheza kamali
mzuri sana katika macasino ya Afrika Mashariki.
Akakribishwa kwa kupigiwa makofi. Kamanda
Amata alijikuta akiwa amekaa uso kwa uso na Don
Andreas.
Mtu mmoja mnene, mwenye sura ya tabasamu
muda wote, alikuwa akimtazama kijana huyu bila
kummaliza. Mchezo ulianzishwa na kila mmoja
alitakiwa kuweka dau la kuanzia lisilopungua $
2500, matajiri hao wakaanza kuweka na kuweka
pesa zao kwa kutumia chungu maalumu
kilichopitishwa mezani na mmoja wa wachezeshaji.
Kila mtu aliweka kiwango anachojua kuwa anaweza
kumudu. Zamu ya Kamanda Amata, kila mmoja
alimtazama usoni, akaingiza mkono ndani ya koti na
kutoa $ 5000 na kuweka katika chungu hicho.
Mcehezo ukaanza taratibu kila mtu akiwa na karata
zake. Mchezo ulikuwa mgumu kidogo kwa maana
kila mmoja alikuwa anatumia akili sana katika
kuzifananisha karata hizo na zile zilizofichwa, kila
aliyeshindwa alitoka, hivyo wakazidi kupungua,
Kamanda Amata alikuwa wa nne kutoka na
kuwaacha watatu, Don Andreas, na tajiri kutoka
Venezuela pamoja na mwanamama tajiri kutoka
Berlini.
Mchezo ukaendelea na mwisho wa mchezo Don
Andreas akatoka mshindi na kukusanya maelfu ya
dola za Kimarekani.
Makofi ya pongezi yakatawala katika meza ile.
Mchezo ule ukaisha, ukatakiwa kuanza mwingine
kwa wale wanaohitaji kuendelea. Wote walirudi tena
mezani na ‘betting’ zikaanza kwa mara nyingine,
chungu kikapita na kila mmoja akatia mkono
kuweka chochote lakini wenzako sharti waone kile
uwekacho, zamu ya Kamanda Amata, kama kawaida
wote walimtolea macho, akaingiza mkono wake
tena katika koti na kutoa kitita kama kilekile, $
5000 zingine akaweka, wengine katika katika
mchezo ule wakaguna, kwa jinsi walivyomtazama
hakuwa na muonekano wa kuwa na pesa kiasi hicho
anachotoa katika kila bett moja.
Yeye mwenyewe hakuwajali, kwa kuwa hakuna
aliyejua mpaka hapo kuwa ni nini anachokitafuta,
hivyo hakuona tatizo kutumia pesa hizo anazopewa
maalum kwa ajili hiyo ili kupata kile anachotaka.
Mchezeshaji aliendelea kuchezesha mchezo ule kwa
makini na mbwembe za hali ya juu. Mchezo
ukaendele, poker, mchezo wa karata ambaon
unatakiwa ucheze kwa kupanga kareta zako zifanane
na ile iliyofichwa ambayo hakuna anayeijua, mchezo
wa matajiri unaochezwa kwa kuwekeza pesa nyingi,
wengine huweka magari au majumba. Kamanda
Amata mchezo huu aliupanda sana na sehemu yake
kubwa ya kucheza ilikuwa pale New Africa casino,
Dar es salaam. Wachezaji walianza kupungua katika
mchezo kwa kuwa hawakufaulu, walizidiwa maarifa
na wengine, mara hii Kamanda Amata alidumu
katika mchezo, japokuwa hakushinda lakini alitoka
wa pili na mchezo wa mwisho alicheza na Don
Andreas, ambapo alizidiwa kwa ujanja mdogo sana.
“Mr Fransisco, unaweza kucheza tena kwa kuwa
umeikaribia bahati, umekaribia utajiri, weka dau
lingine na ucheze tena. Kamanda Amata alijikuta
hana pesa zaidi, alikuwa na kiasi kidogo ambacho
hakingefaa sana kununua token. Mchezeshaji
akawapa breki ya kujiweka sawa. Kamanda Amata
akainuka na kuelekea kaunta ambako aliagiza glass
moja ya pombe kali, akinywa taratibu huku
akiandika ujumbe kwa kupitia saa yake kwenda kwa
Madam S, dakika moja baadae, alipata majibu na
akayafanyia kazi. Mara moja akafanya mchakato
palepale hotelini kuweza kubadilisha pesa
aliyotumiwa na Madam S, $ 1500 si haba kwa
mchezo huo wa mwisho kwa mujibu wa Yule
mchezeshaji.
Meza ilijaa tena wadau, kabla hawajaanza
mchezeshaji akatoa rai yake kama ilivyo sheria ya
mchezo.
“Sasa tunaingia raundi ya mwisho, tumeona wote
waliofanya vizuri katika raundi zilizopita, tumeona
pia uchezaji wa mgeni wetu kutoka Uganda si
mbaya sana, sasa angalisho, kila mtu aweke dau
ambalo hatoathirika katika akiba yake baada ya
kushindwa mchezo huu,” akamaliza kusema kisha
akzungusha chungu, wote wakaweka mapesa kibao,
mmoja wao, Yule tajiri wa Venezuela alikuwa
ameishiwa na kubaki na kiasi kidogo, akaweka dau
gari yake ya thamani, Marcedes Benz CLA45 AMG
4MATIC 355-hp. Ilikuwa ni gari mpya kabisa, toleo
jipya ambalo thamani yake si ya kitoto. Kamanda
Amata akatupia katika chungu kile $ 1500 kama
zilivyo, kila mtu akaguna tena, lakini hawakuguna
kwa Yule aliyeweka gari kwa sababu walijua kuwa
ana uwezo wa kununua nyingine.
Mchezo ulianza na kila mtu alikuwa makini sana
mara hii, hakuna aliyetaka kupoteza mchezo huwo
wa thamani kwa maana atakayeshinda atakuwa ni
milionea wa kutupwa kwa pesa atakazokusanya.
Lakini kamali ni kamali tu, mmoja baada ya
mwingine walianza kupanguka. Mwisho wa mchezo
wakakutana Don Andreas na Kamanda Amata.
Ilikuwa ni nafasi nzuri sana kwa Kamanda Amata
kutazamana uso kwa uso na tajiri huyo ambaye siri
ya safari yake pale Ujerumani iko ndani ya kifua
chake. Don Andreas alikuwa haelewi afanye nini,
mara ajishike nywele, mara shavu, mara ajikune
ilimradi kutaka kushinda mchezo huo wa dhahabu,
wakati Kamanda Amata alikuwa katulia kitini
akimtazama kwa makini tajiri huyo
anavyochachawa. Wakati mchezo huo ukiendelea,
kijana mmoja aliyevalia suti safi nyeupe aliingia
pale mezani na kuzunguka nyuma ya Don Andreas
akamnong’oneza kitu, Don Andreas alipata mshtuko
wa mbali kidogo ambao mpaka uwe mzoefu wa
mambo ya kiintelijensia ndio waweza kugundua.
Kamanda Amata aliisoma hali hiyo, akapata hisia ya
kitu Fulani. Mchezeshaji alimuhamasisha Andreas
kucheza. Mwisho wa mchezo, Kamanda Amata
akaibuka mshindi, makofi mengi yalitawala wakatia
akikusanya kete zote kuwa ni ushindi wake, pamoja
na funguo ya gari ile ya kisasa, aliegemea kiti chake
na kumtazama Don Andreas aliyeonekana kuchoka
ghafla kitini mwake. Wale wengine walianza
kuondoka mmoja baada ya mwingine kwa maana
mchezo ulikuwa umefikia mwisho. Kamanda Amata
aliiegemea tena meza na kumtazama Andreas.
“Sasa tucheze mimi na wewe, wawili tu,” Kamanda
alimwambia Andreas. Don Andreas alimtazama
Kamanda Amata.
“Sina dau kwa sasa la kupoteza, wewe tumia utajiri
uliopata,” Don Andreas akamwambia Amata huku
akijiandaa kuondoka, wapambe wake tayari
walikuwa wamekwishafika. Kamanda Amata
akamzuia Don Andreas kwa kumgusa kiganja cha
mkono alichokisahau mezani, akastuka na
kumtazama Kamanda,
“Dau unalo, tena la gharama sana,” kamanda
Akamwambia Don. Tabasamu la uongo likatoka
katika sura ya Andreas.
“Mostrance, weka dau Mostrance,” kamanda Amata
alimwambia Don. Neon hilo lilimfanya Don Andreas
kukunja sura ghafla na kurudi sawia kwenye kiti
chake kama awali,
“Unasemaje Mr…” kabla Andreas hajamaliza kutaja
jina, Kamanda Amata akajitambulisha rasmi, “…
Kamanda Amata,” akamalizia. Ilikuwa ni kama
tetemeko la ardhi ka Don Andreas kujua kuwa yupo
na nani mbele yake.
“Hutoliona jua la kesho kijana,” Andreas
akamwambia Kamanda Amata.
“Kama wewe ndiwe umeweka jua liangaze mchana,
sawa, ila kama si wewe nitaliona, ila wewe na Bill
sijui nani ataliona kati yenu,” Kamanda Amata
alinyanyuka kitini na kuanza kuondoka huku yule
mchezeshaji akikusanya zile kete tayari kuzibadili
kuwa pesa ili apatiwe Kamanda Amata. Kamanda
Amata alipoanza kuondoka akakutana na binti
mmoja mzuri wa sura, mavazi yake yalionesha
asilimia 80 ya mwili wake usiokuwa na nguo,
wakasimama na kutazamana nyuso zao, Yule binti
akatabasamu, tabasamu la wizi, kamanda Amata
akamshika kiunoni na kuondoka naye mpaka kaunta
ambako aliagiza kinywaji na kuanza kukimiminia
kinywani mwake huku cheers nyingi na Yule binti,
Kamanda alikuwa millionea ghafla, lakini alijua wazi
hatari inayomkabili muda huo.
“Unahitaji cash au tukuwekee katika akaunti yako?”
sauti ilitokea kaunta ikimuuliza Kamanda juu ya
pesa zake, “Weka kwenye akaunti kisha nipe namba
ya muamala wangu kwa ajili ya kuhakikisha,”
alimjibu yule mhudumu wa kaunta.
“Beibi, nimekupenda ghafla,” Yule mwanamke
alimwambia Amata. “Usijali leo ni mimi na wewe
mpaka majogoo yawike,” kamanda Amata aliongea
kwa Kijerumani cha kubabaisha, “Mmmm
aliyekwambia huku kuna majogoo ni nani?” Yule
binti alizidi maneno ya mtego, “Aaaaa jamani
majogoo huyajui,” Kamanda Amata akawuliza Yule
binti. Alipokabidhiwa kadi maalumu yenye namba
za muamala wake, akamshika mkono Yule binti na
kutoka nae pale kaunta, hatua mbili, mkono mmoja
ukazungushwa kiunoni, wakapotelea nje ya hotel
hiyo.
INAENDELEA
 
“Mmmm aliyekwambia huku kuna majogoo ni nani?”
Yule binti alizidi maneno ya mtego, “Aaaaa jamani
majogoo huyajui,” Kamanda Amata akawuliza Yule
binti. Alipokabidhiwa kadi maalumu yenye namba
za muamala wake, akamshika mkono Yule binti na
kutoka nae pale kaunta, hatua mbili, mkono mmoja
ukazungushwa kiunoni, wakapotelea nje ya hotel
hiyo.
§§§§§
BILL VAN GETGAND alishusha mtemba wake kutoka
kinywani, akapuliza moshi mwingi hewani na
kusababisha mchafuo wa mazingira kutokana na
huo moshi taka, akashusha kioo cha gari
iliyombeba mpaka chini kabisa, kisha akatupa kipisi
kilichobaki kwa kulenga katika kasha maalum la
takataka liliwekwa hapo jirani na maegesho.
Alimtazama Kamanda Amata akitoka na Yule binti
wa kizungu, wakiwa wamekumbatian viunoni,
walipolifikia lile gari, wakakumbatiana kwa
kutazamana, wakapeana mabusu ya kuinyonyana
ndimi zao. Kengele za hatari zikagonga katika
kichwa cha Amata, akatoa miwani yake na kuivaa,
alipotazama kwenye maegesho akashuhudia kioo
cha Vogue kikimalizia kupanda juu, akajua kuna
kitu.
“Uko peke yako?” Kamanda Amata akamuuliza.
“Yeah, peke yangu,” Yule binti akajibu.
“Huwa unakuja kufanya nini hapa?” swali lingine
kutoka kwa Kamanda.
“Mmmmm huwa nakuja kutafuta wanaume wazuri
kama wewe,” akajibu Yule binti. Kamanda Amata
akaminya kitufe kwenye funguo ya gari aliyopewa na
Benz moja nyekundu ikawaka taa zake kuashiria
kuwa ndiyo yenyewe, akaiendea na kufungua
milango akajitoma nyuma ya usukani, na Yule binti
akakaa pembeni.
“Unanipeleka wapi?” akauliza Yule binti.
“Beach,” kamanda akajibu huku akiondoa gari ile
katika maegesho. Nyuma yake ile Vogue nayo
ikaondoka, lakini haikuwafuata njia waliochukua
wao. Kamanda Amata aliendesha gari hiyo taratibu
sana akiizunguka mitaa ya mji huo mkongwe kabisa
huko Ujerumani, huku akiwa macho yake yakitazama
nyuma, mbele kwa umakini mkubwa sana kujua
kama kuna anyemfuata au vipi.
Kamanda Amata aliendelea kuzunguka katika mitaa
ya mji huo bila kuegesha gari popote huku akiwa
hana maongezi yoyote na Yule mwanamke katika
gari hiyo.
“Hey beibi, mbona huongei, na wala huniambii
unanipeleka wapi? Mi nataka twende kwangu,” Yule
mwanamke alimuuliza na kumwambia Amata
ambaye alikuwa ametingwa na usukani wa gari hiyo.
“Najaribisha gari yangu mpya, usijali, nikichoka
tutakwenda kwako,” Kamanda Amata alimjibu Yule
bibie huku akiendelea kuchapa mwendo, akipita
barabara hii na kutokea barabara ile. Mara nyuma
yake akasikia ving’ora vya polisi vikija upande wake,
akaangali kwenye kioo cha kuendeshea gari akaona
gari mbili za polisi zikija kwake, akaongeza mwendo
na zile gari zikawa zinakuja kwa kasi.
“Polisi,”Yule mwanmke akamwambia Kamanda.
“Usiogope, hao sio polisi, kwa jinsi
wanavyoendesha gari,” Kamanda Amata akajibu.
“AA 768 G weka gari pembeni!!” ilikuwa sauti
kutoka katika kipaza sauti ambacho polisi wale
walitumia kumsimamisha Kamanda Amata, lakini
badala ya kusimama aliendelea kutimua mbio na
gari lile, sasa alitembea mwendo wa hatari zaidi.
Kamanda Amata kwa ujumla alikuwa akijua kuwa
Andreas, Bill na vibaraka wao lazima watakuwa
wakimnyemelea katika mitaa hiyo hivyo hakutaka
kuuacha mji ule mapema wala hakutaka kurudi
hotelini mapema ili aone nini mwisho wake,
alishajua kuwa kurudi hotelini ni kujiweka kwenye
hatari zaidi.
“Unaitwa nani?” ndio kwanza Kamanda Amata
anagundua kuwa hakuwa amemjua kwa jina yuel
mwanamke.
“Naitwa Hellen,” akajibu huku akijinyoosha kwa
kujipindapinda mwili wake klitu ambacho
kilimsisimua Kamanda Amata hasa alipokuwa
akikiona kile kifua kilichopambwa na matiti mawili
mazuri yakiyotuna kwenye kigauni hicho chepesi
sana.
“Hellen, unamfahamu Don Andreas?” Kamanda
Amata akauliza.
“Ndio, namfahamu sana, kwani kuna mtu ambaye
hamfahamu tajiri huyo matata hapa mjini? Kibosile
mpenda vimwana, vipi una shida naye?” Hellen
akajibu na kurusha swali.
“Hapana siwezi kuwa na shida na mtu masikini
kama Yule,” kamanda Amata akajibu huku
akimtazama Hellen, wakati huo ile Mercedes Benz
ilikuwa inasoma 158 km/h, mwendo mkali
kwelikweli. “Mr Francisco, unajua wewe ni mgeni
sana hapa Aachen,” akaanza dodoso zake za kike.
“Hapana, huwa nakuja mara nyingi sana hapa ila
wewe hujawahi kuniona, kwa nini unauliza?”
kamanda Amata aliendeleza mazungumzo kwa
kuwa alijua nini kitafuata. “
Usimwite Andreas masikini, ana masikio zaidi ya
million hapa Aachen,” Hellen aliongea kwa mapozi.
“Oooh, sikujua huyo atakuwa shetani basi, maana
binadamu kawaida ana masikio mawili tu,” Amata
akajibu kwa utani, lakini alipomwangalia Hellen
akaona hata kutabasamu hakupo usoni mwake,
akajuwa kuwa sasa kaanza kumfika moyoni kwa
maneno yale. Hellen alimtazama Kamanda Amata
hakummaliza, akaingia za mkono wake mkobani na
kutoa kitu kama kikebe cha wino wa mhuri,
akakifungua, ndani yake mlikuwamo na sigara tano
na kiberiti cha gesi, vyote viliweza kutosha ndani ya
kikebe kile. Akachomoa sigara moja na kuiweka
mdomoni, akamtazama Kamanda Amata, kabla
hajafanya lolote Kamanda Amata aliitambua ile
sigara, haikuwa sigara bali ni mfano wa sigara
ambayo ukiiweka mdomoni na kusukuma pumzi
kwa nje, sio kwa ndani kama kawaida ya kuvuta
sigara, hutoa vumbi jepesi sana ambalo litakupa
usingizi ndani ya sekunde kumi tu. Kamanda Amata
alimnyang’anya ile sigara na kuitupa pembeni,
Hellen alipiga kelele, na kitendo hicho kilimfanya
Kamanda Amata kukanyaga breki za ghafla akiwa
katika mwendo mkali. Hellen alikuwa hajafunga
mkanda hivyo alichomoka kwenye kioo cha mbele
na kutoka mpaka nje akadondokea barabarani.
“Bull shit!” aling’aka Amata, akakanyaga klachi ya
gari hiyo na kuweka gia ya kurudi nyuma na gari ile
ikatii amei pale alipoachia klachi na kutimba pedeli
ya kusukuma mafuta, kona moja kali ikamgeuza
kutazama alipotoka na kutupia namba moja, kisha
mbili, mara tatu, akawa amemuacha Hellen pale
barabarani akiwa hoi na yeye kurudi kwa kasi
alikotoka.
‘Mwanamke mpumbavu sana huyu,’ alijisemea
moyoni huku akiongeza kasi ya gari lile ambalo
injini yake bado ilikuwa ikidai gia ya sita wakati
tayari zilikuwa zimekwisha zile zilizopo. Akiwa
katikati ya mawazo yale na kumsonya Yule
mwanamke huku akimtukana kimoyomoyo, aliona
taa kali zikimmulika usoni akashindwa kupambanua
njia halisi iko wapi na hicho pele ni kitu gani.
Puuuuuuuu!!!!! Kishindo kikubwa kikasikika, gari
aliyokuwa akiendesha Kamanda Amata ilikutana uso
kwa uso na katapila la kutengeneza barabara,
ilijipiga kwenye jembe la chuma cha pua, ikapinda
boneti yote kuelekea kwenye kioo cha mbele, kisha
lile katapila likainamisha jembe lake na kuiangusha
ile gari na kuibonda vibaya, ikaibeba tena na
kukokota mpaka kwenye jalala la kutupa magari
mabovu. Yule operetta wa lile katapila aina CAT
aliinua simu yake ya upepo na kuongea na watu
walio upande mwingine,
“Kazi tayari boss (…) hawezi kutoka mpaka Yesu
arudi amtoe kimiujiza,” kisha akakata ile simu na
kuegesha katapila lake pembeni. Range Rover
Vogue, lilifika katika jalala lile ambalo halikuwa
mbali sana na pale ilipotokea ajali ile ya
kutengenezwa, ikasimama na watu wanne
wakashuka, Bill akiwa mmoja wao mkononi akiwa
na ile fimbo yake ya kutembelea.
“Mali hiyo hapo boss,” Yule operetta akamwambia
Bill huku akimuonesha kwa mkono ile Marcedes
ilivyopondwa na kuwa chuma chakavu kwa ghafla
namna hiyo.
“Vizuri sana, alikuwa ananiumiza kichwa sana huyu
jamaa, akapumzike kwa amani, jivu kwa jivu. Vumbi
kwa vumbi,” Bill alipomaliza kusema hayo, akampa
Yule jamaa kitita cha noti kama shukrani kwa kazi
hiyo ndogo aliyoifanya. Kisha wao wakarudi garini
na kuondoka usiku ule, akaigeuza taratibu Yule drva
na kuchukua uelekeo ule waliojia, Bill akainua fimbo
yake na kuigemeza dirishani, ncha ya kutembelea
ikwa imetazama kule aliko Yule operetta,
akakifyatua kijichuma kidogo kilichoupande wa
mshikio na kukivuta kwake, lo, Yule jamaa alikuwa
akishangaa kuiangalia ile Vogue huku akiwa haamini
kupata kile kitita cha noti, alijikuta akipenywa na
kitu kama msumari kifuani mwake, mara
akadondoka na kuanza kuona macho yake yanakuwa
mazito kama yaliyojawa na ukungu, tayari kulikuwa
ni giza muda huo lakini giza linguine zito lilimfunika,
roho yake ikaacha mwili.
Bill alikuwa amemuua operetta Yule kwa risasi
kutoka katika hiyo anayoifanya ni fimbo ya
kutembelea. Kijana mmoja kati ya wale waliokuwa
garini pamoja na Bill akashuka na kwenda mpaka
pale kwa Yule operetta marehemu, akachukua ile
pesa na kurudi garini, akamkabidhi Bill. “Kazi
ngumu lakini imekwisha bila jasho, alale pema
peponi Kamanda,” Bill alizungumza na ile gari
ikaondoka eneo lile.
§§§§§
DON ANDREAS hakuamini anachoambiwa na Bill
kuwa Kamanda Amata hayupo duniani. Akiwa katika
sebule yake kubwa pamoja na mgeni wake kutoka
Vatican, Fr Gustav Maker wakijivinjari kwa vinywaji
vikali, wote waliifurahia taarifa hiyo kutoka kwa Bill.
Dakika chache baadae Bill aliungana nao hapo
sebuleni na tafrija isiyo rasmi ikaendelea.
“Kazi haikuwa rahisi mjomba,” Andreas alikuwa
akimsimulia Fr Gustav juu ya mkakati mzima
mpaka kuipata ile Monstrance.
“Pole sana mjomba lakini maadam umeipata basi
utajiri wako utakuwa wa milele,” Gustav alimwambia
Andreas, akinua glass yake iliyojaa kinywaji na
kujimiminia kinywani mwake, kisha akamwangalia
Andreas na Bill, “Iko wapi hiyo Monstrance?”
akauliza.
“Ipo katika chumba cha siri,” Andreas akajibu,
“Unataka kuhakikisha kuwa ipo au la?” akamtupia
na swali.
“Yeah, hilo ni la msingi, nipeleke nikaione,”
akaomba. Andreas aliinuka pamoja na Bill kisha
wakafuatwa na Fr Gustav. Wote watatu wakaingia
chumba cha siri ambacho ni mtu mmoja tu mwenye
dhamana ya kukifungua, Andreas mwenyewe kwa
kuwa mlango wake unahitaji, namba maalumu ya
kubonyeza, alama ya kidole gumba na alama za
macho, vyote hivyo ni vya Andreas, walipofika pale
alifanya hayo yote, kisha wqakafunga kwa ndani na
kuingia huko ilikohifadhiwa hiyo monstrance.
Fr Gustav, akaitazama ile monstrance kwa makini
sana ikiwa imelazwa juu ya kijisanduku kidogo
ambamo ilitosha kabisa, akainyanyua na
kuigeuzageuza, ilikuwa iking’aa sana kutokana na
taa iliyokuwa ikiwaka ndani ya chumba kile, ilikuwa
ni dhahabu safi ambayo haijachakachuliwa bado.
“Niliambiwa kuwa monstrance hii ina siri kubwa
sana ndani yake, lakini mpaka sasa sijaijua,”
Andreas alimwambia Fr Gustav.
“Ni kweli, na nimekuja hapa kwa sababu hiyo tu, hii
Monstrance lazima irudi Vatican,” Kwa kauli hiyo,
Andreas na Bill walibaki wakitazamana kabla ya
wote kumgeukia Fr Gustav.
“We una kichaa ee!” Andreas alimwambia Gustav.
“Hata kama nina kichaa, lakini monstrance hii
lazima irudi Vatican, siri iliyomo nitakwambia lakini
hiki chombo lazima kirudi”
Gustav akaishika katikati ile monstrance mkono
mmoja upande wa kitako na mkono mwingine
upande wa juu akainyoga katikati kama anaivunja au
anaifungua, ikafunguka, kisha akaweka kitako chini,
akabaki na kipande cha juu. Don Andreas alikuwa
bado akishangaa hakujua kuna nini kinafanyika.
“Na hii ndiyo siri iliyomo katika chombo hiki,”
Gustav akawaambia huku akiinamisha na kikaratasi
kirefu kikatoka ndani ya kile kibomba kidogo
ambacho hushika kitako na sehemu ya juu ya
chombo kile, Gustav akaiweka chini ile monstrance
na kuchukua ile karatasi, akaifunjua kunjua kwa
uangalifu, ilikuwa ni ramani kubwa sana
inayoonesha njia za kupita mpaka kwenye hazina
kubwa ya madini ya dhahabu iliyojificha huko
kwenye milima ya Peramiho, kusini mwa Tanzania,
mawe makubwa amabayo chini yake kulikuwa na
kama mapango yenye madini ya thamani.
Andreas ilikuwa nusu azimie kwa kkile anachokiona,
alikuwa akisoma maandishi yale ya kijerumani huku
akiwa na tabasamu pana kuliko sura yake.
Alipomaliza kuitazama ile ramani na kuyasoma kwa
ufasaha yale maandishi yaliyoandikwa karne kwa
karne lakini hayakuwa yamefutika, bado yalionekana
kwa upya wake. Andreas alitingisha kichwa chake
kuashiria kweli amekubali maneno ya babu yake.
“Gustav, tumekuwa matajiri wa maisha,” Andreas
alimwambia Gustav. “Ni kweli, lakini unajua hazina
hiyo hiko wapi?” akauliza.
“Tanganyika kwa maelezo haya, ambayo ni Tanzania
ya sasa,” Andreas alijibu.
“Na utaendaje huko kufanya hiyo kazi?” lilikuwa
swali la Gustav.
“Aaah Gustav, hiyo sio shida, ni kwenda pale na
kununua eneo lote lile, pesa ninayo, watanikubalia tu
wale masikini kisha tunachimba. Siri ni uwekezaji tu,
tukishawapa kishika mkono basi viongozi wataachia
njia,” Andreas alisema kwa kujiamini.
“Haya nakutakia kila la kheri, lakini mmefanya kosa
kubwa moja ambalo mimi sikulifurahia,” Gustav
akaikatisha furaha ya Andreas.
“Kosa gani?” akauliza.
“Kosa ni watu uliowatumia, kumuua Fr Gichuru ni
kosa kubwa sana ambalo usipoangalia
litakugharimu,” Gustav akamwambia Andreas.
“Kama amekufa amekufa tu,” Bill akashindilia
msumari wa mwisho katika hilo. Andreas akaiweka
ile ramani juu ya kijimeza kidogo kwa minajiri ya
kuja kuisoma vyema baadae, kisha wote watatu
wakatoka nje ya chumba hicho na kikafungwa tena
kama klilivyokuwa mwanzoni.
§§§§§
10
KAMANDA AMATA alijikunguta vumbi, alijitazama
hapa na pale alikuwa na michubuko michache lakini
alisikia maumivu makali sana katika mkono wake
wa kulia, akajaribu kuunyoosha na kuufanyisha
mazoezi. Kidogo ukakaa sawa. Akajiangalia zile
silaha zake nyeti ambazo huzificha ndani ya nguo
zake, bastola yake ilikuwepo, camera na vitu vingine
vyote vilikuwa vimetimia, kwa hatua za taratibu
alijivuta kurudi barabarani.
Ulikuwa ni usilku mnene sana ambapo hakukuwa na
magari mengi katika barabara hii ya kutokea nje ya
mji wa Aachen, zaidi yalipita malori. Alitembea
hatua za taratibu akipandisha kilima kidogo
kilichokuwa hapo, alipofika juu, alikuta kuna Motel,
taa zilikuwa bado zikiwaka na magari machache
yalikuwa yamepaki nje yake. Akaiendea motel hiyo
na kuingia ndani, kulikuwa na watu wachache
ambao walionekana washari washari hivi, wakiwa
wamevaa kiuni, wengine wakilewa [pombe na
wengine wakiwa wanacheza kamali.
“Nahitaji msaada,” alimwambia Yule mwanadada wa
kaunta.
“Tukusaidie nini?” Yule dada alijibu kwa Kijerumani
safi.
“Mna box la huduma ya kwanza?” akauliza Amata.
“Ndiyo; bila shaka,” Yule mhudumu wa kaunta
akajibu na kuingia nyuma ya kaunta akatoka na
kikasha chenye alama ya msalaba mwekundu
akampatia, Kamanda Amata akafungua ndani yake,
akatazama akakuta kuna dawa aina ya Iodine
akaichuku, bomba moja la sindano na kijichupa
kidogo cha dawa aina ya Diclofenac, akavua shati,
akaliweka pembeni, katika mkono wake palikuwa na
jeraha kubwa kiasi kutokana na mburuzo alioupata
alipokuwa akiruka kutoka ndani ya ile gari kabla
haijagongana na katapila, akajipaka ile iodine huku
akikunja sura kutokana na maumivu ya dawa hiyo,
akaijiwekea na pamba kisha akamuomba Yule
mhudumu wa kaunta amfunge bandeji naye
akatekeleza hilo. Kamanda Amata alipoona kuwa
hapo amekamilisha akajidunga sindano ya
Diclofenac kutuliza maumivu. Akaismama na kutoa
shukrani kwa Yule dada, akavaa shati lake jeupe
ambalo sasa lilikuwa halitamaniki kwa vumbi.
Alipokuwa akitoka, mlangoni alikuta kuna majaketi
yametundikwa, akajichagulia moja la rangi nyeusi
akajitupia juu yake na kutoka nje, hakuwa na usafiri.
Akatazama magari yaliyoegeshwa hapo, akaona
moja inayomfaa. Ford Cortiner ya rangi ya buluu
ilikuwa imeegeshwa pembeni kidogo mwa jengo
hilo na mwenyewe alikuwa ameliacha likiunguruma
yeye akiwa ndani kunywa kahawa, bila shaka
lilikuwa linatoka safari ya mbali, Kamanda Amata
aliingia na kukanyaga mafuta akarudi barabarani,
muziki mzuri wa You are not alone uliopigwa na
Michael Jackson alikuwa ukitumbuiza. Saa katika
dashboard ya gari hiyo ilionesha ni saa nane za
usiku ikielekea saa tisa.
Mwendo haukuwa wa kawaida barabarani, Kamanda
Amata akili yote ilikuwa imehamia kwa Bill, sasa
alikuwa anataka kumaliza biashara yake na Bill.
Alikata mitaa michache na kushika barabara
inayopita mbele ya kanisa kuu, akalitazama kwa
mbali na kupitiliza, akalikaribia hekalu la Don
Andreas, kwa kujifanya kuwa hana kazi nalo
alipitiliza na kwenda kusimama mbali kidogo,
akaegesha gari karibu na kituo cha mafuta,
akaliacha linanguruma kama alivyolikuta, alipokuwa
anatoka akawasha taa ya ndani kuangalia hiki na
kile, hakuamini macho yake alipoiona AK 47 double
barrel, akaitoa na kuvunja katikati kama kawaida,
haikuwa na risasi, akapekua hapa na pale akakutana
na kikebe chenye risasi kama kumi hivi
akakichukua, akajaza risasi zote katika mashine hiyo
na kujivuta kwa mguu kulielekea jumba hilo lenye
ulinzi mkali. Haikumchukua muda kuifikia himaya
hiyo yenye utulivu wa pekee, kwa nje ya jumba hilo
alifanikiwa kuona gari mbili zimeegeshwa, moja
ikiwa ni ile Vogue, ‘Hisia zangu zimesema kweli,
Bill yupo hapa na atafia hapa, leo sina huruma na
kiumbe cha mtu,’ kamanda Amata alijisemea
moyoni, hasira ikiwa inamtawala kila baada ya
nukta. Alitazama ulinzi ulivyojipanga akaona kuwa
juu kuna walinzi lakini hakujua atafanyaje
wasimuone. Akachomoa bastola yake yenye
kiwambo cha sauti, akamlenga mmoja na kumpata
sawia kichwani, bajati nzuri aliangukia juu kulekule.
Akaona sawa, mmoja tayari, alipokaribia ule wigo
wa wavu maalum, akasita, kitu kikamwambia geula
kulia, alipogeuka akakutana na taa kubwa
inayoongozwa na sense, ukiingia umbali Fulani
kutoka ule wigo, taa ile inakumulika kwa mwanga
mkali na vingola vinaasha walinzi, hakuwa na mda
wa kuhangaika na taa ya mtu, akaifumua kwa risasi
moja, kisha akarudi nyuma na kutimua mbio
kuuelekea ule wigo akapiga samasoti maridadi
kabisa akapita juu ya wigo ule bila hata ya kuugusa,
alipotua tu tayari AK 47 ilikohoa na kumteremsha
mlinzi mwingine mpaka chini, alipogeuka kushoto
kuna mwingine, kwa kutumia bastola yake
akamfyatulia moja makini sana iliyochana bega
upande wa moyo, Kamanda Amata akahama pale
alipokuwa kwa maana alijua ataonekana, akapenya
katika ya maua na kuifikia maiti ya mlinzi mmoja
akaivua shot gun semi automatic, akaibeba
mgongoni. Kamanda Amata akaendelea kusafisha
nje kote, alihakikisha si mbwa si binadamu
habakishi kitu.
Milio ya risasi ilifikisha taarifa ndani kuwa huko nje
hakufai, Bill akanyanyuka na kuwaambia vijana wake
wawe tayari.
“Bila Shaka, tumevamiwa,” akmwambia Don
Andreas ambaye alionekana wazi presha ikipanda.
“Nani atuvamie wakati Kamanda amekwishakufa?”
Bill akatoka nje ya nyumba hiyo, hakuna mtu, akiwa
amefyumu kwa hasira, akiwagombeza vijana wake
kwa uzembe wa kushindwa kuimarisha ulinzi.
Akarudi ndani, hakumkuta Don Andreas, kaenda
wapi, bahati nzuri vyumba vyake vya siri Bill
anavijua, akaingia cha kwanza, cha pili akamkuta,
“Hapa si pakukaa Andreas, tuondoke,” Bill
alimwambia Andreas.
“Ramani ile pamoja na monstrance lazima tuondoke
nazo,” Andreas alimsisitizia Bill, “Don, hatuna muda
huyu jamaa ni kichaa,” Bill aliendelea
kumnong’oneza. Wakatoka pamoja pale mafichoni
na kuukimbilia mlango mkubwa lakini Andreas
akarudi tena akiuendea ule mlango ambao una zile
hazina zake zote. Bill alimtazama Andreas akiwa
anahangaika kuufungua ule mlango. Bill akapotelea
upande mwingine wa jumba hilo, sasa akiwa na
bastola yake mkononi, akimuwinda huyo aliyevamia.
Kamanda Amata alikuwa akinyata kuuelekea mlango
wa siri uliokuwa ukitokea upande wanyuma,
aliutazama mlango ule ulikuwa wa chuma imara, sio
shida, akaizungusha saa yake nayo ikaanza
kuzunguka kwa kasi na kutoa mionzi iliyoweza
kukata eneo la kitasa la mlango ule, aliporidhika
akaizikma ile saa, akaujaribu mlango ukafunguka
bila kipingamizi, akajitoma ndani. Akiwa katika
kutembea taratibu, akahisi kitu kama kitu chenye
ncha kali kikipenya eneo Fulani la shingoakaanguka
chini na kupoteza nguvu, alijaribu kupambana na
hali hiyo ikawa ngumua sana, akakumbuka vidonge
alivyopewa na Madam S, akapenyeza mkono wake
kwenye mfuko wa ndani wa suruali akachukua
kimoja na kutumia nguvu yake ya mwisho
kukimeza, mara akalegea na kujilaza.
“Ha ha ha ha ha ha ndege mjanja hunasa katika
tundu bovu,” Kamanda Amata alisikia sauti hiyo kwa
mbali sana, akafumba macho. Mara akasikia kitu
kama kiatu kikimkanyaga kwa nguvu kichwani
mwake. Akaamka l;akinin hakuonesha kukurukakara
yoyote, bado alikuwa palepale chini,
“Utafia ughaibuni, Mbwa mweusi wewe, wewe
unaweza nkujifanya polisi wa dunia wewe? Wenzako
FBI wamefeli, we una nguvu bgani na hiko kishirika
chenu cha upelelezi kuvuka mipaka kuja huku, sasa
leo ndio mwisho wako, nitakuua huku nakurekodi
kwenye mkanda wa video niwatumie wenziwako
huko kwenu Afrika wakaushuhudie mwisho wako
ulivyokuwa wa taabu na mateso, mwenzako
anaejifanya kasisi kumbe ni jasusi tayari ninae na
chamoto ameshakiona japokuwa hajafa, nitaua
mmoja baada ya mwingine,” Bill aliwaamuru vijana
wake wamburuze Amata kwenda shimoni kwenye
mashine ya kifo.
 
nitakuua huku nakurekodi kwenye mkanda wa video
niwatumie wenziwako huko kwenu Afrika
wakaushuhudie mwisho wako ulivyokuwa wa taabu
na mateso, mwenzako anaejifanya kasisi kumbe ni
jasusi tayari ninae na chamoto ameshakiona
japokuwa hajafa, nitaua mmoja baada ya mwingine,”
Bill aliwaamuru vijana wake wamburuze Amata
kwenda shimoni kwenye mashine ya kifo.
SEHEMU YA MWISHO
§§§§§
FR FRANK Edson, alipojuwa kuwa Kamanda Amata
ameingia katika mtanange hivyo anaweza kumuwahi
kumpoteza Bill ilhali yeye anatakiwa ampeleke
akiwa hai, aliamua kuyavulia maji nguo na kujikita
katikati ya hatari hiyo, alilivamia jumba la Don
mapema sana hata kabla Bill hajarudi akajificha
katika moja ya stoo zilizokuwa ndani ya jumba hilo.
Kwa bahati mbaya au nzuri alipoikuwa katika
harakati za kutafuata pazuri pa kujificha kamera
ndogo sana ya usalama ilimuona na kupeleka taarifa
panapohusika ndipo shughuli ilipoibuka humo ndani,
kipigo alichokipata kwa mkono wa Iron Man The
Killing Machine alibaki hoi hajiwezi na kutupwa
huko shimoni ambako hakuna hewa hakuna
chochote ni mateso mpaka unakufa.
Fr Frank alishindwa kujitetea kwa jitu hilo la miraba
mine baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi.
Alikuwa nusu mfu katika chumba kile.
Kamanda Amata alijilegeza huku akiburuzwa mpaka
katika lango la chumba hicho ambamo
kinachofanyika ni kukutumbukiza, utakaa umo ufe
kisha inamwagwa dawa maalum ambayo
inakusagasaga na kuwa katika vipande
vidogovidogo kisha wanaflash kama chooni na taka
hizo zote hupelekwa baharini kupitia mfumo wa
maji taka. Walipofika mlangoni, tayari kumtupa mle
shimoni, Kamanda Amata alijitikisa kidogo, wale
jamaa wakashtuka, mmoja akainama kumwangalia
kama ni mzima au la, Amata akamtemea mate, kwa
uzembe wa Yule mlinzi akauchia mkono wa
Kamanda ili ajifute mate usoni, kosa. Konde moja
zito lilitua tumboni kwa jamaa Yule akatema damu,
huyu mwingine hajakaa sawa akachezea kipepsi
kimoja kilichjomfanya ajisjike tumbo, sasa Kamanda
Amata alikuwa huru na nguvu zake zilezile,
alijurusha kiufundi na kuwapiga mateke ya
migongoni kisha wale wawili wakaingia shimoni.
Kamanda akasonya na kurudi kwa njia ileile.
Akapenya hapa na pale na kutokea eneo lenye
veranda kubwa, akawa kizungukazunguka ajui nini
cha kufanya, akiwa katika hali hiyo alihisi mkono
wenye nguvu umekamata bega alipogeuka
akakutana uso na jitu la miraba minne, mara
akasikia vicheko kutoka sehemu asiyoijua. Lile jitu
likamnyanyua na kumbwaga chini, Amata
alijitonesha tena katika majeraha yake, akabaki
kugugumia maumivu tu. Aliinua kichwa na
kumwangalia huyo aliyemfanyia kitendo hicho,
lilikuwa ni jitu lenye pande la mwili, lililojaa misuli
mikubwa, kamanda Amata akaona wazi kuwa Frank
Edson hakuwa na budi kuwa katika hali ile kama
alipambana na dubwana hili, akajikokota
kunyanyuka ajaribu bahati yake, konde la pili
lilimrusha nyuma na kujibamiza vibaya ukutani,
Kamanda Amata akatema damu, alipokuwa akijaribu
kuinuka akapigwa teke la mbavu, nguvu ya teke lile
ilimsukuma mpaka ukuta wa pili, Kamanda alijikuta
akiwa na hali mbaya, alijitahidi kuinuka lakini
ilikuwa ngumu, alibaki kutambaa. Mara sauti
ikasikika kwenye chombo maalumu kilichofungwa
darini, ilianza na kicheko;
“Ha ha ha ha ha ha, Kamanda Amata, wewe unajua
sana kufuatilia nyendo za watu sio za miungu kama
sisi, sasa leo pambana huyo Israel mtoia roho,
kama wewe unaweza kukishinda kifo basi leo
tutaona ujanja wako uko wapi, ha ha ha ha ha ha
hapo ulipo ndio kuzimu ulipokuwa ukikusikia
kwenye vitabu vya dini zenu, pambana na mashine
ya kifo hiyo, ukiishinda nitakupa utajiri wangu wote,”
Maneno yale yaliyokuwa yakisemwa na mtu
asiyemuona yalimtia hasira sana Amata, “Utajiri
wako baki nao mwenyewe, kwa kuwa sikutaka
kukutoa roho sasa umeniladhimisha kufanya hivyo,”
ilikuwa sauti ya uchovu kutoka kwa Kamanda
Amata.
Vicheko vikaanza tena kwenye kile chombo, sasa
vikiwa kwa fujo zaidi, Kamanda Amata alihisi kitu
kama upepo kimepita sikioni mwake pindi
alipokuwa akigeuka, kumbe guu la lile jitu lilipita
akiwa na lengo la kumpiga teke la kichwani pale
chini alipojiinamia, Kamanda Amata kwa kasi
akaona amepata nafasi nzuri ya kufanya mambo,
alipiga ngumi moja iliyotua kwenye korodani za jitu
hilo, likaguna kwa maumivu. Akajiinua kwa ustadi
na kujisahaulisha maumivu yake, akawa wima,
alikusanya nguvu zake zote na kuruka hewani
alikoichanua miguu yake na mateke yote mawili
yakatua shavuni mwa lile jitu, lakini halikutikisika
hata kidogo. Kabla mguu wa Amata haujatua chini,
ulidakwa, Kamanda akautumia kama nguzo na
kujivuta kuelekea usoni mwa lile jitu, akalipiga
kichwa cha jichoni kwa maana alijua kwa vyovyote
atalipoteza maboya, kama aliota.
Kile kichwa kilipotua jichoni lile dubwana lika
muachia Amata na kujishika jicho, Kamanda Amata
akatua sakafuni kwa miguu miwili baada ya kuruka
samasoti safi sana, alitahamaki na kuliona lile jitu
likimjia kasi kama mbogo, akalikwepa nalo
likajibamiza ukutani, Kamanda Amata akatazama
huku na kule akaona taa iliyosimamishwa kwenye
nguzo ya chuma, akaiwahi na kuichukua akaivunja
taa yake nayo ikabaki bila taa, akaiinua na kumpiga
nayo mgongoni, lilipoguka kamanda Amata
akatumia ule mnara wa taa akamchoma tumboni,
lakini hakufanikiwa hata kumtoboa kutokana na
ulaini wa chuma kile lakini alimpiga shoti moja
mbaya ya umeme kutokana na kwamba alikuwa
hajaichomoa kwenye soketi pale ukutani, Amata
akatabasamu kwa hilo.
Lile jitu, lilipigwa shoti iliyolisukuma na likajibwaga
zimazima pale chini. Vicheko katika kile chombo
vikasimama ghafla. Kamanda Amata aligundua
kuwa jinsi ya kulishinda lile jitu sio nguvu bali akili,
alipi mguu chini na mara kitu chenye ncha kali
kikachomoka kwenye sehemu ya mbele ya solo ya
kiatu chake, na mguu mwingine vivyo hivyo,
Kamanda Amata sasa akaanza kutumia miguu
kuilishmbulia lile jitu, mateke ya usoni, mbavuni
yalilifanya jitu lile lipoteze nguvu maana kila
alipopigwa kwa teke aliachiwa jeraha kubwa
kutokana na vile vyuma kenye viatu vya Amata.
Zilikuwa dakika tatu za shughuli kubwa ya
kulikalisha chini lile dubwana. Kamanda akasimama
tayari kwa pambano akiliangalia lile jitu likigalagala
sakafuni huku damu zikitapaka kila mahali.
Upande wa pili, Bill na Andreas walikuwa kimya
wakitazama pambano hilo kupitia luninga ndogo
ndani ya chumba nyeti cha Andreas, hawakuamini
kile wanachokiona, kile kinachofanywa na Kamanda
Amata, jinsi anavyotumia akili kuliadhibu jabali lile,
mashine ya kifo kama wanavyoiita.
Tangu Andreas amnunue binadamu huyo wa ajabu
huko Honduras na kumsafirisha kwa siri mpaka
Ujerumani na kumuhifadhi katika nyumba yake,
alishamtumia kwa kuua watu wengi sana
wakiwezmo maafisa wa polisi, wanajeshi na wote
wanaofuatilia nyendo zake kwa ukaribu, hakuna
aliyewahi kufurukuta, wengi walikata roho kwa pigo
moja tu, kisha miili yao aliitupi ‘kuzinu’ katika
chumba alichokiandaa kwa kazi hiyo,. Akishakutupa
humo hufungulia hewa yenye chemical kali amabayo
hukukausha na kukumeng’enya kuanzia nyama yako
mpaka mifupa vyote vinakuwa unga, kisha maji
mengi huingia katika chumba hicho na kuondoka na
mmeng’enyo huo kupitia mabomba yha maji taka,
watu wako watakutafuta miaka nenda rudi na
hawatakuona, umefutwa katika orodha ya binadamu
duniani.
Leo ilikuwa tofauti, alimshuhudia Kamanda Amata
akitoa dozi mbaya kwa jitu lake hilo analolitegemea
kwa kazi hiyo. Kijasho kilipita kutoka kwapani na
kufika mpaka kwenye kiuno kabla hakijaishia katika
nguo alizovaa.
Kamanda Amata alipohakikisha dude hilo
limezimika alitzama huku na kule ili kuona cha
kufanya, sasa akili yake ilirudi kwa Bill na
mwenzake Andreas, akiwa katika kutazamatazama
mara akasiki kama nyayo za binadamu zikimfuata
kwa nyuma, akatazama kwenye kioo kikubwa kilicho
mbele yake na kuliona lile dude limesimama
likielekea kwake kwa nguvu zote, Kamanda Amata
hakuwa na silaha yoyote ya maana, akajua sasa
kuwa amekwisha, kabla hajaona la kufanya, lile jitu
likamfikia, likiwa na hasira mbaya, lilimpiga
kikumbo Amata akapitiliza mpaka kwenye kioo cha
mbele yake, alijibamiza na kile kioo kikamwagika
pakabaki wazi, Kamanda Amata akadondokea
upande wa ndani wa kile chumba kilichotenganis
hwa na kile kioo. Ilikuwa ni ofisi ndogoi lakini
iliyojaa kila aina ya nakshi na samani za gharama,
Kamanda Amata akanyanyuka na kuchukua chungu
kilichokuwa na ua ndani yake na kukirusha sawia
kichwani mwa jitu lile, likapepesuka kidogo, kabala
halijatuliya, Amata akajirusha doule kick na kutu
kifuani mwa lile jitu, kutyokana na kupoteza nguvu
liliyumba na kujibamiza ukutani, ule mtikisiko wa
ukuta ulifanya pambo la juu ambalo lilikuwa ni
bichwa la Nyati lililotengenezwa kwa chuma.
Lilianguka na kumpiga kichwani, kisha lile bichwa la
nyati liakadondoka sakafuni. Lile jitu likajitahidi
kusimama lakini ilikuwa ngumu kutokana na
kugongwa vibaya na lile bichwa la nyati bandia,
ilikuwa ni nafasi ya Amata ya kumaliza mopja kwa
moja akaanguka juu ya lile sanamu la kichwa cha
Nyati, akachomwa na pembe za nyati
zilizojinyomnga vizuri zikitanguliwa na ncha kali,
likatoa kelele za uchungu huku macho yakiwa
yamemtoka pima, likakata roho. Kamanda Amata
akakung’uta mikono yake kwa kuashiria kazi
imeisha, hakuamini kiama kalimaliza hayawani hilo.
§§§§§
Bill aliinuka na bastola mkononi, akiuelekea mlango
ili atoke nje, mkono mmoja akiwa na ile fimbo yake
ya kutembelea.
“Bill, hapa pameshakuwa pabaya, mi nafunga
vyangu najificha dhidi ya huyo mtu wako,” Andreas
alimwambia Bill, wote wawili walikuwa katika hali ya
kuchanganyikiwa, wakivujwa na jasho jingi. Andreas
alichukua begi tupu, akainyanyua ile monstrance na
kuiti begini kisha ile ramani, akaenda ukutani na
kushusha picha moja, nyuma yake nkulikuwa na
vibonyezo au vitufe kumi na mbili vikiwa na nmba
pamoja na alama chache, akaanza kuvibonyeza ili
mlango wa siri ulio kwenye sakafu ya chumba hicho
ufunguke, nukawa unagoma kufunguka, alipojaribu
mara ya pili nay a tatu mlango ule ukakubali,
taratibu ukawa unapanda juu ili kuwezesha mtu
kuingia. Bill aliona taanyekundu ikiwaka juu ya dari
la chumba hicho, ikiashiri kuna hatari, mara
alishuhudia ule mlango mnene wenye ulinzi mkali
ambao huwezi kuingi bila kuthibitisha vitu vitatu,
namba ya siri, alama za vidole na alama za macho,
na hivyo vyote vilikuwa ni Andreas peke yake
aliyeunganishwa.
Mlango ule ulionekana kwa ndani ukikatwa duara
kutoka nje, Bill akajua sasa hapa Kamanada
anaingia, akaiweka sawa bastola yake, hakuwa
tayari kufa wakati anayemlinda anatoroka,
akainyosha bastola kwa Andreas, Andreas akasikia
mlio wa bastola hiyo ikiwekwa sawa kulipua,
“Bill vipi tena?” Andreas akamuuliza Bill. Sikia
bwege wewe, yaani huna shukrani, kazi yote
niliyokufanyia, sasa hivi unaona mambo
yameharibika unakusanya vyako unataka kutoroka
na kuniacha mimi hata kunipa chochote sio, sitaki
maelezo, nakumaliza mwenyewe,” Bill alimwambia
Andreas kwa ukali.
“Sikia Bill, mi naokoa hii mali ya thamani, wewe
ukishamuua huyo Kamanda Amata tuonane nitakupa
donge nono,” Andreas alijitetea. “Siki, mi si motto,
Kamanda Amata keshakufa mara mbili na kafufuka
sasa unafikiri hapa atakufa tena?” Bill alimuuliza
Andreas, Mara lile pande la chuma linalokatwa kwa
saa ya Kamanda Amata, lilikuwa tayari kutoka
mahala pake na kuruhusu mtu wa nje kuingia ndani,
Bill alipiga risasi moja na kufumua kifua cha
Andreas, Andreas akaanguka chini na kutoa yowe la
maumivu, Bill akanyanyua tena mkono wake
ulioshika ile bastola na kulenga lile tundu ili ampate
Kamanda Amata, alipofyataua, viligongana vyuma
tupu, hakuna risasi, akaitupa chini bastola na
kunyanyua lile begi alilochukua Andreas na kuingia
kwenye ule mlango na kuzama ardhini huku mlango
ule ukijifunga nyuma yake.
§§§§§
Kama alitegemea kupona basi ilikuwa kwa asilimia
ndogo sana, Frank Edson, aliona kile alichofanya
Kamanda Amata pale mlangoni alipokuwa ameletwa
na wale watu ili kutupwa ndani ya shimo hilo
kusubiri kifo chake. Aliona kitu kidogo ambacho
Kamanda Amata alikiangusha kwa makusudi wakati
alipowaadhibu vikali wale jamaa wawili na
kuwatumbukiza mle shimoni.
Ilikuwa ni kitu kama kidonge kidogo, kwa tabu sana
Fr Frank Edson alijivuta kwa kutambaa mpaka
akakipata kile kidonge alipokitazama alikijua vyema,
kidonge kinachotumika kurudisha nguvu kwa haraka
kwa mtu aliyekuwa na uchovu mwingi wa kupigwa
au wa shuruba yoyote, pia kinaondoa maumivu kwa
muda mrefu. Fr Frank Edson alimuona Amata kama
Malaika wake, alikiokota na kukitia mdomoni,
akakimung’unya, muda kumi na tano tu alipata
nguvu taratibu mpaka akawa sawa na maumivu
yake yakapotea, akajinyanyua kutoka pale alipo,
akasimama wima, akatazama wale jamaa waliolala
pale, waliotupwa na kwa kipigo kikali na Kamanda
Amata. Akawapekua katika nguo zao na kupata
bastola moja iliyobakiwa na risasi mbili tu,
‘Sio mbaya’ akajisemea. Sasa kazi ilikuwa atatokaje
kwenye chumba kile kisicho hata na dirisha,
aliuangalia mlango ulikuwa juu umbali wa mita kumi
na ukuta wote ulikuwa umewekwa kitu kama niru
ambayo kamwe huwezi kuzikwea kwa jinsi
zinavyoteleza, ulikuwa mtihani mgumu kwake,
akakizunguka kile chumba akigusa hapa na pale,
baada ya kuchunguza sana ndipo alipogundua ile
sehemu ya kuingizi maji ndfani ya chumba kile,
haikuwa na bomba bali ni uwazi mwembamba wa
futi mbili kwa upana na uwazi wake ulikuwa ni kama
milimita tano, palitengenezwa hivyo ili maji yakitoka
yatoke kwa mbinyo na kasi kubwa kutokana na
msukumo wa pampu. Akapaangalia na kuona kama
anaweza kupita katika upenyo huo, lilikuwa ni wazo
finyu sana hata kama angekuwa motto mdogo,
sehemu ambayo asingeweza kupenya hata mjusi,
lakini yeye alidhamiria kupenya hapo, akiwa kama
aliyechanganyikiwa ndipo akagundua kuwa
haiwezekani kufanya hilo analotaka kufanya,
akajicheke mwenyewe hasa alipojua kuwa yale maji
kuna yanapokwenda, akaenda kwenye moja ya kona
za chumba hicho, alipotazama kwa makini sana
akaona kuna kitu kama kimebandikwa katika ukuta
huo, lakini kilikuwa kimefanana sana na ule ukuta,
akajua kwa vyovyote hapo pana kitu, akaanza
kugongagonga ukuta kwa ile bastola aliofika eneo
hilo akasiki ule mlio unabadilika na kuwa mkubwa
kiasi akagundua kuwa nyuma yake lazima kuna
uwazi, hakuwa na budi, kwa kutumia bastola hiyo
hiyo alifyatua risasi moja na ikatengeneza tundu zuri
ambalo lilimuwezesha kuona mpaka upande wa pili.
Kweli kulikuwa na uwazi mkubwa, Frank alisikia
sauti ya maji yanayotembea, lakini alipochungulia
kwa jicho lake aliona mwanga hafifu sana, akaanza
kubomoa lile eneo kwa kupiga na ile bastola kama
nyundo mpaka akafanikiwa kutengeneza tundu la
kutosha, akajipenyeza na kudondokea kwa ndani.
Lilikuwa ni bomba kubwa la maji taka, aliweza
kutembea kwa kuinama kidogo huku akipita kwenye
maji hayo na asijue ni wapi anaelekea, harufu
iliyokuwa humo haikuwa tatizo kwake, alitembea
mwendo mrefu kidogo, kwa mbele akaona kuna
pacha ya bomba hilo ikiungana na bomba linguine
ambalo nalo lilikuwa likileta maji kuunga na hili
nkisha kuelekea yanakokwenda, Frank alipoifikia ile
pacha akasikia kelele ya mtu anayekimbia katika
maji, akatul.ia kusibri aone mtu huyo ni nani.
§§§§§
KAMANDA Amata alipoona kuwa lile lango la
kwenda chini alikoingia Bill limejifunga, akachoka
ghafla, akatazama huku na kule, alichokiona akajua
tu ni switchi ya mlango huo, akaelekea pale ukutani
hakuwa na akaminya namba ya siri ambayo kuna
jinsi unavyoipanga inaweza kufungua kila aina ya
mlango, akaingiza tarakimu hizo kumi na mbili na
alama Fulani kwa mpangilio maalumu, akabonyeza
ok, akadaiwa kuweka alama ya kidole gumba,
akajua tu lazima ni kidole cha Andreas
kinachohatajika, alimtazama akiwa pale chini
amelala hana uhai, “Ndiyo shida ya dhukuma,
ukidhulumu utadhulumiwa” akaongea mwenyewe
huku akiuendea ule mwili, akachukua kipande cha
kioo kizito kilichovunjika hapo, akakata kidole
gumba cha Andreas na kwenda kukipachika pale
kwenye ile sense, taa ya kijani ikawaka, ule mlango
ukafunguka, haraka akauendea, alipotazama mezani
akagundua kuwa Bill ameisahau ile fimbo yake
Amata akaitazama na kuichukua, alipoigeuza geuza
akagundua kuwa haikuwa fimbo ya kawaida,
akaingia nnayo na ule mlango ukajifunga, alimweza
kumuona Bill kwa mbali akiendelea kwenda,
“Billlllllll…..” aliita, lakini Bill hakusimama. Baada ya
kumfuata kama dakika moja na nusu hivi, akamuona
Bill akisimama na kugeuka alikotoka, akiwa na begi
lake mkononi. Bill hakuwa na ujanja, alikuwa
katikati, huku Frank Edson FBI huku Kamanda
Amata TSA.
“Bill, huna ujanja, mwisho wako umefika,” ilikuwa
sauti ya Fr Frank. Amata aliiskia akajua kuwa ni
Frank anaye ongea lakini bado alikuwa hajamuona
kutokezea. Bill alibaki pale katikati akihema. Mara
Frank akatokezea na kugongana macho na
Kamanda Amata. “Kamanda Amata, niachie Bill
niondoke naye, asante sana kwa kazi kubwa
uliyoifanya ya kunirahisishia kumpata Bill Van
Getgand, asante sana, huyu inabidi afike hai pale
Washington,” Fr Frank alimwambia Kamanda
Amata.
“Sikia Frank, unajua kuwa ulikwishakufa wewe? Kwa
nini husemi asante kwa kukurudishia uhai wako?
Sasa sikiliza Bill utamchukua akiwa hai wala usijali
cha muhimu ni kutafuta njia nya kutoka humu ndani,
na njia hiyo lazima yeye Bill atuoneshe,” Kamanda
Amata akamwambia Frank, Frank akamsogelea Bill
na kumnyang’anya lile begi, Bill hakuwa na ubishi,
Frank akamrushia begi Amata, nae akalidaka.
“Haya, njia ya kutoka humu ndani iko wapi?”
akamuuliza Bill, alipoona ukimya wake unazidi,
akaamua kutumia nguvu, alimshika Bill kwenye
ukosei wa shati na kumbamiza kwenye kingo za
bomba hilo mara kadhaa, Bill alikuwa akitokwa na
damu nyingi katika paji lake la uso.
“Frank! Mbona huna huruma wakati wewe ni
mchungaji wa kanisa?” Kamanda aliuliza,
“Kwa taarifa yako, ukimfanya hivyo hatofika hai
Washington, nifuate njia ipo huku,” akaongeza, kisha
akatangulia na Frank akamfuata na Bill akiwa
katikati mikono akiwa ameshika kichwani.
Walikwenda mpaka kwenye ule mlango, akaufungua
na wakatoka wote, wakaingia kwenye chumba kile
cha siri, kisha wakaelekea katika lile sebule kubwa,
Frank alishangaa kulikuta lile jitu lililomtia adabu
likiwa marehemu, Frank moyoni mwake alikiri kuwa
Kamanda ni kiboko kama amelizimisha jitu hatari
kama lile. Jumba la Andreas lilikuwa kimya ni polisi
tu waliokuja kutoka mjini walikuwa huku na kule
wakifanya upekuzi wa hapa na pale.
“Weka mikono juu!” ilikuwa sauti ya polisi mmoja
wa kike akimuamuru kamanda Amata. Amata
akanyanyua mikono juu ile fimbo aliyoichukua pale
mezani ikaanguka chini, na Yule poilisi akamuamuru
mwenza aichukue. Mara Bill akatokea na nyuma
akiwamo Fr Frank Edson.
“Frank Edson FBI,” akaonesha na kitambulisho,
wale polisi wakaja kumchukua Bill na kumtia pingu.
“Na huyu?” waliuliza juu ya Kamanda Amata,
“Muacheni aende zake, ni mwenzetu kutoka shirika
la upelelezi Tanzania,” Yule askari akamwita na
kumuongoza kuelekea kwenye gari ya polisi. Nje ya
jumba la Andreas kulitanda gari za polisi zikiwaka
vimulimuli vilivyong’aza eneo lote hilo, Kamanda
Amata akatazama saa yake, ilikuwa ni saa kumi na
mbili alfajiri. Polisi walikuwa wakikusanya miili na
kufanya upekuzi wa hali ya juu katika jumba hilo
ambalo siku na miaka yote waliliona ni jumba la
mtu mwema.
Mlio wa Helkopta ulisikika ukikaribia eneo hilo,
Frank akamtazama Amata,
“Kamanda, Bill anaondoka moja kwa moja USA, uje
muagane tafadhali,” FranK alimwambia Amata kwa
nyodo. Kamanda Amata akavuta hatua na kufika
pale aliposimama Bill huku nyuma yake akiwa
ameshikwa na polisi wawili wa kijerumani na Frank
alikuwa alikuwa nyuma yao.
Bill na Amata wakawa uso kwa uso,
“Bill nilikwambia siku yetu inakuja, na ndiyo leo,
nitautwaa uhai wako kwan kisasi cha Fr Gichuru,
Kahaba Rose na wengine wote uliowapotezea
maisha yao pa sin a hatia. Nakuapia, hautakanyaga
gereza la Guantanamo wala wapi sijui,” kamanda
Amata aliongea kwa sauti ya chini ni Bill aliyekuwa
akisikia na wale polisi wawili, Frank alikuwa
akiongea na redio aliyopewa na mmoja makamanda
waliokuja na kikosi hicho. Bill alimtazama Kamanda
Amata, akamtemea mate usoni, Kamanda Amata
akamkazia macho Bill,
“Sintoyafuta mate haya mpaka nihakikishe umekufa
na haupo katika dunia hii, kifo chako ulikinunua
mwenyewe kwa gharama kubwa sana,” Bill
aliposikia maneno hayo aliikumbuka ile fimbo yake
na akaitazama ikiwa nikononi mwa Amata, kisha
Kamanda akageuka na kuondoka kueleka upande
ambao gari za polisi zilegeshwa, waandishi wa
habari kama kawaida yao, walichukua picha huku na
huku na kutafuta majibu ya maswali yao. Dakika
chache helkopta kubwa likakanyaga ardhi yenye
nyasi safi na kutulia tuli, wanajeshi wane waliovalia
sare ya jeshi yenye nembo ya bendera ya Marekani
walishuka na kumchukua Bill tayari kuondoka nae,
itifaki za kuondoka na mtuhumiwa huyo zilifanywa
haraka sana na pande mbili za mataifa hayo rafiki.
Kamanda Amata alikuwa kasimama upande wa pili
wa gari moja ya bpolisi akiwa kaegemeza tumbo
lake kwenye ubavu wa gari hiyo, begi lake kalitupia
ndani ya gari na ile fimbo ya Bill kaiweka juu ya
gari, akiangalia kila kinachoendelea.
Aliishika ile fimbo na kuwa kama mtu
anayeichunguza pale juu ya gari, bahati ilioje
alipogundua kuwa ile haikuwa fimbo bali ni silaha
mbaya sana yenye risasi za mtindo wa msumari,
silaha ya Kirusi iliyotumiwa sana na wanazi wa KGB
ambamo Bill alikuwa mmoja wao nyakati hizo,
aliitazama haraka na kuikuta bado nina risasi tatu,
akaiweka vizuri juu ya gari na kulenga shabaha,
hakuna aliyemwangalia wala kugundua hila yake.
Mguu wa Bill ulikuwa ukikanyaga ngazi ya helkopta
hiyo huku akisukumiwa ndani na wale wanajeshi, Fr
Frank alikuwa akifuata nyuma, lo, mara walishuhudia
Bill akijishika kifua, mara kichwa, akalegea na
kuanguka chini, tafrani ikazuka, walipomwangalia
tayari alikuwa marehemu, lakini hakuonekana tundu
lolote la risasi.
Kamanda Amata aliingia kwenye gari mara tu baada
ya kumaliza azma yake, alikuwa akisubiri Bill
akanyage japo ngazi ya helkopta hiyo, naye palepale
akafyatua bunduki hiyo ya siri, bunduki ya kijasusi,
akamtoa uhai Bill Van Getgand.
Fr Frank Edson akawaacha wale wanajeshi
wakimhudumia Bill ambaye alikuwa tayari
marehemu, akamjia Kamanda pale aliposimama, na
kamanda akatoka pale alipo kumuendea Frank,
akampa mkono, lakini Frank hakuupokea mkono
huo.
“Kamanda Amata, umefanya nini sasa?” Frank
aliuliza.
“tatizo nini, wewe ulimtaka akiwa hai sivyo, si
umemshika akiwa hai, na mimi nilishakwambia
serikali ya Dodoma inataka roho yake tu basi.
Asante sana Frank, umeifanya kazi yangu kuimaliza
kwa wepesi kuliko nilivyofikiria,” kisha Kamanda
Amata akageuka na kuingia kwenye gari iliyokuwa
imekwishawashwa tayari, Frank alibaki kumtazama
hakuwa na la kufanya, aliitazama ile gari ikitoka
getini na kutokomea mjini huku na zingine
zikiendelea kutoka moja baada ya nyingine.
DAR ES SALAAM
Saa 09:30 usiku
SIMU YA kitandani mwa Madam S iliunguruma kwa
fujo usiku huo, alishtuka na kukunja sura kama
kawaida yake kwani alikuwa hapendi sana
kukatishwa usingizi. Aliinyakua simu hiyo na
kuiweka sikioni.
“Madam S!” ilikuwa suti ya Chiba.
“Ee Chiba, niambie, mbona usiku sana,” Madam S
aliuliza.
“Fungua, televisheni yako, Deustche Welle,”
akamwambia na ile simu ikakatika. Madam S
akaiwahi rimoti haraka na kuwasha luninga yake
kubwa iliyofungwa ukutani katika chumba chake cha
kulala. Habari ya dharula aliyoikuta kwenye kioo
hicho ilimfurahisha kuliko habari zote alizowahi
kuzisikia. Ilikuwa ni habari ya moja kwa moja
iliyobebwa na maadishi ‘Breaking News’ ilikuwa
ikieleza juu ya kukamatwa kwa jasusi lililoisumbua
dunia, lakini hata hivyo ikasemekana limejiua kabla
halijapakiwa katika helkopta tayari kupelekwa
Marekani. Habari hiyo ilikuwa ikisifia shirika la
nkipelelezi la Marekani kwa kufanikiwa kulinasa
jasusi hilo. Akiwa katika kutazama habari hiyo, fax
yake ya mezani karibu na kitanda ikaanza kutoa
mlio kama wa mdudu, kijikaratsi chepesi kilikuwa
kikitoka na maadishi. Akaiendea na kuisoma fax
hiyo.
“…kazi uliyonituma nimeimaliza, Bill Van Getgand
amekshaisalimisha roho yake... TSA 1” Madam S
alijua kuwa ujumbe huo umetoka kwa Kamanda
Amata, akatabasamu, akazima luninga yake na
kurudi kitandani.
HATIMA
KAMANDA Amata alikuwa kwenye kititanda cha
wagonjwa katika kliniki binafsi ndani ya mji huo wa
Aachen, akigangwa majeraha na maumivu mengine.
Huku akijisomea magazeti nya siku hiyo akipata
habari za tukio lililotukia usiku wa siku hiyo na
kusoma habari nyingi za kweli na za uongo.
“Kamanda, Sindano!” alishtuliwa na sauti laini ya
kike, kamanda Amata akamwangalia Yule muuguzi
wa kizungu aliyekuwa na chano yake yenye kila kitu
kwa ajili ya tiba hiyo. Kiukweli pamoja na ujasiri
wote, kamanda Amata kwenye swala la sindano
alisalimu amri, aliogopa sana kitu hicho tangu
utoto. Alitamani kulia alivumilia mpaka shughuli
hiyo ilipokamilika.
“Asante dada mzuri, hata sikujua kama
umenichoma sindano,”Amata alimchokoza muuguzi.
“Kwa nini?” Yule muuguzi akauliza. “Kwa jinsi ulivyo
na mikono laini, na upendo unaomfanya mgonjwa
asihisi hata kama anapasuliwa nini kuchomwa
sindano!” Amata aliongea kwa lugha ya uchokozi,
“Hallo,” Kamanda aliita tena wakati Yule muuguzi
alipokuwa akitoka mle chumbani, “Nini? Unahitaji
sindano nyingine?” akauliza huku akirudishia mlango
na kurudi kwa Amata, Kamanda Amata akampa
ishara ya kuwa asogee amwambie kitu, Yule
muuguzi akasoge kumsikiliza, Kamanda akamshika
kwa mikono yake kichwani pande za masikio,
akamvutia kwake, hakukuwa na ubishi, akambusu na
ndimi zao zikabadilishana mawazo. Baada ya dakika
kama mbili za mchezo huo ambao uliwafanya wote
wasahau majukumu na magonjwa yao, akamtoa na
kumtazama usoni. Yule mwanadada alikuwa
akihema kwa nguvu, pepo limechukua nafasi,
akajichomoa kutoka kwenye mikono ya Kamanda,
akavua viatu na kumpandia kitandani, shughuli mpya
ikaamka, Kamanda Amata alipogundua kuwa pazia
la dirisha liko wazi, akshika kimnyororo kidogo cha
kazi hiyo na kukivuta, pazia likarudi mahala pake na
kuwaficha wawili hao kati ulimwengu wa peke yao.
ææææ MWISHO ææææ
 
nitakuua huku nakurekodi kwenye mkanda wa video
niwatumie wenziwako huko kwenu Afrika
wakaushuhudie mwisho wako ulivyokuwa wa taabu
na mateso, mwenzako anaejifanya kasisi kumbe ni
jasusi tayari ninae na chamoto ameshakiona
japokuwa hajafa, nitaua mmoja baada ya mwingine,”
Bill aliwaamuru vijana wake wamburuze Amata
kwenda shimoni kwenye mashine ya kifo.
SEHEMU YA MWISHO
§§§§§
FR FRANK Edson, alipojuwa kuwa Kamanda Amata
ameingia katika mtanange hivyo anaweza kumuwahi
kumpoteza Bill ilhali yeye anatakiwa ampeleke
akiwa hai, aliamua kuyavulia maji nguo na kujikita
katikati ya hatari hiyo, alilivamia jumba la Don
mapema sana hata kabla Bill hajarudi akajificha
katika moja ya stoo zilizokuwa ndani ya jumba hilo.
Kwa bahati mbaya au nzuri alipoikuwa katika
harakati za kutafuata pazuri pa kujificha kamera
ndogo sana ya usalama ilimuona na kupeleka taarifa
panapohusika ndipo shughuli ilipoibuka humo ndani,
kipigo alichokipata kwa mkono wa Iron Man The
Killing Machine alibaki hoi hajiwezi na kutupwa
huko shimoni ambako hakuna hewa hakuna
chochote ni mateso mpaka unakufa.
Fr Frank alishindwa kujitetea kwa jitu hilo la miraba
mine baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi.
Alikuwa nusu mfu katika chumba kile.
Kamanda Amata alijilegeza huku akiburuzwa mpaka
katika lango la chumba hicho ambamo
kinachofanyika ni kukutumbukiza, utakaa umo ufe
kisha inamwagwa dawa maalum ambayo
inakusagasaga na kuwa katika vipande
vidogovidogo kisha wanaflash kama chooni na taka
hizo zote hupelekwa baharini kupitia mfumo wa
maji taka. Walipofika mlangoni, tayari kumtupa mle
shimoni, Kamanda Amata alijitikisa kidogo, wale
jamaa wakashtuka, mmoja akainama kumwangalia
kama ni mzima au la, Amata akamtemea mate, kwa
uzembe wa Yule mlinzi akauchia mkono wa
Kamanda ili ajifute mate usoni, kosa. Konde moja
zito lilitua tumboni kwa jamaa Yule akatema damu,
huyu mwingine hajakaa sawa akachezea kipepsi
kimoja kilichjomfanya ajisjike tumbo, sasa Kamanda
Amata alikuwa huru na nguvu zake zilezile,
alijurusha kiufundi na kuwapiga mateke ya
migongoni kisha wale wawili wakaingia shimoni.
Kamanda akasonya na kurudi kwa njia ileile.
Akapenya hapa na pale na kutokea eneo lenye
veranda kubwa, akawa kizungukazunguka ajui nini
cha kufanya, akiwa katika hali hiyo alihisi mkono
wenye nguvu umekamata bega alipogeuka
akakutana uso na jitu la miraba minne, mara
akasikia vicheko kutoka sehemu asiyoijua. Lile jitu
likamnyanyua na kumbwaga chini, Amata
alijitonesha tena katika majeraha yake, akabaki
kugugumia maumivu tu. Aliinua kichwa na
kumwangalia huyo aliyemfanyia kitendo hicho,
lilikuwa ni jitu lenye pande la mwili, lililojaa misuli
mikubwa, kamanda Amata akaona wazi kuwa Frank
Edson hakuwa na budi kuwa katika hali ile kama
alipambana na dubwana hili, akajikokota
kunyanyuka ajaribu bahati yake, konde la pili
lilimrusha nyuma na kujibamiza vibaya ukutani,
Kamanda Amata akatema damu, alipokuwa akijaribu
kuinuka akapigwa teke la mbavu, nguvu ya teke lile
ilimsukuma mpaka ukuta wa pili, Kamanda alijikuta
akiwa na hali mbaya, alijitahidi kuinuka lakini
ilikuwa ngumu, alibaki kutambaa. Mara sauti
ikasikika kwenye chombo maalumu kilichofungwa
darini, ilianza na kicheko;
“Ha ha ha ha ha ha, Kamanda Amata, wewe unajua
sana kufuatilia nyendo za watu sio za miungu kama
sisi, sasa leo pambana huyo Israel mtoia roho,
kama wewe unaweza kukishinda kifo basi leo
tutaona ujanja wako uko wapi, ha ha ha ha ha ha
hapo ulipo ndio kuzimu ulipokuwa ukikusikia
kwenye vitabu vya dini zenu, pambana na mashine
ya kifo hiyo, ukiishinda nitakupa utajiri wangu wote,”
Maneno yale yaliyokuwa yakisemwa na mtu
asiyemuona yalimtia hasira sana Amata, “Utajiri
wako baki nao mwenyewe, kwa kuwa sikutaka
kukutoa roho sasa umeniladhimisha kufanya hivyo,”
ilikuwa sauti ya uchovu kutoka kwa Kamanda
Amata.
Vicheko vikaanza tena kwenye kile chombo, sasa
vikiwa kwa fujo zaidi, Kamanda Amata alihisi kitu
kama upepo kimepita sikioni mwake pindi
alipokuwa akigeuka, kumbe guu la lile jitu lilipita
akiwa na lengo la kumpiga teke la kichwani pale
chini alipojiinamia, Kamanda Amata kwa kasi
akaona amepata nafasi nzuri ya kufanya mambo,
alipiga ngumi moja iliyotua kwenye korodani za jitu
hilo, likaguna kwa maumivu. Akajiinua kwa ustadi
na kujisahaulisha maumivu yake, akawa wima,
alikusanya nguvu zake zote na kuruka hewani
alikoichanua miguu yake na mateke yote mawili
yakatua shavuni mwa lile jitu, lakini halikutikisika
hata kidogo. Kabla mguu wa Amata haujatua chini,
ulidakwa, Kamanda akautumia kama nguzo na
kujivuta kuelekea usoni mwa lile jitu, akalipiga
kichwa cha jichoni kwa maana alijua kwa vyovyote
atalipoteza maboya, kama aliota.
Kile kichwa kilipotua jichoni lile dubwana lika
muachia Amata na kujishika jicho, Kamanda Amata
akatua sakafuni kwa miguu miwili baada ya kuruka
samasoti safi sana, alitahamaki na kuliona lile jitu
likimjia kasi kama mbogo, akalikwepa nalo
likajibamiza ukutani, Kamanda Amata akatazama
huku na kule akaona taa iliyosimamishwa kwenye
nguzo ya chuma, akaiwahi na kuichukua akaivunja
taa yake nayo ikabaki bila taa, akaiinua na kumpiga
nayo mgongoni, lilipoguka kamanda Amata
akatumia ule mnara wa taa akamchoma tumboni,
lakini hakufanikiwa hata kumtoboa kutokana na
ulaini wa chuma kile lakini alimpiga shoti moja
mbaya ya umeme kutokana na kwamba alikuwa
hajaichomoa kwenye soketi pale ukutani, Amata
akatabasamu kwa hilo.
Lile jitu, lilipigwa shoti iliyolisukuma na likajibwaga
zimazima pale chini. Vicheko katika kile chombo
vikasimama ghafla. Kamanda Amata aligundua
kuwa jinsi ya kulishinda lile jitu sio nguvu bali akili,
alipi mguu chini na mara kitu chenye ncha kali
kikachomoka kwenye sehemu ya mbele ya solo ya
kiatu chake, na mguu mwingine vivyo hivyo,
Kamanda Amata sasa akaanza kutumia miguu
kuilishmbulia lile jitu, mateke ya usoni, mbavuni
yalilifanya jitu lile lipoteze nguvu maana kila
alipopigwa kwa teke aliachiwa jeraha kubwa
kutokana na vile vyuma kenye viatu vya Amata.
Zilikuwa dakika tatu za shughuli kubwa ya
kulikalisha chini lile dubwana. Kamanda akasimama
tayari kwa pambano akiliangalia lile jitu likigalagala
sakafuni huku damu zikitapaka kila mahali.
Upande wa pili, Bill na Andreas walikuwa kimya
wakitazama pambano hilo kupitia luninga ndogo
ndani ya chumba nyeti cha Andreas, hawakuamini
kile wanachokiona, kile kinachofanywa na Kamanda
Amata, jinsi anavyotumia akili kuliadhibu jabali lile,
mashine ya kifo kama wanavyoiita.
Tangu Andreas amnunue binadamu huyo wa ajabu
huko Honduras na kumsafirisha kwa siri mpaka
Ujerumani na kumuhifadhi katika nyumba yake,
alishamtumia kwa kuua watu wengi sana
wakiwezmo maafisa wa polisi, wanajeshi na wote
wanaofuatilia nyendo zake kwa ukaribu, hakuna
aliyewahi kufurukuta, wengi walikata roho kwa pigo
moja tu, kisha miili yao aliitupi ‘kuzinu’ katika
chumba alichokiandaa kwa kazi hiyo,. Akishakutupa
humo hufungulia hewa yenye chemical kali amabayo
hukukausha na kukumeng’enya kuanzia nyama yako
mpaka mifupa vyote vinakuwa unga, kisha maji
mengi huingia katika chumba hicho na kuondoka na
mmeng’enyo huo kupitia mabomba yha maji taka,
watu wako watakutafuta miaka nenda rudi na
hawatakuona, umefutwa katika orodha ya binadamu
duniani.
Leo ilikuwa tofauti, alimshuhudia Kamanda Amata
akitoa dozi mbaya kwa jitu lake hilo analolitegemea
kwa kazi hiyo. Kijasho kilipita kutoka kwapani na
kufika mpaka kwenye kiuno kabla hakijaishia katika
nguo alizovaa.
Kamanda Amata alipohakikisha dude hilo
limezimika alitzama huku na kule ili kuona cha
kufanya, sasa akili yake ilirudi kwa Bill na
mwenzake Andreas, akiwa katika kutazamatazama
mara akasiki kama nyayo za binadamu zikimfuata
kwa nyuma, akatazama kwenye kioo kikubwa kilicho
mbele yake na kuliona lile dude limesimama
likielekea kwake kwa nguvu zote, Kamanda Amata
hakuwa na silaha yoyote ya maana, akajua sasa
kuwa amekwisha, kabla hajaona la kufanya, lile jitu
likamfikia, likiwa na hasira mbaya, lilimpiga
kikumbo Amata akapitiliza mpaka kwenye kioo cha
mbele yake, alijibamiza na kile kioo kikamwagika
pakabaki wazi, Kamanda Amata akadondokea
upande wa ndani wa kile chumba kilichotenganis
hwa na kile kioo. Ilikuwa ni ofisi ndogoi lakini
iliyojaa kila aina ya nakshi na samani za gharama,
Kamanda Amata akanyanyuka na kuchukua chungu
kilichokuwa na ua ndani yake na kukirusha sawia
kichwani mwa jitu lile, likapepesuka kidogo, kabala
halijatuliya, Amata akajirusha doule kick na kutu
kifuani mwa lile jitu, kutyokana na kupoteza nguvu
liliyumba na kujibamiza ukutani, ule mtikisiko wa
ukuta ulifanya pambo la juu ambalo lilikuwa ni
bichwa la Nyati lililotengenezwa kwa chuma.
Lilianguka na kumpiga kichwani, kisha lile bichwa la
nyati liakadondoka sakafuni. Lile jitu likajitahidi
kusimama lakini ilikuwa ngumu kutokana na
kugongwa vibaya na lile bichwa la nyati bandia,
ilikuwa ni nafasi ya Amata ya kumaliza mopja kwa
moja akaanguka juu ya lile sanamu la kichwa cha
Nyati, akachomwa na pembe za nyati
zilizojinyomnga vizuri zikitanguliwa na ncha kali,
likatoa kelele za uchungu huku macho yakiwa
yamemtoka pima, likakata roho. Kamanda Amata
akakung’uta mikono yake kwa kuashiria kazi
imeisha, hakuamini kiama kalimaliza hayawani hilo.
§§§§§
Bill aliinuka na bastola mkononi, akiuelekea mlango
ili atoke nje, mkono mmoja akiwa na ile fimbo yake
ya kutembelea.
“Bill, hapa pameshakuwa pabaya, mi nafunga
vyangu najificha dhidi ya huyo mtu wako,” Andreas
alimwambia Bill, wote wawili walikuwa katika hali ya
kuchanganyikiwa, wakivujwa na jasho jingi. Andreas
alichukua begi tupu, akainyanyua ile monstrance na
kuiti begini kisha ile ramani, akaenda ukutani na
kushusha picha moja, nyuma yake nkulikuwa na
vibonyezo au vitufe kumi na mbili vikiwa na nmba
pamoja na alama chache, akaanza kuvibonyeza ili
mlango wa siri ulio kwenye sakafu ya chumba hicho
ufunguke, nukawa unagoma kufunguka, alipojaribu
mara ya pili nay a tatu mlango ule ukakubali,
taratibu ukawa unapanda juu ili kuwezesha mtu
kuingia. Bill aliona taanyekundu ikiwaka juu ya dari
la chumba hicho, ikiashiri kuna hatari, mara
alishuhudia ule mlango mnene wenye ulinzi mkali
ambao huwezi kuingi bila kuthibitisha vitu vitatu,
namba ya siri, alama za vidole na alama za macho,
na hivyo vyote vilikuwa ni Andreas peke yake
aliyeunganishwa.
Mlango ule ulionekana kwa ndani ukikatwa duara
kutoka nje, Bill akajua sasa hapa Kamanada
anaingia, akaiweka sawa bastola yake, hakuwa
tayari kufa wakati anayemlinda anatoroka,
akainyosha bastola kwa Andreas, Andreas akasikia
mlio wa bastola hiyo ikiwekwa sawa kulipua,
“Bill vipi tena?” Andreas akamuuliza Bill. Sikia
bwege wewe, yaani huna shukrani, kazi yote
niliyokufanyia, sasa hivi unaona mambo
yameharibika unakusanya vyako unataka kutoroka
na kuniacha mimi hata kunipa chochote sio, sitaki
maelezo, nakumaliza mwenyewe,” Bill alimwambia
Andreas kwa ukali.
“Sikia Bill, mi naokoa hii mali ya thamani, wewe
ukishamuua huyo Kamanda Amata tuonane nitakupa
donge nono,” Andreas alijitetea. “Siki, mi si motto,
Kamanda Amata keshakufa mara mbili na kafufuka
sasa unafikiri hapa atakufa tena?” Bill alimuuliza
Andreas, Mara lile pande la chuma linalokatwa kwa
saa ya Kamanda Amata, lilikuwa tayari kutoka
mahala pake na kuruhusu mtu wa nje kuingia ndani,
Bill alipiga risasi moja na kufumua kifua cha
Andreas, Andreas akaanguka chini na kutoa yowe la
maumivu, Bill akanyanyua tena mkono wake
ulioshika ile bastola na kulenga lile tundu ili ampate
Kamanda Amata, alipofyataua, viligongana vyuma
tupu, hakuna risasi, akaitupa chini bastola na
kunyanyua lile begi alilochukua Andreas na kuingia
kwenye ule mlango na kuzama ardhini huku mlango
ule ukijifunga nyuma yake.
§§§§§
Kama alitegemea kupona basi ilikuwa kwa asilimia
ndogo sana, Frank Edson, aliona kile alichofanya
Kamanda Amata pale mlangoni alipokuwa ameletwa
na wale watu ili kutupwa ndani ya shimo hilo
kusubiri kifo chake. Aliona kitu kidogo ambacho
Kamanda Amata alikiangusha kwa makusudi wakati
alipowaadhibu vikali wale jamaa wawili na
kuwatumbukiza mle shimoni.
Ilikuwa ni kitu kama kidonge kidogo, kwa tabu sana
Fr Frank Edson alijivuta kwa kutambaa mpaka
akakipata kile kidonge alipokitazama alikijua vyema,
kidonge kinachotumika kurudisha nguvu kwa haraka
kwa mtu aliyekuwa na uchovu mwingi wa kupigwa
au wa shuruba yoyote, pia kinaondoa maumivu kwa
muda mrefu. Fr Frank Edson alimuona Amata kama
Malaika wake, alikiokota na kukitia mdomoni,
akakimung’unya, muda kumi na tano tu alipata
nguvu taratibu mpaka akawa sawa na maumivu
yake yakapotea, akajinyanyua kutoka pale alipo,
akasimama wima, akatazama wale jamaa waliolala
pale, waliotupwa na kwa kipigo kikali na Kamanda
Amata. Akawapekua katika nguo zao na kupata
bastola moja iliyobakiwa na risasi mbili tu,
‘Sio mbaya’ akajisemea. Sasa kazi ilikuwa atatokaje
kwenye chumba kile kisicho hata na dirisha,
aliuangalia mlango ulikuwa juu umbali wa mita kumi
na ukuta wote ulikuwa umewekwa kitu kama niru
ambayo kamwe huwezi kuzikwea kwa jinsi
zinavyoteleza, ulikuwa mtihani mgumu kwake,
akakizunguka kile chumba akigusa hapa na pale,
baada ya kuchunguza sana ndipo alipogundua ile
sehemu ya kuingizi maji ndfani ya chumba kile,
haikuwa na bomba bali ni uwazi mwembamba wa
futi mbili kwa upana na uwazi wake ulikuwa ni kama
milimita tano, palitengenezwa hivyo ili maji yakitoka
yatoke kwa mbinyo na kasi kubwa kutokana na
msukumo wa pampu. Akapaangalia na kuona kama
anaweza kupita katika upenyo huo, lilikuwa ni wazo
finyu sana hata kama angekuwa motto mdogo,
sehemu ambayo asingeweza kupenya hata mjusi,
lakini yeye alidhamiria kupenya hapo, akiwa kama
aliyechanganyikiwa ndipo akagundua kuwa
haiwezekani kufanya hilo analotaka kufanya,
akajicheke mwenyewe hasa alipojua kuwa yale maji
kuna yanapokwenda, akaenda kwenye moja ya kona
za chumba hicho, alipotazama kwa makini sana
akaona kuna kitu kama kimebandikwa katika ukuta
huo, lakini kilikuwa kimefanana sana na ule ukuta,
akajua kwa vyovyote hapo pana kitu, akaanza
kugongagonga ukuta kwa ile bastola aliofika eneo
hilo akasiki ule mlio unabadilika na kuwa mkubwa
kiasi akagundua kuwa nyuma yake lazima kuna
uwazi, hakuwa na budi, kwa kutumia bastola hiyo
hiyo alifyatua risasi moja na ikatengeneza tundu zuri
ambalo lilimuwezesha kuona mpaka upande wa pili.
Kweli kulikuwa na uwazi mkubwa, Frank alisikia
sauti ya maji yanayotembea, lakini alipochungulia
kwa jicho lake aliona mwanga hafifu sana, akaanza
kubomoa lile eneo kwa kupiga na ile bastola kama
nyundo mpaka akafanikiwa kutengeneza tundu la
kutosha, akajipenyeza na kudondokea kwa ndani.
Lilikuwa ni bomba kubwa la maji taka, aliweza
kutembea kwa kuinama kidogo huku akipita kwenye
maji hayo na asijue ni wapi anaelekea, harufu
iliyokuwa humo haikuwa tatizo kwake, alitembea
mwendo mrefu kidogo, kwa mbele akaona kuna
pacha ya bomba hilo ikiungana na bomba linguine
ambalo nalo lilikuwa likileta maji kuunga na hili
nkisha kuelekea yanakokwenda, Frank alipoifikia ile
pacha akasikia kelele ya mtu anayekimbia katika
maji, akatul.ia kusibri aone mtu huyo ni nani.
§§§§§
KAMANDA Amata alipoona kuwa lile lango la
kwenda chini alikoingia Bill limejifunga, akachoka
ghafla, akatazama huku na kule, alichokiona akajua
tu ni switchi ya mlango huo, akaelekea pale ukutani
hakuwa na akaminya namba ya siri ambayo kuna
jinsi unavyoipanga inaweza kufungua kila aina ya
mlango, akaingiza tarakimu hizo kumi na mbili na
alama Fulani kwa mpangilio maalumu, akabonyeza
ok, akadaiwa kuweka alama ya kidole gumba,
akajua tu lazima ni kidole cha Andreas
kinachohatajika, alimtazama akiwa pale chini
amelala hana uhai, “Ndiyo shida ya dhukuma,
ukidhulumu utadhulumiwa” akaongea mwenyewe
huku akiuendea ule mwili, akachukua kipande cha
kioo kizito kilichovunjika hapo, akakata kidole
gumba cha Andreas na kwenda kukipachika pale
kwenye ile sense, taa ya kijani ikawaka, ule mlango
ukafunguka, haraka akauendea, alipotazama mezani
akagundua kuwa Bill ameisahau ile fimbo yake
Amata akaitazama na kuichukua, alipoigeuza geuza
akagundua kuwa haikuwa fimbo ya kawaida,
akaingia nnayo na ule mlango ukajifunga, alimweza
kumuona Bill kwa mbali akiendelea kwenda,
“Billlllllll…..” aliita, lakini Bill hakusimama. Baada ya
kumfuata kama dakika moja na nusu hivi, akamuona
Bill akisimama na kugeuka alikotoka, akiwa na begi
lake mkononi. Bill hakuwa na ujanja, alikuwa
katikati, huku Frank Edson FBI huku Kamanda
Amata TSA.
“Bill, huna ujanja, mwisho wako umefika,” ilikuwa
sauti ya Fr Frank. Amata aliiskia akajua kuwa ni
Frank anaye ongea lakini bado alikuwa hajamuona
kutokezea. Bill alibaki pale katikati akihema. Mara
Frank akatokezea na kugongana macho na
Kamanda Amata. “Kamanda Amata, niachie Bill
niondoke naye, asante sana kwa kazi kubwa
uliyoifanya ya kunirahisishia kumpata Bill Van
Getgand, asante sana, huyu inabidi afike hai pale
Washington,” Fr Frank alimwambia Kamanda
Amata.
“Sikia Frank, unajua kuwa ulikwishakufa wewe? Kwa
nini husemi asante kwa kukurudishia uhai wako?
Sasa sikiliza Bill utamchukua akiwa hai wala usijali
cha muhimu ni kutafuta njia nya kutoka humu ndani,
na njia hiyo lazima yeye Bill atuoneshe,” Kamanda
Amata akamwambia Frank, Frank akamsogelea Bill
na kumnyang’anya lile begi, Bill hakuwa na ubishi,
Frank akamrushia begi Amata, nae akalidaka.
“Haya, njia ya kutoka humu ndani iko wapi?”
akamuuliza Bill, alipoona ukimya wake unazidi,
akaamua kutumia nguvu, alimshika Bill kwenye
ukosei wa shati na kumbamiza kwenye kingo za
bomba hilo mara kadhaa, Bill alikuwa akitokwa na
damu nyingi katika paji lake la uso.
“Frank! Mbona huna huruma wakati wewe ni
mchungaji wa kanisa?” Kamanda aliuliza,
“Kwa taarifa yako, ukimfanya hivyo hatofika hai
Washington, nifuate njia ipo huku,” akaongeza, kisha
akatangulia na Frank akamfuata na Bill akiwa
katikati mikono akiwa ameshika kichwani.
Walikwenda mpaka kwenye ule mlango, akaufungua
na wakatoka wote, wakaingia kwenye chumba kile
cha siri, kisha wakaelekea katika lile sebule kubwa,
Frank alishangaa kulikuta lile jitu lililomtia adabu
likiwa marehemu, Frank moyoni mwake alikiri kuwa
Kamanda ni kiboko kama amelizimisha jitu hatari
kama lile. Jumba la Andreas lilikuwa kimya ni polisi
tu waliokuja kutoka mjini walikuwa huku na kule
wakifanya upekuzi wa hapa na pale.
“Weka mikono juu!” ilikuwa sauti ya polisi mmoja
wa kike akimuamuru kamanda Amata. Amata
akanyanyua mikono juu ile fimbo aliyoichukua pale
mezani ikaanguka chini, na Yule poilisi akamuamuru
mwenza aichukue. Mara Bill akatokea na nyuma
akiwamo Fr Frank Edson.
“Frank Edson FBI,” akaonesha na kitambulisho,
wale polisi wakaja kumchukua Bill na kumtia pingu.
“Na huyu?” waliuliza juu ya Kamanda Amata,
“Muacheni aende zake, ni mwenzetu kutoka shirika
la upelelezi Tanzania,” Yule askari akamwita na
kumuongoza kuelekea kwenye gari ya polisi. Nje ya
jumba la Andreas kulitanda gari za polisi zikiwaka
vimulimuli vilivyong’aza eneo lote hilo, Kamanda
Amata akatazama saa yake, ilikuwa ni saa kumi na
mbili alfajiri. Polisi walikuwa wakikusanya miili na
kufanya upekuzi wa hali ya juu katika jumba hilo
ambalo siku na miaka yote waliliona ni jumba la
mtu mwema.
Mlio wa Helkopta ulisikika ukikaribia eneo hilo,
Frank akamtazama Amata,
“Kamanda, Bill anaondoka moja kwa moja USA, uje
muagane tafadhali,” FranK alimwambia Amata kwa
nyodo. Kamanda Amata akavuta hatua na kufika
pale aliposimama Bill huku nyuma yake akiwa
ameshikwa na polisi wawili wa kijerumani na Frank
alikuwa alikuwa nyuma yao.
Bill na Amata wakawa uso kwa uso,
“Bill nilikwambia siku yetu inakuja, na ndiyo leo,
nitautwaa uhai wako kwan kisasi cha Fr Gichuru,
Kahaba Rose na wengine wote uliowapotezea
maisha yao pa sin a hatia. Nakuapia, hautakanyaga
gereza la Guantanamo wala wapi sijui,” kamanda
Amata aliongea kwa sauti ya chini ni Bill aliyekuwa
akisikia na wale polisi wawili, Frank alikuwa
akiongea na redio aliyopewa na mmoja makamanda
waliokuja na kikosi hicho. Bill alimtazama Kamanda
Amata, akamtemea mate usoni, Kamanda Amata
akamkazia macho Bill,
“Sintoyafuta mate haya mpaka nihakikishe umekufa
na haupo katika dunia hii, kifo chako ulikinunua
mwenyewe kwa gharama kubwa sana,” Bill
aliposikia maneno hayo aliikumbuka ile fimbo yake
na akaitazama ikiwa nikononi mwa Amata, kisha
Kamanda akageuka na kuondoka kueleka upande
ambao gari za polisi zilegeshwa, waandishi wa
habari kama kawaida yao, walichukua picha huku na
huku na kutafuta majibu ya maswali yao. Dakika
chache helkopta kubwa likakanyaga ardhi yenye
nyasi safi na kutulia tuli, wanajeshi wane waliovalia
sare ya jeshi yenye nembo ya bendera ya Marekani
walishuka na kumchukua Bill tayari kuondoka nae,
itifaki za kuondoka na mtuhumiwa huyo zilifanywa
haraka sana na pande mbili za mataifa hayo rafiki.
Kamanda Amata alikuwa kasimama upande wa pili
wa gari moja ya bpolisi akiwa kaegemeza tumbo
lake kwenye ubavu wa gari hiyo, begi lake kalitupia
ndani ya gari na ile fimbo ya Bill kaiweka juu ya
gari, akiangalia kila kinachoendelea.
Aliishika ile fimbo na kuwa kama mtu
anayeichunguza pale juu ya gari, bahati ilioje
alipogundua kuwa ile haikuwa fimbo bali ni silaha
mbaya sana yenye risasi za mtindo wa msumari,
silaha ya Kirusi iliyotumiwa sana na wanazi wa KGB
ambamo Bill alikuwa mmoja wao nyakati hizo,
aliitazama haraka na kuikuta bado nina risasi tatu,
akaiweka vizuri juu ya gari na kulenga shabaha,
hakuna aliyemwangalia wala kugundua hila yake.
Mguu wa Bill ulikuwa ukikanyaga ngazi ya helkopta
hiyo huku akisukumiwa ndani na wale wanajeshi, Fr
Frank alikuwa akifuata nyuma, lo, mara walishuhudia
Bill akijishika kifua, mara kichwa, akalegea na
kuanguka chini, tafrani ikazuka, walipomwangalia
tayari alikuwa marehemu, lakini hakuonekana tundu
lolote la risasi.
Kamanda Amata aliingia kwenye gari mara tu baada
ya kumaliza azma yake, alikuwa akisubiri Bill
akanyage japo ngazi ya helkopta hiyo, naye palepale
akafyatua bunduki hiyo ya siri, bunduki ya kijasusi,
akamtoa uhai Bill Van Getgand.
Fr Frank Edson akawaacha wale wanajeshi
wakimhudumia Bill ambaye alikuwa tayari
marehemu, akamjia Kamanda pale aliposimama, na
kamanda akatoka pale alipo kumuendea Frank,
akampa mkono, lakini Frank hakuupokea mkono
huo.
“Kamanda Amata, umefanya nini sasa?” Frank
aliuliza.
“tatizo nini, wewe ulimtaka akiwa hai sivyo, si
umemshika akiwa hai, na mimi nilishakwambia
serikali ya Dodoma inataka roho yake tu basi.
Asante sana Frank, umeifanya kazi yangu kuimaliza
kwa wepesi kuliko nilivyofikiria,” kisha Kamanda
Amata akageuka na kuingia kwenye gari iliyokuwa
imekwishawashwa tayari, Frank alibaki kumtazama
hakuwa na la kufanya, aliitazama ile gari ikitoka
getini na kutokomea mjini huku na zingine
zikiendelea kutoka moja baada ya nyingine.
DAR ES SALAAM
Saa 09:30 usiku
SIMU YA kitandani mwa Madam S iliunguruma kwa
fujo usiku huo, alishtuka na kukunja sura kama
kawaida yake kwani alikuwa hapendi sana
kukatishwa usingizi. Aliinyakua simu hiyo na
kuiweka sikioni.
“Madam S!” ilikuwa suti ya Chiba.
“Ee Chiba, niambie, mbona usiku sana,” Madam S
aliuliza.
“Fungua, televisheni yako, Deustche Welle,”
akamwambia na ile simu ikakatika. Madam S
akaiwahi rimoti haraka na kuwasha luninga yake
kubwa iliyofungwa ukutani katika chumba chake cha
kulala. Habari ya dharula aliyoikuta kwenye kioo
hicho ilimfurahisha kuliko habari zote alizowahi
kuzisikia. Ilikuwa ni habari ya moja kwa moja
iliyobebwa na maadishi ‘Breaking News’ ilikuwa
ikieleza juu ya kukamatwa kwa jasusi lililoisumbua
dunia, lakini hata hivyo ikasemekana limejiua kabla
halijapakiwa katika helkopta tayari kupelekwa
Marekani. Habari hiyo ilikuwa ikisifia shirika la
nkipelelezi la Marekani kwa kufanikiwa kulinasa
jasusi hilo. Akiwa katika kutazama habari hiyo, fax
yake ya mezani karibu na kitanda ikaanza kutoa
mlio kama wa mdudu, kijikaratsi chepesi kilikuwa
kikitoka na maadishi. Akaiendea na kuisoma fax
hiyo.
“…kazi uliyonituma nimeimaliza, Bill Van Getgand
amekshaisalimisha roho yake... TSA 1” Madam S
alijua kuwa ujumbe huo umetoka kwa Kamanda
Amata, akatabasamu, akazima luninga yake na
kurudi kitandani.
HATIMA
KAMANDA Amata alikuwa kwenye kititanda cha
wagonjwa katika kliniki binafsi ndani ya mji huo wa
Aachen, akigangwa majeraha na maumivu mengine.
Huku akijisomea magazeti nya siku hiyo akipata
habari za tukio lililotukia usiku wa siku hiyo na
kusoma habari nyingi za kweli na za uongo.
“Kamanda, Sindano!” alishtuliwa na sauti laini ya
kike, kamanda Amata akamwangalia Yule muuguzi
wa kizungu aliyekuwa na chano yake yenye kila kitu
kwa ajili ya tiba hiyo. Kiukweli pamoja na ujasiri
wote, kamanda Amata kwenye swala la sindano
alisalimu amri, aliogopa sana kitu hicho tangu
utoto. Alitamani kulia alivumilia mpaka shughuli
hiyo ilipokamilika.
“Asante dada mzuri, hata sikujua kama
umenichoma sindano,”Amata alimchokoza muuguzi.
“Kwa nini?” Yule muuguzi akauliza. “Kwa jinsi ulivyo
na mikono laini, na upendo unaomfanya mgonjwa
asihisi hata kama anapasuliwa nini kuchomwa
sindano!” Amata aliongea kwa lugha ya uchokozi,
“Hallo,” Kamanda aliita tena wakati Yule muuguzi
alipokuwa akitoka mle chumbani, “Nini? Unahitaji
sindano nyingine?” akauliza huku akirudishia mlango
na kurudi kwa Amata, Kamanda Amata akampa
ishara ya kuwa asogee amwambie kitu, Yule
muuguzi akasoge kumsikiliza, Kamanda akamshika
kwa mikono yake kichwani pande za masikio,
akamvutia kwake, hakukuwa na ubishi, akambusu na
ndimi zao zikabadilishana mawazo. Baada ya dakika
kama mbili za mchezo huo ambao uliwafanya wote
wasahau majukumu na magonjwa yao, akamtoa na
kumtazama usoni. Yule mwanadada alikuwa
akihema kwa nguvu, pepo limechukua nafasi,
akajichomoa kutoka kwenye mikono ya Kamanda,
akavua viatu na kumpandia kitandani, shughuli mpya
ikaamka, Kamanda Amata alipogundua kuwa pazia
la dirisha liko wazi, akshika kimnyororo kidogo cha
kazi hiyo na kukivuta, pazia likarudi mahala pake na
kuwaficha wawili hao kati ulimwengu wa peke yao.
ææææ MWISHO ææææ

Safi sana story ya kibabe sana...

Hawa jamaa Kamanda Amata, chiba, Madam S, Gina na wengineo mambo yao ni ya kibabe sana..

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni EquatorStory
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom