Alabuliwa Risasi Ya Makalio Akizini Ndani Ya Gari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alabuliwa Risasi Ya Makalio Akizini Ndani Ya Gari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Sep 5, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Sep 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Alabuliwa Risasi Ya Makalio Akizini Ndani Ya Gari  Jeshi la polisi limekumbwa na kashfa nyingine baada ya askari wake kudaiwa kumpiga risasi msichana wa miaka 16 baada ya kumkuta akivunja amri ya sita ndani ya gari.

  Msichana huyo alikumbana na mkasa huo Jumatano usiku eneo la Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, aalipopigwa risasi sehemu ya makalio wakati akijaribu kuwakimbia polisi kwa kutumia gari la mpenzi wake.

  Mpenzi huyo alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi ya ubakaji.

  Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana katika wodi ya Hospitali ya Temeke alikolazwa, msichana huyo alisema siku ya tukio alikutana na kijana huyo majira ya saa 8:00 usiku katika baa moja inayoitwa Kindau na kukubaliana kwenda kushiriki tendo la ndoa kwa malipo ya Shilingi 20,000.

  Alisema kutokana na muda huo kuwa usiku sana hawakuweza kwenda katika nyumba ya kulala wageni na badala yake walikwenda eneo la Zakhem na kisha walipaki gari kwenye uchochoro na baadae walianza kubanjua amri ya sita.

  Wakiwa kwenye kilele cha mapenzi yao, ghafla walishtukia gari la polisi likiwajia kwa kasi kwa nia ya kuwakamata, “Tuliagana anilipe elfu ishirini wala hakunibaka kama anavyodai, wao polisi walitukuta tayari tunamaliza lakini kutokana na woga tulikimbia ili tusikamatwe,” alisema msichana huyo.

  Alisema wakati wanakimbia kwa kutumia gari la mpenzi wake askari mmoja alifyatua risasi iliyopenya kwenye taa ya gari na kwenda kumjeruhi sehemu ya makalio yake, “Nilisikia mlio mkubwa wa bunduki, ghafla nilihisi kitu kimeingia mwilini mwangu na kuishiwa nguvu,” alisema kwa uchungu.

  Alisema kwa kuona hali hiyo, mpenzi wake alisimamisha gari kwa kujisalimisha na polisi walipowafikia walimtaka mpenzi wake huyo atoe pesa kama malipo ya kitendo chao cha kukutwa wakifanya mapenzi ama sivyo watampeleka kituoni.

  Alieleza kuwa mpenzi wake hakuweza kutoa pesa hizo ndipo walipoamua kumpiga na kumpeleka kituo cha polisi cha Mbagala na yeye alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

  Hata hivyo, ndugu na jamaa wa mpenzi wake wanapinga hatua ya polisi hao kutumia nguvu kubwa kama watu hao walikuwa watuhumiwa wa ujambazi.

  Wakizungumza wakiwa kwenye kituo cha Polisi cha Mbagala kufuatilia hatma ya ndugu yao, ndugu hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini walisema hatua ya polisi kupiga risasi huku wakitambua watu hao sio majambazi ni kitendo cha kinyama, “Tunachoshangaa ni kwa nini polisi wapige risasi wakati wakijua hawakuwa majambazi ila walikuwa wakifanya mapenzi, hata hilo jalada la kesi walilofungua wanataka kuficha maovu yao na sio vinginevyo,” alisema ndugu mmoja ambaye alijitambulisha kuwa shemeji yake.

  Alisema kimsingi tukio hilo lilikwenda katika makubaliano yao na sio ubakaji kama wanavyodai, ila kinachofanyika kwa sasa ni kutaka kumlinda Askari mwenzao aliyejeruhi kwa risasi.

  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, David Misime, alipopigiwa simu kuelezea tukio hilo, alisema kwa sasa hawezi kulizungumza kwa kuwa yupo nje ya Mkoa kikazi.

  Source :- Nipashe Jumapili
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  It clearly looks like was a consensus among the two, so how did police get into and opened fire to the girl? There is apparently covering up of some of the information which could otherwise reveal the police weaknesses.
   
 3. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  How kud it be possible to shoot the girl who was being raped instead of shooting a man? This is rediculous
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Sep 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Did u read the story..!?

   
 5. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hakuwa anabakwa kulingana na habari yenyewe inavyosema, hata hivyo ni upuuzi tu hata kama angepigwa risasi mwanamke ama mwanamme katika hali kama ile.
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Wawache zinaa na kujiuza.

  Halafu wasingekimbia, kilichowakimbiza ni nini? inaonesha polisi walikuwa wakiipiga risasi gari ili isimame na bahati mbaya risasi ikapenya na kumtandika makalio huyo kijana.

  Wanaume kutembea na msichana wa miaka kumi na sita ni kosa Tanzania? au akiwa anasoma tu? kwani najuwa kuwa si kosa kuolewa wa miaka kumi na sita na hata wa miaka kumi na nne, labda sheria za ndoa ziwe zimebadilishwa.
   
 7. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sheria ya ndoa inasema msichana wa miaka 15 ana weza funga ndoa na wakati sheria ya ubakaji Tanzania inasema ukimtafuna msichana mwenye umri chini ya miaka 18 unakuwa umebaka. Kwenye sheria kuna tatizo na magamba wanayaona haya na hawataki kubadilisha sijui kwanini ndio upuuzi wao huu sijui kipi hawakioni hapo. Ila kutumia nguvu kwenye kupiga risasi huku wakiwa hawana ushahidi nalo ni tatizo kubwa sana.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  huyo mwanamke alikuwa bar...wazazi wake wako wapi? huu ni mfumo duni wa ccm ..mtoto han la kufanya anajiuza..who to blame? CCM and no one else....offcourse kutembea na underage ni kosa kisheria, mteja kaenda bar kakuta malaya kamnunua..au siku hivi wanawake (machangudoa) wanaandikwa miaka yao vifuani?..ccm mnatupeleka wapi? i cant wait hili li CCM kufa
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Sep 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hata ili nalo mnalaumu CCM...! Dah! Kazi kweli kweli.
   
 10. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,554
  Likes Received: 12,829
  Trophy Points: 280
  Kufanya malovedove na mtoto under 18 ,ubakaji though pia nadhani polisi hawakuwa na nia ya kumlabua huyo bint risasi it seems that walitaka watoboe tyre then wawadai kitu kidogo !!!!!!!!!! mi mwenyewe nshawahi kukoswa risasi bar walitukuta nyt kali af wakadai kitu, kidogo wakabeba viti tulivyokomaa nao wakawakaanza fyatua risasi!!! Wanadai ati timevnja sheria weee tulivyozidisha jeuri wakasema et tulitaka kuwapora silaha!!! Waroho sana ndo mana wkt mngne wanavka mipaka
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Ndio maana Serikali ya CCM imeamuwa kutengezesha vitambulisho vya uraia ambapo bar wataweza kuthibitisha umri wa anaeingia hapo bar kama wanavyofanya nchi zingine. Kwa sasa tumlaumu Nyerere aliyekuwa hataki tuwe na vitambulisho vya uraia.
   
 12. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Hoja ya kiswahili inajibiwa kwa kiswahili someni tena mtaelewa ndipo muulize kwa mshangao tena... Kha!

  wao polisi walitukuta tayari tunamaliza lakini kutokana na woga tulikimbia ili tusikamatwe,” alisema msichana huyo.(Msichana alijua kosa lake) Kipolisi ni kosa na Sheria inamtaka atumia arm kumsimamisha kwa ishara kwanza then risasi chini ya kiuno,

  Alisema kwa kuona hali hiyo, mpenzi wake alisimamisha gari kwa kujisalimisha na polisi walipowafikia.

  Huelewi na Majibu yote yapo hapo hapo au mleta habari aandike kwa English?

  Zinaa hawawezi acha hadi goverment irekebishe uchumi wa ukweli sio wa vitabuni na hii ni urithi wa Dunia Zinaa alianza Hawa

  Bahati mbaya! hiyo ni kawaida ya Polisi wetu kusingizia hilo Tuliona kwa Zombe walipiga Juu kwa bahati mbaya zikampata nadhani risasi zao huwa zinaenda juu na kutua kwenye target.

  Wanaume kutembea na msichana chini ya miaka 18 ni kosa la ubakaji hat kama amemuoa hii sheria ilishadadiwa nchi nzima ilifahamu na ubakaji ulipungua pengine jk ndio hakujua hilo akidai ni kiherehere chao.

  Hao Jamaa ni uzembe wao kutowapoza hao polisi sheria itawashika wote.

  Chenge pekee ndio anaweza fanya kosa kisha akaishinda sheria akawa huru Bisha
   
 13. D

  Derimto JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tuache mambo ya ushabiki na kuweka kila kwenye mambo ya kisiasa hivi ni kweli hao wazinzi waliambiwa wafanye hivyo na ccm? au hao polisi walipewa amri ya kufyatua risasi na ccm? Malaya ni malaya tu hata wakiwa ulaya na hawawezi kuacha hata kama wakipewa kazi ikulu wataendeleza umalaya hata na walinzi au wafagiaji ni tabia chafu na malezo mabaya ya wazazi wao.
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  FF hayo ni mawazo mgando...kwa hiyo tumlaumu nyerere kwa vie kulikuwa hakuna internet kipindi chake?
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  pigia mstari hapo....na ina maana hujui sababu ni nini?
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Sep 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hivi uzinzi Tanzania ulianza mwaka gani?
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Mie naongelea vitambulisho wewe unaongelea internet, kwa nini usimlaumu ilikuwa hakuna TV station wakati wake, hata Karume aliweka ZTV?
   
 18. D

  Derimto JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Ndiyo maana nikasema hiyo ni tabia ya mtu hata akiwa anakaa wapi na anapata nini atakuwa malaya tu unataka kuniambia kuwa wale wote malaya unaowaona wana shida kuliko wanawake wengine na hawawezi kufanya kitu kingine cha kujipatia kipato?
   
 19. u

  ureni JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  "Tumlaumu Nyerere" inaonekana kuna harufu ya udini hapa.
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  CCM inahusika kwa 100% kwa sababu haiingii akilini mtoto wa miaka 16 anakuwa hayupo kwene uangalizi wa wazazi au walezi usiku wa manane..Serikali inatakiwa kushape mustakabali wa jamii kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa..badala kufanya yanayowahusu raia wao wako bize kuuza nchi.
   
Loading...