Kwa kuendekeza vitu kama Albadiri hatutofanikiwa kamwe. Na udhaifu unaouona kwetu Waislam moja ya sababu yake ni mambo kama hayo ya "Albadiri".
Nawapa Bishara Njema ndugu zangu Waislam kuwa Allah Atatupa Nusra na Ushindi iwapo tutashikamana na Dini yake kama Alivyotufundisha Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na kama walivyofahamu Maswahaba (Allah Awaridhie). Kama tukishikamana na Tawheed na tukaachana na Shirki na kukaa nayo mbali na kushikamana na Sunnah na kuacha uzushi katika Dini.
Maswahaba pia kabla ya kupewa nguvu, waliwahi kuwa dhaifu na wanyonge wenye kuteswa pia pale walipokuwa Makkah. Can you imagine, Makkah Ambayo ni bora kuliko Palestine iliwahi kuwa chini ya washirikina? Imagine maumivu ya Waislam walipokuwa wakiona Nyumba ya Allah ikiwekwa masanamu, washirikina wakiivunjia heshima kwa kufanya tawafu uchi. Madhila ambayo Waumini walipitia na maumivu ila wakawa na subra, mpaka baadhi wakaamriwa kuondoka Makkah kuhamia Abyssinia (Habasha/Ethiopia). Wamepata shida na walikuwa na subra mpaka walipoamriwa kuhama Makkah wakahamia Madinah. Imagine unyonge na shida walizozipata. Lakini Allah Aliwaahidi Ushindi wakishikamana na Tawheed, wakishikamana na Mwenendo wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake), na Allah sio Mwenye kuivunja Ahadi yake.
Walitekeleza walichoamrishwa na Allah na Allah Akatekeleza Ahadi yake kwao. Yaliyomo katika Historia ni shahidi, hakuna anayepinga Ushindi waliopata Waislam.
Tuwe na Subra na Tushikamane na Dini yetu tusiiache na tutekeleze tuliyoamrishwa na tuache tuliyokatazwa.
Bishara Njema kwetu
وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ لَيَسۡتَخۡلِفَنَّهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ كَمَا ٱسۡتَخۡلَفَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمۡ دِينَهُمُ ٱلَّذِي ٱرۡتَضَىٰ لَهُمۡ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّنۢ بَعۡدِ خَوۡفِهِمۡ أَمۡنٗاۚ يَعۡبُدُونَنِي لَا يُشۡرِكُونَ بِي شَيۡـٔٗاۚ وَمَن كَفَرَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ
Allah has promised those among you who believe, and do righteous good deeds, that He will certainly grant them succession to (the present rulers) in the earth, as He granted it to those before them, and that He will grant them the authority to practise their religion, that which He has chosen for them (i.e. Islam). And He will surely give them in exchange a safe security after their fear (provided) they (believers) worship Me and do not associate anything (in worship) with Me. But whoever disbelieved after this, they are the Fasiqun (rebellious, disobedient to Allah).
(Qur-aan 24: 55)
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوۡمِهِمۡ فَجَآءُوهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَٱنتَقَمۡنَا مِنَ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيۡنَا نَصۡرُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
And indeed We did send Messengers before you (O Muhammad SAW) to their own peoples. They came to them with clear proofs, then, We took vengeance on those who committed crimes (disbelief, setting partners in worship with Allah, sins, etc.), and (as for) the believers it was incumbent upon Us to help (them).
(Qur-aan 30: 47)