Akishitaki atakuwa kamkosea mumewe?

Mie natamani kumwambia aachane na mumewe ila naogopa kumwambia maana moyo wa mtu kichaka. Nafamiana na hii familia siku nyingi na pia naona na nafahamu mateso anayopitia huyu mama. Ila sina ujasiri wa kumwambia ondoka hapo kwako uanze maisha upya.
Ndg... si bora akashtaki na mzee awekewe kikao!!
pili atumie wazee wa ukoo mbali mbali..
au viongozi wa Dini !!
tatu akichoshwa na tabia hiyo amsukume kia mbali mume!! (baada ya kuwaonesha watoto wake hulka ya baba yao ovu) ushahidi kwa wanafamilia utathibitisha kuachana!!
pole yake na ndiyo matokeo ya Ubadhirifu ma udhulati ktk kazi au utumishi alioaminiwa na serikali ua watu wanyonge!! tija hiyo
 
Yaani acha tu, unakuta ndoa ilishajifia ila mmo tu!!

Hahahahaaa yaani inakuwa mazoea tuu ila hatari sana. Unaona watu wanaenda kanisani au kwenye harusi kila mtu na gari lake kila mtu anakuja kivyake na kwenye sherehe kila mtu anakaa meza yake na kuondoka kila mtu anaondoka kivyake ni kuwa tuu wanakaa nyumba moja ya chumbani ndo hayajulikani unaweza master bedroom kuna dabodeka hahahahahahaa aaah sikia tuu kwa jirani aiseeh
 
Kama kwenye raha walikua wote na kwenye shida wabaki wote. Inaonyesha uyo mwanamke anamfanyie mme wake visa kwasababu anajua katumbuliwa.

Ni kweli ni vyema kuvumiliana, pia si kuwa namtetea huyu mama ila namfahamu. Kama kuna wamama wanyenyekevu ma watii basi huyu ni mfano wa kuigwa. Ni msongo wa mawazo wa mumewe ndo umeongeza changamoto.
 
Sijakuelewa nani na nani wawe kwenue mahusiano? Ilo kupunguziana maumivu?
Namaanisha kama ni jinsia tofauti hapo ndio mngejikuta mnaanza mahusiano,ila kwa vile ni jinsja moja muombee tu I'll Mungu aingilie kati
 
Ndg... si bora akashtaki na mzee awekewe kikao!!
pili atumie wazee wa ukoo mbali mbali..
au viongozi wa Dini !!
tatu akichoshwa na tabia hiyo amsukume kia mbali mume!! (baada ya kuwaonesha watoto wake hulka ya baba yao ovu) ushahidi kwa wanafamilia utathibitisha kuachana!!
pole yake na ndiyo matokeo ya Ubadhirifu ma udhulati ktk kazi au utumishi alioaminiwa na serikali ua watu wanyonge!! tija hiyo

Shukria, ntamshauri hili pia iwe kwake kufanya maamuzi.
 
Hehehee avatar inakudanganya hii ya zamani sana.
Mie ntawaacha na huyo mama muongee maana mie kwa sasa sina msongo wa mawazo kuhitaji mawazo au ushauri au maongezi.
Maongezi yangu yatakuwa kuangalia meno tu Mkuu

huyu Mama kazi yake ni ndogo sana nampa maelekezo hakuna kazi kubwa kabisa kwake
 
Ukiruhusu stress za maisha ziongoze maamuzi yako unaweza ukafanya jambo lisilostahiki
 
kweli ukifulia hata shetani hakupendi?
kipindi mume kapata majanga ya kutumbuliwa ndo kipindi huyo baba aliitaji upendo wa kweli,kubaki nyumbani akaambiwa anatembea na mabeki tatu ona alipoishia sasa .huyo shogako ni shwetani tu .hyo baba atakufa siku si nyingi tuone kama atafaidi
 
Habari zenu wandugu,

Mawazo na michango yenu inahitajika kunusuru hii familia.
Ni familia ya mume mke na watoto 5, watoto 3 wako sekondari shule za bweni na wawili ndo wako shule ya msingi wanakaa nyumbani na wazazi wao.

Hii familia kwa miaka 3 mfululizo wamekuwa kwenye changamoto mbalimbali kiasi kwamba wote baba na mama kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitamani kuachana ila kigezo cha watoto ndo huwa kinakuwa zuio.
Changamoto imeongezeka baada ya utawala mpya kuingia madarakani mume au baba mwenye nyumba alitumbuliwa na mheshimiwa na hadi sasa yuko benchi tuu. Tangu huyo baba atumbuliwe amekuwa kero kwenye familia yake. Mwezi mmoja wa kwanza baada ya kutumbuliwa alikuwa anashinda nyumbani asubuhi hadi asubuhi nyingine, yaani alikuwa baba wa nyumbani na akajikuta anakuwa karibu na housegirl matokeo yake kuanza mahusiano na wadada wa kazi. Aibu hii mkewe aliigundua maana wadada walionesha mabafiliko kuna walioonesha jeuri na kiburi na kuna walioaga kuacha kazi gafla maana si waschana wote wanakubali kuwa na mahusiano na baba mwenye nyumba. Hivyo hilo limefanya mke kuwa na kero ya kubadili waschana wa kazi kila leo kama mjuavyo si rahisi kupata waschana wa kazi waweza kaa miezi 3 hadi 4 ukiwa unatafuta bila kupata.

Mke akiongea hii kero na mumewe mume akaona abadili muelekeo na kuanzia hapo akaanza asubuhi mke akijiandaa kwenda kazini na watoto shule yule baba mwenye nyumba anajiandaa nae anatoka. Anakoenda haijulikani basi ya miezi kadhaa mke akagundua kumbe huwa anaenda baa muda wa asubuhi atakula na kunywa maji hadi mchana akihama baa moja kwenda ingine na pale pombe zinaporuhusiwa kuanza kuuzwa basi huzifakamia utasema kuambiwa zinaongeza nguvu za kiume. Anarudi nyumbani akiwa njwii hajitambui anarudishwa na bodaboda hana hata kumi....

Amekuwa akitumia akiba yake kufanya huo ulevi na sasa amekuwa mlevi wa kupindukia. Mke ameshamshauri mara kadhaa aache kufanya hivyo maana hakubadilishi au kumpunguzia msongo wa mawazo alionao badala yake amekuwa mkali kwa mke na watoto. Mke anaona uvumilivu unamshinda maana kila siku afadhali ya jana. Mbali ya hapo bwana mume amekuwa akishusha kipondo kila arudipo amelewa na hapo kuna siku anarudi ananukia marashi ya kike siku ingine shati zina alama za rangi ya mdomo na foundation.... mke anafua tuu.... Kweli jamani na hii avumilie. .... magonjwa je?

Nyie mwaonaje maana hii familia naifahamu na huyu mama huwa tunaongea sana. Sijamshauri cha kufanya nimekuwa nikimpa pole tuu ila ninakoelekea nahisi ntamwambia aachanena mumewe maana huko si kuvumiliana kwa shida na raha khaa.

Kusema ukweli hata mie ndoa yangu ina misukosuko ila si kama ya huyu mama. Na yangu ingekuwa kama ya huyu wallah ningeachika tangu juzi.

Nyie mnashaurije?
Kosa hela tujue tabia ya mkeo!
 
kweli ukifulia hata shetani hakupendi?
kipindi mume kapata majanga ya kutumbuliwa ndo kipindi huyo baba aliitaji upendo wa kweli,kubaki nyumbani akaambiwa anatembea na mabeki tatu ona alipoishia sasa .huyo shogako ni shwetani tu .hyo baba atakufa siku si nyingi tuone kama atafaidi
Nakuunga mkono, kama ni nyege angekuwa anamkamua zoote asubuhi kabla hajaondoka!Wazee wenyewe hata nguvu hawana ataparamia saa ngapi mabeki tatu!?Huyo mama anamuona mwenzie mzigo na ukute keshampakia mimaneno kibao!Ogopa mwanaume akiwa broke halafu ukamsimanga "he turns to a monster that you can hardly handle"
 
Back
Top Bottom