Ndo maana me na wewe ni mabinamu wa damu. Huyo baba anachopitia sasa hivi ni ile frustration ya kupoteza kazi (ingawa ya kutembea na house girls sikubaliani nayo). Hakuna kitu kigumu kama mtu kuzoea kukaa nyumbani helplessly, while alishazoea kuchakarika na kushika pesa zake. Ile ku-adapt maisha ya kutokushika hela ni kazi ngumu mnooo, unless awe na watu wanaomsupport haswa. Hiyo kunywa ni simply anajitahidi kupoteza mawazo. Katika situation hiyo wengi wanabadilikaga kuwa very sensitive, too defensive, insecure and bitter. Tena kama mama ndo umekuwa breadwinner basi ndo jipange haswa, maana ile sense ya Kuwa yeye ndo mwanaume wa nyumba inakuwaga matatani, anajiona useless. So unaweza ukamwambia tu kitu kidogo yeye akakikuza, ataona umekisema kisa tu yeye hana kazi, ili akupruvie kwamba yeye bado ndo man of the house, basi utakula mkong'oto hatari. Atafute tu watu wazima au mwanasaikolojia ili aongee naye amtulize slowly ataanza kurudi kwenye hali yake. Ila mke ndo asichoke kuwa mvumilivu, ni jaribu lao, litapita tu