Akinyi Must Die (Ni lazima Akinyi afe) - 03
Bhoke "Shikamoo mama"
Bhoke alimsalimia yule mama ambaye alikuwa jirani na siti aliyokuwa amekalia.
Mama "Marhaba mwanangu mzuri"
Ile Hiace iliondoka pale stendi ya Tarime mjini kuelekea Musoma.Wakati ile gari ikiwa imeshika kasi kuelekea Musoma,Bhoke ghafla alianza kulia kilio cha kwikwi ambacho kilimshitua yule mama aliyekuwa jirani yake.Yule Mama mtu mzima ilibidi ajaribu kuzungumza na binti Bhoke kama mwanae ili aweze kufahamu ni kitu gani kilichokuwa kimemsibu.
Mama "Mbona unalia mwanangu,umepatwa na nini!?"
Aliendelea "Hebu nieleze mwanangu au unaumwa?"
Bhoke "Hapana siumwi" alijibu Bhoke.
Mama "Sasa mbona unalia?"
Bhoke alifuta machozi akaamua kukaa kimya huku yule mama akiendelea kumshangaa.
Bhoke "Hivi Musoma bado mbali mama?"
Mama "Bado kuna mwendo"
Mama "Kwani hujawahi kufika?"
Bhoke aliitikia kwa kutikisa kichwa akimaanisha hajawahi kufika Musoma.
Mama "Sasa unaenda kwa nani?"
Yule mama aliendelea kumuuliza Bhoke maswali.Baada ya lile swali binti Bhoke alianza tena kulia na safari hii yule mama alijua kutakuwa na tatizo kubwa lilimfanya yule binti mrembo kutoa machozi.Yule mama ilibidi amsogelee Bhoke kwa ukaribu akaanza kumnong'oneza kwa sauti ya chini akimsihi anyamaze ili iwe rahisi Bhoke kumueleza kilichomsibu.Sasa pamoja na yule mama kuendelea kumshangaa Bhoke lakini pia abiria wengine waliokuwa wamekaa siti za nyuma za ile gari walikuwa wakishangaa ni kitu gani kilikuwa kikimliza yule binti.
Bhoke "Nimetoroka nyumbani"
Mama "Umetoroka nyumbani,kwanini umetoroka!?"
Aliendelea kuuliza "Kwanini umetoroka nyumbani binti yangu hebu nieleze nitakusaidia!"
Bhoke "Baba alitaka nikeketwe mi nikawa sitaki ndiyo nilipokwenda shuleni sikurudi tena nyumbani"
Mama "Masikini!,kwahiyo Musoma unaenda kwa nani?"
Bhoke "Naenda kwa Mjomba Maswi"
Mama "Huyo Mjomba wako anafahamu kwamba unakwenda kwake?"
Bhoke "Nikifika ndiyo nitamwambia"
Bhoke aliendelea kulia kwa kwikwi huku akimueleza yule mama waliyekuwa wamekaa nae jirani.
Mama "Sasa mwanangu umesema Musoma hujawahi kufika,huyo mjomba wako unafahamu anapokaa?"
Bhoke "Nitauliza tu nikifika"
Kwa namna Bhoke alivyokuwa akiongea yule mama alitambua kabisa bado alikuwa na akili za kitoto na alidhani uenda mji wa Musoma ulikuwa mdogo kama kijiji cha Magoto kiasi kwamba ukimuulizia mtu inakuwa rahisi kupatikana,kwakuwa yule mama alielewa alichokuwa ameambiwa na Bhoke kuhusu yeye kukimbia nyumbani kwao,yule mama alimwambia atamsaidia wakifika Musoma.
Mama "Basi usilie mwanangu,tukifika Musoma nitakusaidia"
Wakati huo Mzee Gisiri Mnanka aliendelea kumtafuta Bhoke bila mafanikio pale kijijini Nyabitocho,muda ulipozidi kuyoyoma aliamua kurudi tu nyumbani kwake huku akiwa na hasira sana,aliamini Bhoke angerudi tu mwenyewe nyumbani.Mama mseti mpaka wakati huo hakuwa na raha kabisa kutokana na ile hali ya kutoweka kwa binti yake.
Mzee Mnanka alipofika nyumbani hakutaka kabisa kuongea na mkewe kwasababu alifahamu kitendo cha Bhoke kutoroka uenda kilisababishwa na mkewe.Mama Mseti baada ya kuona mumewe yupo kimya aliamua kumuuliza.
Mama Mseti "Vipi baba Mseti,umefanikiwa?"
Baba Mseti "Huyu mtoto ameitia aibu hii nyumba na hii familia"
Mama Mseti "Mtoto atarudi tu nyumbani,hupaswi kuwa na hasira kiasi hicho"
Baba Mseti "Nilikwambia huyo mtoto asipopatikana nitakuua,wewe ndiye umekuwa mstari wa mbele kumfundisha ujinga"
Haikuchukua muda mzee Mnanka alitoka ndani bila kumuaga mkewe.Mzee Mnanka alipoondoka kwake alielekea kwa rafiki yake wa muda mrefu aliyeitwa Chacha Kimori,Chacha na Mnanka walikuwa ni marafiki wa kushibana sana,mzee Chacha Kimori yeye alikuwa ni mstaafu wa jeshi la Wananchi wa Tanzania(Jwtz) akiwa mwenye cheo cha Captain,wakati mzee Gisiri Mnanka yeye alikuwa mstaafu kutoka taasisi nyeti ya kiusalama Tanzania(Tanzania Intelligence and security service - TISS).Hawa wote waliwahi kufanya kazi pamoja,hivyo walikuwa marafiki wakubwa mno.Pia kwasababu walikuwa watu wa kabila moja na ambao walitoka Kijiji kimoja walijikuta wamekuwa zaidi ya ndugu.
Mzee Kimori "Muraa Mnanka,amang'ana Mura"
Mzee Mnanka "Amaiya Mura"
Mzee Kimori "Karibu sana Mura"
Baada ya ukaribisho na salamu ya kilugha,mzee Mnanka alivuta Kiti akakaa.
Mzee Kimori "Nchwaghwa tareta Obhosara"
Mzee Kimori alimwambia binti yake aliyekuwa akiitwa Nchwaghwa amletee Mzee Mnanka Togwa ili akate kiu.Togwa kilikuwa ni kinywaji cha heshima katika kila nyumba ya mkurya kijiji hapo na mtu yeyote iwe mgeni au mwenyeji alipokuwa akifanya matembezi kwa jirani yake,basi alikaribishwa na kinywaji hicho aina ya Togwa.
Mzee Kimori "Mbona umekuwa adimu sana tata!"
Mzee Mnanka "Siunajua tena kazi za minada zinavyochosha Chacha".
Mzee Kimori "Mama mseti anaendeleaje?"
Mzee Mnanka "Unajua yule mwanamke ni mjinga"
Mzee Kimori "Amefanya nini tena?"
Mzee Mnanka "Sitaki hata kumuona"
Aliendelea "Hivi unajua yule mtoto ametoroka Chacha!"
Mzee Kimori "Mtoto yupi?"
Mzee Mnanka "Bhoke humjui mura!"
Mzee Kimori "Bhoke!"
Mzee Mnanka "Yule mwanamke ndiye tatizo na yeye ndiye chanzo cha yule mtoto kutoroka"
Mzee Kimori "Sasa kamekimbia kwasababu gani Tata!"
Mzee Mnanka "Si kamekimbia Saro(Kukeketwa) Chacha"
Mzee Kimori "Umeshakatafuta?"
Mzee Mnanka " Mura hata muda huu natokea hapo Nyabitocho mimi na Mseti lakini hakuna mtu!"
Mzee Kimori "Sasa Mnanka unakuwa kama mtoto na wewe,kwanini usichukue vijana hapa kijijini wakaifanye hiyo kazi,hiyo kazi waachie kina Mseti na wenzie watampata,unadhani atakimbilia wapi,kako hapa hapa kijijini"
Mzee Mnanka "Unajua kameniibia na hela zangu Chacha za mauzo ya Ng'ombe"
Mzee Kimori "Hapo sasa ndipo kuna tatizo,huyo bila kumuwahi Nyamwaga utamkosa Tata"
Aliendelea "Waambie kina Mseti wachukue baiskeli wanyonge hadi Nyamwaga kanaweza kuwa huko kanazurura tu watakarudisha!"
Mzee Mnanka "Atarudi tu Chacha,unadhani ataenda wapi, namna ninavyofahamika najua watamleta tu watu!"
Mzee Kimori "Mtoto wa nyoka ni nyoka Mnanka,niliwahi kukwambia tangia zamani yule mtoto alipaswa afe"
Mzee Mnanka "Sikuwahi kuua watoto wadogo Chacha,niliamua kukachukua ili nikalee kawe kama katoto kangu,wewe mwenyewe unajua nimezaa yote madume tu,nilitaka baadae kanipe ng'ombe mura!"
Mzee Kimori "Kwahiyo sasa utafanyaje Tata?"
Mzee Mnanka "Katarudi tu"
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu,mzee Mnanka alimuaga rafiki yake huyo wa siku nyingi na kuondoka zake.
Mama "Amka tumefika mwanangu"
Baada ya kufika Musoma,yule mwanamke mtu mzima alimwamsha Bhoke aliyekuwa amepitiwa na Usingizi.
Mama "Hapa sasa inabidi tupande daladala kuelekea nyumbani"
Aliendelea "Hebu tutembee hadi pale mbele tukapande daladala mwanangu"
Yule Mama pamoja na binti Bhoke waliingia kwenye Daladala kisha ilipojaa iliondoka,walipofika mitaa ya Mwisenge walishuka na kuanza kutembea kuelekea nyumbani kwa yule mwanamke.
Mama "Nyakwesiiii!"
Aliendelea "Nyakwesi aweeee"
Mama "Abhana bhanu bhalyaki bheeee(hawa watoto wameenda wapi!)"
Mama "Nyakwesiiiii!"
Yule mama aliendelea kuita kwa sauti kubwa ili Yule aliyeitwa akisikia sauti basi aweze kuitikia.
Sauti ya kike "Abeeeee!"
Mama "Waliulyaki bheee!?" -(Ulikuwa wapi?)
Nyakwesi "Nali ku Mama Moze iniringira itivii"-(Nilikuwa kwa mama Moze naangalia TV)
Mama "Muta kulola ji swalo,itivii ilyanu ika,kulwaki muta kuikala ika?" - (Hamuoni hata aibu,TV iko hapa nyumbani lakini hamtaki kutulia)
Nyakwesi "Suuuuuura mama"
Mama "Leloooota"
Aliendelea " Hebu mpeleke ndani huyo mtoto aoge abadili na nguo,umtafutie nguo za Juliana zinazomtosha uumpe avae.
Itaendelea........................