Akinyi Must Die (Ni lazima Akinyi Afe)

Akinyi Must Die (Ni lazima Akinyi Afe)

Akinyi Must Die (Ni lazima Akinyi afe) - 04




Baada ya kuwa wamemaliza kupata chakula cha mchana huo muda wa saa 9 alasiri,yule mwanamke alimchukua Bhoke na kuelekea kwenye ofisi ya mtendaji wa mtaa wa Mwisenge pale Musoma.Nia na lengo ilikuwa ni kwenda kutoa taarifa ya kwamba kuna binti ambaye si wake hivyo ameamua kumsaidia mpaka pale atakapopata msaada.


Mwenyekiti wa mtaa " Oooh Mwalimu Veronica,Wachamaee!"


Mama " Chaaaasugu kaka"

Aliendelea "Jendanu" - (Za hapa)

Mwenyekiti " Eswe chili bhahanga"- (Sisi wazima)

Mwenyekiti "Karibu"

Mama "Ahsante"

Yule mwanamke alikaa kando kwanza Mwenyekiti amalizane na watu wengine aliyowakuta pale ofisini ndipo azungumze nae.Baada ya Mwenyekiti kumalizana na watu waliokuwa pale ofisini walianza mazungumzo na yule mama ambaye aliitwa Veronica.

Mwenyekiti "Mmh ! Mwalimu niambie"

Mwalimu Veronica "Hivi Mazera mbona sikuhizi gari la uchafu halipiti huku mtaani kwetu!?"

Mwenyekiti "Kwani kwenye kikao juzi ukuhudhuria?"


Mwalimu Veronica "Mi nilikuwa Tarime huko bheeee!"

Mwenyekiti "Basi nadhani utaongea na mjumbe wako"

Aliendelea "Walisema zile gharama za mwanzo zilikuwa ndogo kulinganisha na mahitaji ya vifaa,hivyo mapemdekezo ni kila kaya angalau ilipe elfu moja na mia tano kwa mwezi"

Mwalimu Veronica "Tutakoma mwaka huu,kila kitu kimepanda,yaaani!"

Aliendelea "Tuachane na hayo,nadhani haka ka binti unakaona"

Mwenyekiti "Ndiyo"

Mwalimu Veronica " Wakati natoka Tarime nimekutana nae kwenye gari lakini hakuwa sawa,nilipojaribu kumuuliza inaonekana amekimbia ukeketaji ambao wazazi wake ndiyo walikuwa mstari wa mbele kulazimisha"

Aliendelea "Sasa amedai huku Musoma yupo Mjomba wake,tulipofika nikaona nimchukue kwanza niende nae kwangu kwasababu bado ni binti mdogo,akimpata huyo mjomba wake basi atakuja kumchukua"


Mwenyekiti "Aisee"

Aliendelea "Unaitwa nani binti?"

Bhoke "Naitwa Bhoke"

Mwenyekiti "Unaitwa Bhoke nani?"

Bhoke "Bhoke Mnanka"

Mwenyekiti "Tarime mnakaa sehemu gani?"

Bhoke "Tunaishi Magoto"

Mwenyekiti "Nilijua tu,vijijini ndiyo bado kuna huu ujinga,pamoja na serikali kupiga vita ukeketaji lakini bado hawasikii"

Aliendelea "Mjomba wako unamfahamu?"

Bhoke "Ndiyo"

Mwenyekiti "Anaitwa nani?"

Bhoke "Anaitwa Mjomba Magubo"

Mwenyekiti "Unapajua anapoishi?"

Bhoke "Sijawahi kuja kwake"

Mwenyekiti " Mwalimu hili suala ni zito lakini pia ni jepesi kwa upande kama serikali,ni zito kwa maana kwamba huyu mtoto kama amekimbia ukeketaji itakuwa ni ngumu kwake kurudi kwa wazazi wake kwasababu kama tuwajuavyo wale mabwana,huyu atakeketwa,lakini kwa upande wetu ni jambo jepesi kwa maana kwamba hao wazazi wake wanapaswa kutiwa nguvuni kwasababu serikali ishatoa muongozo kuhusu ukeketaji kwa mabinti"

Aliendelea " Lakini pia nitawasiliana na Afande Getruda anayesimamia polisi jamii upande wa dawati tuone namna ya kumsaidia huyu mtoto"

Mwenyekiti " Pia pale Mkendo jirani na kanisa la Roma kuna ofisi za Save the Children of Musoma,hawa huwa wanawasaidia sana mabinti waliokimbia kuozeshwa na walisalimika na ukeketaji"

Aliendelea "Nadhani pia watapaswa wajulishwe itakuwa vema wakatoa msaada wao kwasababu wanawasomesha mabinti wengi tu"

Mwalimu Veronica "Sawa,kwahiyo nikae nae hadi mnijulishe au!"

Mwenyekiti "Hebu subiri kabla hujaondoka nimpigie Afande Getruda kwanza"


Mwenyekiti alifanya mawasiliano na yule Askari ambaye ndiye alikuwa akishughulika na masuala ya dawati;Aliambiwa huyo mtoto siku itakayofuata waandamane na mwalimu Veronica hadi kituo kikuu cha Polisi ili kuweza kupata maelezo yaliyojitosheleza.

Siku iliyofuata Mwalimu Veronica baada ya kufika Polisi,aliambiwa yule mtoto ampeleke kwenye shirika lililokuwa likijihusisha na masuala ya watoto pamoja na mabinti waliokuwa wanapitia ukatiri kwa namna moja ama nyingine.Binti Bhoke aligoma kupelekwa kwenye Shirika lilijihusisha na masuala ya watoto(SAVE the CHILDREN) yeye aliomba akae kwa Mwalimu Veronica.

Mwalimu Veronica kwakuwa alikuwa akifundisha shule ya Msingi Mwisenge wakati huo,alimtafutia Bhoke nafasi ya kuendelea na shule.

Baada ya kumaliza elimu yake ya shule ya msingi,Bhoke alimwambia mwalimu Veronica ya kwamba ingekuwa vema akarudi nyumbani kwao kijijini Magoto ili kuwasalimia wazazi wake wakati huu ambao alikuwa akisubiria matokeo ya kujiunga na shule ya Sekondari kwakuwa ni takribani muda ulikuwa umepita,Mwalimu alijaribu kumwambia kama itawezekana waondoke wote ili hata kama kungetokea jambo baya iwe rahisi kupata msaada.

Bhoke "Wala usijali mama,nitakwenda na nitarudi,naenda tu kumuona mama yangu"

Mwalimu Veronica "Sawa mwanangu wewe nenda na kama ukiona bado wanafikra za zamani hurudi haraka,tayari ushakuwa binti mkubwa naamini unafahamu baya na jema"

Bhoke "Nimekuelewa mama"

Bhoke alianza safari ya kurejea tena Tarime katika kijiji cha Magoto kwa ajili kuwaona wazazi wake hasa mama yake mzazi.

Alipofika nyumbani kwao kila mmoja alimshangaa namna alivyokuwa amenenepa kwa kipindi kifupi vile.Mama yake alipomuona binti yake alilia kwa furaha na alitaka kufahamu kwa muda wote huo alikuwa wapi.

Mama Mseti "Kwahiyo omona wane muda wote huo upo Musoma"

Aliendelea "Uliutesa sana moyo wangu!"


Bhoke "Kaka Mseti na Mnanka mdogo wako wapi?"

Mama Mseti "Mseti si yupo kwake huko ila kaka yako Mnanka yeye anasema amepata kazi Mwanza"

Bhoke "Baba Je!"

Baada ya Bhoke kumuulizia Baba yake,mama yake alianza kulia tena,alilia kiasi kwamba Bhoke nae akaanza kulia.

Mama Mseti " Baba yako alifariki mwanangu"

Taarifa ile ilikuwa ni mbaya kwa Bhoke kwani iliuchoma moyo wa Bhoke kisha akaanza kutililikwa machozi,ingawa Baba yake alikuwa ni mtu ambaye alikuwa mkali siku zote lakini Bhoke hakuacha kumlilia Baba yake kwasababu licha ya mambo yote lakini alimpenda kama Baba.

Bhoke "Alikuwa anaumwa?"

Mama Mseti "Aliuawa"

Bhoke "Mlimzika wapi?"

Mama Mseti "Alizikwa kule Shambani"

Bhoke na mama yake waliondoka kuelekea kwenye shamba lao la familia ambako Baba yake alizikwa huko,Bhoke alihitaji kwenda kutazama kaburi la Baba yake ili ajiridhishe kwamba ilikuwa kweli Baba yake alikuwa amefarariki.Alipofika Shambani na kuliona kaburi la Baba yake kilio kilianza upya yeye na mama yake.

Kwa muda wote ambao matokeo yalikuwa hayajatoka Bhoke ilibidi asimame kama binti mkubwa ndani ya boma la bwana Gisiri Mnanka,maisha hayakuwa rahisi lakini alipambana kuhakikisha mama yake anakuwa na furaha.

Matokeo yalivyotoka binti Bhoke akawa amefaulu kwa daraja la kwanza na alipangwa Kwenda katika Shule ya Sekondari ya Arusha(ARUSHA GIRLS HIGH SCHOOL).


Itaendelea.........
 
Back
Top Bottom