Mnafiki Wa Kujitegemea
JF-Expert Member
- Dec 30, 2022
- 4,723
- 7,795
Omsigaji (Ujitani), Umughaka (Ukuryani).
Pamoja.
Pamoja.
Endeleee kijana mm bado sijaanza kufanya review ila very soon nitaweka kambi hapa tutapambne vzr ole wako ucheleweshe ndio utajuwa hujuiAkinyi Must Die (Ni lazima Akinyi Afe) - 05
Sauti ya kike "Kama nilivyo ahidi kwenye kikao cha kwanza,nitahakikisha kila kitu kinakwenda sawa"
Aliendelea "Malipo yenu nitamwambia muhasibu awaingizie kwenye akaunti muda siyo mrefu"
Sauti ya kike "Ok nadhani tutawasiliana"
Sauti "Sawa Madam"
Sauti ya kike "Halafu Amigo ukitoka nje naomba uniitie Mudy"
Amigo "Sawa "
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya mwanamke mmoja wa makamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiselikari la JERUSALEM IS OUR HOME(JoH)lililokuwa likijihusisha na Utoaji wa misaada kwa watu wasiojiweza.
Alipenda sana watu na watumishi wenzie wamuite Madam Suzy lakini jina lake halisi alifahamika kama Suzanne Mtigandi Galabi.Watumishi wenzie walimuogopa kutokana na misimamo yake na alikuwa si muongeaji sana bali alikuwa ni mtekelezaji tu.
Ni katika makao makuu ya ofisi za kampuni yake yaliyopo Jijini Mwanza katika wilaya ya Ilemela ndipo mara zote alikuwa akifanya vikao na wahusani pamoja na watu wake wa karibu.Safari hii alikuwa na kikao na jamaa watatu ambao aliwapa kazi ya kuifanya na alikuwa akipokea mrejesho wa kazi yenyewe.
Mudy "Yes Madam"
Suzanne "hebu rudishia huo mlango vizuri!"
Aliendelea "Sasa naomba unisikilize kwa makini jembe langu"
Suzanne "Roby amenipa taarifa kuna jamaa wana mzigo wa dhahabu hapo Geita na taarifa zilizopo wamepata escoti ya G4s kuuleta hapa Mwanza kwa ajili ya kuuzwa,nimezungumza na askari wetu ambao tunashirikiana nao nahitaji mkafanye ambush haraka,bado naendelea kuwasiliana na Roby na nitaomba uondoke wewe na Kerry"
Mudy "Sawa Madam,ni leo hii au"
Suzanne "Yeah Jamaa wanaleta leo,siunajua Roby ndiye infomer wetu kule,sasa kabla hawajafika Mwanza kamalizeni shughuli"
Mudy "Sawa Madam nimekupata"
Suzanne "Mchukue Kerry muondoke,chukueni hiyo Prado nyeusi na muwe makini"
Mbele ya macho ya watu lile shirika la JoH lilikuwa likijifanya kutoa misaada kwa watu wenye matatizo mbalimbali lakini ukweli ni kwamba,nyuma ya pazia kuna mambo ya hovyo yalikuwa yakiendelea ikiwemo kuutoa wa uhai wa binadamu ili kujipatia fedha haramu.Suzzane Galabi aliyekuwa akionekana muungwana mbele za watu hakuwa hivyo kama watu walivyodhani,alikuwa ni mwanamke mwenye uchu na tamaa ya mali za wenzie kupita maelezo.
Kwenye ile Prado kulikuwa na watu wawili ambao kimuonekano usingedhani ni mafia waliokubuhu;ile gari ilikuwa ikiendeshwa na mwanamke mzuri na mrembo aliyejulikana kama Kerry na pembeni yake alikaa Mudy ambaye alikuwa akiaminiwa sana na Suzanne.
Ile gari ilipofika maeneo ya Usagara ilisimama kisha wakapanda jamaa wawili ambao mmoja wao alikuwa amebeba begi la kuning'iniza mkononi.Baada ya jamaa kupanda ile gari iliondoka kuitafuta Kigongo ferry ili wavuke.Baada ya kuhakikisha wamevuka salama upande wa pili,ile gari iliondoka kwa spidi uli kuwahi katika utekelezaji wao huo wa mpango haramu,walipofika Sengerema katika kijiji cha Igaka kwa mbele,waliamua kuweka kambi hapo.
Walifanya mawasiliano na Roby ambaye alikuwa Geita kama infomer wa Madam Suzanne na kujihakikishia ya kwamba zile gari zimeshatoka na zikaribia maeneo waliyokuwepo wao.
Baada ya kupewa taarifa hiyo,mmoja wa wale jamaa wawili alifungua lile begi lililokuwa na nguo upande wa juu na chini lakini katikati kulikuwa na silaya 2 aina ya SMG,walitoa zile silaha na kuwa tayari kwa ajili ya shambulizi.
Ilikuwa ni mida ya saa 9 alasiri milio ya risasi ilianza kurindima katika njia ile ambayo hakusogea mtu bali zilisikika sauti za vishindo vikubwa,baada ya kufanikiwa kwenye shambulizi lao hilo walichukua mzigo wa dhahabu na kutokomea.Suzzanne na vijana wake walikuwa hawapati usumbufu kabisa kwasababu wakuu wengi wa Idara katika jeshi la polisi alikuwa anakula nao sahani moja,akipatacho basi walikuwa wakigawana ili kila mtu afe na chake,ilikuwa ni toa nikulinde ukipata nimepata.
---------------
Mara zote Bhoke alipokuwa akifunga shule iwe likizo ndogo au kubwa alikuwa akikaa kwa mwanamke ambaye alizaliwa na Mwalimu Veronica tumbo moja,Mwalimu Veronica yeye alikuwa mkubwa kwa mwanamke huyu ambaye alikuwa akijishughulisha na biashara ya Samaki pamoja na Dagaa kuwatoa Musoma na kuwapeleka Arusha,bhoke alikuwa akimuita mwanamke huyu Mama Mdogo.
Baada ya kuhitimu masomo yake ya kidato cha sita hali haikuwa nzuri,alipata matokeo ambayo yasingemwezesha yeye kupata mkopo wa chuo bali alipaswa gharama zote za chuo ziwe juu yake,kutokana na ugumu wa maisha wa nyumbani kwao,Bhoke aliamua asiende chuo bali aingie mtaani kujichanganya na vijana wenzie kuisaka riziki,binti Bhoke alijikuta safari hii ameangukia kwenye uchimbaji wa madini aina ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee eneo la Mirerani.
Kutokana na ile kariba ya Kikurya iliyomjenga tangu mdogo,Bhoke hakupata tabu sana kuungana na wana apolo wengine katika maduara na kuanza kuchoronga miamba ili kujipatia riziki.Ingawa alikuwa ni binti mrembo sana ambaye tangu udogo wake hadi kukua kwake hakuwahi kumjua mwanaume,aliamua kuishi kikauzu na kampani yake muda mwingi ilikuwa watoto wa kiume.
Kila mwanaume alipokuwa akimtazama Bhoke aliishia tu kumtamani na hakukuwa na uwezekano wa kumpata kwasababu katika kuwa yake hakutaka kabisa masuala ya kujihusisha na wanaume,wanaume ambao walikuwa watu wake wa karibu mwanzo walipata taabu kutokana na uzuri wake lakini walipomzoea akawa mshikaji wao wa kufa na kuzikana.
Siku kubwa kabisa ya kusherehekea siku ya mfanyakazi duniani ijulikano kama mei mosi ilikuwa ikifanyika Arusha,taasisi pamoja na mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yalikutanika kwa pamoja na kusherehekea siku hii muhimu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapo.
Simon " Wanangu mnajua Tripple A kesho TmK Wanaume Family ndani ya nyumba"
Wenzie "Hiyo haina kufeli babuu huko lazima twende"
Bhoke "Kleruu ameenda wapi?"
Simon "Jamaa atakuwa ameenda kwenye masanga kama kawaida yake"
Bhoke "Asije akaenda kuhonga malaya zake hela yangu mbwa yule"
Simon "Unamdai?"
Bhoke "Hela yangu ya mzigo wa jana hajanipa"
Simon "Andika maumivu"
Bhoke "Asiponipa najua wapi nitakapomkamatia,atanipa tu labda amenisahau!"
Walipomaliza kufanya shughuli zao siku hiyo walikubaliana kesho wangeondoka kuelekea Arusha kwa ajili ya kuwaona TmK wanaume family kila mtu alikuwa na shauku ya kwenda kumuona Sir Nature na kundi lake ambalo kwa wakati huo ndiyo ilikuwa habari ya mjini.
Itaendelea..............
Kala ban sasa sijui ni ya muda ganIs it me naona vibaya au ndugu yetu mleta story kapigwa ban?
kweli Akinyi must die. .Kala ban sasa sijui ni ya muda gan
😂 akili zako bhanakweli Akinyi must die. .
wegero kwetu yaani kuna roho fulani hivi inakusakama.Kuna kisa nasimulia huko kwenye jukwaa la Hoja Mchanganyiko,nikimaliza narudi tena na huku,kila sehemu ni muhimu wakuu
[emoji23]kweli Akinyi must die. .
Umeona ID yake?😀😀😀wegero kwetu yaani kuna roho fulani hivi inakusakama.
Roho gani mkuuwegero kwetu yaani kuna roho fulani hivi inakusakama.
Ina shida ganiUmeona ID yake?[emoji3][emoji3][emoji3]
Irritating spiritRoho gani mkuu
Kama ndio kaingia Town leoUmeona ID yake?😀😀😀
Si mchezoUmughaka Yuko banned huenda ndio maana haonekani!
View attachment 2577424
Nina hamu sana kufahamu kilichosababisha UMUGHAKA kula ban! Kwani, huwa sizioni "vurugu" zake hapa JF. Inaweza ikasaidia na wengine tusipite njia hiyo, ambayo imemponza yeye!Umughaka Yuko banned huenda ndio maana haonekani!
View attachment 2577424
Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa soma hii hadi jumatatu itakuwa inaishaYes,labda iishe ndio uanze. Poker alikuwa na story nzuri sema akasepa akaacha watu wanalia