Akina dada mpunguze kuomba omba

Akina dada mpunguze kuomba omba

Habari za asubuhi wana MMU. Nimeona nitoe darasa kidogo kwa baadhi ya akina dada wanaopenda vya mteremko.
Ni hivi; kuna wadada(baadhi ila ni wengi wao) wanapenda kuombaomba pesa kwa watu wasiowafahamu vizuri! unakuta anafanya kama anatania kumbe ndio hivyo tena. Hii huwa inanitokea sana, huwa nashangaa mtu sina ukaribu nae wowote anakuja kuniambia nimpe hela akale chips wakati mimi mwenyewe napiga miayo tu, huwa najiuliza hivi hawajui kuwa wengi wetu pesa ni tatizo?
Acheni hiyo tabia.

Mkuu ungewauliza pia ni kwa nini wanahusisha mapenzi na pesa wakati wote tunanogewa na wote tumepewa bure? Yaani usipompa atakuchukia milele!
 
Na wewe mnyime kama unatania tania hivi, hapo mtakuwa mmefika kwenye equilibrium..

Mimi nikiona wanataka kupiga kirungu huwa nawawahi, namwambia dah, njaa inauma. ataniuliza si uende kula, namwambia hela sina.
 
Konda wa bodaboda lazima una pesa za kumsaidia dada chakula - hajaomba makubwa - ni cha tumbo tu.
 
Konda wa bodaboda lazima una pesa za kumsaidia dada chakula - hajaomba makubwa - ni cha tumbo tu.

Hiyo ni kuendekezana tu, watu wanaoombaomba ni wengi, halafu inakuaje mtu uwe na smart phone ya laki tatu halafu hata vocha iwe tatizo? kila siku wanaenda saluni na kuoshwa kucha wakati watu tunakaa miezi sita bila kunyoa ili kubana matumizi.
Konda wa bodaboda.
 
Last edited by a moderator:
wanaume wa siku hz walalamishi....!kkaaaah!sijui mnataka nini?
 
Back
Top Bottom