Mambo ya kazini ni ya kazini na ya nyumbani ni ya nyumbani. Pia katika hili hapo hapakuwa na ndoa imara, unapokuwa kwenye ndoa lazima umpende mwenzako katika shida na raha, upendo hauhesabu makosa, mabaya nk. Alitakiwa kukaa chini na kuongea na mwenzi wake na kumwombea kwa Mungu aachane na yote mabaya ya kazini na huyo kimada. Hakika kwa uzembe wetu na papara tunaziweka ndoa zetu katika mazingira magumu na pengine hata kuzivunja.
Tutende mapenzi ya Mungu daima katika maisha yetu ya kila siku, na pale tunapokosea tulekebishane maana sisi sote ni binadamu wa kawaida na tunaishi na mapungufu yetu na Mungu daima anatupenda tumrudie yeye.
Hasira hasara, imeandikwa (uwe na hasira lakini usitende dhambi), na tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi na uchafu.