Aki na ukwa kutua dar valentine day


Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
38,378
Likes
7,310
Points
280

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
38,378 7,310 280
WASANII maarufu wa nchini Nigeria, Aki na Ukwa wanatarajia kutumbuiza katika tamasha la watoto yatima, na wale wanaoishi katika mazingira magumu Februari 14 mwaka huu.

Akizungumzia tamasha hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi inayoshughulikia masuala ya elimu kinadharia Clement
Kambengwa amesema kuwa tamasha hilo linatarajiwa kufanyika siku ya wapendanao katika viwanja vya TTCL, Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Aki na Ukwa watakuwa nchini kwa lengo wa kucheza na kufurahi na watoto mbalimbali wahishio kwenye mazingira magumu.

Watasindikizwa na wasanii wengine wa ndani wanaotarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Ze Comedy, Q-Chief, Mr.Nice, Rose Mhando na Mrisho Mpoto.

Vijana hao Chinedu Ikedieze (Aki), Osita Iheme (Pawpaw au Ukwa) wamejizolea umaarufu mkubwa kwenye tasnia ya filamu kwa kuingiza kama watoto watukutu na wasiosikia.

Wamefanikiwa kuanzisha taasisi yao ijulikanayo kama “Aki and Paw Paw Foundation."Kwa lengo la kusaidia vijana na watoto Nigeria wahishio kwenye mazingira magumu.

Wakati mwingine wamekuwa wakisafiri sehemu mbali mbali kwa lengo la kusaidi watu waishio na virusi vya Ukimwi, watoto walioathirika na HIV pamoja na watoto yatima katika sehemu mbalimbali Afrika.

Kambengwa amesema lengo la tamasha hilo ni kujaribu kuwaonyesha upendo watoto hao, pamoja na kuzindua rasmi tamasha hilo maalumu ambalo litakuwa linafanyika kila mwaka.

Amesema kuwa jamii inadhani watoto yatima huwa wanahitaji malazi, mavazi na chakula pekee kumbe wanahitaji zaidi ya hivyo.

Hata hivyo amesema vituo vingi vimekuwa na ufinyu wa maeneo ya michezo, hiyo imewalazimu Asasi hiyo kujikita katika kuhakikisha yale yote ambayo vijana wengine wanapata na wao wanapata kupitia michezo na ziara za kielimu.

Pia tamasha hilo litashirikisha vituo vyote vya kulelea watoto yatima kutoka katika Wilaya zake za Kinondoni, Temeke na Ilala, pamoja na baadhi ya shule zitakazoaliwa ili kuwajumuisha na vijana wenzao.
"Kila kituo, shule watapaswa kutoa washiriki 20 tuna watoto walengwa ni umri wa miaka 14 tu, kuwa juu ya umri huo watapaswa kuchangia ili washiriki,"amesema Kambengwa.
 

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
3,673
Likes
30
Points
0

Sajenti

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
3,673 30 0
..Good..Vile vijamaa huwa vinanifurahisha sana kwenye sinema zao...Mwisho lazima viharibu...!! Karibuni
 

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Messages
40,146
Likes
4,630
Points
280

Katavi

Platinum Member
Joined Aug 31, 2009
40,146 4,630 280
Hapa sasa inabidi comedians wa Tz wapate wasaa wa kujifunza kutoka kwa tule tujamaa.
 

blackpepper

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
382
Likes
2
Points
33

blackpepper

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
382 2 33
Pdidy umesema hawa vijana machachari watasindikizwa na Ze comedy....fafanua ni hawa ze comedy watakaofanyiwa usaili New World Cinema kwa ajili ya EATV???au ni wale Orijino Comedy wa TBC
 

Forum statistics

Threads 1,203,875
Members 457,010
Posts 28,132,902