Tamasha la Cigogo labeba ujumbe wa maadili mema kwenye jamii

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana amefungua Tamasha la 14 la Muziki wa Cigogo Julai 22, 2023 Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma ambalo limebeba ujumbe wa kuhimiza jamii kufuata maadili mema na kuepuka vitendo viovu ikiwemo ubakaji, madawa ya kulevya na ukatili wa kijinsia.

Waziri Chana amesema Matamasha kama hayo yanaleta watu pamoja na kurithisha, kuendeleza na kukuza mila na desturi za jamii husika, huku akisistiza kuendelea kuboresha zaidi tamasha hilo kwa mwaka ujao.

"Naelekeza jamii kupitia makabila mbalimbali kuiga mfano huu wa kabila la Wagogo, wizara ipo tayari kutoa ushirikiano kwakua matamasha kama haya yanasaidia kufikisha ujumbe kwa haraka na kutoa burudani kwa jamii" amesema Chana.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Gift Msuya amempongeza waandaaji wa tamasha hilo kwa kuleta Tamasha hilo ambalo linatoa nafasi kwa wafanyabiashara kunufaika, lakini pia akihimiza watoto pamoja na washiriki wa tamasha hilo kuwasisitiza watoto waendelee na masomo yao.

Awali Mwanzilishi wa tamasha hilo ambaye pia Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana amesema lengo la Tamasha hilo ni kuendelea kuenzi Utamaduni wa wagogo pamoja na kutoa elimu kwa jamii hiyo ikiwemo umuhimu wa elimu, kupinga vita rushwa na kuburudisha.

Tamasha hilo limeshirikisha vikundi 40 ambapo 34 ni kutoka Dodoma na sita vinatoka nje ya nchi vikiwa na wasanii takriban 900.

IMG-20230722-WA0071.jpg
 
Back
Top Bottom