BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
Akirudisha namba imekula kwenu kwa kumpiga hadi kusababisha kifo chake. Waswahili walisema hasira hasara!!!!
Wana JF, siku chache kabla ya PASAKA nilitoa angalizo kuwa, watu waitumie Pasaka vema, wazazi wawaangalie watoto wao hasa wa kike n.k. Sasa kuna kabinti ka form two hapa kwetu town alikuwa amepotea tangu jumamosi usiku alipo kuwa ameenda kwenye mkesha wa Pasaka, jana kutwa nzima hakuoneka, katika kutafutatafuta, vijana wakamtonya baba wa binti kuwa mwanao atakuwa kwa Emmanuel, leo hii mida ya saa 12 asubuhi, tukavamia nyumba ya akina Emmanuel na kumkuta bado kalala na mtoto wa form two! Hapo kilichoendelea ni kipigo na kijana kapoteza fahamu na hadi sasa hajaziduka, bado yupo chini ya uangalizi maalum wa madaktari! Sasa jamani, kwanini vijana wakazanie vitoto na watu wazima (wasichana) wamejaa tele? Kwanini tunatumia sikuu tena za kiimani kukwapua watoto wa watu?