Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,577
Ajiunga CCM na kuibua siri nzito NCCR
na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa NCCR-Mageuzi taifa, Bhakome Mugeta, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akitoa tuhuma nzito za usiri wa upatikanaji wa magari na fedha zilizotumika kwenye kampeni za uchaguzi uliopita, wakati chama hicho hakikuwa na ruzuku.
Bhakome alisema hakuna kiongozi yeyote zaidi ya Mwenyekiti James Mbatia, anayejua jinsi magari hayo zaidi ya sita aina ya Land Cruiser, yalivyopatikana wakati chama hakikuwa na fedha.
Moja ya sababu iliyonifanya mimi nitoke NCCR-Mageuzi ni usiri, unauliza magari hayo na fedha za kampeni tumepata wapi, hupati majibu, usiri huu wa nini? alihoji, Bhakome.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, Bhakome alisema ameamua kujiunga nacho kutokana na kuridhishwa na jinsi CCM inavyokubali kukosolewa na kuchukua hatua.
Leo naipenda CCM, kimekuwa chama bora, kinakubali kukosolewa, kujisahihisha na kuchukua hatua, alisema Bhakome.
Alisema hali hiyo ni tofauti na kambi ya upinzani na kutolea mfano wa chama chake cha NCCR-Mageuzi kwamba kimekuwa cha kikabila, usiri, ubinafsi na sasa kimekuwa miliki ya koo.
Wewe unanijua, nimekuwa mageuzi kwa muda mrefu sana, lakini nimefika mahala nimechoka, chama hakikui, kimebaki kukumbatia ukabila, usiri, ubinafsi na sasa kimekuwa chama cha ukoo, hakuna kukosoana, alisema Bhakome.
Bhakome amekuwa ndani ya chama hicho tangu kilipoanzishwa na wakati wa mgogoro kati ya kambi ya aliyekuwa mwenyekiti wake wakati ule, Augustine Mrema na Katibu Mkuu, Mabere Marando, alikuwa upande wa Marando na ndio waliochangia kwa kiasi kikubwa kumbwaga Mrema, aliyeamua kukimbilia Tanzania Labour Party (TLP).
Wanachama wengine waliorejea CCM jana kutoka upinzani ni Naibu Katibu Mkuu wa UPDP, Haji Mbelwa.
Wengine ni Katibu wa CHADEMA, Wilaya ya Korogwe, Musa Sanyo na Katibu wa chama hicho, Bakari Rajab, Wilaya ya Handeni.
Makamba alisema hayo ni matunda ya CCM kukubali kujikosoa, kukosolewa na kuchukua hatua. Alisema CCM isihukumiwe kwa makosa ya watu wachache.
Wakati huo huo, CCM Mkoa wa Dar es Salaam jana ilifanya maandamano ya kuunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma.