Ajira zote za jeshi la polisi zianzie ngazi ya Diploma

Kama tunataka kuifanya nchi hii kuwa bora hatuwezi kuendelea kukumbatia mawazo na mitazamo ya kinyonge kama hii.
Mbona hilo lilishawekwa wazi kuwa asilimia kubwa ya majeshi yana hitaji watu wenye elimu ndogo ya form 4, kwani ndio wenye majukumu mengi kwenye majeshi kulinganisha na hao wasomi, hao wasomi huwa ni wasumbufu sana, mtu anatafuta kazi kama kujiegesha tu , huko anakosubiria penye maslahi mazuri tu pakitiki anakimbia, kingine wanakuwa wasumbufu sana kudai maslahi, mala kwenda kutaka kuongeza elimu.lakini ukimchukua form 4, hadi aje ajiendeleze apate digrii sio leo, kama ni kwata ameshapigishwa sana, na huwa wanakuwa wavumilivu.
 
Hii taarifa yako ni ya kutia mashaka sana, sidhani kama nchi ina polisi 12,000 tu
Zaidi ya Polisi 20 ni PhD holders
Zaidi ya Polisi 100 wana masters
Zaidi ya Polisi 6000 Tanzania wana digrii,
Zaidi ya Polisi 1000 wana diploma
Zaidi ya Polisi 4000 ni form VI
Waliobaki ndo form iv na Std VII wasiozidi 500 kwa sasa.
Kama unaona polisi wanafanya vibaya si kwa sababu wote hawana Elimu, ila ni kwa sababu si chombo huru toka kwenye mikono ya wanasiasa. Hao uliosikia wameteliwa Jana wanakwenda kutoa amri kwa Polisi kufanya chochote wanachoona wao kinafaa, na kama OCD husika hajiongezi ndo utakuta madudu na mafyongo kama ya Kaliua juzi ambako DC anasema "familia ilipanga mtoto wao afe kwa moto ili kuikomoa serikali".
 
Hii taarifa yako ni ya kutia mashaka sana, sidhani kama nchi ina polisi 12,000 tu
Uwe mwelewa basi, nimekwambia katika kipengele cha mwisho;
Waluobaki ni form IV na Std VII wasiozidi 500, yaani sijataja form IV wako wangapi ila la saba waliobaki Polisi hawazidi 500 maana waliacha kuajiri std VII tangu 1998.
 
Tuna wasomi wengi wa Degree na Diploma,
Waajiriwe hao kwenye nafasi zote.
Police kuna graduate wa kutosha na dip nyingi sana.
So kwenye mgawanyo wa majukumu lazima F4 nao wawepo
 
Kama tunataka kuifanya nchi hii kuwa bora hatuwezi kuendelea kukumbatia mawazo na mitazamo ya kinyonge kama hii.
Sio nchi hii tu, mbona ni nchi nyingi tu za kiafrika?!hata mwaka jana kenya walitoa tamko
Zaidi ya Polisi 20 ni PhD holders
Zaidi ya Polisi 100 wana masters
Zaidi ya Polisi 6000 Tanzania wana digrii,
Zaidi ya Polisi 1000 wana diploma
Zaidi ya Polisi 4000 ni form VI
Waliobaki ndo form iv na Std VII wasiozidi 500 kwa sasa.
Kama unaona polisi wanafanya vibaya si kwa sababu wote hawana Elimu, ila ni kwa sababu si chombo huru toka kwenye mikono ya wanasiasa. Hao uliosikia wameteliwa Jana wanakwenda kutoa amri kwa Polisi kufanya chochote wanachoona wao kinafaa, na kama OCD husika hajiongezi ndo utakuta madudu na mafyongo kama ya Kaliua juzi ambako DC anasema "familia ilipanga mtoto wao afe kwa moto ili kuikomoa serikali".
Acha kupotosha hizo takwimu zako sio sahihi, haiwezekani wenye digrii wakawa wengi kuliko form 6!!na form 4,
 
Sio nchi hii tu, mbona ni nchi nyingi tu za kiafrika?!hata mwaka jana kenya walitoa tamko

Acha kupotosha hizo takwimu zako sio sahihi, haiwezekani wenye digrii wakawa wengi kuliko form 6!!na form 4,
Hivi wingi wa wenye digrii kuliko form iv unautoa wapi? Kuhusu form Vi kuwa wachache kuliko degree hilo halina ubishi sababu wengi wamejiendeleza kufikia degree.
 
Polisi/jeshi ni kazi za amri na sio kazi za kutumia akili nyingi, mtu yeyote mwenye akili timamu, mkakamavu na mwenye uzalendo anaweza kua polisi/mwanajeshi.
... kama nimekuelewa unamaanisha ni kazi isiyohitaji kutumia akili au ubunifu zaidi ya "kushikiwa akili" na boss; mhusika anabaki kuwa msukule au roboti tu la utekelezaji! Hatari sana kaz za aina hii.
 
Hivi wingi wa wenye digrii kuliko form iv unautoa wapi? Kuhusu form Vi kuwa wachache kuliko degree hilo halina ubishi sababu wengi wamejiendeleza kufikia degree.
Mkuu hilo sio kwamba nalisema mimi bali ni kauli ya aliyekuwa naibu waziri wa mambo ya ndani MASAUNI, alipoulizwa bungeni, ni kwanini ajira za polisi zinapotoka wengi ni wenye sifa za form 4, kuliko , wasomi!!akajibu kuwa ndio watendaji wakubwa wa shughuri za kila siku, tena sawa watu wanajiendeleza lakini ukweli bado uko pale pale, form 4, form 6, ndio wengi zaidi na sio polisi tu, ni kwa majeshi yote nchini, na ndio maana hata kupata nafasi ya kujiendeleza ni shughuri pevu sana, kwani wao wanaona ni kwa faida yako zaidi kuliko taasisi!!na sio Tz, tu hata kenya mwaka jana serikali ilibidi itoe tamko kabisa kuwa wasomi hawahitajiki sana, kwani ni wasumbufu wanataka kazi za ofisini tu, ambazo kwa jeshini ni chache, na wanataka kupanda vyeo haraka haraka tu!!
 
Ili kuboresha utendaji na weledi wa jeshi la polisi nchini ni vyema serikali ikaweka kigezo cha elimu kama kipaumbele kwa ngazi zote za polisi.Hii ni kutokana na umuhimu na unyeti wa kazi za ulinzi wa usalama wa raia na mali zao.

Waajiriwe vijana waliomaliza diploma, digrii na masters tu katika jeshi la polisi. Hakuna sababu tena ya kuendelea kuajiri watu ambao hawajafika kiwango hicho cha elimu kama tunajinasibu tunaipa elimu kipaumbele katika nchi yetu, pia vijana wa ngazi hizo za elimu wamejaa mitaani wakizurura na bahasha zao kutafuta ajira na wengine wameanza kuendesha boda boda kitu ambacho ni matumizi mabaya ya rasilimali watu.

Tulifanye jeshi la polisi kuwa la kisasa kwa kuipa elimu kipaumbele katika ajira zake kwani inawezekana.
Itakuwa poa sana,hakuna haja ya kuajiri kijana wa form six wakati vijana wenye diploma,shahada,mpaka za uzamili wapo kibao,hii ifanyike kwenye majeshi yote,itaruondolea vijana mbulula waliojaa kwenye majeshi ambao hawana wanachokijua zaidi ya ubabe kwa Raia tu
 
Tuzingatie elimu kuboresha jeshi letu la polisi
 
Back
Top Bottom