Ajira za TRA tumetoboa. Ushuhuda wangu!!

Ajira za TRA tumetoboa. Ushuhuda wangu!!

Mdogo wangu wa kike hatimaye amepata Ajira TRA. Tunamshukulu sana Mwenyezi Mungu na serikali yetu Tanzania!!! Kwani Ajira zimekuwa changamoto sana sahivi!!!!!!

Iko hivi, hiki kitu kilikuwa msalaba mzito sana mgongoni kwangu...kwani..Huyu dogo toka yuko form2...., Ni jukumu langu na kibaya zaid' hata alipomaliza form Six.....Huko chuo alikosa mkopo!!

Just imagine... baba nguzo kuu ya familia alistaafu utumishi 2014....Fedha ziliyayuka tuu.....

Mama Ni mama wa nyumbani ndugu zangu wengine wanaunga unga tu....

Kwa hisani yake Mola, nilipomaliza shule 2012(Form4,) sikukaa sana home nikajichanganya huku na kule na zali la kwenda kulitumikia taifa Serikalini likaniangukia.

Na hatimae mnyororo wa umasikini tukaupunguza, na nisingeweza kumuacha mdogo wangu ikiwa O level kapiga 2.... Na Six amebutua vizur tu.

Nilijibana bana.....tukaanza Kama mchezo huku wazee wakinipa baraka zote nikae nae.....na hakuna ndugu aliewahi hata kumuulizia mishe zake.....

Nisiwachoshe......nilipambana mpaka nilikuwa nalia sometimes, Chuo hana mkopo mara mashetani ya ukoo hayataki asome duu ..(Kulogwa)

N.B
Sijahonga popote..... Wala hatuna connection...

Ni Mola ametuona tu, Nina 27 yrs, dogo Sasa anaitafuta 24.

Na Kikubwa zaidi hela anayolipwa asee inasomeka parefu kuzid mim huku.

Goz is Good in all ze tym:...
Naomba nimuoe mdogo wako😉
 
maneno mazito sana haya umeongea, ni kweli tupu!

mi nashauri hili kwa mtoa mada; kamshauri huyo mdogo wake kutumia mshahara wake wa kwanza katika kutoa sadaka kwenye nyumba ya ibada kama shukrani kwa Mungu na ombi la kubariki kipato chake kiwe chenye baraka tele......wengi tulikosea kwa kutofanya hili na athari tunaziona! aende nacho chote hata kama hatotoa chote, kule kitapata ulinzi wa ushetani hicho kitakachobaki mpaka vinavyofuata.

hongereni sana, ndugu yangu ni mkubwa kuliko wewe mtoa mada, lakini tangu 2015 anahangaika na hajapata ajira mpaka sasa.....kila akiomba majibu yanakuwa mabaya kwa upande wake ingawa vyeti viko safi tu. mwaka wa tano huu sasa anajitolea tu na taratiiiibu namuona anavyokata tamaa na maisha yenyewe haya. unaingia jf wakati mwingine kutaniana na watu katika mambo ya siasa n.k huku maandishi yakionekana kama unacheka au una furaha kumbe una mengi.
Mkuu hii dunia si yetu.

La muhimu Ni kumludia muumba tuu " afany sana ibada japo nafsi yake itakua na Aman hapa dunian!!!

Hizi Ajira Kama ipo ipo tuu:
 
Kwenye utawala wa haki kila mtu anastahiki kupata bila kujali dini,kabila au rangi.

Hongera mkuu kwa kumkumbuka na kumshukuru Mungu. Pia ni muhimu kukumbuka pia Rais Samia.
 
Naomba no yake nimuowe tufaidi mpunga huo Asante Shem kwa kunipa mke mwenye mshahara.
 
Naomba no yake nimuowe tufaidi mpunga huo Asante Shem kwa kunipa mke mwenye mshahara.
Acha ujinga Wewe,Mimi nilishawahi.Unataka nikushike ugoni??.Mimi sitaki shida na watu.Achana na mke wangu huyu mtarajiwa.
 
Hivi hamuwezi kuishi bila ajira dah inasikitisha sana
Ndo maisha yetu na ni haki yetu Kama ...wananch wa TZ!!!!

Licha ya hvo nimeajir vijana wawili pia katika vibiashara vyangu!!!

So kuna lingine mkuu:
 
Hongera sana ndugu 😍😍😍 pia hongera ziende kwake kwa kuweka akili kwenye malengo/ndoto zake maana mpk kufika hapo na hana mkopo kakwepa mishale mingi
 
Back
Top Bottom