Ajira mpya Wizara ya Afya

jobtz

New Member
May 8, 2021
2
5
(Ajira mpya Wizara ya Afya) May 2021.
As for MoHCDGEC announces vacancies for graduates to apply through the website www.moh.go.tz and other media like magazines based on the cadres as per employer requirements. The applicant will then apply through www.ajira.moh.go.tz and fill their information’s as per modules which are Registration, Personal Details, Educational Details, Professional Details, Experiences Details, Documents Details, and Application.

Jobs by Ministry of Health (Ajira Wizara ya Afya) May, 2021

===

MUHIMU: KWA WAOMBAJI WOTE​

Sifa za Mwombaji​

  1. Awe raia wa Tanzania
  2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 45
  3. Awe hajawahi kuajiriwa Serikalini na kupata cheki namba na endapo mwombaji atakuwa alishaajiriwa Serikalini na kupata Cheki Namba, atatakiwa kuzingatia Utaratibu wa uhamisho au kurejea katika Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe 07 Agosti, 2012.

Maombi yote yaambatishwe na nyaraka zifuatazo​

  1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa
  2. Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne/Sita
  3. Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts)
  4. Nakala ya cheti cha Usajili Kamili (Full Registration)
  5. Waombaji waliosoma nje ya Nchi waambatanishe na Ithibati (Accreditation) kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
  6. Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship)
  7. Maelezo Binafsi (CV)
  8. Picha ndogo (passport size) mbili za hivi karibuni

Maelezo ya ziada kuzingatia​

  1. Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa watumishi. Hivyo utatakiwa kuchagua eneo ambalo ungependa kupangiwa endapo utafanikiwa kupata nafasi hiyo; Aidha, hakutakuwa na kubadilisha kituo pindi utakapopata nafasi hiyo
  2. Nakala za Vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili
  3. Waombaji wanaojitolea katika mikoa mbalimbali waambatishe barua inayomtambulisha kutoka kwa Mganga Mkuu/Mfawidhi wa Mamlaka husika.
  4. Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao (online) kupitia mfumo wa kielektroniki unaopatikana kupitia anuani ifuatayo ajira.moh.go.tz
  5. Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja ofisini hayatafanyiwa kazi.
  6. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25 Mei, 2021 saa 9.30 Alasiri.

Kwa maelezo zaidi jinsi ya kutumia mfumo huu pakua maelezo haya
Instructions on how to Apply?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom