Jambo la muhimu hapo ni kujitahidi kubuni miradi mingine ya kukuongeza kipato ili kukidhi mahitaji!.
Tena uanaambiwa huyo ni meneja. Je akina sisi wa kima cha chini vp? Mshahara unatoka unaishia kulipa madeni tu
ukiweka na takrima hautoshi mkuu
Hiyo miradi utafanyia ktk ofisi hiyo hiyo ulimoajiriwa? Au unataka uweke mtu asimamie, baada ya week unakuja jf kulalamika tena kuwa nduguyo kakuchakachua? Pagumu kidogo, kuwa na kazi ya ajira na kuwa na mradi mbali na ofisi yako. Ni mchango tu, yaweza isiwe kweli kwa wengine.
Mkuu Malila kuna kitu unataka Sema hapa ila kama hutaki kufunguka zaidi.
Tushirikishane miradi ambayo kwa uzoefu yako mtu anaweza kuifanya huku akiwa na ajira na akaweza kuisimamia vyema
Ni kweli nimeshuhudia wafanyakazi wengi wakikopa na kuingiza fedha ktk miradi inayoishia kuwaneemesha watendaji/wasimamizi wa miradi husika. Hata mimi kuna mradi uliishia kuwa mradi wa kijana wangu na mimi nikawa napewa hesabu feki, ila nilishituka mapema na kubadili mwelekeo.
Mradi wa vyumba uswahilini maeneo ya mijini unaweza kuwa bora zaidi kama hutaki stress. Nimejaribu wakati fulani, kidogo ni nafuu. Tafuta kiwanja Uswahilini, jenga vyumba vya kawaida kabisa,kodisha, na kila mwaka jenga vingine. Ukifikisha vyumba 20,unaweza kuishi bila hofu sana. Au ukiwa njema kidogo, jenga godown kisha kodisha. Ipo mingi, ila kwa leo tujadili hii miwili.
unazungumzia mtu mwenye mshahara tajwa hapo juu au???

Nimekusoma sana mkuu
Nina eneo la ekari mbili segerea kama km moja kutoka gerezani, wazo la Godown litalipa kwa hiyo location?