MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 319
- 755
Wingu zito la mgogoro ndani ya CHADEMA juu ya wanaounga mkono na wanaopinga Kampeni ya No Reforms na No Election limeendelea kutanda na sasa limefikia hatua mbaya zaidi, wameshindwa kuuficha mgogoro wao na sasa wameamua kuchapana makonde kwenye mikutano ya hadhara.
Chokochoko zilianza kwenye mkutano wa Kondoa Mkoani Dodoma baada ya wafuasi wa CHADEMA wanaotaka Chama hicho kishiriki uchaguzi, kupaza sauti mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa John Mnyika wakimsisitiza kuwa wanataka washiriki Uchaguzi, kwani kususia sio suluhisho la mageuzi ya kweli ya demokrasia.
Vuguvugu hilo likahamia kwenye mkutano wa John Heche, Singida mjini baada ya wafuasi wa CHADEMA wanaotaka Chama kishiriki uchaguzi kupaza sauti tena kwenye mkutano wa hadhara wakitaka Heche aitishe kikao cha Kamati Kuu wajadili namna ya kushiriki uchaguzi, lakini Heche kama kiongozi mkuu aliyebaki hakutumia busara kuwajibu badala yake aliwapiga mkwara kuwa ataagiza vijana wawafinye hadi wapotee, maneno ambayo yaliwakasirisha wanachadema wanaotaka Chama kishiriki uchaguzi.
Mungu si Athumani, hasira za wanachadema zimeshindwa kuvumilia kiburi na matusi ya John Heche anayoyatoa hadharani na leo hii wakiwa Igunga, Heche akawaagiza vijana wake wanaounga mkono No Reforms No Election wapambane na wenzao wa CHADEMA wanaopinga No Reformd No Election.
Tangu CHADEMA ianzishwe kipindi cha Bob Makani na Mzee Mtei, Mwenyekiti Freeman Mbowe, hakijawahi kushuhudia Wanachama wakigombana wenyewe tena hadi kuumizana hadharani kwa sababu ya kupigania misimamo ya watu wachache yenye maslahi yao binafsi, lakini kipindi Uenyekiti wa Lissu na Heche yamewezekana Wanachama wanapigana hadharani, wanakosa nidhamu, na pengine mengi makubwa zaidi yanakuja.
Wito kwa Watanzania kwa sasa ni kwamba msijitokeze kwenye mikutano, muwaachie waende wenyewe maana imetoka kuwa mikutano ya hadhara imekua mikutano ya kupigana ngumi kati ya wanaounga mkono na wanaopinga No Reforms No Election.