Ajari mbaya maeneo ya Riverside Dar

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,048
1,102
Nimetoka kushuhudia ajari mbaya ambapo mtu mmoja amegongwa na pick up ikitokea ubungo mataa kwa kasi imemgonga na kichwa kupasuka ubongo kusambaa tapatapa barabarani" bahati nzuri kulikuwepo na trafick mmoja akiwa na pikipik na kuikimbiza gari iliyohusika! itc too painfull kiukweli" binafs najiuliza kulikoni eneo hili mara kwa mara hutokea ajali mbaya sana. Source mi mwenyewe nipo maeneo haya
 
maeneeo kama hayo inatakiwa vidaraja vya juu kwa ajili ya kuvukia waenda kwa miguu, lakini kwa vile serikali haiko kwa ridhaa ya wananchi, watu kufa inaona sawa tu!!
 
watu wazembe sana eneo hilo wanatembea as if wako bed room kwao....mi napasua mtu tu kama anavuka bila utaratibu

mpendwa,

sikuungi mkono unaposema kuwa "mi napasua mtu tu kama anavuka bila utaratibu" lakini nakuunga mkono kuwa watu wamezidi uzembe! na madereva nao wamezidi bangi! pale kuna njia nne, inakuwaje mtu kabla hajavuka asiangaklie kwanza magari yanakotokea? mbona huwa kuna foleni kubwa sana pale? na akiona magari yameruhusiwa anashindwa vipi kusubiri hizo dk chache hadi yasimamishwe tena?

jamani mamabo mengine yanasikitisha sana na papo hapo yanatia uchungu wa hasira! tuweni waangalifu wapendwa, madereva wetu ni walevi wa bangi na matatizo ya maisha na UDHAIFU WA SERIKALI.

hata hivyo nakiri, ajali haina kinga, ila uzembe una kinga.

tupendane na kuombeana daima

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
poleni wafiwa, ila nadhani hapa sio mahala pake,Mods tafadhali
 
Sawa kabisa uzembe wa wanaovuka nao unachangia kwa kiasi kikubwa! Mfano ajari ya leo jamaa alijifanya ana haraka wakamuwahisha zaidi!
 
maeneeo kama hayo inatakiwa vidaraja vya juu kwa ajili ya kuvukia waenda kwa miguu, lakini kwa vile serikali haiko kwa ridhaa ya wananchi, watu kufa inaona sawa tu!!

Mkuu hi project mbona ilishindikana kuwa successful?, Kama unakumbuka daraja la Manzeselilikuwa mahsusi kwa ajili hiyo, badala yake limegeuka kijiwe cha vibaka na wavuta bangi, ukipandisha kule juu ujue unaenda kuwaachia ulivyo navyo. Suala jingine ni human behaviour na hali ya hewa ya dar. Mtu anaona kutumia both potential and kinetic energies ni upuuzi bora akatize tu (only kinetic energy is used).

Design ya barabara na usimamizi wa sheria za barabarani ni mbovu. Serikali inakaa inaunda kamati za kutafuta vyanzo vya mapato na kila siku kupandisha bei ya bia na sigara wakati kuna potential ya kupata about 15% of Govnment income from law enforcement penalties. Kuna makosa yanayoikosesha serikali Tzs 400m kila siku Dar peke yake. Mfano kama serikali itaweka alama zote muhimu barabara kuanzia no parking zone, speed limits na kuajiri watu amabo kazi yao si kugombana na madereva bali ni kupiga picha za matukio na kuandika PCN (penalty charges Notice) kwa makosa ya barabarani nina hakika hii ni moja ya main source of income. Mfano unaweka sheria kuwa

1. kupaki eneo lisilotakiwa penalty ni Tzs 150,000 kama utalipa ndani ya siku 14 na itaongezeka kwa 100% simple kila mwezi kwa miaezi miwili, baada ya hapo tunakamata gari na kuliuza kupata hela yetu.Kama mtu atagoma kulipa gari lake linakamatwa na TRA na anapewa siku 14 kulipa ama kupoteza gari.

2. Speed Limit, unawapatia vijana speed cameras na kazi zao ni kuwa na gari la patrol katika kila kilometer tatu, penalty yake inakuwa ni laki tatu kwa overspeeding.

3. Vijana hawa unawalipa 20% ya makusanyo ya penalty kwa siku. Hii itainua sana utii wa sheria za barabara.

Tatizo tunahitaji short cut. Hii itasaidia sana kuongeza utii wa sheria za barabarani. Kitu kingine cha ku-discourage watu kuvuka barabara ni kuweka fensiupande mmoja kwa maeneo hatari ili atakaevuka awe na uwezo wa kuruka fensi.
 
maeneeo kama hayo inatakiwa vidaraja vya juu kwa ajili ya kuvukia waenda kwa miguu, lakini kwa vile serikali haiko kwa ridhaa ya wananchi, watu kufa inaona sawa tu!!
kwani Mbunge wenu mliemchagua hayupo kila kitu Serikali hata kuvuka barabara? Mm nawapa Pole wafiwa na RIP aliyegongwa
 
watu wazembe sana eneo hilo wanatembea as if wako bed room kwao....mi napasua mtu tu kama anavuka bila utaratibu
usiseme maneno mabaya haya. kumbuka ni jukumu letu kutetea uhai wa kila mmoja wetu. wewe unafahamu kuwa watu hapo wanatembea as if wako bedroom kwao... sasa kwanini nawe usiendeshe taratibu?. nafahamu ni ngumu kufuta hayo maneno yako kwa maandishi , hapa. lakini ninakushauri uyafute ndani ya kichwa chako na ubadilike kwaajili ya uhai wako mwenyewe na uhai wa wengine
 
Nimetoka kushuhudia ajari mbaya ambapo mtu mmoja amegongwa na pick up ikitokea ubungo mataa kwa kasi imemgonga na kichwa kupasuka ubongo kusambaa tapatapa barabarani" bahati nzuri kulikuwepo na trafick mmoja akiwa na pikipik na kuikimbiza gari iliyohusika! itc too painfull kiukweli" binafs najiuliza kulikoni eneo hili mara kwa mara hutokea ajali mbaya sana. Source mi mwenyewe nipo maeneo haya

Hizi sio habari nzuri kuzisikia au kuzishuhudia,"mwenye enzi Mungu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen".
 
Nadhani wengi wa wahanga wa hizi ajali ni stress za maisha, kuna wakati watu wanatembea lakini wako pale kimwili tu. Maana tukisingizia madereva kwa kila kosa hatutakuwa sawa, au tukitupia lawama mamlaka za kiserikali pia tutakuwa hatupo sahihi kwa asilimia kubwa, maana ukiangalia barabara zenye matuta katika nchi zote zilizotuzunguka sisi ndio tunaongoza. Maajabu hata highway za kuuunganisha mikoa ni matuta kwa kwenda mbele, hii inashangaza kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom