Mkuu hi project mbona ilishindikana kuwa successful?, Kama unakumbuka daraja la Manzeselilikuwa mahsusi kwa ajili hiyo, badala yake limegeuka kijiwe cha vibaka na wavuta bangi, ukipandisha kule juu ujue unaenda kuwaachia ulivyo navyo. Suala jingine ni human behaviour na hali ya hewa ya dar. Mtu anaona kutumia both potential and kinetic energies ni upuuzi bora akatize tu (only kinetic energy is used).
Design na usimamizi wa sheria ni mdogo, Serikali inakaa inaunda kamati za kutafuta vyanzo vya mapato na kila siku kupandisha bei ya bia na sigara wakati kuna potential ya kupata about 15% of Govnment income from law enforcement penalties. Kuna makosa yanayoikosesha serikali Tzs 400m kila siku Dar peke yake. Mfano kama serikali itaweka alama zote muhimu barabara kuanzia no parking zone, speed limits na kuajiri watu amabo kazi yao si kugombana na madereva bali ni kupiga picha za matukio na kuandika PCN (penalty charges Notice) kwa makosa ya barabarani nina hakika hii ni moja ya main source of income. Mfano unaweka sheria kuwa
1. kupaki eneo lisilotakiwa penalty ni Tzs 150,000 kama utalipa ndani ya siku 14 na itaongezeka kwa 100% simple kila mwezi kwa miaezi miwili, baada ya hapo tunakamata gari na kuliuza kupata hela yetu.Kama mtu atagoma kulipa gari lake linakamatwa na TRA na anapewa siku 14 kulipa ama kupoteza gari.
2. Speed Limit, unawapatia vijana speed cameras na kazi zao ni kuwa na gari la patrol katika kila kilometer tatu, penalty yake inakuwa ni laki tatu kwa overspeeding.
3. Vijana hawa unawalipa 20% ya makusanyo ya penalty kwa siku. Hii itainua sana utii wa sheria za barabara.
Tatizo tunahitaji short cut. Hii itasaidia sana kuongeza utii wa sheria za barabarani. Kitu kingine cha ku-discourage watu kuvuka barabara ni kuweka fensiupande mmoja kwa maeneo hatari ili atakaevuka awe na uwezo wa kuruka fensi.