Ajali ZNZ: Vodacom waanza kugomewa

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,956
1,342
Aliyesema majnga yakitokea kila kitu kinasimama?kuna watu jana wamefunga ndoa wakacelebratrete kama kawa..sasa mbona hilo amlizungumzii?Nawenyewe wangehairisha basi..

pascaldaudi

JF-Expert Member
Mar 25, 2009
534
96
Ukweli hili suala lina utata!! Ila kwa desturi na tamaduni zetu wabongo, walipaswa kucancell! maana ni msimba wa kitaifa!

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,419
12,548
Kuna sms zinatumwa na watu Unguja, Pemba na baadhi ya watu Dar kuwa Vodacom wamekuwa insensitive kufanya MISS TANZANIA on the same day Tanzania imekumbwa na janga zito.

I think kwenye hili MWAMVITA MAKAMBA amechemsha na sijui Voda watafanya nini kujitetea

Kutoa misaada haisaidii watu

Acheni ushabiki wa kiwivu na kijinga, mbona hamzungumzii chama tawala kutoahirisha uzinduzi wa kampeni zao huko Igunga. Voda wako kwenye business, afterall that is not their target market as the area is dominated by Zantel subscribers.

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,419
12,548
Kuna sms zinatumwa na watu Unguja, Pemba na baadhi ya watu Dar kuwa Vodacom wamekuwa insensitive kufanya MISS TANZANIA on the same day Tanzania imekumbwa na janga zito.

I think kwenye hili MWAMVITA MAKAMBA amechemsha na sijui Voda watafanya nini kujitetea

Kutoa misaada haisaidii watu

Acheni ushabiki wa kiwivu na kijinga, mbona hamzungumzii chama tawala kutoahirisha uzinduzi wa kampeni zao huko Igunga. Voda wako kwenye business, afterall that is not their target market as the area is dominated by Zantel subscribers.

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
13,604
23,276
Kuna sms zinatumwa na watu Unguja, Pemba na baadhi ya watu Dar kuwa Vodacom wamekuwa insensitive kufanya MISS TANZANIA on the same day Tanzania imekumbwa na janga zito.
I think kwenye hili MWAMVITA MAKAMBA amechemsha na sijui Voda watafanya nini kujitetea
Kutoa misaada haisaidii watu

Wazanzibar wengi wanatumia Zantel hivyo hiyo kampeni yao haina mashiko. Halafu hao Wazanzibar si huwa wanaupinga sana muungano?

Kwani mambo ya Miss ya Tanzia yamo katika mambo ya Muungano? Miss Tanzania ni kama suala la mafuta. Kila upande unashughulika kivyake.

Waandae Miss Zanzibar kama imewauma sana Miss Tanzania kufanyika.

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,216
1,648
Hakuna Gaidi Kweli? isije kuwa walikataa kutii amri ya al-Shaabab wakadunguliwa

Lofefm

Senior Member
May 22, 2011
128
11
Kuna sms zinatumwa na watu Unguja, Pemba na baadhi ya watu Dar kuwa Vodacom wamekuwa insensitive kufanya MISS TANZANIA on the same day Tanzania imekumbwa na janga zito.

I think kwenye hili MWAMVITA MAKAMBA amechemsha na sijui Voda watafanya nini kujitetea

Kutoa misaada haisaidii watu

ndugu yangu mbona sio hilo tu sherehe na matukio mengine mengi tu yaliendelea lakini watu mna wasema vodacom tu. Huu ni ushabiki usio na manufaa. Mnalalamikia kutokupewa msaada tukumbuke msaada ni hiyari ya watu kwa hiyo hamna sababu ya kulalamikia hilo. Let us think first

ikhwan safaa

Senior Member
Jul 24, 2011
106
27
739-ebLNM.Em.55.jpg
residents_attempt_to_identify_the_bodies_of_their__4e6bcef9cb.JPG

739-ebLNM.Em.55.jpg
DSC06056.JPG

[/QUOT]

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
283

Hii ni tweets kutoka kwa Mh. Zitto: @zittokabwe

kwani akisema Zitto ndo nini? Acheni uvivu wa kufikiri, Vodacom ni sponsors tu, waandaaji wa Miss Tanzania ni kina Lundenga na kampuni yake. Sikujua kama kuna watu vilaza kwa kiwango hichi cha kutisha, mnashindwa kutofautisha owner wa event na sponsor! Kweli mnashangaza sana!!!

Silas A.K

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
807
153
Hivi mnawajua waandaaji wa Miss Tanzania nyinyi? Anayeandaa Miss Tanzania siyo Vodacom jamani! Vodacom ni sponsors tu kwa kiswahili ni mdhamini tu siyo waandaaji.Muulizeni Hashimu Lundenga

Mwendabure

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,138
1,029
Ni lini wazanzibari wameanza kuitambua mis TZ? Nijuavyo mimi iwe siku njema au mbaya ZNZ ni marufuku mashindano hayo. Kelele za nini hapo? Tusihalalishe uovu...mis TZ ni uovu dhahiri unaopaswa kukemewa siku zote na kwa nguvu zote. Kwa mwendo huu ipo siku tutalalama wauza cocaine nao wasiuze siku za maafa. Tuipinge Mis Tz ndipo usahihi au upotofu wa voda utajiweka bayana, vinginevyo tukio hili litakuwa kipimo tosha cha upungufu wa utambuzi tulionao wa Tz ktk hili. Tulie na Mis TZ kisha voda!

SURNAME

Member
Feb 10, 2011
81
7
Tuache ushabiki wa kijinga,vodacom sio waandaaji wa miss tanzania wao ni wadhamini tu,waliotakiwa kufuta au kuhairisha tukio lile ni waandaaji ambao ni lino agent au serikali,zitto asitake umaarufu ktk hili,tena wadhamini walikuwa wengi kama redds,cfao-Dt dobbie why iwe vodacom tu?

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,488
15,184
Nimeandika makala hii nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi Mmoja hapa Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani nilitaka hisia zangu ziwe as raw as possible - Zitto Zitto and not Zitto a Politician).

Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu 2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba. Habari hazikuwa za uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii.

Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.

Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa Umma kuhusu msiba huu.

Watanzania waliokoa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za asili.

'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha kusikitishwa kwake na kituo hiki. Mpaka jioni tulikuwa tumepata taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570 hivi walikuwa wameokolewa.

Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla alipona, aliokolewa. Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni. Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa.

Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi hii kubwa ya kuokoa. Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana, ilitulia na kuonyesha uongozi dhabiti katika juhudi za uokoaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta. Akatangaza siku 3 za kuomboleza.

Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha shindano la Urembo usiku huo. Wangepata hasara! Hata wafadhili wao Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao miongoni mwa waliofariki wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano hili. Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu.

Nimeamua kutotumia simu ya ngu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba huu kwa Taifa.

Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi watawajibika au kuwajibishwa!

Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800! Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12. Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria.

Natumai mara baada ya kumaliza maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa. Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.

Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama hii.

Mwenyezimungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu wa haraka majeruhi wetu.

Zitto Kabwe.

source: Wavuti - Habari

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,404
1,228
Wewe kamanda unayeweka picha za Miss Tanzania ku-justify argument yako, unasahau kuwa kuna tukio la CCM ambalo lilikuwa aware na mkasa huu Zanzibar but viongozi wetu wa CCM hawakujali kitu?!

Mi nadhani kama ni kutoa lawama, basi tulaumu kwanza kampeni ya CCM na watu wanaohusika na nchi hii directly kabla ya mambo binafsi. Lakini sishangazwi kwani mapachoni pa wengine hili haliwezi kuonekana, kwani wanaohusika na jambo hilo ni "wenzetu"!!

attachment.php

attachment.php

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom