Ajali yaua watatu Bunju B, Dar

Ajali yaua watatu Bunju B, Dar

Juzi nimeshuhudia boda x2 a kikanyagwa na lori na kupasuka kichwa pale Mafiga Morogoro. Kumbe wanashindania alfu kumi kwa kasi ya kwenda Mzumbe na kurudi. Trafiki kusikia sababu akaona derev wa lori hana kesi akamwachia huru asubuhi hiyo bila kumweka mahabusu. Amini usiamini hao ndo natrafik ba bodaboda wetu.
 
Juzi nimesuhudia boda x2 a kikanyagwa na lorina kupaduka kichwa Rombo MafigaMoro. Kumbe wanashindania alfu kumikwendaMzumbe na kurudi. Trafiki akana hana kesi akamwachia huru dereva wa lori
 
Tumekuwa tukiona mara kwa mara waendesha bodaboda wakiwa wanaendesha rafu barabarani na wanapokumbwa na ajali huwa wanakusanyika na kuwafanyia fujo madereva wa magari huku wakiiba vitu kwenye gari husika na kulivunja vunja vioo. Serikali mpaka sasa sijawahi kusikia wakidhibiti hizi fujo kiasi kwamba kinawatia kiburi cha hali ya juu hawa waendesha boda boda. Mfano mmojawapo ni kwenye traffic lights ambako utakuta waendesha boda boda hawatii amri za maaskari wa usalama barabarani au hata taa hizo za barabarani na kupelekea kuvuka hata bila ya kuruhusiwa na wanapokumbwa na ajali basi dereva wa gari husika anakuwa matatani.

Tuulizane, ni kweli kuna madereva wa magari wanaweza kuwa nao wana shida lakini je ni haki kwa hawa bodaboda kufanya fujo kiasi hicho na kufikia wakati mwingine kuwapiga madereva na kuwadhuru na hata kuiba mali za mwenye gari ambazo zitakuwemo garini au kwenye mifuko ya mwenye gari..? Tumesikia waendesha boda boda wakikamatwa kwa makosa mbalimbali na wenzao kukusanyana na kuvamia vituo vya polisi hadi kuwatoa wenzao.. Hili kama sio bomu la fujo zisizozuilika kama zile za waendesha piki piki katika baadhi ya miji duniani ni nini..? Ni kweli serikali imeshindwa kudhibiti fujo za hawa waendesha boda boda..?

Leo katika pitapita yangu kwenye mitandao nimekutana na hilo tukio hapo chini la gari kuchomwa moto maeneo ya Bunju na sintoshangaa nikisikia ni waendesha bodaboda ndio waliolichoma hilo gari na sitashangaa kutoona hatua stahiki kutochukuliwa.

Kama kuna viongozi wa serikali au jeshi la polisi humu jamvini hebu mtushauri wananchi kwa sababu siku hizi watu wanaendesha kwa kuhofia kuwagusa bodaboda sio kwa sababu ni jukumu lao kama madereva bali kuhofia matukio kama haya..
 
Juzi nimesuhudia boda x2 a kikanyagwa na lorina kupaduka kichwa Rombo MafigaMoro. Kumbe wanashindania alfu kumikwendaMzumbe na kurudi. Trafiki akana hana kesi akamwachia huru dereva wa lori
 
So sad! kwa nini jamani tunajichukulia sheria mkononi ?

Uwa tunajifanya tuna hasira kali kwa vitu vidogo,natamani siku moja hiyo hasira kali tuitumie kuiondoa serikali inayokubali magari chakavu na pikipiki za chini ya kiwango zinazoua ndugu zetu kila uchao.

Pia ata pesa za umma za Eskrow tungezidai kwa hasira kali

Bring back our tanganyika

hizi hasira kali tungekuwa kunazipeleka kwenye mambo ya maana Tz ingekuwa sehemu nzuri sana.
 
Siipendi hii tabia ya hawa bodaboda kuchoma moto magari baada ya ajali na ukizingatia mara nyingi wao ndo husababisha ajali hizi.

Poleni wafiwa na pole kwa aliyechomewa gari yake.
 
Mhh mungu atunisuru aisee tumalize mwaka salama!!
 
Nianze na kusema sitetei watu kuchukua sheria mkononi...
Na niseme kuna umuhimu wa kuwa na silaha...

Ila nimejua kwa nini wamechoma moto gari...
Kuna uwezekano wameona mzungu analeta dharau baada ya kupiga risasi hewani...
Sasa alipoondoka na kuacha gari wakaona wamalize hasira zao kwa kuchoma gari...

Kwa kuwa ni mzungu chances are atakuwa na bima comprehensive...

Walivojaa wampige mzungu kapiga risasi juu wakasambaa kaita gari nyingine kafaulisha vitu vyake ndani kasepa bodaboda acha tu
 
Wananchi hiyo gari hamjaitendea haki ila muna hasira za kijinga kwasababu mngekuwa na hasira za kweli wezi wa escro tusingekuwa nao duniani.
 
Ningekuwepo ningemchoma moto mzungu gari nikaicha, siyapendi kweli haya majamaa, juzi yamemkaba bonge wa watu hadi akashindwa kupumua, kisa sigara, leo limechomewa gari mnalionea huruuuuma, miswahili hovyo kabisa.
 
Haha mpka mzungu amewaachia gari hapo mjue anajiamini na bima yake.. Wala hana presha..
 
Nakumbuka bodaboda waliwahi kuicoma moto iace ya mpemba pale karibu na hospitali ya IMTU madhara yake mpemba akawasomea albadili walikufa utafikiri kumbikumbi.
 
Viongozi haijali sasa kwasababu wanaoumia na kuharibiwa mali zao ni wananchi wa kawaida,wametulia kwao hawana muda kwa kujiuliza kwanini vijana hawa wenye bodaboda na wengine wanachanganyikiwa na kuchukua maamuzi kama hayo bila kuogopa serikali, hadi wengine kuingilia kufanya shughuli za ujambazi.
Wahenga wanasema usipoziba ufa utajenga ukuta,naona viongozi wamesahau kuwa mapinduzi mengi yaliyotokea hivi karibuni yamefanywa na vijana na haswa kwasababu wamekata tamaa ya maisha kwa kukosekana kwa ajira, sasa wafahamu kuwa hivi vikundi vikichoka kufanya fujo kwa wananchi, watashangaa pale watapohamia mjini kuvunja maduka, kuiba mali za watu na kufanya fujo na hapo watachodai si ajira tena bali ni mabadiliko ya serikali na watakuwa tayari kufa kama yaliotokea Tunisia.
 
kwanza hakuna kitu kidogo kwenye uhai wa binadamu. pili, mhusika alikuwa mzungu ndani ya VX na wala sio wale wa ESCROW account. na tatu wananchi walitaka kummaliza huyo mzungu lakini bahati yake alikuwa na bunduki akapiga hewani ndo wakakimbia na yeye kufanikisha kuuta gari lingine na kuweza kufanikisha kufaulisha vitu vyake, kinyume chake sasa hivi angekuwa kashawasili huko ahera.
So sad! kwa nini jamani tunajichukulia sheria mkononi ?Uwa tunajifanya tuna hasira kali kwa vitu vidogo,natamani siku moja hiyo hasira kali tuitumie kuiondoa serikali inayokubali magari chakavu na pikipiki za chini ya kiwango zinazoua ndugu zetu kila uchao.Pia ata pesa za umma za Eskrow tungezidai kwa hasira kaliBring back our tanganyika
Tanzania bhana, badala ya kuwaua wezi wa Escrow, EPA n.k tunachukua hatua kali kwa matukio ambayo athari zake zinaweza kuwahusu watu 10 tu!
Kwanini wananchi wanajichukulia sheria? pole waliofiwa na kuchomewa gari
Hawakuwemo wezi wa ESCROW?
Daah, VX?!
 
Ajali imetokea Bunju B na kuua watu watatu papo hapo ambao ni madereva wa bodaboda na VX kuchomwa moto.

Dereva wa VX katoka mzima ila gari lake limechomwa moto na wananchi.

Maiti zimepelekwa Kituo cha Polisi Bunjua A.

attachment.php
attachment.php
attachment.php


Hiyo itakuwa ni gari ya ESCROW wanapoteza ushahidi tuu.
 
Ajali imetokea Bunju B na kuua watu watatu papo hapo ambao ni madereva wa bodaboda na VX kuchomwa moto.

Dereva wa VX katoka mzima ila gari lake limechomwa moto na wananchi.

Maiti zimepelekwa Kituo cha Polisi Bunjua A.

attachment.php
attachment.php
attachment.php


Sasa Baada Ya Kuchoma Hilo VX Je Hao Waliokufa Wamefufuka au Wamerudi Kupambana Na Maisha Haya Magumu?
 
Back
Top Bottom