kwanini uwezi kumsaidia?
Kuna siku jamaa alishuhudia mwendesha boda boda anagongwa na gari ya mbele yake. Ile gari ikakimbia, yeye akasimama kumsaidia, alichokipata Mungu mwenyewe anajua. Waendesha bodaboda wenzake na aliyegongwa walivyofika hawakuuliza kama yeye ndiye kagonga au ni mtoa msaada walianza kutoa kipondo kwa msamaria mwema na gari lake likavunjwa vunjwa vioo..
Twende mbele turudi nyuma, serikali inalichekea hili tatizo la wahuni wanaoendesha boda boda na wasipokuwa makini hii nchi itajenga genge la wahalifu ambao watakuwa wanaendesha nchi kuliko jeshi la polisi huku wakishambulia wananchi bila ya kusemeshwa na mtu. Nimerudia tena hapo juu, mnapoona hawa waendesha boda boda wanafikia kuvamia vituo vya polisi na kumtoa mwenzao na wakaendelea kupeta mitaani, huku ni kuwadekeza na matokeo yake sitaki kuyafikiria.
Kama kuna viongozi humu jamvini hebu lifanyieni kazi hili swala, msisubirie mpaka kiongozi mmoja wa serikali avamiwe au hali iwe mbaya zaidi ndio mu-act.
