Ajali yaua watatu Bunju B, Dar

Ajali yaua watatu Bunju B, Dar

Ni kweli kabisa Mkuu, ndiyo sababu kila siku mpya inapoanza huku ukiwa salama na wote uwapendao wako salama inabidi kumshukuru Muumba wetu na hata siku inapoisha pia ni vizuri kumshukuru.

Dah...mtu unaweza kufikiri umemaliza mwaka 2014 kumbe bado parefu. Chochote kinaweza kutokea hapo katikati
 
kuna umuhimu wa kuwa na bastola barabarani... huyo mzungu kupiga hewani wakatawanyika .. katumia akili sana ... wabongo wengi waoga
 
pangekua na Highway pengine uwezekano wa maafa haya ungekua mdogo,sasa tatizo pesa wamezikalia akina Chenge!na zake pekee tu escrow/Rada nazingetosha kufikisha double road toka njia panda mbuyuni hadi mapinga!
 
waliochoma wanajulikana, ni vibaka in the name of bodaboda, kuna haja ya kuwalamba mvua kadhaa waache

kama kweli ni gari la serikali, then wacha tuone mkono wa serikali yetu upo au umeingia mitini na escrow
 
Bodaboda ni reserved jeshi la uasi. One day makubwa yatatokea bongoland.
 
Poleni sana wahanga. Hii tabia ya kuchukua sheria mkononi imeachwa weee mpaka imefikia hapa. Siku hizi kibaka anaweza kukunyang'anya simu na kukuambia ukipiga kelele za mwizi tunakugeuzia kibao hapo inabidi unyamaze tu. Sasa hii tabia imeota mizizi na kwa bahati mbaya hakuna anaechukua hatua. Inashangaza eti matukio kama haya yanapotokea kuna msemo huu wa wananchi wenye hasira wamefanya hivi au vile hii si sawa.

Kuna wengine huuawa kwa kupigiwa kelele za mwizi wakati mwingine si wezi bali visasi tu na kwa tabia za watu hata huwa hawaulizi kamuibia nani wao huanza tu kupiga na kumwaga petrol. Tunaomba wanaohusika wafanye wajibu wao na si kila wakati kuwaacha wananchi wenye hasira wachukue hatua kwa namna isyokua ya kawaida.
 
Bodaboda ni reserved jeshi la uasi. One day makubwa yatatokea bongoland.

Wazee kama wewe ni hasara kwa taifa hili.Yani wakati wengine tunashukuru walau huku mitaani vijana wenzetu wanabangaiza kupitia hizi boda boda,wewe povu linakutoka eti ni jeshi la uasi.
Tusiwalaumu tu hawa bodaboda tutazame kwanini walifikia kuichoma moto hiyo gari.Je dereva huyo angekuwa anaendesha kwa mwendo wa kawaida hayo yangetokea?
Nimeona wengi tu humu povu likiwatoka na kulipa gari thamani kuliko roho za watu hawa wa3,v8 sidhani hata kama askari wetu wa barabarani huzisimamisha kuzifanyia ukaguzi hata wa matairi .Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni vijana hawa hawajafa katika ile staili tuloizoea ya wao kujichomeka ,dereva wa gari angekuwa kwenye mwendo wa kawaida ingesaidia.Watanzania pia tupunguze tabia ya kuchukua sheria mkononi.R.i.p bodaboda
 
Hebu tuambie cahanzo cha ajali nini...Maana huenda landcriser ilikuwa haina makosa...Maana boda boda wengi wanakunywa viroba..

Mkuu c virobo tu akipakia mshkaki hawezi kua n balance n control hpo ndio husababisha ajali,wameshatia wa2 hasara sana kuwachomea magari yao
 
Nchi hii wananchi wake wengi ni wajinga sana, na ujinga huu ndio viongozi waomba uendelee ivivi kwa wananchi. Haya mambo ni only in Tz inapotokea ajali dereva anapigwa mpaka kuuliwa, how come? Gari kuchomwa ni ujinga mtupu sijui nani kawaroga wabongo kuwakosesha elimu
 
kuna umuhimu wa kuwa na bastola barabarani... huyo mzungu kupiga hewani wakatawanyika .. katumia akili sana ... wabongo wengi waoga

Dawa ya hao wapuuzi wa boda boda ni kutembea na "UZI" na Mkanda wake wakizunguka gari tu unaachia kama 50 hivi hewani halafu unaondoka na gari safi kuelekea kituo cha polisi kwa speed ya 40km/h tu hakuna atakayekuja kukufata.
 
Nimeona wengi tu humu povu likiwatoka na kulipa gari thamani kuliko roho za watu hawa wa3,v8 sidhani hata kama askari wetu wa barabarani huzisimamisha kuzifanyia ukaguzi hata wa matairi .Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni vijana hawa hawajafa katika ile staili tuloizoea ya wao kujichomeka ,dereva wa gari angekuwa kwenye mwendo wa kawaida ingesaidia.Watanzania pia tupunguze tabia ya kuchukua sheria mkononi.R.i.p bodaboda
Mkuu SAUTI YAKO yaani una nguvu kabisa ya kumtetea mwendesha bodaboda ambaye yeye mwenyewe thamani ya maisha yake haithaminishi sawasawa na wewe ufanyavyo? Hivi umejiuliza iweje wagongwe mkupuo kwa gari moja? Unadhani walifuatwa walipopaki?
 
Last edited by a moderator:
Bodaboda ni matokeo ya serikali yenye maono mafupi...
 
Mkuu SAUTI YAKO yaani una nguvu kabisa ya kumtetea mwendesha bodaboda ambaye yeye mwenyewe thamani ya maisha yake haithaminishi sawasawa na wewe ufanyavyo? Hivi umejiuliza iweje wagongwe mkupuo kwa gari moja? Unadhani walifuatwa walipopaki?

Madereva wa bodaboda ni vichwa panzi sana,hawapo makini barabarani ndio maana wanagongwa kila siku barabarani,hawapo makini 100%! Mtu anajifunza pikipiki asubuhi jioni anaanza kubeba abiria unategemea nini? Huku kwetu mikoani akijipendekeza unampandia juu na tyre tu au unamtupa ndani ya mtaro.
 
Last edited by a moderator:
Dawa ya hao wapuuzi wa boda boda ni kutembea na "UZI" na Mkanda wake wakizunguka gari tu unaachia kama 50 hivi hewani halafu unaondoka na gari safi kuelekea kituo cha polisi kwa speed ya 40km/h tu hakuna atakayekuja kukufata.

hahaha hiyo ndio dawa ....
 
Jamii forum bwana! muda mwingine unafiki wa watu humu unapanda hadi geji ya mwisho, ni vibaya sana...
Mbaya zaidi hakuna aliyeongelea ajali imetokeaje kuonyesha nani alikua ana makosa kati ya Mzungu na hao Bodaboda 3 ( Mungu awarehemu).....

Assumptions zilizotengenezwa hapa nyingi ni za Ki layman tu, eti kosa la bodaboda! mbona mnapenda kugeneralize, mnajua uchungu walionao hao waliowapoteza wapendwa.wao?

Kwani boda boda wote hapa Tanzania wanaendesha vibaya, bodaboda zimeanzia Tanzania kwani? afu nyie wenyewe wanafiki humu ndio wa kwanza kupanda, iambie serikali yenu iweke mikakati mizuri jinsi ya kuwahandle bodaboda na sio blabla za kinafikifiki tu, hiyo ni ajira na wanasomesha kama nyie mnavyofanya....

Eti wangetumia nguvu hiyo kwenye issue ya Escrow, nyie mmefanya nini cha maana zaidi ya kutoa mapovu nyuma ya keyboard! kwani hili ni taifa la bodaboda, huu ugonjwa wa kutupiana mizigo ndio unaofanya mpaka wezi wanakwiba tu.....
 
Hao vijana wa bodaboda inabidi wapewe elimu na ushauri wa kutosha juu ya matumizi sahihi na salama ya hizo bodaboda. Askari wa usalama na serikali kwa ujumla nao inabidi wawe wakali zaidi kwa vijana wanaoendesha hizo bodaboda pasipo kujali sharia wala usalama wao binafsi.

Mnapoamua kuchoma gari moto bila kuangalia nani amesababisha ajali inasaidia nini ilhal pengine mwenye gari atalipwa na bima huku wahanga mlioonesha hasira mnabaki vilema, wajane au yatima pasi na msaada wowote.
 
GAUTAMA hujui uongealo,Bodaboda ni careless! Sipandi bodaboda kabisa maana nawajua jamaa ni vilaza hawakawii kukuingiza uvunguni mwa Scania!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom