Ajali ya Mh Regia - tuna tatizo

Mkuu MCHOMAMOTO nakupa bigup kinoma, baadhi yetu tumejenga tabia ya kumuhusisha MUNGU na upuuzi wetu,Ajali za kujitakia utasikia Oh Mapenzi ya MUNGU.Ujinga huo unanikera sana , MUNGU wa aina gani Mshenzi kiasi hicho anayetaka Kiumbe wake aliyemuumba kwa mfano wake akampulizia pumzi ya Uhai afe kwa Kuangukiwa na Container lenye tani 50 halafu tuseme ni mapenzi ya MUNGU, naapa MUNGU wa namna hiyo simtaki na nitajenga urafiki na Shetani ambaye hawezi kuua Wanadamu kwa mtindi huo.Lini tutakubali kwamba hizo ni kazi za shetani kupitia kwa washenzi wanaokula rushwa na kutoa Leseni nyuma ya Mlango hata kama Muhusika haja Qualify kupata hiyo Leseni.Lini tutasema Mungu amemjalia Mchomamoto juhudi katika kazi zake hadi ameweza kujenga nyumba na kununua gari, badala yake tutasema Mchomamoto ametumia nguvu za giza kupitia maombi ya Mchungaji fulani kupata pesa zilizomletea maendeleo.Simo kwenye unafiki wenu, RM amechangai kifo chake kwa 100%.Jambo la kujadili hapa ni kuwataka wengine wenye mawazo kama yake Marehemu RM,wasithubutu kurudia alichokifanya kwa kuwa LAZIMA WATAKUFA KWA AJALI na itafika mahali hata kama tunawapenda kiasi gani, kamwe sitawalilia

Naungana na wewe kwenye hoja kuwa ni vema tukawa makini tunapotaka kusema mambo mengi yanayotupata binadamu ni mpango wa Mungu..wakati mwingine ni uzembe na kutojali..mfano wengi tunakufa kwa magonjwa mbalimbali kwasababu ya kula vibaya au kutokuwa na utaratibu mzuri wa kula....ila hapo kwenye red nadhani umepotoka,UMFAHAMU VIZURI SHETANI jaribu uone....
 
Mimi ninachojiuliza kwa nini air bag za hili gari hazikufyatuka (deployed)? Gari inaonekana ni jipya, nani ambaye ana tender ya kuwauzia magari wabunge? Je anawauzia magari famba....
 
Kama kuna vitu ambavyo watanzania tunatakiwa kuviangalia ni vifo visivyokuwa na ulazima. Angalia barabara ya Morogoro ilivyobusy almost 18 hours! lakini sidhani kama inaweza kufanyiwa marekebisho hivi karibuni. Inshu hapa nii hizi barabara zetu ni nyembamba mno! mazingira hayaruhusu kuovertake kabisa.

Nikija kwenye suala kanuni, sheria na taratibu! watanzania wengi hatufuati taratibu sehemu yeyote, tumefanya ule uvunjifu wa kanuni au sheria au taratibu ndiyo kawaida. Chukulia mfano: Mko kwenye daladala, konda anajaza watu kwenye gari hadi mnashindwa kupumua vizuri, lakini watu hamtaki hata kumkemea!! unategemea nini hiyo hali? Jibu mkikaa kimya, konda anafanya kuwa ndo utaratibu.
 
kamanda mwenyezimungu anapoamua kuchukua kiumbe chake ameamua hata kama angekuwa haendeshi yeye kama wakati wake ulikuwa umefika asingekwepa,pamoja na ulemavu wake alimudu kuendesha gari hilo,ukitafuta ni nani mwenye makosa unakosea na tena unamkufuru mungu ambaye ndie anaetoa uhai na kuuchukua kwa wakati apendao,regia ametangulia nasi tuko nyuma yake kwani ni njia ya wote hiyo kikubwa tumuombee mh wetu mungu ailaze roho yake mahali pema peponi AMIN.

Romee,
Ndege ya BOEING au AIRBUS inapoanguka watu kwa makumi au mamia hupoteza maisha, (sielewi kama ni Mungu kapanga - is another power beyond my thinking), Wataalamu wa Boeing au Airbus huenda kwenye scene ya accident na kujua chanzo cha ajali. Uchunguzi hufanywa na wakigundua chanzo, kama ni pilot (human) error au machine error (fault) wanafanya marekebisho siyo tu kwa sababu ya wale waliopotea; bali kurekebisha yasitokee madhara mengine kama hayo.

Kwa magari ni hivyo hivyo; kama dereva aliendsha na kufanya makosa au tatizo lilikuwa ni gari uchunguzi ufanyike ili usaidie kurekebisha sheria au matatizo ya magari ili baadaye tuokoe maisha ya watu wengine.

Mie naona barabara zetu ni ndogo mno hazitoshi kupishana na kuachiana nafasi.

Au; unataka tuamini theory yako kuwa kifo kimepangwa na Mungu? Tusifanye uchunguzi ?
 
Kweli wewe ni INTRESTED OBSERVER, ukifuatilia uchunguzi wa ajali kwa wenzetu utapenda; watu wako makini, hakuna majibu mepesi kwa mashwali magumu. Fuatilia hii hapa:
https://www.youtube.com/watch?v=iOGK8UhJFKk

Wataalamu walitoa sababu ambazo mzazi wa kijana aliyekufa kwenye ajali hawakuridhika nazo na akafanya uchunguzi mwenyewe na baadae uchunguzi wake ulionekana sahihi. HAKUNA MAJIBU MAPESI KWA MASWALI MAGUMU.
 
Jamani Baadhi ya viongozi wetu waliopata ajali ni pamoja na Regia Mtema, Dr.Mwakyembe, Prof.Kapuya, Mzee Mwaikambo, Mudhiri, etc. hawa wote walipata ajali wakiwa na magari aina ya Toyota Landcruiser SAV. Tunaweza sema haya magari sio salama kwa viongozi wetu? Kuna kipindi Dr.Magufuli alisema kuendesha Toyota XV nisawa na kutembelea fuso! akashauri viongozi watumie Benz ambazo ni salama zaidi, watu wakamjia juu!

Uchunguzi wakina unahitajika juu ya hii ajali. Je Air bags zake zilikuwa zinafanya kazi, UBS zilikuwa nzima, matairi yake je? service lilifanyiwa kwa mara ya mwisho lini na wapi? Hili Gari navyoona lilikuwa mtumba! alilinunua watu? ndo mara ya kwanza kupata ajali? isijekuwa lilikuwa na matatizo tangu zamani mama Regia akashikiswa! Wabunge wengi wananunua magari mitumba wabakiwe na chenji!
 
siko mbali sana na wewe ntamaholo.:hatari:

hata mimi, naunga mkono. Ila kwa namna hii hatujengi nchi. Hii ndio sababu kubwa ya kushambulia au kushabikia personalities badala ya issues.
Ukiwa humpendi mtu hata akifanya jema utalifunika na baya la mwaka jana ndio uliangalie!! Utalionaje?
Tujifunze kuangalia issues
 
Haika

Nashukuru kwamba umeweza kuliona tatizo...lkn bado tunahitaji ufafanuzi wako...nahisi kwamba labda naliangalia hili kwa mtazamo tofauti...
Kwani ukiwa mlemavu huwezi kuendesha gari??????Gari ambayo ni Automatic mtu yeyote anaendesha sio kama Standard.... kwa hivi sioni kama ilikuwa kosa kwa Regia kupewa leseni. Hii ni ajali kama ajali zingine.
 
Jamani Baadhi ya viongozi wetu waliopata ajali ni pamoja na Regia Mtema, Dr.Mwakyembe, Prof.Kapuya, Mzee Mwaikambo, Mudhiri, etc. hawa wote walipata ajali wakiwa na magari aina ya Toyota Landcruiser SAV. Tunaweza sema haya magari sio salama kwa viongozi wetu? Kuna kipindi Dr.Magufuli alisema kuendesha Toyota XV nisawa na kutembelea fuso! akashauri viongozi watumie Benz ambazo ni salama zaidi, watu wakamjia juu!

Uchunguzi wakina unahitajika juu ya hii ajali. Je Air bags zake zilikuwa zinafanya kazi, UBS zilikuwa nzima, matairi yake je? service lilifanyiwa kwa mara ya mwisho lini na wapi? Hili Gari navyoona lilikuwa mtumba! alilinunua watu? ndo mara ya kwanza kupata ajali? isijekuwa lilikuwa na matatizo tangu zamani mama Regia akashikiswa! Wabunge wengi wananunua magari mitumba wabakiwe na chenji!

Eddy;
Unajua kuwa Mercedes benzi imewahi kugongana na landcruiser ikamwua Waziri mkuu wa Nchi ya URT(United REpublic of Tanzania); Mri Edward Moringe Sokoine?? Can you imagine Waziri Mkuu wa nchi anagongwa na gari??

Upo too "general"; umeshamanisha kuwa Toyota Landcuiser si gari ya kuaminika, na kwa kuwa John Pombe Magufuli (your index) alisema Mercedes benz ni salama; kwa hiyo wewe unaona kuwa mercedes benz ilikuwa ni solution kwa ajali.

Kihesabu, je umetoa Landcruiser zilizoendeshwa Tanzania, na VIPs uliowataja zilipata ajali. Je unaweza ukajiuliza kuwa gari hiyo hiyo inaendeshwa ulimwengu mzima na haina hiyo record; please correct your point; what did you want to tell us? Something is missing!!

This is a banana REpublic; a Prime Minister can be killed by a highway accident!
Don't bring another clarification : Mr Palme (Sweden Prime Minister was stubbed to death by South Africa security agents (during arpatheid)!!

Tuache uongo Nchi yetu haina Sheria inaendeshwa kiujanja ujanja tu!
 
Interested Observe, nimemuelewa Eddy; anasisitiza uchunguzi wa kina unapaswa kufanyika ukihusishwa wataalamu wa aina mbalimbali tofauti na tunavyofanya kwa sasa kwamba polisi wanatoa taarifa ambazo hazina uchunguzi wa kina, kama ajali hii siku hiyo hiyo polisi wana-conclude chanzo cha ajali sifikiri kama uchunguzi wa kina ulifanyika. Ni kweli kuna baadhi ya magari hayaendani na miundo mbinu eneo fulani (barabara), kwa hiyo hayakupasa kutumika. Utakumbuka kuwa ndege aina ya concorde zilikuja kuonekana kwamba hazifai kutumika kutokana na miundo mbinu iliyopo, pale ambapo air france iliposhindwa kusimama wakati ina take off huku ikiwa imeshaanza kushika moto.
 
magari used na ya muda mrefu sio salama kwa maisha ya binadamu, ukitumia is at owners risk. Wabunge wasiachiwe kununua magari magari used tuachiwe sie wagonga nyundo manake uchaguzi ni gharama kubwa na madereva wawe ktk payrol za bunge au vyama vyao.
 
Nadhani gari lilikuwa specially made kwa ajili yake na ulemavu wake. Traffic wasingemruhusu kuendesha ikizingatiwa mguu wake wa kulia ndio ulikuwa na tatizo.
Wakulu

Nimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya Mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.

Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia.Gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.

Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa Marehemu? wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni)

Nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba Regia alikuwa ni hazina ya taifa...... mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ...kwa kuruhusu uzembe,kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo?

Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya TRA, Trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.k

Sheria , kanuni na taratibu zipo kutulinda.....naamini TUNA TATIZO KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.....

Naomba tujadili objectively...bila jazba...
 
Watu wengi wamekuwa wakificha udhaifu wao kwa kuitaja Bahati mbaya! Ukweli ni kwamba ajari nyingi hapa kwetu zinatokea kwa sababu ya uzembe au makusudi.Zaidi ya 78% ya ajari zinatokea Tanzania ni uzembe wa madereva-kamanda Mpinga.
 
da rejia alimfukuza dereva wake kwa sababu alikataa kuokoka.hii ni kwa mujibu wa mtu wake wa karibu
 
aliwahi kusimamishwa na trafic akatakiwa kuonyesha leseni.aliwajibu kuwa msinisumbue,au hamnijui?me ni mbunge ati,tena wa chadema.
 
mi bado sijaelewa logic unayojenga hapa ni nini??

je unauliza swali mamlaka gani iluruhusu yeye kuendesha gari???

au unataka kutuambia kuwa ni uzembe wake???

au unailaumu serikari???

anywai ni hivi 'MHESHIMIWA MBUNGE ALIYEKUWA NA ULEMAVU WA MGUU ALIPATA AJALI YA GARI ALILOKUWA ANALIENDESHA MWENYEWE, NA ALIFARIKI DUNIA HAPO HAPO! (Sasa hayo mengine yaache kama yalivyo, kama ni uzembe wake au serikali au dreva wake poa, mungu amuweke mahari pema peponi)

hapo kwenye red,unataka kuolewa?
 
Mkuu MCHOMAMOTO nakupa bigup kinoma, baadhi yetu tumejenga tabia ya kumuhusisha MUNGU na upuuzi wetu,Ajali za kujitakia utasikia Oh Mapenzi ya MUNGU.Ujinga huo unanikera sana , MUNGU wa aina gani Mshenzi kiasi hicho anayetaka Kiumbe wake aliyemuumba kwa mfano wake akampulizia pumzi ya Uhai afe kwa Kuangukiwa na Container lenye tani 50 halafu tuseme ni mapenzi ya MUNGU, naapa MUNGU wa namna hiyo simtaki na nitajenga urafiki na Shetani ambaye hawezi kuua Wanadamu kwa mtindi huo.Lini tutakubali kwamba hizo ni kazi za shetani kupitia kwa washenzi wanaokula rushwa na kutoa Leseni nyuma ya Mlango hata kama Muhusika haja Qualify kupata hiyo Leseni.Lini tutasema Mungu amemjalia Mchomamoto juhudi katika kazi zake hadi ameweza kujenga nyumba na kununua gari, badala yake tutasema Mchomamoto ametumia nguvu za giza kupitia maombi ya Mchungaji fulani kupata pesa zilizomletea maendeleo.Simo kwenye unafiki wenu, RM amechangai kifo chake kwa 100%.Jambo la kujadili hapa ni kuwataka wengine wenye mawazo kama yake Marehemu RM,wasithubutu kurudia alichokifanya kwa kuwa LAZIMA WATAKUFA KWA AJALI na itafika mahali hata kama tunawapenda kiasi gani, kamwe sitawalilia

Mkuu KANYANGA tuko pamoja sana,huwa nakerwa sana na neno "MAPENZI YA MUNGU" ni Mungu wa namna gani huyo jamani kwa kila kifo??hivi kweli ukae kwenye reli gari moshi likupitie useme mapenzi ya Mungu duuh!!hata nami kama ni hivyo simtaki huyo Mungu!!!!!!walai tena, watu tunapashwa kuelewa tu mambo mengine ni suala la tahadhari tuu.Big up mkubwa!!!
 
Naungana na wewe kwenye hoja kuwa ni vema tukawa makini tunapotaka kusema mambo mengi yanayotupata binadamu ni mpango wa Mungu..wakati mwingine ni uzembe na kutojali..mfano wengi tunakufa kwa magonjwa mbalimbali kwasababu ya kula vibaya au kutokuwa na utaratibu mzuri wa kula....ila hapo kwenye red nadhani umepotoka,UMFAHAMU VIZURI SHETANI jaribu uone....

Mkuu sidhani kama umefikiria kwa kina hasa na umelielewa hilo neno alilolitoa Kanyanga!!??fikiri vizuuuri sana alafu tafuta maana.
 
Wakulu

Nimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya Mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.

Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia.Gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.

Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa Marehemu? wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni)

Nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba Regia alikuwa ni hazina ya taifa...... mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ...kwa kuruhusu uzembe,kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo?

Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya TRA, Trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.k

Sheria , kanuni na taratibu zipo kutulinda.....naamini TUNA TATIZO KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.....

Naomba tujadili objectively...bila jazba...
Umejuaje? Labda gari Lake lililetwa Automatic Unahitaji Muguu Mmoja wowote
 
Nimependa comment yako mkuu, tuache mawazo finyu sisi binadamu!!uache kufunga mkanda, tuendeshe magari kwa speed kali tupate ajali useme Mungu amependa??? ni Mungu gani huyo anaependa watu wake wafe kwa uzembe!!!??
kaka sijui nadhan ni iman yako.
sidhan kama huyu dada ni mara yake ya kwanza kuendesha gari au kuovertake au kutofunga mkanda ndio tusimamie ktk hoja izo.
huyu dada siku yake ilifika basi, wala hakuna haja ya kuraise maswali kibao na wengine kumkufuru mungu.
ofcoz amevunja sheria lkn pia, ndio! lakin kufa ni kwamba siku yake ya kutwaliwa ilifika.
pumzika kwa aman dada regia.
 
Back
Top Bottom