Aisee kumbe Jk alitoa hiyo ya DNA? Hiyo ni kali kwa kweli. Yeye anadhani kama anavyotamka DNA kwa urahisi kwa herufi tatu basi hata matumizi ya sayansi na technologia yake yatakuwa rahisi. Halafu raisi mwenyewe hatumii hata logic; nchi iliyo bado kwenye matatizo ya giza itawezaje kuwa na advanced fingerprinting techniques kama za DNA?
Mimi nijuavyo, hata hicho kipimo hicho cha DNA kinahitaji utaalamu wa hali ya juu wa watu watakaoweza kufanya mahesabu ya kistatistics ili kutenganisha huo mfanano wa DNA na kutambua ni yupi hasa ndugu wa karibu bila makosa yoyote ya kiufundi. Wanatakiwa highly technically trained molecular geneticists; na Tanzania hapa ninavyofahamu hakuna mtu hapa kwenye hizo fani, achilia mbali hivyo vifaa vya kuweza kuziisolate,kuzifragment, kuziamplify na kuzilinganisha sawa kwa sawa kuona wapi kwenye mfanano au vipi; Sasa shule zenyewe za bongo ni mkopo wa shilingi 5000 na wenyewe serikali wanaona wamekusaidia kwelikweli halafu anatokea zuzu mmoja na kusema majukwaani eti waliozama wapimwe DNA,tuna rais rahisi kweli kweli!!!