Njoeni hapa DNA ya mahusiano inataka kuharibu ndoa ya mtu hapa

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Ndugu zangu wana jf naombeni radhi kwa kuwakurupua sana.

" SOMA KWA MAKINI UELEWE , RUDIA KUSOMA POLE POLE KAMA HUJAELEWA"

Ndugu zangu unapopima DNA wanachukua sampuli za maeneo 15 kutoka kwa mama na baba pamoja na mtoto ili kupata muunganiko wao na uhalali wa mtoto katika kuondoa utata wa vina saba na yupi ni mzazi halali .

Ndugu zangu kama tujuavyo shangazi (dada yake na baba yako) walikua ndugu na hivyo ni damu moja maana maeneo 15 ya kwake yameoana na mama na baba hali kadhalika hivyo hivyo kwa huyo baba yako.

Shangazi yako anapo olewa anaondoka na uhalisia wa vina saba vya baba yako anaenda kuplus na vingine vya mumewe na kupata mtoto watakao share nae vinasaba.

..Yaani ki hesabu ni anaondoka na nusu anajumlisha na nusu ya mumewe anapata moja ambaye ni mtoto walie zaa utakaye muita binamu. Mtakua ndugu kwa mama ila siyo ndugu kwa baba.

Ndugu zangu kwa mantiki hii . kama baba yako mzazi atazaa nje mtoto wa kike ukienda kupima DNA utakuta na utata wa nusu kwa nusu yaani 50% mmeshare vina saba, hapa mtakua na uwiano wa baba na sii mama. Hapa mtakua ndugu kwa baba ila si ndugu kwa mama

Atakua ana DNA za baba ila za mama haziendani na wewe maana huyo siyo mama yako, kulekwa shangazi nako ni hivyo hivyo , ila mtoto shangazi yako aliye zaa na mwanaume mwingine lazima 50% mtakua mmeshare vina saba

Sasa kama mtoto wa nje aliye zaa baba yako mzazi na mchepuko wake mnakua mmeshare vinasaba kwa 50% ya DNA, na mtoto aliye zaa dada yake na baba yako (shangazi) nae mmeshare 50% ya DNA.

1: Je, kwa mgawanyiko huu wa vina saba , ni sahihi kuoa /kuolewa na mtoto wa nje wa baba yako mzazi kama tuu binamu yako ni halali kumuoa au kuolewa nae isipokua wanatupiga tu dana dana hapa huku wakisingizia maadili?

2: Kwa kuzingatia ndugu sasa hivi hatujuani kwa 99% na wanaume kwa wanawake wana chepuka sana , je. Kama siyo sahihi kwenye swali la kwanza ,. Vipi basi kwa hawa ndugu wa mbali wa sio juana kwa kuzaliwa nje kwenye michepuko yetu ikitokea wameoana kibatili na kupata watoto?

3: Kama fomula ya DNA ina utata na inampishano wa binamu na mtoto wa nje wa familia yenu. je, ni nini kifanyike ikitokea ndugu wameoana sawa sawa na hayo maelezo hapo juu na vipi maandiko matakatifu sawa sawa na imani zenu yanasemaje kuhusu kuoa au kuolewa na binamu au mtoto aliye zaa baba yako au mama yako na mchepuko?

ONYO: USIJIBU KAMA HUJATAFAKARI, TAFAKARI NDIYO UTOE MAJIBU.
 
Kwa upande wangu Elimu ya DNA napendelea ilale kwenye Magonjwa.

Namaanisha nini?

Kwenye KOO au FAMILIA fulani mara nyingini tunaona kuna aina ya ugonjwa au aina ya tabia zinakuwepo. Na hizi zinazunguka katika Vinasaba.

Sasa nilikuwa nashauri sana watu waangalie background ya Watu wanaojiingiza katika mahusiano.

Mfano ili ku determine umri wa mtu wa kuishi mie naangalia Wazazi wake kama wapo hai, na wana Umri gani? Hii inanipa picha halisi ya survivability ya Mwenza wangu apart from majanga kama Ajali etc. Kwamba huyu Mwenza wangu ataishi kwa makadirio ya miaka fulani.. (kuna familia wana vinasaba vya kuwahi kuzeeka na kufa mapema)

Magonjwa ya Akili, hasira, mpaka na masuala ya Uzazi na Intelijensia.

Tukija upande wa Pili, Vinasaba ambavyo si vya kibaiolojia yaani spiritual DNA's..

Laana, Kutofanikiwa, Mikosi etc..

Kuna watu ktk DNA zao kuna mrundikano wa Mikosi so kuoa au kuzaa nae unashare cost.. unalipia deni ambalo halikuhusu...

NB.

Nimeingia na kutoka ndani ya Mada..
 
Ndugu zangu wana jf naombeni radhi kwa kuwakurupua sana.

" SOMA KWA MAKINI UELEWE , RUDIA KUSOMA POLE POLE KAMA HUJAELEWA"

Ndugu zangu unapopima DNA wanachukua sampuli za maeneo 15 kutoka kwa mama na baba pamoja na mtoto ili kupata muunganiko wao na uhalali wa mtoto katika kuondoa utata wa vina saba na yupi ni mzazi halali .

Ndugu zangu kama tujuavyo shangazi (dada yake na baba yako) walikua ndugu na hivyo ni damu moja maana maeneo 15 ya kwake yameoana na mama na baba hali kadhalika hivyo hivyo kwa huyo baba yako.

Shangazi yako anapo olewa anaondoka na uhalisia wa vina saba vya baba yako anaenda kuplus na vingine vya mumewe na kupata mtoto watakao share nae vinasaba.

..Yaani ki hesabu ni anaondoka na nusu anajumlisha na nusu ya mumewe anapata moja ambaye ni mtoto walie zaa utakaye muita binamu. Mtakua ndugu kwa mama ila siyo ndugu kwa baba.

Ndugu zangu kwa mantiki hii . kama baba yako mzazi atazaa nje mtoto wa kike ukienda kupima DNA utakuta na utata wa nusu kwa nusu yaani 50% mmeshare vina saba, hapa mtakua na uwiano wa baba na sii mama. Hapa mtakua ndugu kwa baba ila si ndugu kwa mama

Atakua ana DNA za baba ila za mama haziendani na wewe maana huyo siyo mama yako, kulekwa shangazi nako ni hivyo hivyo , ila mtoto shangazi yako aliye zaa na mwanaume mwingine lazima 50% mtakua mmeshare vina saba

Sasa kama mtoto wa nje aliye zaa baba yako mzazi na mchepuko wake mnakua mmeshare vinasaba kwa 50% ya DNA, na mtoto aliye zaa dada yake na baba yako (shangazi) nae mmeshare 50% ya DNA.

1: Je, kwa mgawanyiko huu wa vina saba , ni sahihi kuoa /kuolewa na mtoto wa nje wa baba yako mzazi kama tuu binamu yako ni halali kumuoa au kuolewa nae isipokua wanatupiga tu dana dana hapa huku wakisingizia maadili?

2: Kwa kuzingatia ndugu sasa hivi hatujuani kwa 99% na wanaume kwa wanawake wana chepuka sana , je. Kama siyo sahihi kwenye swali la kwanza ,. Vipi basi kwa hawa ndugu wa mbali wa sio juana kwa kuzaliwa nje kwenye michepuko yetu ikitokea wameoana kibatili na kupata watoto?

3: Kama fomula ya DNA ina utata na inampishano wa binamu na mtoto wa nje wa familia yenu. je, ni nini kifanyike ikitokea ndugu wameoana sawa sawa na hayo maelezo hapo juu na vipi maandiko matakatifu sawa sawa na imani zenu yanasemaje kuhusu kuoa au kuolewa na binamu au mtoto aliye zaa baba yako au mama yako na mchepuko?

ONYO: USIJIBU KAMA HUJATAFAKARI, TAFAKARI NDIYO UTOE MAJIBU.
sijaelewa, ila naona una complicatisha maisha
ishi maisha yako achana na hizi sarakasi
 
Back
Top Bottom