Ajali ya Meli: Kikwete na hoja ya upimaji DNA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya Meli: Kikwete na hoja ya upimaji DNA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hossam, Sep 13, 2011.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Katika kauli tata na zisizokuwa na maana ni ile ya Mkweree majuzi kwamba waliofariki kwa ajali ya meli huko Nungwi wapimwe DNA ili kuwatambua kwa urahisi. Jamani huyu rais wa ajabu kabisa sasa sijui ile kauli aliitoa akiwa na mgandamizo wa mawazo ya ile kesi ya Dr Batiliada Burianii huko Arusha. Maana huyu mama ndio ilisemekana akapimwe DNA ili kubaini ukweli wa kauli ya Kada wa chadema huko. Sasa labda alikuwa anawaza sana ishu hiyo hadi kujikuta karopoka mahala isipotakiwa.

  Nijuacho mie DNA ya utambuzi ni lazima pawe na data base inayokuwa ama ina taarifa ya mtu anayepimwa, ama wajitokeze baba na mama mzazi wa mpimwaji wapimwe wao kwanza na ndipo na huyo marehemu apimwe ili kuona common genes. Sasa huyu jamaa anaibuka na kusema 'wapimwe DNA' hivi wajameni huyu mtu ana nini kichwani, ama niulize hivi... hivi hana washauri wanaompa jinsi ya kuongea mbele ya kadamnasi? Rais asione haya kufundishwa speech na namna ya kuongea na hadhira, wote huwa wanapewa darasa huwezi ku win hadhira kama unaongea vitu ambavyo havipo duniani.

  Utambuzi wa nani tu anamiliki Kagoda Tanzania imekuwa kama kuchunguza hivi ni nani baba yake Mungu! Sasa hiyo DNA hivi Tanzania imefikia advansi level kiasi gani katika forensic investigation? Kama tuko kamili vipi mauaji ya kule kibaha ya yule dereva taksi maskini yakawa mistery!! Nimeskitika sana aisee na siwezi kukaa kimya huyu jamaa anaweza kuja kutuadhiri hata ugenini huko anakopenda kuzurura tukawa sisi madaktari tukiomba kazi tunaambiwa tukapimwe kwanza DNA ili kubaini uwezo wetu wa kufikiri na kiwango cha uendawazimu wetu.

  Kwa faida ya wana JF, ona hilii ''DNA ni kifupi cha DeoxyriboNucleic Acid ambayo nijina la molekuli kubwa ndani ya seli za viumbehai. DNA Inabeba ndani yake habari zote za urithi wa kiumbehaiyaani habari za tabia zote zinazopokelewa na wazazi. Molekuli ya DNA inaumbo kama ngazi mbili za kupanda zilizounganishwa pamoja na kupindwa kama sukurubu.DNA ina uwezo wa kujinakili. Wakati wa kuzaa inajipasua katikati ya pande mbiliza "ngazi" yake. Hivyo nusu "ngazi" ya upande wa mzazi mmojainaungana na nusu "ngazi" ya mzazi mwingine.Tabia kama ukubwa, rangi ya ngozi au nywele ziko kilamoja mahali pake; zikiunganishwa kemia inaamua ni upande gani yenye athirazaidi''

  Inatia hasira sana aisee, Nawasilisha kwa huzuni kabisa.

   
 2. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii kauli ilikua kali ya kufungia mwaka! Nami iliniacha hoi kabisa!
   
 3. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Raisi wetu nayeye hajui kitu! Anaiga tu kutoka nchi zilizoendelea! Sasa wapimwe DNA tutawajuaje kwamba huyu ndiye flani ilahari hata data base ya yule mtu haijulikani? Hajawahi kupimwa,wazazi wake hawajawahi kupimwa DNA,sasa utamjua vyp? Haya bana labda watawapima marehemu halafu wapime na ndugu zao,gharama hiyo sijui nani ataisimamia!
   
 4. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichwa cham nazi yule. Mbona inaeleweka kitambo? Hata huko ugenini sijui huwa anasemewa? Maana kama anaongea mwenyewe imekula kwetu haswa!
  Si ulimcheki mwenyewe alivyokuwa anaongea pale, anachekacheka msibani?. Hapa presidaa tunaye kwelikweli.
   
 5. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwanini tusiipime Akili yake DNA ili tujue amerithi wapi huu ujuhaa.Maaana nahisi kuichikia hata sauti yake kila niisikaapo.
   
 6. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mkulu alishangaa kwa nini mpaka sasa marehemu hawajapimwa DNA..akauliza je ni kwamba hakuna wataalam??
  ..haya maneno yamenishangaza kwa kweli!!
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi nilicheka vibaya sana....anadhani kupima dna ni kama kupima kinyesi kujua kama mtu ana amoeba au hana..jk bwana
   
 8. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  kama mtakumbuka ktk mahojiano na yule daktari alijaribu kum'bishia kuwa tuwapige picha kwani kawaida baharini mtu anaweza kukaa hata siku tatu na mwili wake ukabaki fresh hivyo ni bora kuwapiga picha lkn yeye akaonyesha udaktari wake zaidi kwa kufananisha na ajali ya mv bukoba eti maiti nyingi ziliharibika kiasi cha kutotambulika
   
 9. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #9
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  huyu ndio Jakaya.
  -mzee wa ajira 1000,bajaj 400, International Airport Kigoma(ujenzi haujaanza na kabakiza miaka 4.)
  na tusisahau alisema ataunganisha school zote za serikali tanzania na mtandao wa internet.
  tatizo lake hana aibu ndio mungu alivyomuumba.
  Haya sasa juzi kaibuka na hili la DNA! sijui keshokutwa atasemaje tena.
  Kazi ipo! Tulitegemea Nape kijana mwenzetu angalau angekuwa na wazo mbadala huko magambani lakini wapi, naye ni boga, boga, boga!!!!!!!!!!!!!
   
 10. m

  maoniyangu Member

  #10
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mpumzisheni ****** inaonekana hana hata idea hicho kipimo cha dna kinatumikaje na kwe wakati gani. huku kupenda sifa huku iko siku atakuja kutukana hadharani.
   
 11. m

  maoniyangu Member

  #11
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  au labda alimwona mwenzake shain akitoa huduma ya kwanza akaona nae atafuta cha kufanya ili aonekane ni wa msaada? hajui mwenzake ni dokta wa kusomea na sio kupewa??
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mimi nilijua Mh wa Ki.kwere anatania tu! Napendekeza akapimwe akili huyu hes is so cheap. DNA fingerprints haifanyiki kama alivyozoea kuchakachua
   
 13. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Labda DNA yakutumia ramli! Jamani JK ni msanii full!
   
 14. P

  Polisario Member

  #14
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani nyie mlitaka asemeje????!!!!!! Mbona nyie ha2jackia maoni yenu mpaka sashv acheni unafiki nyie
   
 15. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ....bora umekuwa wakwanza kumfunga paka kengele,mimi sio daktari ila ndio nlikuwa nakusanya taratibu namna kipimo cha dna kinavyifanyika halafu niipost hapa!!!nathani nikiendelea kuandika nitakosa adabu kwa mr rais,naishia hapa.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Uko kwenye Muhadhara?
   
 17. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  FF hajaiona hii akawajibu?
   
 18. m

  maoniyangu Member

  #18
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we na yeye hamna tofauti, ila sio kosa lako.
   
 19. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Rais 'much know'!..nafikiri tunaoaibika zaidi ni sisi tuliyempatia Urais maana anawakilisha Watanzania wote!ni mtazamo tu
   
 20. opwa

  opwa Member

  #20
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nilikuwa makini but hapo nilicheeeeka, afu nikawaza angeongezwa muda angesema wapimwe vvu pia ili tujue records zao ktk mahitaji ya takwimu tehe tehte
   
Loading...