Mimi napingana kabisa na Mheshimiwa Mwakyembe. Kwanza kabisa, yeye siyo polisi na siyo subject matter expert katika eneo hilo. Yeye mwenyewe amenukuliwa kwa mara ya kwanza akisema kwamba gari yake ilikuwa inaipita lori halafu akaingia kwenye pot hole tairi ikatoka gari lika anguka na kubiringika. Ya pili alisema kuwa gari yake ilikuwa inaipita lori halafu lori likagonga gari yake kwa nyuma upande wa kushoto gari ikapinduka. Ukiangalia kwa scenario zote mbili zinaonyesha kuwa driver wake hakuwa makini. Kwani kama alikuwa anaipita gari bila kuiscan njia halafu akaingia kwenye pot hole, basi alikuwa na makosa, maana ni mzembe hajapata big picture ya barabara kabla ya kufanya uamuzi wa kuovertake. Hili la pili la kugongwa kwa nyuma, kuna mambo mengi lakini tuangalie mawili, either driver alirudi upande wa lori haraka na mwendo wake ulikuwa mdogo kuliko wa gari kubwa, maana yake atakuwa amekanyaga break au kupunguza mwendo immediately baada ya kuovertake. La pili kama gari kubwa lilimgonga kwa nyuma upande wa kushoto maana yake, driver wa gari kubwa alikata kona haraka sana na alikuwa kwenye mwendo mkali, hivyo nalo gari lingeyumba hata kuanguka ama lingeigonga gari ya Mheshimiwa kwenye ubavu. Na hili kwenye ubavu halipo kwani halijasemwa. Hivyo possibility in kwamba driver wa Mh. Mwakyembe alirudi haraka kabla ya kumaliza kuovertake na kujibamiza kwenye gari kubwa, hapa tena kosa ni la driver wa Mh. Mwakyembe. Ninacho taka kusisitiza hapa ni kwamba madriver wanahitaji kusoma kitu kinachoitwa Defensive Driving, na somo litawasaidia madriver wote kuwa makini barabarani. Madriver wa magari ya serikali na za waheshimiwa wanaendesha rafu sana bila kufuata sheria wakidhani wao wako juu ya sheria maana wako na Mheshimiwa hivyo hata traffic police hawezi kumsimamisha au kupiga faini. Ok, hasimamishwi wala hapigwi faini lakini ajali itampata na tumeshapoteza wakubwa wengi kwa uzembe huu. Hawa madriver wanahitaji defensive driving. TIT inafundisha course hii na haichukui zaidi ya wiki. Uendeshaji wa gari siyo leseni na kunyooshea barabara ni pamoja na kufahamu matumizi sahihi ya barabara kwako wewe na mwingine na kuepuka ajali. Driver mzuri na hodari ni yule anayeanza na kumaliza safari yake vizuri. Mh. Mwakyembe anafanya swala hili kuwa la kisiasa yeye mwenyewe. He is already popular he don't any further cheap popularity. Lazima awe mfano wa kukemea unsafe driving kama iliyoonyeshwa na driver wake. Bongo hii mambo ya wakuu kutetea madriver wavunje sheria ni kawaida, kuna wakati naibu waziri wa wizara inayoshughulikia mambo hayo ya usalama alimripoti police aliyelirudisha gari lake ili lifuate sheria. Kitendo kama ilitakiwa imwajibishe waziri kama huyu ambaye analea uendeshaji mbaya ambao unaweza kupelekea ajali na kugharimu maisha ya watu. Ajali za barabarani zimeshagharimu Watanzania wengi maisha yao. Lazima tubadili tabia ya kuendesha magri. Lets observe Defensive Driving. Asanteni sana. It is possible to reduce road accidents.
Kombe anatakiwa ajiuzuru kulinusuru jeshi la Polisi
'dereva ndiye chanzo cha ajali ya dk. mwakyembe'
Hayo yamo katika taarifa ya Kamati iliyoundwa na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuchunguza chanzo cha ajali hiyo .
Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabara nchini, James Kombe alisema baada ya uchunguzi wao kamati imebaini kwamba chanzo chake hakikuwa roli lililokuwa linapitwa kama alivyopata kunukuliwa mbunge huyo, bali dereva wa mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo mkali.
Kamati imefika eneo la tukio na kuwahoji mashuhuda walioona gari la mbunge huyo kabla na baada ya kupata ajali, kukagua gari la mbunge pamoja na kumhoji mtaalam wa magari aliyesomea uingereza, Francis Mwakatundu ambaye ameonyesha kupingana na kauli ya mbunge huyo kuwa aligongwa baada ya kuchunguza gari hilo na kuona hakuna sehemu ambayo ilionyesha kugongwa alisema.
kwi kwi kwi kwi kwi..... so kulingana na huyu mtaalamu aliyesomea Uingereza. Tuamini kuwa gari lilifanikiwa kugonga jiwe kubwa na kuling'oa na kisha likafanikiwa kugonga mti mkubwa circumference 115cm na kuung'oa? are these guys serious with this report.Alisema uchunguzi wao haukuona alama yoyote ambayo inayothibitisha kwamba gari la mbunge huyo liligongwa kwa nyuma au upande mwingine wowote. Alisema mikwaruzo iliyopo ni ile iliyotokana na gari hilo kuacha njia na kubiringika porini zaidi ya mita 60 kabla ya kugonga jiwe kubwa na kulingoa na baadaye kuparamia mti mkubwa wenye mzunguko wa sentimeta 115 hadi kuungoa na hivyo kupinduka.
So kukiwa na utata wa taarifa polisi inaunda tume, na kupingana na tarifa za wahusika wakuu? Lawyers will help here, why not send it to court.Kamati hiyo iliundwa baada ya kuwepo na taarifa tofauti toka jeshi la Polisi, Mbunge huyo na dereva wake.
Mkuu unamaanisha nini? Kwani waligongwa na nini? Mbona siku zote tunaelezwa ni lori? Au ni jini?