Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ah! Si walitaka uchuzi? Au walitaka hisia zake ziwe ndio hisia za watu wote?
 
kwa taarifa hii Nalazimika kusema kuwa ajali ya hii imetengenezwa kwa nia ya kutoa maisha ya Dr..... nauliza MPAKALINI WATU WANAOTETEA WANYONGE WATAENDELEA KUUAWA?????

naomba mwenye cv ya elimi ya polisi kombe aiweke hapa.......
 
Mungu ni mwema ana makusudi kamili ya kuendelea kumweka ndugu mwakyembe hai. Cha muhimu tumshukuru mungu na aendelee kufanya kazi kweli tena kweli kweli.
 
Pole sana DR.Nakushauri usiwaogope wanaotaka kukuhamisha katika sura ya dunia,endelea kuomba sana mungu utashinda.Tunakutakia kila la kheri na upone haraka uweze kuendeleza mapambano.
 
Mimi napingana kabisa na Mheshimiwa Mwakyembe. Kwanza kabisa, yeye siyo polisi na siyo subject matter expert katika eneo hilo. Yeye mwenyewe amenukuliwa kwa mara ya kwanza akisema kwamba gari yake ilikuwa inaipita lori halafu akaingia kwenye pot hole tairi ikatoka gari lika anguka na kubiringika. Ya pili alisema kuwa gari yake ilikuwa inaipita lori halafu lori likagonga gari yake kwa nyuma upande wa kushoto gari ikapinduka. Ukiangalia kwa scenario zote mbili zinaonyesha kuwa driver wake hakuwa makini. Kwani kama alikuwa anaipita gari bila kuiscan njia halafu akaingia kwenye pot hole, basi alikuwa na makosa, maana ni mzembe hajapata big picture ya barabara kabla ya kufanya uamuzi wa kuovertake. Hili la pili la kugongwa kwa nyuma, kuna mambo mengi lakini tuangalie mawili, either driver alirudi upande wa lori haraka na mwendo wake ulikuwa mdogo kuliko wa gari kubwa, maana yake atakuwa amekanyaga break au kupunguza mwendo immediately baada ya kuovertake. La pili kama gari kubwa lilimgonga kwa nyuma upande wa kushoto maana yake, driver wa gari kubwa alikata kona haraka sana na alikuwa kwenye mwendo mkali, hivyo nalo gari lingeyumba hata kuanguka ama lingeigonga gari ya Mheshimiwa kwenye ubavu. Na hili kwenye ubavu halipo kwani halijasemwa. Hivyo possibility in kwamba driver wa Mh. Mwakyembe alirudi haraka kabla ya kumaliza kuovertake na kujibamiza kwenye gari kubwa, hapa tena kosa ni la driver wa Mh. Mwakyembe. Ninacho taka kusisitiza hapa ni kwamba madriver wanahitaji kusoma kitu kinachoitwa Defensive Driving, na somo litawasaidia madriver wote kuwa makini barabarani. Madriver wa magari ya serikali na za waheshimiwa wanaendesha rafu sana bila kufuata sheria wakidhani wao wako juu ya sheria maana wako na Mheshimiwa hivyo hata traffic police hawezi kumsimamisha au kupiga faini. Ok, hasimamishwi wala hapigwi faini lakini ajali itampata na tumeshapoteza wakubwa wengi kwa uzembe huu. Hawa madriver wanahitaji defensive driving. TIT inafundisha course hii na haichukui zaidi ya wiki. Uendeshaji wa gari siyo leseni na kunyooshea barabara ni pamoja na kufahamu matumizi sahihi ya barabara kwako wewe na mwingine na kuepuka ajali. Driver mzuri na hodari ni yule anayeanza na kumaliza safari yake vizuri. Mh. Mwakyembe anafanya swala hili kuwa la kisiasa yeye mwenyewe. He is already popular he don't any further cheap popularity. Lazima awe mfano wa kukemea unsafe driving kama iliyoonyeshwa na driver wake. Bongo hii mambo ya wakuu kutetea madriver wavunje sheria ni kawaida, kuna wakati naibu waziri wa wizara inayoshughulikia mambo hayo ya usalama alimripoti police aliyelirudisha gari lake ili lifuate sheria. Kitendo kama ilitakiwa imwajibishe waziri kama huyu ambaye analea uendeshaji mbaya ambao unaweza kupelekea ajali na kugharimu maisha ya watu. Ajali za barabarani zimeshagharimu Watanzania wengi maisha yao. Lazima tubadili tabia ya kuendesha magri. Lets observe Defensive Driving. Asanteni sana. It is possible to reduce road accidents.
 
Jeshi la Polisi nchini lijirekebishe haraka. Mh. Mwakyembe ndiye mhusika mkuu katika ajali hii na alieleza wazi kuwa alikuwa macho na aliona mwanzo hadi mwisho. Sasa huyu mwingine anayetaka kumsemea ana mamlaka gani ya kufanya hivyo??

Mara huko Wazo Hill tunaambiwa mbakaji kaachiwa na mbakwaji katiwa mahabusu na polisi, jamani hii nini IGP Mwema???? Huna watu, watimue wote kazi ili kusafisha jeshi la polisi laa sivyo kuna siku yatatokea makubwa zaidi.

Mh. Mwakyembe pole sana na Mungu akujalie upone haraka urejee kwenye mapambano. Kuna siku nilikupa hongera ulipojiuzulu ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC kwa kutovumilia maovu yanayotendeka huko, sasa polisi nao wanataka ujiingize kwenye uongo wao, na wakome kabisa. Hivi wao polisi wana ushirika gani na gazeti la Tanzania Daima?? Loh, Mungu tunusuru na wabambika kesi hawa.
 
Mwaka juzi nilipata ajali pale makutano ya IFM na Makao Makuu ya Magereza. Mimi niko njia kuu na yule dereva mwingine akitokea njia panda akanigonga. Ilikua wazi kwamba yeye ndo mwenye makosa. Bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa.

Alikuja trafiki na cha kwanza akachora jinsi yale magari yalivyokaa baada ya ajali. Kisha akanihoji mimi, akafuata dereva wa lile gari jingine halafu mashahidi wachache waliokuwepo. Baada ya kuchukua ushahidi na maelezo yote akamdokeza yule dereva mwingine kwamba ni wazi yeye ndo mwenye makosa lakini kama hakubaliani na hilo, kesi iende mahakamani ili ikaamuliwe huko nani aliyekuwa na makosa kulingana na ushahidi uliokusanywa. Bahati nzuri yule dereva mwingine alikubali kosa kwahiyo wote tukaongozana trafiki central ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya aliyesababisha ile ajali pamoja na masuala ya bima ili niweze kufidiwa.

Huu ndo utaratibu nnaoufahamu pale inapotokea ajali ya barabarani, iwe inamhusu raia wa kawaida kama mimi au mwanasiasa. Iwe hakuna majeruhi au wamekufa watu 60.

Huu utaratibu wa kuunda tume pale ajali ya barabarani inapomhusu mwanasiasa ni usanii wa hali ya juu. Ni njama za kuficha ukweli na kupotosha jamii. Mifano miwili ni ajali iliyomhusu Mh Chenge na hii ya sasa inayomhusu Mh Mwakyembe.

Ile ya Mh Chenge ni straight forward case ya reckless driving. Umegonga kwa nyuma, umeua watu wawili na isitoshe gari ilikua haina insurance. Hiyo tume ilikua mwanzo wa mkono wa mtu kumkwepesha mtuhumiwa kuwajibika kwa mujibu wa sheria.

Hii ya Mh Mwakyembe tunaona polisi na Tume wakifanya madudu ya wazi kabisa. Kwa jinsi walivyochemka inaelekea wametumwa lakini hawakuwa na "Plan B", yaani uzushi wa kueneza kama Mh Mwakyembe angepona. Lack of professionalism iko wazi kabisa kwenye hili tukio, ikiwemo na mikwala ya kitoto.

Ni usanii tu.
 
Mimi nimependa malumbano yanayoendelea humu ndani inaelekea kuwa watanzania sasa wameamka na wanauwezo wa kuchambua ngano ni ipi na makapi ni yapi.

Mheshimiwa Mwakyembe pole kwa yaliyokukuta,hizo ndozo siasa za Tanzania.Ukiwasema sana wanatafuta namna ya kukunyamazisha,usinyamaze kwani kuna jeshi kubwa sana nyuma yako kukusaidia.
 
Kwanza nimpe pole mwakyembe kwa kupata ajari mbaya na baadae kusalimika,Mwakyembe asitafute mchawi katika ajali hii ajue kila jambo hupangwa na Mungu.Kama ambavyo sisi tunajua dua la kuku halimpati mwewe,ndivyo na yeye aamini siku zake bado ingawa kwa Mungu zinahesabika.
 
Na kama Mwakyembe angefariki kwa ajali walah Dereva huyu angekiona cha mtema kuni kwani angebebeshwa mzigo wa kesi yote, pona yake naye engekufa ajalini.

Hii serikali ni mahututi kifikra kweli. Nilishangazwa na Kombe aliposema kuwa mtaalam wa kupima ile ajali amesomea Uingereza hivyo anaishawishi jamii iamini kuwa kamati ilikuwa makini. Sasa napata picha kwa nini kamati nyingi za uchunguzi hazihusishi polisi kwa sababu wa ukilaza wao wa sheria. Na huyo msomi wa uingereza anaweza kweli kufananisha system zetu za barabara na za kule??? WENZETu wanatumia CCTV kufanya uchunguzi ambapo wenzao wa hapa wanatumia ramli.

Ah we acha tu
 
Mimi napingana kabisa na Mheshimiwa Mwakyembe. Kwanza kabisa, yeye siyo polisi na siyo subject matter expert katika eneo hilo. Yeye mwenyewe amenukuliwa kwa mara ya kwanza akisema kwamba gari yake ilikuwa inaipita lori halafu akaingia kwenye pot hole tairi ikatoka gari lika anguka na kubiringika. Ya pili alisema kuwa gari yake ilikuwa inaipita lori halafu lori likagonga gari yake kwa nyuma upande wa kushoto gari ikapinduka. Ukiangalia kwa scenario zote mbili zinaonyesha kuwa driver wake hakuwa makini. Kwani kama alikuwa anaipita gari bila kuiscan njia halafu akaingia kwenye pot hole, basi alikuwa na makosa, maana ni mzembe hajapata big picture ya barabara kabla ya kufanya uamuzi wa kuovertake. Hili la pili la kugongwa kwa nyuma, kuna mambo mengi lakini tuangalie mawili, either driver alirudi upande wa lori haraka na mwendo wake ulikuwa mdogo kuliko wa gari kubwa, maana yake atakuwa amekanyaga break au kupunguza mwendo immediately baada ya kuovertake. La pili kama gari kubwa lilimgonga kwa nyuma upande wa kushoto maana yake, driver wa gari kubwa alikata kona haraka sana na alikuwa kwenye mwendo mkali, hivyo nalo gari lingeyumba hata kuanguka ama lingeigonga gari ya Mheshimiwa kwenye ubavu. Na hili kwenye ubavu halipo kwani halijasemwa. Hivyo possibility in kwamba driver wa Mh. Mwakyembe alirudi haraka kabla ya kumaliza kuovertake na kujibamiza kwenye gari kubwa, hapa tena kosa ni la driver wa Mh. Mwakyembe. Ninacho taka kusisitiza hapa ni kwamba madriver wanahitaji kusoma kitu kinachoitwa Defensive Driving, na somo litawasaidia madriver wote kuwa makini barabarani. Madriver wa magari ya serikali na za waheshimiwa wanaendesha rafu sana bila kufuata sheria wakidhani wao wako juu ya sheria maana wako na Mheshimiwa hivyo hata traffic police hawezi kumsimamisha au kupiga faini. Ok, hasimamishwi wala hapigwi faini lakini ajali itampata na tumeshapoteza wakubwa wengi kwa uzembe huu. Hawa madriver wanahitaji defensive driving. TIT inafundisha course hii na haichukui zaidi ya wiki. Uendeshaji wa gari siyo leseni na kunyooshea barabara ni pamoja na kufahamu matumizi sahihi ya barabara kwako wewe na mwingine na kuepuka ajali. Driver mzuri na hodari ni yule anayeanza na kumaliza safari yake vizuri. Mh. Mwakyembe anafanya swala hili kuwa la kisiasa yeye mwenyewe. He is already popular he don't any further cheap popularity. Lazima awe mfano wa kukemea unsafe driving kama iliyoonyeshwa na driver wake. Bongo hii mambo ya wakuu kutetea madriver wavunje sheria ni kawaida, kuna wakati naibu waziri wa wizara inayoshughulikia mambo hayo ya usalama alimripoti police aliyelirudisha gari lake ili lifuate sheria. Kitendo kama ilitakiwa imwajibishe waziri kama huyu ambaye analea uendeshaji mbaya ambao unaweza kupelekea ajali na kugharimu maisha ya watu. Ajali za barabarani zimeshagharimu Watanzania wengi maisha yao. Lazima tubadili tabia ya kuendesha magri. Lets observe Defensive Driving. Asanteni sana. It is possible to reduce road accidents.

Mengi ya uliyosema ni sahihi,hata hivyo nimeonelea nigusie kwenye highlights.

Kama unajaribu ku imply kuwa Mwakyembe anamtetea dereva wake ambaye karibia masababishie kifo,basi uko wrong. Mwakyembe kwa utashi wake hawezi kufanya hivyo.

Siwezi kuprejudge mambo mengi kama vile kumrundikia lawama dereva huyo kwani sijui ni kwa muda gani amekuwa akimwendesha Mwakyembe na sijui maoni ya Mwakyembe kuhusu uendeshaji wa dereva huyo kwa muda wote aliofanya naye kazi kabla ya ajali.

Pia sijui ni mara ngapi wameshawahi kusafiri pamoja na kupita njia hiyo kiasi cha kwamba nije hapa na kumake conclusions kuhusiana na umakini ama uzembe na kutokujua sheria za barabarani plus kutokuijua barabara hiyo ambayo inaonekana Mh Mwakyembe amekuwa akiitumia mara kwa mara.

Sijui sheria zetu za barabarani zitakavyoamua kuhusiana na ajali hii mara baada ya ushahidi wa pande zote kukusanywa,hata hivyo hai ingii akilini kwamba Mwakyembe anamtetea dereva mzembe aliyetaka kumsababishia kifo unless anajitetea yeye mwenyewe kwa kumtetea dereva.

Ni wazi ajali nyingi hutokea kutokana na uzembe wa madereva pamoja na barabara mbovu,lakini kutokana na maelezo yako hapo juu,umeonekana kufikia conclusion kwamba mwenye makosa ni dereva wa Dk,na hilo ni kutokana na ripoti zenye utata kutoka polisi ambazo zimepishana na zile za victims ambao kila mmoja alijieleza nadhani without the other's presence,na hivyo dhana kwamba walipanga haipo,na kwa mantiki hiyo basi,huwezi kufikia conclusion kutokana na madai yanayotofautiana eti kwa sababu possiblity zote mbili zinaonyesha dereva wa Dk ndiye mwenye makosa,tukifanya hivyo hatutajua ukweli wa mambo na itabakia siasa tu....Na kama ni kweli unajua kuwa politics haziitajiki hapo,then ni vyema tukajua kwanza nani mkweli kabla ya kufikia conclusion za kishabiki ama kisiasa.
 
Kwanza nakupa pole DR. Pili nakutahadharisha kwa usemi wa filamu ya James Bond iliyoitwa "you only live twice". Dr. Mwakyembe unavuna ulichopanda - mtu huwezi kupanda mpunga ukavuna mahindi. Mimi ni moja wa watu waliokuasa toka utoe ripoti yako kuhusu Richmond ulipokubali kutumiwa kuficha baadhi ya ukweli eti kuinusuru serikali (you threw integrity out of the window when you allowed yourself to be compromised).

Wakati huo nilikukumbusha usemi maarufu wa Mwalimu kuwa mficha ficha maradhi, kilio humuumbua. Kwa bahati kama ya mtende, wewe umepewa second chance - kilio kimeahirishwa, mpaka lini ? hilo sijui. If you really feel you cant fight them, join them but never let yourself be compromised on the things that you value most - honour, integrity and principle. That is a naked sign of weakness and you gave it to them on a silver platter.

By your action so far, it looks like you are spoiling for a fight - may be suddenly you realize that some things cannot just be let die and buried, they have this bad habit of raising their ugly head at some unexpected moment. Je, umeamua kunyoa ama kusuka ? The time is now, I doubt if they will give you another chance - your best option is attack. Dr. Slaa is a living example of the toughness that keeps the hungry hyenas at bay - et tu Brutus ?
When the going gets tough, only the tough keep going.
 

"Taarifa hiyo ya Polisi inakanusha maelezo yangu yote na ya dereva wangu kuhusu ajali ilivyotokea na kunitaka nijiepushe kutoa matamshi kuhusiana na ajali hiyo kwa madai kwamba sina utaalamu na masuala ya ajali"
tatizo wanazani bado ni mwaka 1990, pole sana niamini nikisema mungu yuko na wewe na sisi watanzania tuko na wewe mpaka mwisho.

"kuwa ushahidi wangu na wa dereva wangu haukuwa sahihi, ni ukiukwaji wa mgawanyo wa madaraka wa vyombo vya dola au kwa maneno mengine ni uingiliaji wa mamlaka ya Mahakama kinyume na Katiba ya Nchi.
Uamuzi wa Kamati hiyo Maalum wa kumkamata na kumshitaki dereva wangu ambaye tayari Kamati hiyo imemhukumu mapema (pre-judged) kuwa mwongo na mzembe hivyo afunguliwe mashtaka mahakamani, hauendani na utawala wa sheria na misingi ya haki"
dola wanataka kumshitaki mengi kwa line hii hii ya kudai ana miss inform jamii nadhani uko kwenye position ya kuweza, na una privilege ya kuweza kutaka kujua kwa nini kupitia mahakama ila hakikisha Grace Mwakipesile ni mmoja wa majaji.

"Kamati hiyo Maalum inadai kwamba nilikuwa nimelala ati kwa sababu ningekuwa macho ningeliumia."
bado awapo kwenye dunia ya ukweli hawa watu wanadhani wa-Tanzania ni watoto wa miaka mitano still on the process of being socialized therefore will believe anything ajabu mpaka Dr(Phd Educated) nae ni mjinga wa hivyo jamani awa watu mbona inaonekana ni wapuuzi mno, pole sana.

Kwanza, ni utaalamu gani unahitajika kuelezea kitu kilichomsibu mtu?
"yaani hapo inabidi ni cheke, mimi ndio najua kama nilijikwaa iweje unilazimishe lazima nilisukumwa wakati nishawaeleza nilikua mwenywe nani alinisukuma sasa" jamani mbona wapuuzi basi ata uongo kutunga awajui.

MUNGU YU NAWE DR.MWAKYEMBE
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU MMBARIKI DR.MWAKYEMBE
 
Kombe anatakiwa ajiuzuru kulinusuru jeshi la Polisi

Nilishangaa sana kuona IGP Mwema anampa madaraka makubwa James Kombe wakati IQ yake ni ndogo mno.

Alipata sifa akiwa RPC hapa Arusha kwa sababu ya RCO wake Godfrey Nzowa ambaye alistahili sifa zote kwa kuchukia sana ufisadi, aliwahi kumfukuza mhindi alipojaribu kumpa rushwa ofisini lakini Kombe alikuwa anapokea na kumfrustrate kabisa RCO wake katika mapambano dhidi ya uhalifu.

Kama umekaa na kuongea na Kombe ana kwa ana utakubaliana nami kuwa uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana
 
'dereva ndiye chanzo cha ajali ya dk. mwakyembe'
Hayo yamo katika taarifa ya Kamati iliyoundwa na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuchunguza chanzo cha ajali hiyo .
Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabara nchini, James Kombe alisema baada ya uchunguzi wao kamati imebaini kwamba chanzo chake hakikuwa roli lililokuwa linapitwa kama alivyopata kunukuliwa mbunge huyo, bali dereva wa mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo mkali.

....so wanapingana na ushahidi wa shihidi No 1!

“Kamati imefika eneo la tukio na kuwahoji mashuhuda walioona gari la mbunge huyo kabla na baada ya kupata ajali, kukagua gari la mbunge pamoja na kumhoji mtaalam wa magari aliyesomea uingereza, Francis Mwakatundu ambaye ameonyesha kupingana na kauli ya mbunge huyo kuwa aligongwa baada ya kuchunguza gari hilo na kuona hakuna sehemu ambayo ilionyesha kugongwa” alisema.

So kusoma kwake Uingereza ndio tuamini report yake? ajari hii haikuwa head-on collition, so possibly even a mine push can be dangerous anyway. so how do he justify that?

Alisema uchunguzi wao haukuona alama yoyote ambayo inayothibitisha kwamba gari la mbunge huyo liligongwa kwa nyuma au upande mwingine wowote. Alisema mikwaruzo iliyopo ni ile iliyotokana na gari hilo kuacha njia na kubiringika porini zaidi ya mita 60 kabla ya kugonga jiwe kubwa na kuling’oa na baadaye kuparamia mti mkubwa wenye mzunguko wa sentimeta 115 hadi kuung’oa na hivyo kupinduka.
kwi kwi kwi kwi kwi..... so kulingana na huyu mtaalamu aliyesomea Uingereza. Tuamini kuwa gari lilifanikiwa kugonga jiwe kubwa na kuling'oa na kisha likafanikiwa kugonga mti mkubwa circumference 115cm na kuung'oa? are these guys serious with this report.

Kamati hiyo iliundwa baada ya kuwepo na taarifa tofauti toka jeshi la Polisi, Mbunge huyo na dereva wake.
So kukiwa na utata wa taarifa polisi inaunda tume, na kupingana na tarifa za wahusika wakuu? Lawyers will help here, why not send it to court.
 
Mkuu unamaanisha nini? Kwani waligongwa na nini? Mbona siku zote tunaelezwa ni lori? Au ni jini?

ndiyo swali.. polisi walijuaje kuna lori linahusika? Hilo lori likowapi na ni la nani? hivi lori likiletwa wiki ijayo na kuoneshwa halina mikwaruzo yoyote na wakawaambia " unaona halina alama ya kugonga au kugongana na gari lolote" mtakubali?

well.. watu watasema "polisi wafunga mjadala wa kuonesha lori lililohusika na ajali ya mwakyembe halina mikwaruzo!"
 
Nianze kwa kumpa pole Mhesihimiwa Mwakiembe kwa ajali uliyoipata.

Mimi nilishangazwa sana na maelezo aliyoyata Afande Kombe yaliyokuwa yamejaa vitisho kana kwamba anamtishia mtoto mdogo. Lakini kilichoniudhi zaidi na kunifanya niandike, ni pale alipomwonya Mh. Mwakiembe kwa kumweleza asijiingize kwenye masuala ya kitaalamu! Kisha akaja na ramli zake anazotaka tuamini kuwa ni utaalamu wake.

Akasema Mheshimiwa alikuwa amelala kwa kuwa wakati wa ukaguzi wa kamati walikuta kiti chake kimelala kwa nyuma. Kwa utaalamu wake, mtu akitaka kulala kwenye gari lazima alegeze kiti kilalie nyuma la sivyo hatapata usingizi. Lakini amesahau mambo ya msingi ambayo yeye na wataalamu wa aina yake kwenye hiyo kamati hawakuyajuwa:-

a) Mwendo kasi wa gari (kwa kitaalamu Velocity)tumeambiwa ulikuwa zaidi ya 120km/hr. Mh. nakadiria ana uzito sio chini ya kilograme 90. Kwenye Physics, kuna kitu tunachokiita momentam. Momentam inapatikana unapozidisha velocity na uzito{120km/hrx90kg}.Momentam hii ilirudishwa kuwa sifuri kwa muda mfupi tu baada ya ajali kutokea na madhara yake huwa ni makubwa na ndicho kinachoumiza watu ajali inapotokea kwa kuwabamiza kwenye bodi za magari. Kwanza angeweza kuvunja lock zote ambazo hutumika kurekebisha kiti ili kikae kwa kufuata matakwa ya abiria au hata kuvunja frame za kiti au hata kukata bolt zilizotumika kufungia kiti hicho. Sasa sielewi hawa wataalam kama walikagua kiti kile baada ya kukikuta kimelala nyuma au walikurupuka na kuandika kuwa alikuwa amelala?

b) Lakini hata kama kiti kile kilikuwa kimeegemea nyuma baada ya ajali na uchunguzi ukaonyesha kuwa lock zake na frame hazikukatika(?) wakati wa ajali, bado yawezekana baada ya ajali kuna wasamaria wema wakati wakimtoa kwenye gari ilibidi walegeze zile lock ili aweze kutoka kwa urahisi na hawakuwa na sababu ya kukirudisha kiti kile sehemu yake kwa kuhofia majibu ya kipuuzi kama hayo yaliyotolewa. Je waliwauliza wale waliotoa msaada walifanyaje wakati wa kumtoa kwenye gari?

c) Hivi ni kwanini hatuambiwi chochote kuhusu lile lori? Walilikagua na kuona kuwa halikuwa na rangi yoyote inayofanana na gari la Mh? Na kama dereva wa lori aliona ajali ikitokea, kweli kiubinadamu na kwa kutambua hayakuwa makosa yake asingelisimama na kutoa msaada hata kama ni wa kuokoa mali kama abiria wamefariki?

Kama majibu yale ndio ya wataalamu wa ajali za barabarani basi tumepata jibu kwani magari yanazidi kuuwa Watanzania wasiokuwa na hatia kila siku.

Sina hakika kama Kombe na wataalamu wake huko jeshini wanajuwa mahusiano ya mwendo kasi (v), Kipenyo cha kona ya barabara (r), center of gravity (g) na uzito wa gari na ajali zinazotokea kwenye maeneo ya kona kali!Kwa kifupi kuna kitu kinaitwa centrifugal and centripetal forces, hawa wataalamu wanazijuwa? Nina wasi wasi kuna wakati watatueleza kuwa ajali za maeneo yale zinatokana na mashetani yaliyo kwenye mibuyu maeneo yale ambayo huwa yanataka damu za binadamu.

Namshauri Kombe aendelee na kazi ya kuwapeleka watuhumiwa mahakamani ili sheria zifuate mikondo yake na kamwe asijiingize kwenye masuala ya kitaalamu ambayo hajayasomea kule CCP MOSHI!
 
Na Mwandishi Wetu
MwanaHALISI


AJALI ya gari iliyomhusisha Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe imeanza kuibua mengi, MwanaHALISI limegundua.

Joseph Msuya, dereva wa Mwakyembe, amenukuliwa akisema askari wa Usalama Barabarani (trafiki) hakuwa wa msaada wowote kwake na Mwakyembe ambaye alikuwa bado hajajitambua.

Gazeti hili limeelezwa kwamba trafiki huyo alikuwa akisimamisha magari, akionyesha kuwa anataka yasaidie majeruhi kwenda Iringa, lakini alikuwa akiyaruhusu yaondoke bila kutoa huduma hiyo kwa sababu ambazo hazijafahamika hadi sasa.

Gari ambalo hatimaye lilitoa msaada kwa Mwakyembe lilisimamishwa na dereva wa mbunge hyo baada ya kuona “kulikwa na mchezo wa kuigiza.”


Taarifa zilizozagaa kwenye eneo la ajali, kabla na baada ya Mwakyembe kujitambua, zinasema trafiki huyo alikuwa amemwambia dereva Msuya kuwa yeye aende kupata matibabu hospitalini Iringa mjini “kwa vile Mwakyembe alikuwa tayari amefariki.”

Hata hivyo, Msuya alipoulizwa juu ya kauli hiyo alisema, “Sina la kuwaambia sasa hivi. Sina la kusema… Kama lolote basi tusubiri kutoka vyombo vya sheria.” Hakukanusha kusikia au kuambiwa hayo.

Taarifa hizo ambazo hazikuweza kuthibitishwa zinasema ushauri wa trafiki ulifanywa wakati Mwakyembe alikuwa hana fahamu na alionekana kama aliyekufa.

“Lakini kwa bahati nzuri, Dk. Mwakyembe alipata fahamu na kuanza kukohoa na ndipo hata trafiki huyo aliposhindwa kuendeleza ushawishi wake wa kutaka mbunge huyo atelekezwe," zimeeleza taarifa.


Trafiki alikuwa mmoja wa trafiki wawili waliokuwa wakisafiri kwa gari aina ya Coaster lililokuwa likitoka Iringa, na lilipishana na gari la akina Mwakyembe lililokuwa linaelekea Dar es Salaam.

Mwakyembe, akiwa katika gari lake aina ya Toyota Lancruiser, Na. T 362 ACH, Alhamisi iliyopita, alipata ajali eneo la Ihemi, mkoani Iringa na kupata mstuko wa shingo wakati dereva wake, Msuya alipata michubuko mwilini.

Taarifa za mwishoni mwa wiki iliyopita zinasema polisi kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam walikwenda nyumbani kwa Mwakyembe wakitaka kumchukua dereva Msuya kwa madai kwamba “wanataka kwenda naye kwenbye eneo la tukio, lakini ndugu zake waliwakatalia.

“Hatuwezi kumruhusu atoke hapa. Wanamtaka aende kufanya nini? Kama ni suala la vipimo, basi polisi wa iringa tayari waliishapima. Hatoki hapa,” ameeleza mmoja wa wanafamilia akinukuu mjadala uliojitokeza kati ya polisi wa ndugu zake nyumbani kwa Mwakyembe.


Msimamo wa familia unafuatia kutofautiana kwa maelezo ya polisi na maelezo yale ya mwakyembe na dereva wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi, amenukuliwa katika vyombo vya habari nchini akisema gari la Mwakyembe lilianguka kutokana na kile alichoita “uzembe wa dereva.”

Nyombi amekaririwa akidai kuwa uzembe huo wa dereva ulitokana na mwendo wa kasi ambao unadaiwa kumfanya ashindwe kumudu gari hilo.

Hata hivyo, maelezo ya Nyombi yanatiliwa mashaka kwa vile taarifa zinasema gari la Dk. Mwakyembe liliangukia upande wa kushoto; kwa maana kuwa lilikuwa limefanikiwa kulipita lori lililokuwa mbele yake.

Zaidi ya hayo, polisi wa usalama barabarani hawakuweza kusimamisha na kutambua lori hilo, ambalo Dk. Mwakyembe na dereva wake wanasema ndilo lilisababisha ajali. Ni hali hii inayozidi kujenga mashaka juu ya taarifa ya Kamanda Nyombi.

Hadi gazeti linakwenda mtamboni, hakukuwa na taarifa zozote juu ya lori hilo, dereva wake wala mmiliki wake kukamatwa na kuhojiwa na polisi.

Vilevile, hatua ya polisi kutoa taarifa ya ajali hiyo hata kabla uchunguzi kamili haujafanyika, imejenga mashaka na kufanya wengi wahoji kama hakuna kinachozibwazibwa.

Polisi walitoa taarifa Alhamisi jioni, siku ambayo ajali ilitokea, wakisema hakukuwa na mchezo wowote mchafu katika tukio hilo.

Hata hivyo, maelezo ya Dk. Mwakyembe, dereva wake na taarifa kwamba trafiki hawakutoa msaada zinazidi kuweka giza katika tukio zima la ajali hiyo.
 
Kamati Yadai ripoti rasmi imewasilishwa jana kwa IGP

*Ni baada ya Mbunge huyo kudai ukweli umefichwa

Edmund Mihale
Majira

SIKU moja baada ya Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe kutoa taarifa ya kutoridhishwa na taarifa ya Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema kuhusu mazingira ya ajili yake, Jeshi hilo limeikana taarifa hiyo.


Taarifa hiyo inayolalamikiwa na Mbunge huyo, ni ile iliyotolewa Mei 26 mwaka huu, iliyoeleza uamuzi wa kukamatwa na kufikishwa mahakamani dereva wake kwa kosa la uzembe na kusababisha ajali iliyotokea Mei 21 mwaka huu eneo la Ifunda.

Akizungumza na Majira Makao Makuu ya Jeshi hilo jana, Dar es Salaam, Ofisa Mnadhimu Kitengo cha Habari katika Jeshi hilo,Bi Suzane Kaganda, alisema Polisi haitambui taarifa hiyo kwani taarifa inayotambulika ya ajali ya Dkt. Mwakyembe, iliwasilishwa jana asubuhi ofisini kwa IGP Mwema.


"Mimi nashangaa kusikia taarifa hiyo katika magazeti kwa kuwa mzungumzaji wa taarifa hiyo ni IGP pekee na ndiye aliunda kamati hivyo, waliotumwa walipaswa kuileta kwake na leo (jana) ndio amekabidhi hiyo taarifa," alisema Bi. Suzane.

Alisema kimsingi kamati hiyo ilipewa kazi ya kuchunguza mazingira ya ajali na kutoa majibu ya uchunguzi wao kwa IGP na endapo itabainika uzembe ulifanyika katika ajili hiyo itapelekwa kwa mwendesha mashitaka wa Serikali naye atatolea maamuzi kupelekwa mahakamani mhusika.

Bi.Suzane alisema kamati hiyo haikutumwa kuhukumu mtu yeyote kwani haina mamlaka ya kufanya hivyo na kama itafanya hivyo, itakuwa imeingila uhuru wa Mahakama ambayo kisheria ndiyo yenye mamlaka.

Alipoulizwa kuwa taarifa iliyotolewa na Dkt. Mwakyembe kuwa ilikuwa ni ya kukurupuka kwa kuwa hakustahili kufanya hivyo, Bi. Suzane alisema Dkt. Mwakyembe kama raia anayo haki ya kueleza hisia zake kwa mujibu wa sheria za nchi lakini alisisitiza kuwa taarifa kamili ipo kwa IGP na si hiyo aliyoijibu.

Alipoulizwa kuhusu taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Bw.Advocate Nyombi kupitia vyombo vya habari kuwa dereva wa Mbunge huyo anatafutwa na Jeshi hilo,Bi Suzane alisema anachofahamu ni kuwa taarifa hiyo si sahihi kwani naye amekuwa akiisoma katika vyombo vya habari na kwamba taarifa kamili itasomwa na IGP Mwema.

Alisema Jeshi hilo linafuata taratibu za kisheria na halikurupuki katika maamuzi yake hivyo kama itaonekana dereva huyo amefanya kosa atahukumia kutokana na sheria zilizopo.

Juzi Dkt. Mwakyembe alilijia juu Jeshi la Polisi akidai kutokana na ripoti hiyo limeonesha jeuri na kiburi kisichokuwa na tija na ni kielelezo kuwa baadhi ya viongozi wa vyombo vya dola wamelewa madaraka.

Alisema purukushani zinazofanywa na Jeshi la Polisi zinamfanya aingiwe na wasiwasi kuwa ajali yake haikuwa ya kawaida.

Alielezea kushangazwa na kitendo cha Kamati Maalumu iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Mwema kuchunguza ajali hiyo kushindwa kumhoji yeye na dereva wake ili kupata picha hali na kamilifu kuhusu ajali hiyo.


"Kama mimi na dereva wangu tungesikilizwa nina uhakika taarifa ya Kamati Maalumu isingesomwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kukosa umakini na viwango," alikaririwa akisema Dkt. Mwakyembe.

Alifafanua kuwa hatua ya Jeshi la Polisi ina mwelekeo wa kisiasa kuliko utaalamu na upepelezi wa uendeshaji mashitaka.

Alipinga vikali kauli ya kamati hiyo kuwa wakati ajali hiyo inatokea alikuwa usingizini.

" Ningetegemea madai hafifu kama hayo yangetolewa na mganga wa kienyeji anayetumia ramli kufanya maamuzi kuliko Jeshi la Polisi linalotumia utaalamu," alikaririwa akisema.

 
Back
Top Bottom